Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, August 31, 2010

Dish|Kutu

Jamaa mmoja alinunua dish la tv. Baada ya kulitumia kwa muda mrefu likawa limetengeneza kutu karibu loote.

Siku moja akalipaka rangi iliuiepuka ile kutu. Baada ya hapo hakukamata hata channel moja tena.

Monday, August 30, 2010

Naumwa

Marafiki wawili walikaa sehemu wakiongea. Mmoja akamuