Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, June 30, 2010

Kabla ya ndoa

Kaka mmoja kabla hajaoa dada wa mchumba wake alimuita kwenye maongezi kwa wake zake. Alipofika akamkuta shemeji yake peke yake (dada).

Yule dada akamwambia anaomba afanye nae mapenzi kabla hajamuoa dada ake na kumuambia amfute chumbani jamaa amfuate nyuma.

Jamaa akafikiria kwa muda na kuamua kwenda nje. Huko akakutana na wazazi wakwe wakamwambia 'wow umefaulu kishawishi, karibu kwenye familia yetu'

Jamaa kimoyo moyo akasema 'always kumbuka kuacha condom kwenye gari, nilikua nazifuata.'

Tuesday, June 29, 2010

Mpira wa miguu

Mwanamke mmoja alipokua anaongea na rafikie ghafla akakumbuka kitu na kumuuliza, ''leo kuna mpira live?''

Rafiki yaka akamjibu, 'ndio shoga angu, kulikoni?'

Yule mwanamke, ''mwenzangu sijui nani atasogeza ile coffee table ya kioo pale nyumbani?''
Rafikie... ''kulikoni na hiyo coffee table?''

Mwanamke, ''mwenzangu mume wangu yupo nyumbani jana si alipiga teke jagi la maji... Midadi ya mpira kwenye tv''

ATM

Mwanaume na ATM.
1. Atatoa kadi ya ATM.
2. Ataichomeka.
3. Ataingiza namba ya siri.
4. Atachukua pesa, card na risiti.

Mwanamke na ATM.
1. Ataitoa kadi ya ATM.
2. Atajichek kwenye kioo cha makeup.
3. Atazima gari.
4. Ataweka funguo kwenye pochi.
5. Ataitafuta ATM kadi kwenye pochi.
6. Atachomeka kadi.
7. Atatafuta kikaratasi chenye namba za siri.
8. Atasoma maelekezo kwa dk.2.
9. Atabonyeza CANCEL.
10. Ataingiza namba ya siri upya.
11. Ataangalia balance.
12. Atatafuta kibahasha.
13. Atatafuta peni kwenye pochi.
14. Atatoa hela.
15. Atarudi kwenye gari.
16. Atajiangalia makeup tena.
17. Atatafuta ufunguo kwenye pochi.
18. Atawasha gari.
19. Atarudi tena kwenye ATM.
20. Ataenda chukua kadi na risiti.
21. Ataweka kwenye walet.
22. Atajiangalia makeup tena.
23. Ataondoka km chache na kutoa handbreak.

Wanaume

Kaka mmoja alikuwa bar baada ya kupata mbili tatu akajikuta akisema ''inaonyesha wanaume wengi wana sababu moja ama mbili, wanakaa sana bar kwasababu hawana wake nyumbani au wanao wake nyumbani...''

Gitaa

Kaka mmoja alikuwa akimuambia mwenzake kuhusu yeye kuhama alipokuwa akiishi na jirani yake.

Rafiki akauliza, ''kwa nini umehama?
Jamaa akajibu ''kwa sababu ya kelele za gitaa kila siku usiku kwa muda wa saa moja''

Rafiki yake: Gitaa? Jamaa: ndio lilikuwa lapiga kelele sana usiku.
Rafiki yake: So ukaamua kuhama eneo kwa kuepuka kelele za gitaa? Si ungewaambia waache hizo kelele?

Jamaa: Nilihama, ni mimi nikiepiga gitaa...

Darasani matokeo

Mwalimu akiwaambia wanafunzi. ''kwa kweli sijaridhishwa na majibu yenu kwenye mtihani''

Mwanaftnzi nae akarukha na kujibu, 'hata sisi hatujaridhishwa na maswali'

Monday, June 28, 2010

Mh! Bure

Mama mmoja akiwa na mtoto wa miaka miwili alienda nunua nyama. Alipofika muuza nyama akamwambia ''ntakua nakupa nyama bure mpaka mtoto atakapofikisha miaka 16'' mama akashukuru sana.

Miaka kadhaa baadae mtoto alipoenda nunua nyama akamwambia muuza nyama ''natimiza miaka 16 kesho''
Muuza nyama akajibu ''najua''

Muuza nyama: Pia kamuambie mama yako muda wa nyama ya bure umeisha na mwangalie usoni ataipokeaje?.

Mama nae baada ya kuambiwa nae akamttuma mtoto... ''kamuambie kwa kipindi chote nimekuwa nkipata mikate, maziwa bure halafu mwangalie usoni ataipokeaje?

Sunday, June 27, 2010

Kulingishia

Katoto kamoja ka kiume kalimringishia mpira wa fubol mwenzake wa kike.
Yule wakike akalilia kwa mama ake akanunuliwa.

Siku ingine akalingishiwa baiskel nayo akanunuliwa.

Mara ya tatu yule wakiume akavua kaptula na kumuambia yule wa kike ''mama yako hawezi kununulia hii'' akimaanisha naniliu...

Wa kike akamjibu ''mama kaniambia kwa vile nnayo hii (naniliu) naweza kupata hizo nitakavyo''

Ndoa

Maisha ndoa bwana.
Mwaka wa kwanza, mwanaume anaongea mwanamke anasikia.
Mwaka wa pili, mwanamke anaongea mwanaume anasikiliza.
Mwaka wa tatu, wote wanaongea majirani wanasikiliza.

Soma hii

Josh: Halow, naongea na Esta?
Esta: Ndio.
Josh: Esta yule nlikutana nae usiku tukaondoka wote?
Esta: Ndio, ukanisifia sana nna mapaja mazuri...
Josh: Nakumbuka kabisa. Za siku?
Esta: Njema tu nna mimba yako.
Josh: Enhe! Wrong namba.

Kasuku part ii

Kuna jamaa mmoja aliambiwa ''huyu kasuku akinyanyua mguu wa kushoto anaongea kiswahili, wa kulia anaongea kidhungu.

Jamaa akauliza ''je akinyanyua miguu yote je?"

kasuku akadakia na kujibu ''we fala nini, si ntakua napaa?''

Jani

Vijana wawili walikua wamekaa chini ya mti na ka-giza giza fulani. Mmoja akamuambia mwenzake.

''kama ningekuwa na tochi vile...'' jamaa mwenzake akamuuliza, ''kwa nini?''

Jamaa akajibu ''umekuwa ukila majani kwa dakika 20 sasa.''

Dada na kaka

Maongezi ya dada na kakafulani.
Kaka: Enhe, ulisema umeolewa enh?
Dada: Niliolewa nanguruwe nkaachika nkenda kuishi nakapanya.

Nanguruwe na Nakapanya ni maeneo/vijiji fulani.

Kasuku...

Kuna kasuku mmoja alikuwa anafugwa kwenye danguro. Mama mmoja akataka amnunue akaambiwa lakini kasuku ana matusi, yule mama akasema ntamnunua hivyo hivyo.

Alipomnunua akamueka kwake. Kasuku akaongea.
Kasuku: Hee! Danguro jipya, boss mpya. (akimaanisha matha house).

Kidogo wakaingia watoto wa mwenye nyumba wawili kasuku akasema.

Kasuku: Hee, danguro jipya, malaya wapya.
Kidogo akaingia baba mwenye nyumba. Kasuku akasema.
''hee! George karibu kwenye danguro jipya.

Mkanda wa gari

Jamaa mmoja alikuwa anaongelea kuhusu kufunga mkanda kwenye gari mambo yalikuwa hivi:
1: Mimi kwenye gari lazima nifunge mkanda.
2: Hata mimi kila mara.
3: Mimi mke wangu kanizoesha mpaka nikifuata kitu kwenye gari nafunga mkanda kwanza.

Saturday, June 26, 2010

Oda

Jamaa alienda bar, akaagiza mishkaki. Ilichukua takribani nusu saa akiisubiri baada ya muda kidogo mhudumu akaja na kumuambia ''samahani kaka umeagiza mishkak?''
Kaka akajibu ''ndio''

Mhudumu akamjibu ''oh! Ndio wanamchuna ngozi ng'ombe vumilia kidogo tu''

Simu hospitali

Mwanaume mmoja alipiga simu hospitali ya wagonjwa wa akili akapokea mtu wa mapokezi na kumuambia, ''kuna mgonjwa yeyote chumba namba 30?''

Mtu wa mapokezi akaenda kuangalia na kurudi akamjibu yule mtu kwenye simu ''hamna mtu kwenye hicho chumba.''

Jamaa kwenye simu akaongea... ''oh! hiyo inamaanisha nimefanikiwa kutoroka.''

Darasani

Mwalimu mmoja aliwauliza wanafunzi wa darasa la kwanza swali ''baba yako akikopa sh 1,000/= halafua akienda kukopa sh 1,000/= atakuwa anadaiwa sh ngapi?

Mtoto: Hatolipa kitu.
Mwl: We mtoto una akili kweli.
Mtoto: Ndio ninazo kwa sababu humjui baba yangu.

Mbio mbio...

Jamaa alifumaniwa na akatoka mbio bila nguo...kufika kwake mkewe akamuuliza vip?jamaa akajibu nimevamiwa na majambazi wamenipora kila ki2 mpaka nguo.mkewe akamjibu kweli hao majambazi kiboko wamekuvalisha mpaka condom..!! Tafakari!

Friday, June 25, 2010

Padre na sista

Padre na sista walienda kutafuta hotel ya kulala ugenini, bahati mbaya chumba kikapatikana kimoja. Ikabidi wakichukue hivyo hivyo.

Usiku wakatenga mpaka kitandani kwa kutumia mito. Wakalala mpaka asubuhi.

Asubuhi wakati wanamtafuta mtu wa mapokezi ili waondoke akawa haonekani. Sista akamwambia padre ''si turuke ukuta?''

Padre akamjibu, ''umeshindwa kuruka mto jana usiku utaweza ukuta?''

Nyama

Jamaa alinunua nyama kilo 2 aliporudi house boy akamwambia paka kala yote! Kumpima paka ana kilo 1 jamaa akauliza hyo kilo 1 imeenda wapi?

Kidogo ajali

Gari moja ilisikika ikiliza breki kwenye lami kwa sauti ya kukoswa koswa mtu kugongwa...

Jamaa waliokuwa kijiweni mmoja akatamka kwa wenzake ''dah jamaa hana shabaha''
akimaanisha dereva.

Kusafirisha maiti.

''Ndege moja lilikuwa linasafirisha maiti, bahati mbaya ikaanguka na watu wote wakafa.'' jamaa akimsimulia mwenzake.

Jamaa aliekisimuliwa akanena la kwake na yeye ''haa! Kwa hiyo maiti ikafa tena?''

Ajali

Jamaa aligonga mtu bahati mbaya akiwa na pick-up hakusimama. Akakanyaga mafuta mpaka polisi kurepoti alipofika akawa anaelezea sasa:

Dereva: ...nimegonga mtu pale mkwedu.
Polisi: Maiti umeiacha wapi?
Dereva: Pale pale.

Polisi kufika kuikagua gari ndo wanaiona maiti imeangukia kwenye pick-up nyuma.

Ujauzito

Mwanamke mmoja alienda kwa daktari. Alitafuta mtoto kwa miaka 10 bila mafanikio.

Daktari: Majibu yanaonyesha huu mjamzito.
Mwanamke: Ashukuliwe mungu loh!

Daktari akatoa story fupi kidogo.

Daktari: Nakumbuka nilikuwa na kuku wangu mda mrefu hakutaga, nikabadilisha jogoo akaanza kutaga.

Mwanamke kuchangia stori akajibu ''me too.?'

Tiket

Danny: Ima unaelekea wapi?
Ima: Naelekea ubungo kukata tiketi ya kwenda zanzibar.

Yero...

Mmasai alikuwa safarini njiani akaomba achimbe dawa, alipomaliza akaendelea na safari, ghafla akakumbuka akamwambia dereva "Eeh rafiki nimesahau ile fuko ya Matako" akimaanisha chupi.

Mhudumu hotel

Jamaa alipokelewa mizigo hotelini na mhudumu mpaka chumbani. Kisha mhudu akauliza ''kingine cha ziada?''

Mume akajibu ''asante, hamna.''

Mhudumu akauliza tena ''labda mkeo atahitaji kitu?'' mume akajibu ''oh, nashukuru kwa kunikumbusha, mnauza kucha za kubandika?''

Hii nayo

Jamaa mmoja alikuwa anamsifia msichana mmoja mzuri aliemuona kwa rafiki yake.

''...unasikia kaka aise huyo dada mzuri mguu upo, bambataa ya uhakika... Ana tiles mpaka kwenye ulimi...''

Mwenzake akamuuliza ''tiles?''
akamjibu 'eenhe ivo ivo'

Hii nayo

Jamaa mmoja alikuwa anamsifia msichana mmoja mzuri aliemuona kwa rafiki yake.

''...unasikia kaka aise huyo dada mzuri mguu upo, bambataa ya uhakika... Ana tiles mpaka kwenye ulimi...''

Mwenzake akamuuliza ''tiles?''
akamjibu 'eenhe ivo ivo'

Chabo

Watoto wawili na wazazi wao walikuwa wamepanga chumba kimoja. Kitanda cha ghorofa, juu wanalala watoto chini wazazi.

Siku moja mtoto mmoja alimuuliza mwenzake ''we umewasikia madingi jana usiku?', dogo akajibu ''hapana.''

Basi ngoja leo ntakustua. Ilipofika usiku wakati wazazi wameanza vitu vyao yule mtoto akaamwamsha mwenzake kimya kimya ''oya.. oya.. Wameanza''

Dogo kwa sababu analala upande wa ukutani wakati anajiandaa kupiga chabo si akaporomoka mpaka chini yaani katikati ya shughuli za madingi....

Mtoto na baba

Mtoto akimuuliza baba yake:
Mtoto: Mbona umechelewa sana?
Baba: Oh, mwanangu ndege ilipata matatizo kidogo angani.
Mtoto: Ilipata pancha?

Baba: Hapana mwanangu ni ya umeme umeme tu.
Mtoto: Usiniambie umeme waliwakatia tanesco?
Baba: !

Simu ipo wapi?

Mama akimuuliza mwanae mtundu mtundu.
''Josh simu yangu ilikuwa mezani ipo wapi?"

Yule mtoto kwa kujiamini kabisa alimjibu mama yake ''ai ma.a.ma simu ilivyo chafu vile? Me nataka nkusafishie nimeiloweka kwanza.''

Mikumi

Siku moja mtoto mmoja alikuwa kwenye gari na baba ake na mama ake. Kale katoto kakaona pundamilia wa kuchorwa, papo hapo kakakumbushia ahadi alopewa na baba yake.

'Daddy... Daddy... Ulisema utanipeleka mikumi kuona wanyama halafu simwambii mama unamletaga anti mama akisafirigi''

Vocha

Jamaa alipata ofa siku moja ya dola tano aweke kwenye simu yake. Jamaa akajibu ''mi nshazoea mia tano mia tano''

Jamaa akawa anaendelea kusema ''naogopa simu yangu itachanganyikiwa nkiweka vocha kubwa kubwa''

Akimsifia msichana

Jamaa mmoja alikuwa anamsifia msichana mmoja mzuri aliemuona kwa rafiki yake.

''...unasikia kaka aise huyo dada mzuri mguu upo, bambataa ya uhakika... Ana tiles mpaka kwenye ulimi...''

Mwenzake akamuuliza ''tiles?''
akamjibu 'eenhe ivo ivo'

P. O. P.

Daktari mmoja alikuwa anapoke sana rushwa, hivyo siku moja aliekewa mtego baada ya kutaka hela toka kwa mtoto wa kigogo. Ikawa hivi:

Mtoto alienda na hiyo pesa, daktari akamchoma sindano ya usingizi kisha akamfunga ile P. O. P. mkononi.

Mtoto kutoka nje baada ya sekunde polisi wakaingia kusach ile hela hawakuipata.

Siku ya kuling'oa lile P.O. P. alienda kwa Daktari yule yule. Daktari akamng'oa na pia akazichomoa zile pesa zilikuwemo ndani ya lili p.o.p kisha akamuambia yule mtoto 'kamwambie baba ako kuwa ile pesa ndo naenda itumia sasa.'

Shuka...

Mtoto mmoja alizoea sana kumtania baba yake, siku moja baba yake alikuwa amesimama nje uku amevaa shuka kama msuli vile.

Basi yule mtoto akamfuata na kumuambia ''baba hujafunga zipu...''
baba wacha ashtuke.

Konda

Kondakta mmoja kituo fulani wakati akiita abiria kwenye daladala ''k'koo k'koo gari, haki ya mungu kariakoo gari...''

Thursday, June 24, 2010

Magazeti

Mama mmoja aliwekea mwanae wa kike magazeti siku ya harusi kwenye pichu. Jamaa baada ya kujibebea jiko akawa sasa anataka tunda, ikawa kila akifunua anakutana na kipande cha gazeti.

Ikabidi aulize kwenye simu kwa mama mkwe ''halo... nanihi ya mwanao ipo ukurasa wa ngapi?''

Wakili

Kaka mmoja alienda kwa wakili na kuuliza kuhusu gharama.
''elfu hamsini kwa maswali matatu'' wakili alijibu. ''ni ghari ivo?'' mkaka aliuliza.

Wakili akajibu ''ndio'' kisha akaendelea wakili ''...na swali lako lat tatu linasemaje?''

Mke na Mume...

Mwanamke mmoja alimuambia mumewe walipokutana na ahera... ''afadhali tumekutana tena huku...'' yule mumewe akamjibu ''wee! Tulikubaliana mpaki kifo kitutenganishe, huku mie singo''

Mapenzi na simu

Dada mmoja kwao mambo safi kidogo, siku moja alimpigia simu boi frend wake wakawa wanaongea malavi davi kwa simu ya mezani.

Maongezi yalitafuna muda ile mbaya mpaka opareta wa kampuni husika ya simu akaingilia maongezi. ''dada samahani, unapiga simu toka kwa mzee...'' yule dada akajibu ''ndio.'' Basi yule dada wa Kampuni akamuambia ''bill kubwa jamani unamsabishia mlipaji''

*true story*

Hii toka duka la madawa...

Mwanamke mmoja alienda kununua dawa fulani ambayo alihojiwa na m-pharmacia:

Pharmacy: We unaihitaji hii ya nini?
M'ke: Nataka kwenda kumuua mume wangu.
Pharmacy: Hapana siwezi kukupatia kwa kweli.

Mwanamke akatoa picha ya mume wake akiwa kitandani na mke wa M-pharmacia kisha mfamasia akasema ''ngoja nakupa sasa hivi, sasa mbona ukusema kama una vigezo?''

Tumetokea wapi?

Mtoto mmoja akimdadisi mama ake, "mama, kwani si binadamu tumetokea wapi?'' mama yake akamjibu kuhusu Adam na Eva....

Baadae akamuuli swali lile lile baba ake baba akamjibu kulingana na historia ya sokwe mtu mpaka kuwa binadamu.

Mtoto akabaki ??? Akaenda kwa mama tena. 'mama mbona baba amenielezea kuhusu sokwe nk nk?'
Mama akamjibu, ''well my son, mimi nimeelezea upande familia yetu na yeye ya kwao...''

Yakhee mmoja

Yakhe mmoja wa kipemba aliletewa supu kwenye mgahawa. Baada ya kuikagua kagua akawa haielewi elewi akamuita mhudumu amuulize:

Yakhe: Yakhe samahani hii nyama ya sehemu gani atii?
Mhudumu: Mzee hii nundu hii.
Yakhe: Aaah yakhe hii mbona kama sio.

Yakhe akaendele kuongea.

Yakhe: Yakhe hii si nyama ya nku*&%u hii?
Aah hii nyama ya nku*@€u yakhe nibadilishie...

Konda akidai chake

Siku moja kwenye daladala wakati anadai nauli hali ilikuwa hivi:

Konda: Ma mdogo hapo nauli yako.
Ma mdogo akajibu, ntakupa nimekaa vibaya.

Konda: Haya, na akina mama hapo mbele?
Akina mama, tutakupa subiri.
Konda: Akina baba huko nyuma?
Akina baba wakajibu, ''aaah we mtoto we shika adabu yako''

Wednesday, June 23, 2010

Vichaa

Wagonjwa wa akili wawili walikuwa pembeni mwa bwawa la kuogelea. Mmoja akaingia, yule wa pili akaingia na yeye kumuokoa mwenzake.

Baadae daktari akamuambia yule wa pili ''hongera sana umefanikiwa muokoa mwenzako, tutakuachia huru umepona sasa''
yule wa pili alifurahi sana.

Daktari akaendelea: ila bahati mbaya mwenzako kajinyonga tumemkuta. Yule kichaa wa pili akajibu ''oh, hapo nilimuweka mimi ili akauke''

Uuwiii

Mama mmoja alienda kumuangalia mumewe, maongezi yakn na dokta yalikuwa hivi:

Dokta: Mumeo atakufa siku yoyote karibuni.
Mke: Usiniambie kitu nnachojua tayari, we niambie kama kutakuwa na upelelezi...

Mtoto huyu mh

Mtoto mmoja alienda chumbani kwa mama ake akakuta anavaa sidiria. Akamuuliza mama alipoziona chuchu. ''mama hizo nini?'' mtoto aliuliza. Mama akamjibu ''haya ni maputo siku nkifa yatanifanya nielee ahera.''

Siku mbili mbele akaja kwa mama yake mbio mbio, ''mama.. mama.. anti mage anakufaa amelala chini maputo yake yote yanaisha hewa, baba anayajaza uku anti anapiga kelele fulani.''

Ndoa...

Vijana wa makamo wawili walikuwa wakiongelea maisha yao kama ifuatavyo:

Wa kwanza, ''nataka nioe nimechoka kuiona nyumba vululu vululu, vyombo vichafu na nguo chafu za kuvaa''

Wa pili, ''naitafuta talaka kwa sababu hizo hizo ulizotaja.''

Mwanakijiji mmoja...

Mwanakijiji mmoja alikuja Dar es Salaam, na aliporudi kijijini kwao ili asionekane mshamba akawa anawasimulia wenzake kwa confidence kubwa tu.
"Dah Dar nime-enjoy sana, nilienda hoteli moja inaitwa Sheratoni nikala vyakula tofauti tofauti nakumbuka kimoja kinaitwa wireless dah achaaa!!"

Matembezini

Vijana wawili walikuwa wanatembea mmoja akamwambia mwenzake hivi baada ya kumuona mbwa anajukuna "golori zake mbili"
Josh: Aisee i wish nami ningefanya vile.."
Ima: Wee! huyo mbwa atakung'ata akikusikia"

Mpenzi na mpenziwe

Siku moja dada mmoja alimuandikia meseji mpenzi wake, na maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Dada: Honey unafanya nini?
Kaka: Nasoma meseji yako.
Dada: Anha nha! Mi nauliza unafanya nini now?
Kaka: Nasoma meseji yako ingine.
Dada: Jamaani, niini lakini? Mi nauliza unafanya nini?
Kaka: Haya, najibu meseji yako.
Dada: Mhh! Umeshinda.

Kipindi redioni

Jamaa mmoja alikuwa katika maongezi na mwenzake:
Jamaa: Hivi we mwenzangu unapendelea haswaa kipindi gani redioni?
Rafiki: Aisee mimi mpenzi sana wa kipindi cha matangazo ya vifo.

Tuesday, June 22, 2010

WorldCUP

Jamaa mmoja alienda kwa jirani yake kuangalia mechi za world cup. Alipofika jamaa ikawa hivi:

Jamaa: Yakhee! Mzimaa?
Jirani: Mzima yakhee!
Jamaa: Nimekuja cheki mechi ya Nusu fainali bwana za world cup.
Jirani: Duh! Zishafika nusu fainali!?
Me tv yangu si unajua ya mchinaa... Leo ndo kwanza inaonyesha ufunguzi wa world cup.

Soma hii

Jamaa walipata msiba wakaenda kununua jeneza. Baada ya kununua ama kuuziwa yule mchonga majeneza akawaambia ''karibuni tena''

Makaburini

Mwanamke mmoja alienda kudhuru kaburi la mumewe, wakati anatoa sala nk nk majani yalianza kugusa gusa sketi aliyovaa kulingana na upepo ukiovuma eneo lile, yule mwanamke akanena: "taratibu mpenzi wangu we umeshakufa bwana."

Fundi bomba

Mtoto mmoja alikutana na ka_rafiki kake na kuambiwa na huyo rafiki yake "unajua watu wazima wana siri wote?" kale katoto kakajibu "kweli?"
Mwenzake akamwambia nenda kajaribu kama watu watatu kesho uje na jibu...

Mtoto alipofika kwao akamfuata mama yake na kumuambia "najua ukweli wote" mama akatoa elfu tano akampa na kumuambia "usimuambie baba yako"

Mtoto aliporudi baba yake akamfuata na kumuambia "najua ukweli wote" baba akatoa elfu kumi akampa na kumuambia "usimuambie mama yako."

Asubuhi mtoto akamfuata fundi bomba na kumuambia "najua ukweli wote" yule fundi bomba akasimama na kumuambia "oooh, vizuri. Njoo umkumbatie baba yako mzazi"

Hoi

Cha pombe mmoja alishinda karibu usiku mzima, aliporudi nyumbani kesho yake asubuhi wakati bado ameutwanga usingizi mkewe aliamka na kuanza kubwata"...muone kwanza umeenda kulewa tena..."

Jamaa akauliza "umejuaje sasa kama nimelewa jana?" mkewe kwa sauti ya hasira akamjibu "mhudumu wa bar amanipigia simu amesema umeacha wheelchair bar tena."

Walevi wawili...

Wawili wawili walilewa chakari, wakawa wanabishana kuhusu mwezi wanaouona juu.
Mmoja akawa anasema ni wa kijani na mwingine anasema ni mwekundu. Wakaamua kwenda kumuuliza polisi mmoja aliekuwa doria, "eti askari sie tunabishana ule mwezi juu ni wa kijani au mwekundu?" Yule askari akaangalia juu na kuwauliza baada "upo sasa wa kushoto au kulia?"

Monday, June 21, 2010

Tv set

Jamaa mmoja alienda duka moja na ikawa hivi:

Jamaa: Nahitaji nunua hii TV.
Dukani: Hapana siwezi kukuuzia.

Jamaa akatimua na siku ya pili akabadili aina ya mavazi, akajibiwa vile vile.

Mara ya tatu akaenda ikawa hivi:

Jamaa: Nahitaji nunua hii TV.
Dukani: Siwezi kukuuzia.
Jamaa: Kwani shida ipo wapi?
Dukani: We si ndo yule yule uliekuja mara ya tatu sasa?

Jamaa akauliza: Umejuaje wakati una wateja wengi?
Dukani: Kwasababu hii ni Microwave na si TV.

Maneno matamu.

Siku moja mtoto alikuwa na glasi ya maji ameishikilia tu, mama yake akatokea na kumuuliza ''Josh mbona hunywi maji hayo?''

Mtoto akajibu ''mbona mama sikuoni?''
Mama akauliza ''wapi mwanangu?''

Mtoto akajibu ''baba si anakuambiaga akinywa maji anakuona kwenye glass?''

Usiku na mtoto

Mtoto mmoja usiku aliamka na kujiona mpweke akaamua aende chumbani kwa mama ake.

Akamkuta mama yake kasimama mbele ya kioo uku akisema ''nataka mwanaume*3"

Usiku wa pili dogo akakuta yale yale.
Usiku wa tatu akamkuta mama ake na mwanaume.

Usiku wa nne akasimama na yeye mbele ya kioo na kusema ''nataka baiskeli*"

Hausi boi

House boy mmoja alimwandikia house girl wa nyumba ya jirani barua ya mapenzi na moja ya mistari aliyoandika ni hivi ''nakupenda kama nnavyoupenda mwisho wa mwezi.''

Mama nanihii

Siku moja mama nanihi... Alisikika akimuambia mwanae kwa ukali ''wee mwana kesho ukanyoe nywele hizo unaongoza humu ndani kumaliza sabuni''

Mtoto jeuri nae akauliza ''zipi sasa?''

Bafuni...

Fundi mmoja baada ya ujenzi wa nyumba moja, jioni wakati anaoga kwenye bafu mlango gunia alidondosha sabuni.

Sasa wakati anaitafuta alikuwa amefumba macho, ameitafuta huku akiogopa kufumbua macho sabuni isimuwashe machoni huku upepo ukipuliza mkali kidogo, alijikuta yupo nje ya bafu watu wakimshangaa...

Kumbe gunia mlangoni lilim-time na ule upepo.

Umeanza lini...

Marafiki wawili walikuwa wanaongea. Wakati wanaongea mmoja akamuuliza mwenzake baada ya kuona kitu...

''toka lini uweanza kuvaa hiyo pea ya stockings na suspenders? (stocking ni ile kama skin tight toka miguuni mpk kiunoni-tight pichu).

Mwenzake akajibu ''tangu mke wangu alipoifuma pae moja kwenye siti ya nyuma.''

*cheka unenepe*

Kufukuzwa na polisi

Kibaka mmoja alikuwa anafukuzwa na polisi gizani vichochoroni. Ngoma ikawa hivi, kila akigeuka nyuma polisi wapo nae. Akaona eeh! Isiwe shida.

Akafika sehemu akainama akaitanua fensi ya nyaya mbili (yaani kaishika kwa mikono mmoja katanua kwenda juu na wa pili kwenda chini) halafu akapenya mguu mmoja baada ya mwingine.

Kisha akairudishia ile fensi kama alivyoitanua kiasha akaanza mbio tena (hiyo ni kitendo cha sekunde chache mno)

Wale polisi waliiona picha yote walipofika pale eneo la tukio wakapunguza mwendo huku wakipapasa gizani labda wataigusa hiyo fensi isijewajeruhi kumbe hapakuwa na fensi wala nini...

Dokta na mgonjwa wake.

Mzee mmoja baada ya kupata matibabu maongezi yao na dokta yakawa hivi:

Mgonjwa: Nashukuru sana dokta.
Dokta: Usijali.
Mgonjwa: Nilitaka nikupe hela, lakini badala yake nimekujumlisha kwenye barua ya urithi.
Dokta: Oh! Kiko wapi kile cheti kuna kitu nataka badilisha...?

penda wadogo zao

Mzungu mmoja alitembelea mkoa fulani na akaona watoto wengi wengi tu wamebeba watoto akasema, "Huku watoto wengi wanapenda sana wadogo zao..."
Mwenyeji wake akamjibu "hao sio wadogo zao ni watoto wao"
Mzungu "ooh!!!!!"

Kumbukumbu

Kijana mmoja alienda kwa daktari kumuelezea tatizo alilonalo:
Kijana: Dokta nimekuja nina tatizo la kusahau sana.
Dokta: Ndio karibu, Lini mara ya uligundua una hili tatizo?
Kijana: Tatizo gani?

Toto tundu...

Mtoto mmoja alimuona baba yake akianza mambo ya ukubwa kwa mama yake, ghafla akatokea mtoto wao na kuuliza "baba unafanya nini?" Baba akajibu "Najaza tanki la mama yako."

Mtoto akaendelea kuongea "ujaze vizuri kwa sababu fundi cherahani leo asubuhi amejaza haraka haraka"

Jogoo

Mchungaji mmoja alipoteza wakati anamtafuta jogoo alietoweka katika mazingira ya kutatanisha. Wakati wa ibada ilimbidi atumie mwanya wake kuuliza kama kuna aliemuona.
"nani ana jogoo?" wanaume wote kanisani wakasimama akiwepo mzee wa miaka 87. A

kaona amekosea kuuliza, akauliza tena "nani ameona jogoo" wanawake/wasichana wote wakasimama akiwemo mwanae wa miaka 13. Ikabidi asema "ooh no no simaanishi hivyo..."

Ikabidi aulize tena "nani ameona jogoo wangu wiki mbili zilizopita?" Wahudumu/wanachama wa kike wa kanisa wote wakasimama.

Sura mbaya

Jamaa mmoja mwenye sura mbaya alienda kuwapa kazi (dei waka) vijana fulani wachimbe bwawa, siku kadhaa mbele akatembelea kwa ukaguzi wa bwawa hilo. Alipofika akauliza "myaani mmeanza kufuga na viboko humu?" kumbe ni taswira ya sura yake kwenye maji ya bwawani.

Juu ya mti

Kuna mtoto alipanda juu ya mti hakuvaa chupi, padre wa kizungu akamkuta akamuita halafu akampa yule mtoto elfu tano. Mtoto aliporudi nyumbani akaenda msimulia mama yake. Kesho yake mama yake nae akapanda juu ya mti na yeye bila chupi, padre akamkuta akampa shilingi mia mbili na kumuambia "kanunue wembe"

Sunday, June 20, 2010

Bwenini...

Mwalimu wa zamu siku moja aliingia bwenini majira ya saa nne, akakuta taa imezimwa na wanafunzi wapo vitandani.

Mwalimu akauliza kwa sauti ''wangapi wamelala humu ndani?''

Wanafunzi kadhaa wakanyoosha vidole. Mwalimu akauliza ''walio lala wananyoosha vidole?''

Za ofisini...

Siku moja mume alirudi nyumbani:

Mume: Mke wangu nimepata sekretari mpya, imagine eti ana bra nyeupe na nyekundu. Unajua hizi ni rangi za timu yangu. Sio ishu lakini.

Siku ilofuata mume aliporudi, ''mke wangu si bra tu pia na 'pichu' .
Sio ishu lakini.

Siku ya tatu aliporudi akamuuliza mkewe ''mke wangu za kazi?''

Mke akajibu, ''oh, nimepata boss mpya, @&*€ yake imezidi inch mbili ya kwako.
Sio ishu lakini.

Mtoto na babu

Mtoto akimuuliza babu yake.
Mtoto: Babu enzi zenu hakukuwa na matatizo na magonjwa mengi enh?
Babu: Ndio mjukuu wangu.
Mtoto: Na mlikuwa mnatumia nini kwa safe sex?
Babu: Oh! Tulikitumia pete ya ndoa.

Potea njia...

Jamaa mmoja alikua anaendesha gari ghafla akahisi amepotea.

Akapaki pembeni kwenda kuuliza. Akafika kugonga mlango, akafukua bibi na kumsalia kisha akauliza ''kuelekea michiga ni wapi?''

Bibi akajibu: Sifahamu kwa kweli.

Basi jamaa akakubali matokeo na kuondoka. Kidogo kabla hajafika mbali akasikia sauti kabla hajafika mbali, akachungulia kwenye kioo akamuona yule bibi akijaribu onyesha ishara jamaa arudi.

Jamaa akageuza gari mpaka pale bibi akamwambia kijana ''huyu hapa ni mume wangu, na yeye hajui pia.''

Tofauti ya umri.

Kuna tofauti gani ya wasichana kwa umri wa miaka 8, 18, 28, 38, 48, 58 na 68?

8 - unampeleka kitandani na kumpa stori.
18 - Unampa stori ndio unampeleka kitandani.
28 - Huna haja ya kumpa stori, mpeleke kitandani.
38 - Atakupa stori na kukupeleka kitandani.
48 - Unampa stori kuepuka kwenda kitandani.
58 - Unakaa nae kitandani kuepuka stori.
68 - Ukienda nae kitandani hiyo itakuwa stori.

Mtoto akitoa habari

Mtoto mmoja akimuita baba yake kwa sauti ''baba.. baba.. Njoo haraka, njoo baba... Mama amegongwa na pikipiki huku...''

Baba akajibu ''yupi?''

Duh! Mke huyu...

Mume wakati anarudi kwake ghafta akasikia sauti mkewe ikipiga kelele. Kuingia ndani anamkuta mkewe sebuleni uchi wa mnyama akamuuliza 'nini tatizo?'

Mke akajibu 'heart attack...' Uku kelele akipiga.

Mume akaenda kunyakua simu ampigie dokta, ghafla mwanae akaja na kumuambia 'baba... baba... njoo kuna mwanaume kwenye kabati la nguo uchii.''

Jamaa kufika si anamkuta rafiki yake na kumuambia kwa sauti ''Deo! ...mke wangu amepata heart attack, anawatisha watoto we unajificha?''

Wivu wa mapacha

Mapacha wawili wadogo walikuwa wanaoneana sana wivu kwenye maziwa ya mama yao.

Siku moja pacha mmoja akaja na kupaka sumu chuchu moja.

Kufika asubuhi baba kafa.

Maziwa ya mama

Wanafunzi darasani waliulizwa swali na mwalimu wao ''nini faida nne za maziwa ya mama?''

Mwanafunzi mmoja wa kiume akanyoosha kidole na kujibu.
1. Huna haja ya kuyachemsha.
2. Nyau hawezi yaiba.
3. Yanapatikana anytime
4. (huku akifikiria mwanafunzi) ...ya nne ...ya nnee... Eenh 'yanapatikana kwenye kontena zinazovutia.'

Mke wa mtu

Mwanamke mmoja aliingiza mume mwenza kwake, wakati wapo chumbani wakasikia mlango umefunguliwa na kufunga.

Mke: Mume wangu huyo karudi.
Mume jizi: Wapi upo mlango wa nyuma?
Mke: Hatuna.
Mume jizi: Wapi unataka uwepo mlango wa nyuma?

Kipofu kuopoa

Kipofu mmoja aliopoa binti mrembo na kwenda nae hotelini, walipofika ndani wakati binti ana mpa jamaa mabusu moto moto kipofu akauliza.

Kipofu: Samahani...
Bintii: Bila samahani.
Kipofu: Wewe sio Jesca, wa cBe dodoma?
Binti: Ni mimi ndio, umejuaje?
Kipofu: Huwa sisahau sura.

Wapi upo?

Mama mmoja alikaa nyumbani akaboreka, akanyakua simu ili ampigie mumewe ajue yupo wapi akajumuike nae.

Mke: Halow mume wangu kipenzi?
Mume: Halow honey.
Mke: Upo wapi nije? Nyumbani panaboa.

Mume: Nipo Zanzi bar.
Mke: Enhee...!!? Yaani usafiri mpaka zanzibar, bila kuaga, unantafuta wewe.... (aliwaka kwenye simu mwanamke)

Mume akamkatisha, ''mke wa-a-ngu, kuna bar inaitwa NZANZI...''

Honi ya gari

Baba akimpeleka mwanae shule ghafla akapiga honi bahati mbaya. Mwanae akamgeukia na kumuangalia, baba akasema,

Baba: Sijapiga honi makusudi, ni bahati mbaya tu.

Mtoto: Najua dady!
Baba: ...!! Umejuaje?
Mtoto: Kwa sababu hujatukana baada ya kupiga...

Hii kali hahaha

''Je, baba wa mtoto ataruhusiwa kuja kushuhudia mkewe akijifungua?'' aliuliza mmoja wa manesi.

Mama mjamzito akadakia na kujibu, "hapana,si yeye wala mume wangu kuja.''

Migration

Mkorea mmoja wakati yupo migration anakaguliwa passport yake na mkewe aliuulizwa 'sex?' maana alikuwa haeleweki kama ni mwanaume au mwanamke, jamaa akajibu (mkoreha) ''twice a week''

Ndipo afisa akamwambia hatumaanishi huko unakodhania....

Maongezi kijiweni.

Jamaa mmoja akitwanga stori na wenzake kuhusu nini cha kumfanya mwanaume utaemfumania na mkeo. Hali ilipendeza kwa staili hii:

Kijana 1: Me namfumua fumua nywele hata kama hajasuka.

Kijana wa 2: Aisee, me ntamkata na ulimi kabisa.

Kijana 3: Haa! Mimi? Mi aise nam-logaa akisimama tu na mwanamke yeyote tu ana-jamba jamba.

Jamaa akipa moyo

Mkaka mmoja alimfumania mkewe na njemba ingine. Sasa rafiki yake akawa anampooza hasira.

Rafiki: Ndugu yangu usijali sana, hii imetokea sio ndio mwisho wa dunia. Sahau yaliyopita.

Mwenye mke: We unasema tu jamaa angu. Ingekuwa ndio wewe umemkuta mtu ana... mkeo wa ndo ungefanyaje?

Rafiki: Mhh! Ningemvunja shingo mara tatu na kutoboa macho.

Penseli

Mtoto: Mmoja akimsimulia mama yake:
Mtoto: Basi maama si akaja yule rafiki angu.
Mama: Enhee mwanangu halafu?
Mtoto: Akawa analalamika penseli yake imepotea.
Mama: Sasa ukafanyaje mwanangu?
Mtoto: Mi nkamuonea huruma, nkampa ile penseli ya chumbani kwako ya pinki pinki hivi...
Mama: Weee....!!! Ule ni wanja wangu....

Wezi na mkakati

Jamaa wakati anapita sehemu kichochoroni akasikia maongezi ya vibaka wakipanga mikakati yao:
Kibaka wa kwanza: Sasa leo nyumba ngapi?
Kibaka wa pili: leo nne hivi sio mbaya, hatuna njaa sana.
Kibaka wa tatu: Leo nipo nanyi bega kwa bega.

Kibaka wa kwanza akamgeukia kibaka wa tatu na kumuambia: "we leo huendi popot''

Kibaka wa tatu akauliza "kwa nini nsiende nanyie?''
Kibaka wa kwanza akajibu ''una kikohozi''

Kwenye dala dala

Dala dala moja la mbagala lilijaa mpaka mlangoni. Kijana mmoja akajitolea kukusanya nauli, alietoa elfu 10 haya, alietoa elfu 5 haya huku akiwaambia subiri ntakupa chenji. Mwisho wa siku konda mhusika alipoanza kukusanya nauli watu wakamuambia tumeshampa mwenzako na chenji tunamdai. Kumtafuta kwenye basi jamaa kalala mbele zamaani...

Changudoa

Jamaa mmoja alishalewa pombe za kienyeji, akanyanyuka kwenza kuimbisha changudoa mmojawapo kati ya waliopo sokoni siku hiyo. Si mbali na alipo hali ikawa hivi:

Mlevi: Haya leo bei gani?
Changu: Elfu tano tu mzee wangu.
Mlevi: Mbona Bei mbaya hivi na VAT umo umo?
Changu: Hapana ila biashara ngumu tu.

Mlevi: Si ufungue branch lingine pia? Vipi discount?
Changu: Discount mpaka xmas mzee wangu.
Mlevi: Saa hizi saa ngapi?
Changu: Saa tatu usiku.

Mlevi: Ndio maana bei ipo juu, basi ntakuja tena saa sita usiku...

Kuopoa

Jamaa mmoja alienda club kujirusha, baada ya masaa kadhaa na pombe tena kama unavyojua...
Si akaopoa mrembo wa kwenda kujivinjari nae. Ndani ya club wakakubaliana vyeema kabisa walipofika nje jamaa akamuuliza yule dada ''samahani kidogo hivi ndio wewe tulieongea ndani?'' yule dada akajibu ''ndio.''

Yule jamaa akashindwa kuvumilia akamuambia ''mbona umezeeka ghafla?''
Yote hiyo kumbe taa za disco zilimrembesha yule dada.

Saturday, June 19, 2010

Kofia...

Kulikuwa na mama mtu mzima kidogo akipita maeneo fulani, ghafla upepo mkali ukapita.
Papo hapo akapita kaka na kumuambia yule mama,

'mama unathubutu kuachia gauni lapeperuka na upepo unashikilia kofia.

'mama akajibu huko kila kitu uko chini kuna umri wa miaka 70, hii kofia brand new''

Kiziwi

Mzee mmoja tariji tajiri kidogo alikuwa na tatizo la kusikia. Siku moja alienda kwa daktari wake baada ya miezi miwili na daktari akatambua tatizo alokuwa limeisha akamwambia.

Dokta: ''familia yako itakuwa imefurahi sana kuona unasikia tena''

Mzee akajibu,"oh, sijawaambia bado, bado nasikiliza maongezi yao. Nimebadilisha urithi mara tatu.''

Taa za ndege

Mama mmoja alikwea pipa(ndege) kwa mara ya kwanza kwenda majuu.

Kama unavyojua tena tule tutaa twa ndege tunavyowaka waka.

Basi ndege ilipaa usiku na huko angani akichokiona ni ile taa tu ikiwaka waka. Hakuelewa somo akamuita muhudumu wa kwenye ndege na kumuambia ''samahani kamwambie pilot amesahau kuzima taa ya indiketa ya kushoto inawaka mda mrefu sasa?''

!!

Wadada wawili wakipiga stories mmoja akamuuliza mwenzake. ''nasikia umeolewa tena?''

Dada akajibu "oh yes, ndoa ya kwanza na milionea, ndoa ya pili na mcheza sinema, na ndoa ya tatu mchungaji, na sasa nimeolewa na mwendesha kibaka.''

''Unamaanisha nini?'' yule dada wa kwanza aliuliza.

Akajibu, ya kwanza kuchuna pesa, ya pili kuuza sura, ya tatu kupunguza dhambi na ya nne kujifunza kupiga sachi (kuiba)?''

Pombe bwana...

Jamaa usiku mmoja aliamka kwenda kukojoa huku akiwa bado pombe, aliporudi chumbani akamwambia mke wake wa ndoa, ''mke wangu bafuni umefanya nini?''

Mke akauliza: Mh! Kwani vipi mume wangu?

Mume: Nimeshangaa ukifungua mlango taa inawaka ukifunga inazima.''

Mke akadakia ''shenzi we umekojoa kwenye friji.

Mtoto na maneno

Mtoto mmoja alimfuata mama yake na kumnong'oneza.
''mama... nimeiona shati la baba limechorwa alama nyekundu ya x, sijui ndio bomoa bomoa inakuja?''

Usingizi...

Dada mmoja Sara alikuwa anasinzia mno popote, darasani, kanisani...

Siku moja alikaa karibu na kaka mmoja.
Mwalimu akauliza swali ''nani ameiumba Dunia?''

Yule kaka akamchoka ka-sindano Sara mguuni akashtuka toka usingizini na kusema ''Oh GOD''

Mwalimu akadaki ''vizuri sana Sara''
haya swali lingine ''God ni nani?'' Mwalimu aliuliza.

Jamaa akamchoma tena sindano mguuni Sara akashtuka na kusema ''JESUS...''

ATM

Kuna jamaa mmoja alilewa chakari, sasa ikawa anataka kwenda atm kujazia mfuko. Alipofika atm si akachomeka kati ya kupigia kura....

*cheka unenepe*

Mwalimu mbele ya wanafunzi

Mwalimu wakati anaandika darasani ghafla akaingia mwanae wa miaka mitano (kwa vile hakai mbali na eneo la shule), kale katoto kalipongia kwa sauti kakasema ''maama... maama... nimemuona baba anamvalisha blauzi chumbani dada wa kazi.''

Tobaa vichaa...

Dokta aliwajaribu wagonjwa wa akili watatu.

Dokta: Haya mchague nani anyongwe mpaka kufa?, nani apigwe risasi ya kichwa? Nani achomwe sindano yenye damu yenye virusi?

Kichaa wa kwanza na wa pili wakachagua namba moja na mbili.
Huyu wa tatu akajichagulia kuchomwa sindano: ''hehe bora unichome sindano yenye virusi vya ukimwi maana nshavaa condom.

From: Sunbella Kyando.
Thanks.

Barafu

Kaka mmoja alienda kuomba maji ya kunywa kwa jirani.

Kaka: Habari?
Jirani: Nzuri tu karibu.
Kaka: Asante. Nilikuwa naomba maji ya kunywa.
Jirani: Hamna shida, lakini ya kawaida sina friji.
Jamaa: Haina shida nlishameza barafu asubuhi itapooza tumboni.
Jirani: ....!!

Mtoto na swali...

Siku moja mtoto alimuliza baba yake:

Mtoto: Mimi mlinipata wapi?
Baba: Mh! Ngumu kuelezea... Nilikununua super market.
Mtoto: Na kaka yangu je?
Baba: Na yeye pia supermarket.
Mtoto: Na dada je?
Baba: Na yeye pia.

Mtoto akabaki kwenye mshangao akamuuliza baba yake tena.

Mtoto: Kwani wewe hufanyagi mapenzi?

Duka la dawa...

Kijana mmoja alienda pharmacy kununua condom. Alipofika akauulizwa wataka za aina gani?

Jamaa akajibu, za long weekend maana kuna mrembo mzuri kweli, afta mlo wa mchana kwao na wazazi wake twaenda holiday kula maisha.

Mchana kwa wazazi wa binti, jamaa akapewa nafasi kuombea chakula. Alipomaliza msichana akamnong'oneza ''hujawahi niambia kuwa ni mtu wa dini mzuri''

Jamaa nae akamnong'oneza, ''hujawahi niambia kuwa baba yako anauza pharmacy''

*cheka unenepe*

Kwenye jokofu

Mtoto mmoja aliulizwa na mama yake, ''mdogo wako yupo wapi?''

Mtoto: Amelia sana, mempa maziwa hataki, mkate hataki...
Mama: Sasa yupo wapi?

Mtoto: Nimemfungia kwenye friji achague mwenyewe anachotaka kula...

Size nayo mh...

Jamaa mmoja kwasababu ya woga wake wa size aliyonayo. Aliamua kwenda gizani na msichana wake ndipo akamshikisha, yule msichana akajibu ''asante kwa ofa, situmii sigara''

Friday, June 18, 2010

Baba mtata

Mwanaume mmoja alipiga simu kitengo cha dharura:
''...tafadhali njoo haraka mwanangu kameza kondom!''
Baada ya dakika 5, akapiga tena simu kule kule... ''basi msije nimepata ingine''

Mshahara wa kwanza

Boss alipomuajiri driver mpya:
Boss: Nakuajiri wewe kama dereva mshahara wa kuanzia ni elfu sabini.

Dereva: Asante sana boss, mshahara wa kuanzia upo sawa... lakini na wa kuendesha gari shiling ngapi...?

Mchungaji

Trafiki alimkamata mchungaji mmoja aliekuwa amelewa.

Mchungaji: Nini shida ofisa?
Trafiki: Umelewa?
Mchungaji: Hapana, mimi ni mchungaji wajua?
Trafiki: Na humo kwenye chupa kuna nini?
Mchungaji: Maji ya baraka.
Trafiki: Hebu ninuse.
Akanusa na kujibu,

Trafiki: Sio maji ya baraka ni pombe mchungaji.
Mchungaji: Oh! Miujiiza!!!

Simu kwa dokta

Baba mmoja alimpigia simu daktari wake ili apate msaada wa haraka (huduma ya kwanza).

Mzee: Dokta mwanangu amemeza penseli yangu nifanyeje...
Dokta: Pole sana tumia peni.

Njo... Njo...

Watoto wawili wakati wanamuelekeza baba yao nyumbani wakati anarudi nyuma nyuma ili hivi:

Watoto: Njo... Njo... Njo... Njoo... Mpaka gari ikagonga taa ikavunjika. Wale watoto wakasema ''hapo hapoo!''

Haraka haraka...

Jamaa mmoja alikuwa anaongea na mwenzake, kidogo simu ikaita. Alipopokea aliempigia alikuwa anaongea spidi sana akamuuliza ''khaa! Mwenzangu mbona unaongea haraka sana?''

Jamaa kwenye simu akazidi mwendo ule ule. Ikabidi amuambie ''ndugu yangu una haraka kama una-oga nje?''

Lift kwa jirani

Jirani mmoja alipewa lift, sasa wakati wa kuingia barabara kubwa mmiliki wa gari alikua haoni vizuri akamuuliza yule jirani ''kwako kuna gari?'' jirani akajibu hamna.

Ile kuingia barabara kubwa wakapaja ajali. Mwenye gari akamuuliza ''we si nlikuuliza kwako kuna gari....?''
Jamaa akajibu: Mi nlidhani nyumbani kwangu.

Restaurant

Mu-italiano mmoja aliingia Sheraton Hotel na hivi ndivo ikawa:

Mu-italy: Waiter, what is this?
Mhudumu: It's bean soup.
Mu-italiano: I'm not asking what it's been, i'm asking what it is!?

Msala...

Jamaa alimfuata rafiki yake ili amsaidia kujibu kesi inayomuandama kati yake na mkewe.

Ali: Ima nikikupa laki moja utanisaidia kujibu maswali mawili kwa mke wangu kieleweke?
Ima: Ndio haina shida. Swali la pili linasemaje?

Lahaulaa...

Haya hii nyingine...
Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi alimfuata mwalimu wake wa tuition na kumuuliza:

Mwanafunzi: Unaweza niadhibu kama sijafanya lolote?
Mwalimu: Hapana.
Mwanafunzi: Vizuri, kwasababu sijafanya homework.

Kitoto hiki...

Mtoto mmoja alikua amekaa akijiongelesha ongelesha na wazazi wake... ''mom and dad..." wazazi wake wakaitikia ''yes dear''

Katoto kakaendelea, ''i like school very much, especial when it's closed''

Darasa la kingereza

Mwalimu wa english aliwataka wanafunzi wake watamke sentensi ifuatayo ya kizungu iwe katika 'simple present'

Mwalimu: Any one can put the verb ''to walk'' in simple present?

Mwanafunzi mmoja akajitokeza: I walk. You walk...

Mwalimu akamkatisha na kumuambia: Quicker please.

Mwanafunzi: I run. You run...

Bi. Mkubwa

Bi. Mkubwa mmoja alikuwa hajamuona mjukuu wake siku nyingi... Siku alipomuona:

Bi. Mkubwa: ...marhaba mjukuu wangu. Sijakuona siku nyingi sana.
Mjukuu: Nipo tu bibi angu.
Bi. Mkubwa: Unafanyia wapi kazi siku hizi?
Mjukuu: Akaitaja kampuni.
Bi. Mkubwa: Ndio wanashughulika na nini hiyo kampuni?
Mjukuu: Kutengeneza vifanyio?
Bi. Mkubwa: Vifanyio...!? Vifanyio...?? Vifanyio..? Mh! Ndio nini mjukuu wangu?
Binamu akadakia: Bibi vifanyio si condom...

Barua kwa baba

Mtoto wa kwanza akimuandikia barua baba yake kumtaharifu kuwa kapata msichana wa kuoa.

Dear baba,

Nimebahatika kupata msichana tuliependana na kushibana, kwa ufafanuzi zaidi ni mrefu, ana pua, macho mawili, masikio mawili, kope pia anazo...

Samaki wawili

Samaki wawili kwenye tanki dogo la kufugia wakiongea mmoja akimwambia mwenzake.

"my dia friend wiki ijayo mi naondoka kwenye hili tanki, ila ntaondoka na haya maji yote we ntakuachia tanki''

Mvuvi

Mvuvi mmoja alikuwa anavua na ndoano yake huku amekaa kisehemu cha juu... Huku anawaza *hawa samaki leo wamefunga nini?*

Kidogo anatokea mamba na kumuuliza yule mtu ''unahitaji kitoweo?'' jamaa akajibu 'ndio.'

Mamba akamwambia ''sasa kwa nini usije kuogelea?''

Hela

Mtoto mmoja alichelewa kurudi nyumbani toka shuleni, mama yake akamuuliza ''mbona umechelewa sana leo kurudi?''

Mtoto akajibu ''kuna mtu alidondosha hela yake''
Mama akauliza ''sasa wewe inakuhusu nini yeye kuidondosha?''

Mtoto: ''nilikuwa nimeikanyagia mpaka alipoondoka nkaikota''

Wanaume watatu

Wanaume watatu walipokufa uko peponi hali ikawa hivi:

Wa 1: Ambae hakutembea nje ya ndoa alipewa private jet.
Wa 2: Alitembea mara 1 tu akapewa sports car.
Wa 3: Alitembea mara nyingi akapewa mkweche (gari).

Wa 1 na Wa 2 wakamwambia usijali tutakupa vyetu uendeshe.

Wa 3 akajibu hiyo sio shida, mke wangu kafa nae yumo humu humu yeye kapewa baiskel...

Ushabiki kombe la dunia...

Jamaa mmoja alikuwa na tiketi mbili za kombe la dunia.

Alipofika uwanjani jamaa mwingine akaja na kuomba kukaa ile siti isiyo na mtu pembeni yake. Kisha maongezi yakaendelea.

Aliyetoa siti: Hii siti ilikuwa ya mke wangu, ila bahati mbaya amefariki.

Aliyepewa siti: Ooh, pole sana, sasa si ungempa ndugu yeyote akaja kuangalia mpira badala yake?

Aliyetoa siti: Wote wameenda kwenye mazishi...

Kibendi

Mama mmoja alipogundua kwa dada wa kazi za ndani ni mjamzito alienda kumtaharifu mumewe:

Mke: Mume wangu, huyu house girl ana uja uzito. Na alikuwa hatoki kabisa kabisa humu ndani:

Mume akajibu, ''kwani mimba inatafutwa siku nzima?''

Puto

Mtoto mmoja alienda dukani kununua mapambo kwa ajili ya b'day yake:
Dukani: Karibu mtoto mzuri, nikusaidie nini?
Mtoto: Mekuja nunua maputo ya besdei yangu.
Dukani: Ooh! Yameisha kabiisa.
Mtoto: Hata kama yale anayonunuaga baba?
(akimaanisha condom)

Thursday, June 17, 2010

Khaa!

Baba mmoja rafiki ake walienda hospitali kumuangalia mtoto wake mdogo. Akachukua miwani yake mpya ya macho akaivaa (sijui amuone vizuri mtoto? Huku nesi yu pembeni pia) na kumuangalia na kumuongelesha chwi... chwi... chwi... Huku akiongea angalia angalia anatabasabu.

Rafiki yake akamjibu ''mwanao hajatabasamu lakini.''
Baba: Nazumngumzia nesi...!

Jino lipi?

Mzee mmoja alisindikizwa na mkewe kung'oa jino. Alipofika akamuambia dokta
''dokta nna haraka sihitaji hata ganzi fanyafanya niwahi...''

Dokta akasema: Ningepata 6 kama wewe ingekuwa swafi sana. Haya jino lipi linasumbua...?

Yule mzee akamgeukia mkewa na kumuambia... ''darling muonyeshe''

Majibu mengine...

Dokta: Ndugu yangu nna habari mbaya na nzuri... Sijui nianze kukupa ipi?

Mgonjwa: Anza na mbaya.
Docta: Habari mbaya ni ndani ya miaka miwili utakuwa umekufa.
Mgonjwa: Eenh? Haya na hiyo habari nzuri je?
Docta: Una Alzheimer. Ndani ya miezi mitatu utasahau kila kitu nlichokuambia.

Boss...

Boss mmoja alimtuma msaidizi wake akamchukulie majibu ya vipimo vyake. Aliporudi ikawa hivi.

Msaidizi: Boss... Nna habari mbaya.
Boss: Wewe kila siku wanipa habari mbaya tuu, hebu nipe japo mara moja habari njema basi enh?
Msaidizi: Sawa bosi majibu yanaonyesha wewe ni tasa.

Kung'oa jino

Dada mmoja alienda kung'oa jino. Kazi ilikuwa tamu pale dokta alipomchoma ganzi. Yule dada akapeleka mkono wake na kumkamatia nyeti zake yule dokta.
Dokta akamwambia ''dada unatambua kuwa umenishikilia ikulu?''

Dada akajibu: Ndio natambua, nna imani hamna atakaemuumiza mwenzake...''

Kichaa balbu

Mgonjwa wa akili mmoja alikua amejining'iniza kichwa chini miguu juu kwenye dari. Dokta alipokuja akamuuliza mgonjwa mwenzake: ''anafanya nini mwenzako hapo juu?''

Kichaa akajibu: Eti anajifanya taa ya balbu.
Dokta: Kamsaidie kumtoa basi ataumia.
Kichaa: ''Haaa! Yaani nifanye hiyo kazi na giza?''

Wodi ya wagonjwa akili

Siku moja wagonjwa wa akili walichorewa kuku ukutani, wakaambiwa wakamkamate.

Woote kasoro mmoja tu ndio hakwenda. Ndipo walihisi huyu ndie mwenye nafuu, kilichofuata wakamuuliza kulikoni?

Yule mgonjwa wa akili akawajibu huku akinong'ona ''shhhh! Nat.a.a.ga''

*cheka unenepe*

Vichaa

Wagonjwa wa akili siku moja walipimwa akili kama wana mabadiliko. Wakapelekwa kwenye bwawa la kuogelea (swimmin pool) lisilo na tone la maji.

Wakaambiwa waingie waogelee, sita kati ya saba wakajitupia bwawani. Mmoja akabaki pembeni akiwaangalia wenzake. Madaktari wakamuuliza 'wewe mbona hujafanya kama wenzako?'

Akajibu ''sina boya la kuogelea''

Umri

Mtu na mkewe walikuwa chumbani, mke akamuuliza mumewe umri wake ''mume wangu kwa kuniangalia unahisi nna miaka mingapi sasa?''

Mume akajibu: Kwa kuangalia ngozi yako una miaka 20, nywele zako una 18, vidole mhh una 25.

Mke: Jamaaani...

Mume: Subiri kwanza bado sijaijumlisha yote.

cheka unenepe.

Malavi davi

Mke alipokuwa ameketi pembeni ya mumewe alimvua miwani yake ya macho na kumuambia ''ukiwa hujavaa miwani unakuwa yule handsome wangu alienioa''

Mwanaume nae akajibu ''bila miwani bado unaonaka huu mzuri na mrembo sana.''

Mke afta bia

Mlevi mmoja alipokuwa chakari kwa pombe alimuona mwanamke akamfuata, akaanza mshika kiuno, mara shavu... Yule mwanamke akafyumu... Jamaa akaomba msamaha 'samahani nilidhani ni mke wangu, umefanana nae'

Yule mwanamke akazidi kuwaka kama mbogo aliejeruhiwa ''msh**z wa tabia... Unavamia tu watu... &*@£''

Jamaa akadaki tena ''teena nae mkali kaama wewe ivo ivo''

Ulevi huu khaa

Mlevi mmoja alimuuza mkewe apate bia kadhaa. Alikuwa bar akaanza kulia mwenzake akamuuliza:
'vipi kulikoni?' jamaa alimuuliza.

Mlevi: Nimemuuza mke wanguu ili nipate bia.
Jamaa: Khaa! Sasa unamtaka tena?
Mlevi: Ndio.
Jamaa: Unampenda bado?
Mlevi: Hapana, nna kiu tena.

*cheka unenepe*

Mtoto...

Mtoto mmoja alikuwa amekaa na mama yake, kidogo akasikia honi ya gari ya baba ake ikipigwa. Kale katoto kakamgeukia mama yake na kumuambia ''mama boyfriend wako huyo amerudi''

Salamu njiani...

Dada mmoja akipita njiani, kidogo akakutana na kaka nae akipita njia.

Kaka: Dada habari yako?
Yule dada kimyaa.
Kaka akasilimia tena na tena yule dada kimya.
Mwishowe akamwambia ''dada salamu haitii mimba.''

*cheka unenepe*

Zuzu...

Jimmy akimueleza rafiki yake shida inayompa wakati mgumu. ''Ima mwenzako sijapata choo siku ya nne sasa inabidi niende hospitali kwa kweli.'' Ima ni kama alishikwa na mshangao hivi kisha akamjibu ''hujapata choo siku nne? Kwani kwenu kuna vyoo vingapi?''

Maongezi

Alfred alimkuta rafiki yake akiongea na dada mmoja.

Alfred: Habari yako Josh?
Josh: Njema tu karibu.
Alfred: Asante, dada habari yako?
Dada: Nzuri tu.
Alfred: Dada samahani kama nakufananisha.
Dada: Bila shaka, na nani?
Alfred: Na dada mmoja hivi anasoma cbe.
Dada: Aanha, ni mdogo wangu yule.
Alfred: Duh! Mdogo wako? Aisee mmefanana ka biscuti.
Dada wa watu Hoi kicheko.

Bar na wanywaji...

Wanywaji wawili walienda bar na kuagiza bia mbili. Zilipoletwa yule wa kwanza akasema ''muhudumu ngoja kwanza usiifungue'' akaichukua akaiangalia, akaigeuza geuza kisha akaiweka mezani.

Mwenzake akamuuliza, ''vipi unatafuta nini?''

Jamaa akamjibu ''we hujawasikia wachina?''

Kifo

Mtoto mmoja wa umri wa miaka mitano, siku moja alitoka shule na kukuta msiba kwao. Kalipofika kwa mama yake kakamuuliza mama ''mama mbona unalia?'' mama akamjibu ''baba yako amekufa mwanangu''

Kale katoto kakajibu ''sasa unalia nini?''
Mama akamshangaa mwanae na kumuuliza ''mwanangu why unasema hivyo?''

Mtoto akajibu ''me nilidhani dad ndo kakufa kumbe baba?''
Mtoto alizoea mwita baba yake dad siku zote.

Mke mbabe...

Siku moja njemba moja ilirudi nyumbani kwake, ghafla mlangoni akakutana na mwanaume anatoka chumbani kwake, hasira zilmpanda akataka amparamie, ghafla sauti ya mkewe chumbani ikasikika: ''baba ima huyo ukimgusa atakutoa ngeu, subiri dakika chache ataingia mwingine kimbau mbau mwenzako...''

Doli doli

Mama mmoja ili kumjenga mjukuu wake asifanyiwe ama kushikwa eneo nyeti na mtu yeyote mtoto aje kusema. Bibi uku akimuogesha alimwambia mjukuu wake ''toto zuri mtu yeyote asikushike doli doli yako enh! Umesikia enh?''

Mjukuu akashika neno.

Siku moja housegirl wakati anamuogesha uku akimsafisha na kumpaka sabuni mjukuu alichoropoka na sabuni yake mpaka kwa bibi yake, alipofika tu kwa bibi cha kwanza ni kusema ''biibi... biibi... dada amesha doli-doli yangu''

Walindeni watoto.

Bango

Watoto wawili walikaa sehemu wakiangalia mafundi wakiotengeneza bango kubwa la matangazo. Bahati mbaya lile bango lilitaka kuteleza, na chini yake mpita njia akipita. Ndipo mtoto mmoja akasema ''maskini lingemdondokea yule mtu akafa na asijue nini kimemuua.''

Mini-skirt

Mke: Mume wangu nnunulie mini-skirt...
Mume: Ili ukivaa nani akuone?
Mke: Si wewe mume wangu...

Siku mbili mbele mume akamnunulia. Mke akakijaribu na kutaka kwenda outing, alipofika mlangoni mume aka... ''eenhee!? Waapi na hiko ki-mini?

Mke: Si naenda kutembea mume wangu?
Mume: Hicho kimini ulisema ukivae akuone nani?
Mke: Si wewe mume wangu au?
Mume: Haya nimeshakuona, kakivue.

Maji jikoni

Mtoto mmoja alitumwa na mama yake akaangaliie maji aliyoyaacha jikoni kama tayari yamechemka.
Yule mtoto alipoenda na kukuta maji yanachemka akamuita mama yake kwa sauti ya kupaza ''mamaa... Mama.. Maji yanaungua hukuu!

Lazima ucheke

Mtoto wa kike Mwajuma alikuwa anapenda kucheza na wavulana wanapanda juu ya miti. Baba mwajuma akampiga mkwara mwajuma:Hao watoto wa kiume wanakuchungulia chupi ukipanda mti, acha mchezo huo mara moja. Mwajuma akajibu, nimewagundua, leo nimepanda bila chupi.

*cheka unenepe*

Wednesday, June 16, 2010

Tv

Mke: We mume wangu tangu kombe la dunia hutulii nyumbani.

Mume: Mke wangu hii tv ya nyumbani ya mchina itanidanganya...

*cheka unenepe*

Wallet part ii

Cha pombe mmoja alilewa na kuopoa changudoa. Mwisho wa siku akaja gundua baada ya yule changudoa kuondoka nae akagundua kumbe wallet yake pia imelambwa (kuibiwa).

Alipotoka nje ya ile guest house akamuuliza mlinzi ''aisee umeona wallet imepita hapa?''

*cheka unenepe*

Mchele

Wakati wanakula wali kwa maharage familia moja kwa bahati mbaya mmoja akatafuna jiwe/mchanga...
Mwenzake katika group hilo akasema ''halijaiva hilo....''

*cheka unenepe*

Chumvi

Baba mmoja alirudi nyumbani akakuta chakula tayari. Alioonja mboga akakuta chumvi nyingi akauliza ''nani mpishi wa leo?''

Wakajibu fulani...

Mtoto wake mmoja akauliza ''vipi kwani baba?''

Baba akajibu ''mpishi wa leo hajapiga mswaki, hata test ya chumvi haja....''

Mboga ya leo

Mtoto mmoja wakati wapo mezani wanakula alikuwa yupo kimya sana mpaka baba yake akamuuliza.

Baba: Jo mbona upo kimya sana leo?
Mtoto: Baba kwani siku hizi umefulia? (fedha)

Baba akabaki na mshangao swali limekujaje pale mezani?

Baba: Hapana mwanangu, kwa nini umeuliza?
Mtoto: Mbona ukiwa haupo tunakula nyama kila siku? Kuna anko anakujaga nyumbani.

Mama aliwepo mezani pia...

Wallet

Jamaa alienda kula msosi kwenye restaurant fulani, kasheshe ilikuja wakati wa kulipa alijisachi na kukuta kumbe wallet ameiacha kwenye suruali ingine.

Palikuwa hapatoshi, ilibidi aitwe meneja wa restaurant,

akashauri aache viatu ile kuvua tu harufu kali, restaurant akasema viatu 'NO.'

Ndipo aliposema (aliekula) ''naombeni basi niache simu''
meneja akauliza "sio ya mchina?''

*cheka unenepe*

Chips...

Kijana mmoja alienda nunua chips kavu. Muuza chips baadae kidogo akamuuliza ''niweke kila?'' jamaa akajibu 'ndio'

Chakula kilipoletwa jamaa akauliza 'we si uliniuliza uweke kila kitu? Mbona hamna mshkaki, kuku, soseji nk?''

Kumbe muuza chips alimaani tomato, chili, chumvi, chachandu.''

Pombe mtu.

Jamaa mmoja alikuwa mlevi kupitiliza, wenzake wanaekaa nae nyumba moja walijaribu kumuasa apunguze, hasa kutopitiliza na kulala nje (juu kwa juu)

Mlevi huyo siku moja alirudi nyumbani akiwa chakari saa 11 na nusu alfajiri na kuwaambia wenzake ''unaona mi silali nje kabisa, si hivi nimerudi.''

Unaikumbuka hii?

Famila moja ilikodi ndege kwenda vekesheni. Kwenye ndege watoto wakawa wanacheza na kelele, mama yao akafanya utaratibu.

Mumewe alipotoka msalani akauliza watoto wapo wapi? Mama akajibu 'wapo nje wanacheza humu ndani wanapiga kelele sana'

Watoto bafuni.

Watoto wawili wakioga bafuni wa kike na wa kiume:

Ka kike kalimungalia eneo nyeti mvulana na kumuuliza:

Wa kike: Naweku kuigusa hiyo?

Wa kiume: Hapana, we ya kwako umepoteza.

Moyo

Mwalimu darasani alifundisha watoto kuhusu moyo na kazi yake.

Baadae katoto kamoja kakauliza swali:

Katoto: Mwalimu 'moyo una miguu?'
Mwalimu: Hapana, kwa nini umeuliza hivyo?
Katoto: Jana usiku nlimsikia baba akisema 'sweet heart open your legs'

Kimemo

Jamaa aliagiza supu bar akaenda msalani, huku nyuma akaacha kikaratasi kimeandika ''nimetemea mate supu hii''

Aliporudi akakuta kikaratasi kingine kimeandikwa ''na mimi nimetemea mate''

From: Helena Sylvester

Kazi kwa muhindi...

Muhindi mmoja aliajiri wafanyakazi wawili Juma na Ali. Hivyo ili kulinda mali zake alimuita mmoja mmoja kwa wakati wake na kuwaambia...
''Juma linda Ali"
"Ali linda Juma"

Mwisho wa siku Juma na Ali walipofukuzwa kazi wakauliza ''mwenzangu vipi tumetoka bila kitu kulikoni?''

'mi nliambiwa nikulinde wewe'' Juma alisema.
'na mimi nliambiwa nikulinde wewe' Ali alisema.

Mswaki

Siku moja mwanafunzi mmoja katika hostel fulani walikuwa wanashea friji. Ikawa kila akiweka maji ya kunywa anakuta wamekunywa. Akabuni lake siku ingine akaweka maji yake kama kawaida yake na akatumbukizia mswaki ndani yake ili mwizi wa maji yake ashindwe kunywa. Baadae jioni aliporudi akakuta mswaki wa pili ndani yake.

*real story*
cheka unenepe.
chekazone.blogspot.com

Naniliu mpya

Mzee mmoja aliletewa 'pichu' 3 na mjukuu wake toka majuu. Sasa kuna siku alisahau kuvaa na akawa bahati mbaya watoto wa mtaani wakawa wanaonyeshana vidole uku wanacheka, yule mzee alipowaona akawaambia ''mnaishangaa hiyo? Nnazo zingine ndani mpyaaa''

Mfungo...

Jamaa mmoja alikuwa hawezi kabisa suala la kufunga mwezi mtukufu. Siku moja mama yake mzazi akamuuliza ''hivi wewe utaanza lini kufunga?''

Jamaa akamjibu ''mbona nimeshaanza mama kufunga, shida iko wapi?''

Mama akauliza tena ''mbona wakati wa kufuturu haujumuiki nasi?''

Jamaa akajibu ''kwasababu huwa nafunga usiku''

Zahanati

Dada mmoja mwenye ujauzito wakati anachukuliwa maelezo yake na nesi pindi alipohudhuria clinic:

Baaada ya kuulizwa jina, umri nk ikafika kipindi cha kuulizwa jina la Baba wa mtoto.

Nesi: Baba anaitwa nani?
Mjamizito: Sina.
Nesi: Sasa umeipataje hiyo mimba?
Mjamzito: Ameikataa mimba.
Nesi: Mi nipe jina tu nijaze haka kasehemu mengine unayajua wewe.

Kabla hajajibu kuna mgonjwa mmoja wa kiume alikuwa karibu na mahojiano hayo akadakia na kusema ''basi niandike mimi''

Kauli...

Fredy alimuona msichana mzuuri akashindwa vumilia na kumuambia...
Fredy: Dada nimekupenda sana.
Dada: Kwa nini mimi?
Fredy: Wewe ni mzuri sana.
Dada: Ooh! Kuna msichana mzuuri zaidi yangu anakuja na nadhani utampenda zaidi. Yupo nyuma yako.

Fredy akageuka kuangalia kisha akajibu.

Fredy: Mbona hamna mtu?
Dada: Ingekuwa unanipenda usingegeuka kumuangalia mwingine.

Tuesday, June 15, 2010

Lift

Mwanamke na mwanaume walikwama kwenye lift. Wana dakika 3 tu kabla hawajafa, mwanamke akamuambia yule mwanaume ''nifanye nijisikie kuwa mwanamke.'' Yule mwanaume akavua nguo haraka haraka na kumpa na kumwambia kazinyooshe na pasi.

Kuopoa

Jamaa mmoja aliopo changudo akalala nae mpaka asubuhi. Kulipokucha akavaa suruali yake vizuri halafu akatoka nje kifua wazi huku akimuambia yule changudoa ''nakuja nna shida na mtu wa mapokezi''

Hatua chache toka ilipo gesti hausi kuna wauza mitumba ya sagula sagula, jamaa akanunua t-shirt ya bei chee akasonga mbele.

Tusi la...

Mtoto mmoja alitukanwa na mwenzake ''fuck u''

Alipoenda kumsemea kwa mwalimu. Yule mtoto alietukanwa akaulizwa na mwalimu, ''amekutukanaje?''

Yule mtoto aliogopa kulikopi kama lilivyo maana ingekuwa limehamia kwa mwalimu so akajibu ''amenitukana tusi la kwenye kanda ya Tupac''

Maagizo kwa watoto

Mgeni: Hodi.
Mtoto: Karibu.
Mgeni: Baba yupo?
Mtoto: Hayupo.
Mgeni: Kaenda wapi?
Pale pale getini kwa sauti kubwa akauliza
''eti baba niwaambie umeenda wapi?''

Joto

Warembo wawili walipata dili ya kufanya usafi kwa jamaa mmoja. Sasa wakati wapo ndani joto lilizidi kwani ac ilikuwa mbovu, hivyo mmoja akashauri kwa vile wapo wao tu wavue nguo na kufanya usafi wa nyumba. Ghafla mlangoni 'ngo ngo ngo'

Mmoja akadakia 'we nani?' mtu alie mlangoni akajibu 'kipofu' ooh wakafungua mlango.

Jamaa alipoingia akasema ''naitwa kipofu, wow matiti mazuri''

Tembo

Mtoto mmoja hakuwahi muona tembo. Sasa siku moja kwa nyuma kwenye gadeni akila kabeji na ndio akamuona kwa mara ya kwanza bila kujua huyu ndio tembo.

Akapiga simu polisi:
Mtoto: Kuna mnyama hapa nyumbani... anakula kabeji kwa kutumia mkia wake.

Polisi: Anafanya nini?
Mtoto: Kama nkikuambia anaziingiza wapi huwezi niamini!

*cheka unenepe*

Maneno

Mwanaume mmoja alikua anaendesha gari kwnenye double road. Pembeni yake kulikuwa na gari pia ikiendeshwa na mwanamke.

Yule mwanamke akageuka kumuangalia mwanaume upande alipo na kutamka kwa sauti ''MBWA'' yule mwanaume nae akamjibu kwa sauti ''bitch.''

Hamadi yule mwanaume akagonga mbwa aliwepo mbele.

Pasi

Siku moja katika maongezi kwenye simu, mume na mke:
Mke: Mume wangu huku umeme umekatika.
Mume: Oo! Pole sana mke wangu.
Mke: Nna lingine la kukuambia mume wangu.
Mume akashtuka kidogo na kuendelea.

Mume: Enh! Niambie mke wangu.
Mke: Gari yako imepigwa pasi...
Mume: We si umeniambia umeme umekatika? Asa pasi uwewashaje?

Kwenye bus

Jamaa mmoja kwenye daladala alikuwa anasikiliza mziki, alipobanwa na gesi tumboni aliamua kupumua uku akifuatisha midundo ya mziki ili abiria wengine wasisikie sauti akijamba.

Baada ya yeye kijana kushuka kwenye daladala akaja gundua kuwa alikuwa anasikiliza nyimbo kwa headphones zake.

Kidhungu tata

Mtoto mmoja mdadisi alimfuata baba ake kwenye garden na kumuuliza ''baba.. nini maana ya sex?''

Baba alivuta pumzi na kumuambia kwa kina kuhusu sex ikiwemo mbegu za uzazi, mzunguko wa mayai ya uzazi nk nk.

Baba alipomaliza akamuuliza mwanae we umelipata wapi hili neno?

Mtoto: ''Mama kaniambia nije kukuambia kuwa lunch would be ready in a couple of sec's...''

Duh!

Mtoto mtundu siku moja asubuhi alimuuliza bibi yake. ''bibi, mama na baba wapo wapi?''

Bibi akajibu ''bado wamelala'' mtoto akaenda shule, aliporudi akauliza swali lile lile akajibiwa vile vile. Jioni napo vivyo hivyo.

Bibi akamuuliza, ''mbona wauliza kila dakika swali hilo?''

Mtoto akajibu huku akicheka na kutikisa kichwa: ''Jana baba kuniomba vaseline mimi nikampa super gluu.''

Changudoa na mzungu.

Siku moja mzungu alisimama mtaa wa machangudoa ili aopoe mmoja akajivinjari. Alitokea mmoja aliejiona kidogo kimombo kinapanda akamwambia mzungu ''look.. look... My milk standing''

Mume kicheche

Kijana mmoja wa kiume alimpeleka mpenzi wake kwa wazazi kumtambulisha kuwa ndie atae muoa, baba akamwita chemba na kumuambia ''mwanangu unajua mama yako sio mzuri sana kitandani. Hivyo nlikuwa nkitoka nje na huyu uliekuja nae ni dada yako yani mwanangu''

Kijana alistuka akachoka. Akaleta mwingine na mwingine hali ikawa ile ile. Akashindwa vumilia akaenda kwa mama yake.

Kijana: Mama me nimechoshwa na baba, kila mchumba nimletae asema eti ni mwanae wa nje''

Mama: Usimsikilize huyo atakuumiza kichwa kwanza si baba yako mzazi.

Coca cola

Mmasai mmoja alienda dukani:
Maasai: Habari ya saa hii?
Muuza Duka: Njema.
Maasai: Ile soda nyeusi ipo?
M. Duka: Ipo.
Maasai: Leta, nausaje?
M. Duka: Sh 200 tu.

Ikaletwa mbele yake maongezi yakaendelea.

Maasai: Fungua.
M. Duka akaifungua.
Maasai: Leta glasi.
Ikaletwa.
Maasai: Pimia mimi ya 100Tsh tu.

Tishia mbwa

Mtoto mmoja alikua mvivu wa kula sana, siku moja wakati analishwa chakula aliekuwa anamlisha aliamua kutumia nafasi ya kumuambia mtoto ''kula bwana ntamwita bobi aje akung'ate'' akimaanisha mbwa wa hapo kwao. Kale katoto kuonyesha kuwa hakaogopi hata chembe kakadakia na kumuita mbwa ''bobi... bobi... uyu-uyu-uyu''

Hiyo uyu-uyu-uyu ndio akipiga mluzi kumuita bobi.

Ili inoge tamka uyu-uyu kama ilivyoandikwa ndivyo alivyotamka.

*cheka unenepe*

Msg

Mtoto mmoja umri wa kujifunza kuongea siku moja akimuambia mama ake kuwa kuna meseji imeingia, hali ilikuwa hivi: ''Mama... Mama... shemeji yako imeingia uku''

Cheti cha ndoa

Siku moja baba mmoja aliulizwa na mkewe:

Mke: Mume wangu ni muda mrefu umekaa hapo ukiangalia cheti chetu cha ndoa kulikoni?

Mume: Nilikua nakiangalia nkitafuta expire date.

Chai

Jamaa mmoja alileta utata, ni baada ya kutengeneza chai na kuwatayarishia wenzake kisha akamuuliza mtu wa kwanza ''samahani sukari nimeishiwa na je! nikuwekee vijiko vingapi vya chumvi?''

Wazo la mtoto

Siku moja baba alimkuta mtoto wake amekaa tulivu huku macho yote kwenye chupa ya konyagi.
Baba yake akaamua kumuuliza:

Baba: Mwanangu hiyo chupa mbona inaiangalia sana kwa muda mrefu sasa?

Mtoto: Baba me nashindwa kuelewa nimemsubiri huyu mtu kwenye hii picha ashushe mikono mpaka nimechoka, hivi hachoki?

Mtoto...

Mtoto mmoja akiwa anasoma akajikuta anamuuliza baba yake labda atapata msaada wa swali linalomsonga kichwani mwake:

Mtoto: Baba, Chile ipo wapi?
(akimaanisha nchi ya Chile)

Baba: Sijui, muulize mama yako sijui kaiweka wapi?

Mgonjwa...

Mgonjwa mmoja aliekewa drip ya maji:

Mgonjwa: Nesi samahani naweza kuuliza?
Nesi: Uliza tu.
Mgonjwa: Haya maji ya kwenye drip ni ya Uhai au Kilimanjaro?

Monday, June 14, 2010

Mwenda wazimu

Mwenda wazumu mmoja wa kiume alitembea uchi kwenye mbuga za wanyama; Wanyama wakaanza kumkimbia akiwemo na simba. Fisi akamuuliza simba ''hata wewe unakimbia?'' simba nae akajibu ''wee toka nizaliwe sijawahi ona mnyama ana mkia mbele''

Kujiua

Mwanaume mmoja aliamua kujirusha toka ghorofa ya 4 ili ajiue kutokana na maudhi apatayo toka kwa mkewe, kwa bahati mbaya hakufa akavunjika vunjika tu na kulazwa hosp:

Siku mkewe alipoenda kumtembelea hosp akamuambia hivi ''siku ingine ukitaka kujiua panda ppf tower''

Kunyongwa...

Kulikuwa na watuhumiwa wa kunyongwa watatu siku ya kunyongwa kwa kwa nyakati tofauti hali ilikuwa hivi:

Mtuhumiwa 1: Alisimama kwenye kizimba akafikiriaa na kusema kwa sauti kubwa ''tetemeko tetemeko'' watu pakawa hapatoshi na yeye akapata mwanya wa kutoroka.

Mtuhumiwa 2: Kabla ya hukumu yake alifikiria nakupiga kelele ''Mafurikoo mafurikoo'' pakawa hapatoshi na yeye akapata mwanya wa kutoroka.

Mtuhumiwa 3: Huyu nae kabla ya muda wa kunyongwa akasimama na kusema kwa sauti kubwa ''moto motoo!!......''

Zawadi ya babu...

Kizee kimoja kilienda kwa daktari wake:

Dokta: Babu umri wako unazidi songa mbele sana, nikununulie nini unikumbuke milele?

Babu: Ooh! Mjukuu wangu niwezeshe meno na nywele ziote tena. Nimemiss sana ku-brush meno na kuchana nywele.

Msaada kwa dokta

Kaka mmoja alienda kwa dokta ''dokta nisaidie niweze kucheka nna shida mie sichekagi kabisa''

Dokta akamjibu ''Ooh, usijali we nenda mtaa wa pili utakuta mtu, kila anaepita na kumuona anacheka, utacheka tu''

Jamaa akajibu ''bahati mbaya huyo mtu mwenyewe ndio mimi''

Kunyonyesha

Mama mmoja wa watoto wawili alikuwa anamnyonyesha mwanae wa pili, yule wa kwanza akamuuliza mama ake ''mama kwa nini unamnyonyesha mdogo wangu halafu mimi huninyonyeshi''

Mama akamjibu ''ooh! Huyu mdogo wako hana meno so hawezi kula'' mtoto hakutosheka na jibu akamuuliza mama ake tena ''mbona babu na yeye humnyonyeshi?''

Paka na panya

Siku moja kwenye chimbo fulani panya wawili walimuona paka kwa nje amekaa. Panya mmoja akamwambia mwenzake ''nna uwezo wa kumfanya paka akimbie'' panya mwenzake akamuuliza ''kivipi?''

Yule panya wa kwanza akabweka kama mbwa ''bow wow!'' kidogo wakamuona paka anakimbia. Kisha akageuka na kumuambia mwenzake ''unaona faida ya kujua lugha nyingine ya ziada?''

Kupokea simu

Wanaume kadhaa walikuwa kwenye chumba kimoja cha kubadilisha nguo za michezo ghafla simu ikaita. Mwanaume mmoja akawaambia wale wote wakae kimya akaipokea simu:
Mwanaume: Halo?
Mwanamke: Halo honey, upo club?
Mwanaume: Ndio.

Mwanamke: Nipo mlimani city nimeona suti ya laki 6 ni sawa nikiinunua?
Mwanaume: Ndio mpenzi inunue tu.
Mwana ke: Pia nimeona Lexus ya 2008 mpya kwa $ 55,000 nimeipenda sana.
Mwanaume: Oh! Kwa pesa hiyo bila shaka.

Mwanamke: La mwisho mpenzi kuna nyumba masaki kwa Milioni 150 ipo full loaded.
Mwanaume: Consider it done.

Baada ya maongezi kuisha jamaa akatabasamu na kuiweka simu pale alipoikuta na kuuliza
''yeyote anaemjua mwenye simu hii nani?''

Weita na mteja

Mzee mmoja alienda kwenye restaurant:
Mzee: Weita njoo. Onja hii supu.
Weita: Hapana mzee hairuhusiwi mimi kufanya hivyo.
Mzee: Nakuomba onja supu.
Weita: Mzee itakuwa ngumu.
Mzee: Tafadhali onja supu, just onja tu.

Weita akaamua kuingia line ili aonje.
Wakati anainama ili aonje akasita na kumgeukia yule mzee na kuongea ''Siwezi onja hamna kijiko''

Mzee: Aha!

Mke na mume

Jamaa mmoja alienda kupata ushauri kwa daktari baada ya kuhisi kama mkewe hasikii vyema (dalili za ukiziwi). Dokta akamuambia ukirudi nyumbani wakati anapika simama hatua 15 nyuma yake na muulize kama hasikii sogea mbele kidogo vivyo hivyo na uliza swali hilo hilo.

Aliporudi home akakuta mkewe anapika, akasimama hatua 15 nyuma na kumuuliza ''mke wangu leo unapika chakula gani cha jioni?''

Hakupata majibu, akasogea kidogo mke hakusikia tena, akasogea tena hakupata jibu tena, mwisho akamsogelea kabisa na kumuuliza tena ''mke wangu leo unapika chakula gani cha jioni?''

Mke akamjibu, ''kwa mara ya nne najibu, nimesema Kuku''

*cheka unenepe*

Kumbukumbu ya ndoa

Mke alimuambia mumewe, ''mume wangu leo tumetimiza miaka 10 ya ndoa yetu, je, inakuwaje mpenzi?''

Mume: Tusimame kwa dakika moja kimya.

Ndoa

Mwanamke mmoja akizungumza kwa hasira na mumewe ''kabla sijaolewa, nlikua naenda out na wanaume wa maana zaidi yako''

Mumewe akamjibu ''naamini hilo'' kwa hasira akasisitiza ''hata hivyo walikuwa na akili ya ziada kutofanya makosa nliyofanya''

Zobaa

Vijana wawili walikuwa wakitembea mbele yao akawa anakuja dada ametoboa kipini kwenye pua na ameweka ki-cheni kimeunganika mpaka kwenye hereni.

Mmoja ya wale akina kaka akamuuliza mwenzake, ''haogopi akigeuka kichani chake kukatika akigeuka?''

Mwenzake akamjibu ''usiwe zoba wewe, sikio na pua hugeuka pamoja na kichwa''

Pharmacy

Kaka mmoja alifika duka la dawa baridi na kumkuta mdada anaeuza dawa. Alipoingia akiwa na mwenzake akamwambia yule dada hivi: ''habari ya saa hizi?'' kisha akaendelea baada ya salamu, '' mpatie mwenzangu Koflyn ya baridi na mie Mucolyn ya moto...''
(kama Bar vile)

Pipi

Siku moja kaka mmoja alikaa kwenye lecture room wakimsikiliza lecture. Ghafla jamaa akatoa viksi kingo na kuitumbukiza mdomoni kisha akamgeukia mdada alie pembeni yake na hali ikawa hivi:

Kwa kumnong'oneza,
Kaka: Samahani dada una maji hapo?
Dada: Hapana sina, ya nini kwani?
Kaka: Nataka nimezee vix kingo.

Kwenda juani...

Nchi mbili wakiwa ktk mazungumzo:

Nchi A: Sisi ni wa kwanza kwenye anga.

Nchi B: Sisi wa kwanza kwenye mwezi.

Nchi C: Sasa ndo iweje? Sisi tutakuwa wa kwanza kwenye jua.

Nchi A na B wakabaki mdomo wazi!

Nchi C: Mnadhani sisi wajinga? Hatutoweza ungua kwa jua, tutaenda usiku.

Utingo

Utingo mmoja wa lori wakati wapo safarini kwa mbaali wakaona traffic polisi kanyanyua mkono kuashiria wasimame. Ndipo utingo akamuambia dereva leo niachie mimi niongee nae...

Lori likasimama ndipo tingo akamuambia yule traffick polisi ''habari ya leo? Una buku mbili hapo? Leo nimeuwawa mno...''

Kutoa mahari

Mpima viwanja mmoja alienda kutoa mahari. Baada ya kutozwa hela nyingi takriban milioni moja, alishindwa kuvumilia akawauliza wakwe.... ''hiiivi hiyo nanihii ya mtoto wenu ipo karibu na main road au?''

English media

Baba mmoja shule ilimpitia kushoto kidogo. Bahati nzuri alifanikiwa mpeleka mwanae moja ya shule za siku hizi za dotcom.

Siku moja mtoto alirudi toka shule kwa likizo kazi ikawa hivi.

Mtoto: Daddy, help me to do my homework.

Baba kwa vile kimombo hakipandi kabisa:

Baba: Mama Jesca (aliita kwa sauti) hebu njoo unisaidie.

Mama Jesca alipokuja hali ikawa hivi:

Uku akimnong'oneza
Baba: Hivi wanafungua lini shule hawa wakina Jesca...

Mtoto wa maswali

Mtoto mmoja alienda na kumuuliza mama ake.

Mtoto: Mama orgasm ndio nini?
Mama: Sijui, muulize baba ako.

Mtoto akaenda kwa baba kuuliza apate jibu.

Mtoto: Baba eti orgasm (kilele) ndio nini?
Baba: Sijui my son, kamuulize housegirl.

Mtoto akarudi kwa mama.

Mtoto: Mama, baba nae hajui ameniambia nikamuulize housegirl.

Mapacha watatu

Mama mmoja alikuwa mja mzito wa mapacha watatu tumboni. Humo tumboni wale watoto maongezi yao kama ifuatavyo:

Mtoto 1: Mi nkitoka humu ndani lazima niwe fundi umeme hili giza humu ndani limezidi.

Mtoto 2: Mimi ntakuwa mkulima maana njaa inazidi sa zingine humu ndani.

Mtoto 3: Mimi ntakua muwindaji, huyu nyoka anaeingia ingia humu ananikera sana. (uume)

Mimba

Siku moja mume na mkewe mjamzito wakati wanafanya tendo la ndoa ghafla ya mume ikanasia ndani.

Mume akachukua jukumu la kumpigia simu daktari wake kwa msaada zaidi.

Mume: Dokta nanihii yangu imenasa kwa mke wangu.

Dokta: Tafuta pipi umpe mama aimeze.

Dakika chache baadae akampigia simu tena dokta.

Mume: Dokta nashukuru imechomoka. Mbona sijaelewa kuhusu pipi?

Dokta: Mtoto tumboni kaona pipi akaiachia nanihii...

Ushamba

Jamaa mmoja alinunua gari. Baada ya siku kadhaa akaenda kwa fundi:

Mwenye gari: Fundi nimekuja nna swali kuhusiana na gari yangu.

Fundi: Oh, uliza tu.

Mwenye gari: Eti nnasikia nikiwa naendesha matairi yanazunguka?

Fundi: !

Kununua gari.

Jamaa mmoja mjasiliamali aliamua kujitolea uvivu akamuita rafiki yake ampe ushauri, maongezi yao kama ifuatavyo:

Frank: Kaka nimekuita nataka unipatie ushauri.
Deo: Bila shaka kaka ushauri gani una uhitaji toka kwangu?

Frank akamjibu bila wasiwasi.

Frank: Nina plan ya kununua gari siku za usoni.
Deo: Ooh! Wazo zuri sana, enhe endelea...
Frank: Nishauri nimeshindwa kujua nianze kununua kimoja kimoja je nianze break au honi?

Wodini

Wagonjwa watatu katika wodi moja ya wanaume kila mmoja kwa wakati wake:

Mgonjwa one: Nesi, nesi nataka kukata gogo.
Akisema kwa sauti.

Nesi: We usiseme hivyo. Sema unataka huduma namba moja.

Mgonjwa two: Neesiii, nataka kwenda nnya.

Nesi: Wewe! Hatutumii hiyo lugha hapa, sema nataka huduma namba mbili.

Mgonjwa three: Nesi, Psss.
Nesi akaja (akaanza kumnong'oneza)
''nataka kwenda haja kubwa lakini sijapewa namba bado''

Wawili na wake

Wanaume wawili wakiwa katika maongezi yao ya kawaida.

Wa kwanza: Nnafurahi sana mke wangu ni malaika.

Wa pili: Ooh! Mimi wa kwangu bado yupo hai.

Yero...

Maasai mmoja alenda stationary na kuona karatasi zikitolewa copy, yaani unaweka moja inatoa nyingi.
Akaondoka na kurudi na chapati moja maongezi yakawa hivi:

Maasai: Rafiki tolea mimi kumi na mbili tapelekea mama yeyoo singine.

Begi la abiria

Jamaa mmoja baada ya kushuka toka kwenye ndege wakati anasubiri sehemu ya kupokelea mizigo bahati mbaya yeye pekee ndio hakuona mzigo wake, hivyo akaamua akaulize kwa wahusika wa ndege husika aliotua nayo:

Abiria: Samahani nimepotelewa na mzigo wangu sijauona niliposhuka.
Mfanyakazi wa kampuni: Ooh! Utaupata tu usiwe na wasi wasi, hawa wanafanya kazi yao vizuri sana.

Baada ya kusema hivyo akaongezea maongezi ya ziada.
Mfanyakazi wa kampuni: Ndege yako inatua saa ngapi?

Kali kuliko

Wakaka fulani pombe ikiendelea kuchapwa ghafla ukimya ukatawala baada ya kupita dada mmoja wa makamo, baada ya nusu dakika kupita mmoja kati ya waliokua wameduwaa akajikuta anasema kama ifuatavyo:

''Mhh! Jamani huyu dada aliepita hapa jinsi alivyo nikisimamishwa mimi na yeye mimi (mwanaume) ndio ntaolewa.

Wenzake hoi kwa kucheka.

*cheka unenepe*

Chagua wimbo

Jamaa mmoja alipiga simu studio za radio fulani ya fm na kutuma salamu, maongezi yao yakawa hivi:

Studio: Chagua nyimbo ya kusindikiza salamu zako.

Msikilizaji: Ooh! Nachagua wimbo wa anko Sam ''i don't ever wanna see you again'' dedication kwa mpenzi wangu. Ujumbe nampenda sana.

Toto tundu...

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake maswali kama ifuatavyo:
Mtoto: Baba kuna nini katikati ya miguu ya mama?
Baba: Ooh! Ni Paradisie.
Mtoto: Na je, katikati ya miguu yako je kuna nini?
Baba: Ufunguo wa kuingia Paradise.
Mtoto: Ooh! Bora ubadilishe ufunguo wa Paradise baba Ima nae ana ufunguo.

Sunday, June 13, 2010

Milionea...

Wanamke mmoja akitwanga stori na shoga ake:
Mimi ndio nliemfanya mume wangu kuwa Milionea.
Shoga ake akauliza: Awali alikuwaje kwani?
Bila wasi wasi mke akajibu ''alikua Bilionea''

Housegirl mpya

Mama mmoja alipata housegirl mpya na katika maisha ya hapo nyumbani siku hadi siku yule mama alijiuliza swali moja ambalo jibu lake ilibidi alitafute kwa housegirl wake.

Mama: Dada, hivi hizi toothpick zinatumika kweli? Mbona zipo vile vile kila siku.
Housegirl: Eeh! Mama zinatumika, me nkimalizaga kutumia tu nazirudishiaga humo humo....

*cheka unenepe*

Kamba

Dereva mmoja alimuambia konda wake afungue kamba iliyokuwa imefungiwa mzigo juu ya keria ya gari husika. Konda wakati anaifungua kamba husika kulingana na ilikuwa ngumu mno kuifungua alijikuta akimuuliza derava wake.
''alieifunga hii kamba alikua amekasirika nini?''

Dawa ya kupaka...

Mgonjwa alipofika kwa daktari ili kupata maelekezo vizuri kama alivyoagizwa siku chache nyuma hali ilikuwa hivi:
Mgonjwa: Daktari nimekuja.
Daktari: Karibu sana, nini shida?
Mgonjwa: Dokta, hivi ile dawa ya kupaka uliniambia ninywe mara ngapi?
Dokta: !!?

Mchango wa harusi

Jamaa mmoja wakati wa harakati za kuwakumbusha na kufuatilia mchango wa harusi yake alifika kwa bwana mmoja ili kama mchango wake upo tayari auchukua hali ilikuwa hivi:

Bwana harusi mtawajiwa: Kaka nimekuja kukukumbushia mchango wa harusi.
Jamaa akajibu: ''njoo na picha ya bibi harusi kwanza''

Toothpick

Jamaa mmoja alimtoa outing girlfriend wake mpya kwenye restaurant moja nzuri tu.
Baada ya kula maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanaume: Vipi nikuagizie toothpick?
Mwanamke: Henh! Asante nimeshiba sana tayari.

Kupima...

Jamaa mmoja alienda kupima ajue afya yake kama ana VVU au la!
Majibu yalipokuja baada ya kupatiwa counceling hali ilikuwa hivi:
Mtoa majibu: Majibu yako yanaonyesha una Upungufu wa Kinga Mwilini...!
Mpokea majibu: Ooh! Afadhali me nlijua nna AIDS.

Kibao cha shule

Mwalimu akimuuliza wanafuzi watatu waliochelewa shuleni:
Mwalimu: We Abraham kwa nini umechelewa leo?
Abraham: Kwa sababu ya kile kibao.
Mwalimu: Kibao gani?
Abraham: Cha barabarani ''school ahead go slow''
Mwalimu: !!

Mwalimu: Haya na wewe Kulwa kwa nini umechelewa shule?
Kulwa: Nilikua naota nimepanda KLM to...
Mwalimu: Na wewe doto kwa nini umechelewa?
Doto: Nilimsindkiza Kulwa Airport kwenye ndoto.

Mtoto atoboa siri

Mama: Josh amka amka muda wa kwenda shule umefika.
Mtoto: Nooo mama mi siendi shule leo.

Mama: Kwa nini hutaki kwenda shule leo.
Mtoto: Nataka nimuone tena na leo baba akienda chumbani kwa housegirl.

Gia ya bus...

Siku moja kwenye basi la abiria maasai mmoja alikuwa akimyangalia jinsi dereva anavyoendesha basi uku akiingiza gia moja nk nk.

Ilipofika muda wa kula baada ya safari ndefu dereva akapaki basi ili abiria wakapata kula cha mchana.
Waliporudi kwenye basi dereva akakuta gia ya basi imeng'olewa ndipo maasai akadakia ''asee rafiki me meona wewe napata shida ng'oa hii, me tayari saidia wewe''

Maasai muda wote alijua dereva anajaribu kuing'oa kumbe ni jinsi tu ya kuweka na kutoa gia.
Safari ikazorotea papo hapo.

Kituko cha maasai

Mmasai mmoja alipanda kwenye bus na mkewe! Baada ya safari ndeefu akamuuliza:

Maasai: Konda kwani mutu kama meoa naruhusiwa kula chakula yake.

Konda: Ndio.

Maasai baada ya kujibiwa akageuka na kuita.

Maasai: Mama yoyoo, leta ile chakula ya usiku.....

Watu kwenye basii ''aaaahh! Sio humu tafadhali... Sio humu... (maasai alikuwa ana maanisha malove davy na mkewe).

*CHEKA UNENEPE*

Tugawane...

Jamaa mmoja wakati anasoma kwa ajili ya mitihani ya chuo na wenzake wanne baada ya kuona mambo hayapandi akasonya. Mwenzake mmoja akamuuliza ''kulikoni mwenzangu''
jamaa akajibu ''nasoma haviingii''
akaendelea kuongea kwa staili ya kubana pua ''halafu kesho na kesho kutwa tugawaane maali''
Room mate wenzake walicheka sana.
2006@Mabibo Hostel

Kapeti lenu

Siku moja jamaa mmoja alienda kuwatembelea rafiki zake, sasa wakati yupo mlangoni akiongea na wenyeji wake maongezi yao yalikuwa hivi:
Mwenyeji: Karibu bwana ndani, karibu.
Mgeni: Hapana usijali hapa hapa tu panatosha sikai sana.

Jamaa mwenyeji akazidi kusisitiza.
''karibu ndani bwana pita tu na viatu''
Mgeni: Aa! Naogopa kuingia na viatu kapeti lenu litanichafulia viatu vyangu.

Baba na mama

Baba na mama walioana wakiwa na watoto wao kila mmoja toka alikotoka. Sasa siku moja watoto wao wakaanza kutwangana mangumi. Mkewe sasa wakati anamuita mumewe ilikuwa hivi:
''mume wangu.. Mume wangu... Wanao na wanangu wanapigana njoo haraka.''

Bahiri...

Bahiri mmoja alinunua mbuzi akamwambia mpishi,

''sikiliza ee... nusu ya nyama ipikie pilau na nusu ingine iweke kwenye friza. Kichwa kichune tutafanya supu na miguu tutafanya mchuzi chukuchuku...
Ngozi usiitupe tutafanya msala. Utumbo tutapika na ndizi. Mifupa tutawauzia wenye mmbwa.
Mbuzi aliposikia akamuuliza ''hutaki sauti yangu uweke kwenye simu yako? (ringtone)

Muuza mihogo...

Muuza mihogo mmoja alikamatwa na askari wa jiji wakabeba mihogo yote halafu wakatimua.
Ghafla askari mmoja akarudi na kumuamrisha yule mwenye mihogo ''we chumvi iko wapi?''

Mtoni

Jamaa mmoja alienda pembezoni mwa mto, upande wapili kulikuwa na mzungu nae akishangaa shangaa. Jamaa akavunja ukimya akaamua kumuuliza:
M-tz: Hey yoo! How can i get to the other side?
Yule mzungu akaangalia huku na kule na kumjibu:
Mzungu: You are on the other side already.

WorldCup

Mume alipokuwa anaangalia mpira maongezi yao na mkewe yakawa hivi:
Mke: Mume wangu njoo itengeneze hii taa ya jikoni.
Mume: Now? I don't think so.
Mke: basi njoo uurekebishe huu mlango...
Mume: I don't think so.
Mke: Basi pale kwenye sinki panaleta shida.
Mume: Not now.
Mume akaona kero akaondoka kwenda kuangalizia mpira Bar. Wakati yupo huko akajiona amefanya sivyo ndivyo akaanza kurudi nyumbani.
Akakuta kila alichoambiwa kimetengenezwa. Akauliza:

Mume: Imekuwaje hivi vitu vyote vimetengenezwa?
Mke: Alikuja kijana mmoja akanikuta nje hapo nalia ndipo akaamua kunipa msaada, na sikuwa na cha kumpa zaidi ya ile TV set yetu.

Mume na mke

Mume: Kuanzia leo kauli yangu ndio ya mwisho ndani ya nyumba hii, nataka uniandalie chakula now, then maji ya kuoga.
Halafu jiulize nani atakaenichana nywele zangu?

Mke: Muosha maiti.

Cheka...

Mama mmoja aliwapeleka wanae mapacha wa kike kuangalia wanyama, wakati wapo huko mtoto mmoja akaona nyani wanafanya mapenzi akauliza.
Mtoto: Mama wale wanafanya nini?
Mama: Wanatengeneza keki.

Next time akaona mbwa, jibu akapewa lile lile.

Siku moja wakati wapo nyumbani mtoto mmoja akamwambia kaka yao:
''kaka mama na baba wametengeneza keki''
Kaka: Wewe umejuaje?
Mtoto: Si melamba ice ilodondokea kitandani.

*cheka unenepe*

Barua kwa mtoto...

Mama mmoja akiandika barua kwa mwanae:
Dear child,
I am writing this letter slow because i know you can't read fast....

*cheka unenepe*

Fumanizi

Jamaa mmoja aliporudi home akakutana uso kwa uso na njemba ina-do na mkewe wa ndoa. Katika purukushani za hapa na pale ikafanikiwa kuchoropoka. Mwenye mke alipotoka nje kulitafuta njemba hilo akakutana na vijana na maongezi yao yakawa hivi:

Mwenye Mke: Aisee hamna ona mtu kapita na mb*** mbichi mbichi hapa?
Wale vijana walibaki wameduwaa.

Mtuhumiwa

Polisi mmoja wakati anamtafuta mtuhumiwa mhusika kati ya watuhumiwa wanne aliwaamuru kama ifuatavyo:

Askari: Kila mmoja atasema maneno yafuatayo ''toa pesa la sivyo ntakuua sasa hivi''
Kibaka mmoja kati ya wale wanna akadakia kwa sauti ''mimi sikusema hivyo''

*cheka unenepe*

Mama na Mtoto

Mtoto: Mama kwa nini tunalisukuma gari kuelekea mteremkoni?
Mama: Shhhh! Utamuamsha baba ako.

Kibaka kituo cha polisi

Jamaa mmoja alienda kituo cha polisi ili amuone mwizi alie ingia kwake usiku wa jana yake, kitioni polisi mahojiano yalikuwa hivi:

Alieibiwa: Naomba kumuona yule mwizi alievamia kwangu jana usiku.
Polisi: Utaonana nae mahakamani.

Alieibiwa: Tafadhali nisaidie nataka nimuulize amewezaje kuingia bila mke wangu kumsikia?
Maana nimejaribu kwa miaka mingi sijafanikiwa.

*cheka unenepe*

Pombeka...

Walevi watatu:
Mlevi 1: Mi nikilewa nasahau gari bar kila siku.
Mlevi 2: Mi nikilewa nakumbuka madeni.
Mlevi 3: Mi nikilewa nasahau kutembea kabsaaa!

Fumanizi

Mwanamke mmoja alisikia kuwa mumewe ana mwanamke wa nje. Akaamua kwenda kununua pistol. Siku ya siku akabahatika kumfumania mumewe chumbani na kimada. Ikawa hivi:

Mwanamke akajilengesha ile pisto kichwani kwake,
Mwanaume: Mke wangu mke wangi tafadhali usijiue.... Ni shetani tu.....

Mwanamke: Nyamaza huko, you are next.

*cheka unenepe*

Vibaka

Vibaka wawili walipata wakati mgumu sana kumpora jamaa mpaka wakafanikiwa kumpora wallet yake. Mmoja wa vibaka akamuuliza jamaa waliemuibia:

Kibaka: Sasa nguvu zote zile ukizozitumia kupambana nasi kumbe una elfu mbili tu kwenye wallet.

Jamaa: Nilikuwa sitaki mjue kama nna elfu 80 kwenye kiatu.

*cheka unenepe*

Dokta na Mgonjwa.

Baada ya uchunguzi wa afya yake kwa ujumla daktari akarudi kwa mgonjwa wake mzungu na maongezi yao yakawa hivi:
Dokta: Am afraid i've some bad news you're dying and don't have much time.

Mzungu: How long time i got?
Dokta: Ten.

Mzungu: Ten? Ten what? Months? Weeks? What?
Dokta: Ten, Nine, Eighty, Seven.......

Pombe na glass

Walevi wawili baada ya pombe kukolea kila mmoja alikua na la kumuambia mwenzake na maongezi yao yalikuwa hivi:

Mlevi no.1: Glasi yangu bado nusu kuisha.
Mlevi no.2: Glasi yangu bado nusu kujaa.

*cheka unenepe*

Mchina na omba-omba

Ombaomba mmoja alipewa noti ya shilingi elfu kumi na mchina, ombaomba yule akaikataa ile elfu kumi ombaomba mwenzake akamuuliza:

Ombaomba: We mbona umeikataa ile noti?
Mwenzake akamjibu kwa kujiamini.
''aa! Hawaaminiki hawa, kama feki je?''

Kung'oa jino...

Jamaa mmoja alienda kun'goa jino, daktari baada ya kumdunga sindani ya ganzi akatoka kidogo. Aliporudi akamkuta jamaa kasimama pembezoni mwa trei la vifaa vya kung'olea meno, dokta akamuuliza ''unafanya nini hapo?''

Jamaa kwa kujiamini kabisa akajibu ''natoa vifaa nisivyovitaka''

Kishoka wa kike...

Mama mmoja akitembea bila kujijua kuwa chuchu moja ipo nje mara akakutana na polisi, mahojiano yao yakawa hivi:

Polisi: Mama unajua kwamba chuchu moja ipo nje?
Mama: Ooh! Mungu wangu nimemsahau mtoto kwenye bus AGAIN.

Walevi na kioo

Walevi wawili wakiwa njiani waliokota kioo kidogo cha make-up hali ikawa hivi wakati wanajiangalia:

Mlevi One: Hii sura si ngeni ila jina sikumbuki kabisa.

mwenzake akamnyang'anya na kujiangalia kisha akasema hivi:
Mlevi Two: Aaah, we chizi kweli, si mimi huyu.

Kimbwanga cha radio

Jamaa mmoja alikua na tabia ya kulala chini ya mti huku akipunga upepo na radio ikiongea pembeni yake.

Siku moja vijana (vibaka) wakam-time na kufanikiwa kuondoka na radio huku yeye amelala.

Alipokuja kuamka hakuiona radio, kilichofuata wakati anaitafuta mtaa wa jirani mambo yakawa hivi:

Mwenye radio akiuliza kila aliemkuta ''aisee umeona radio ikipita hapa?''

Mtihani wa hesabu

Mtoto: Mama naweza kukuazima kikokotoa (calculator) chako kwa ajili ya mtihani wa hesabu kesho shuleni?

Mama: Ntakupatia mwanangu. Na je, kama nisingekuwa na kikokotoa si ingebidi utumie kichwa kufanya hesabu?

Mtoto: Mama that's cheating, haturuhusiwi kutumia kichwa.

*cheka unenepe*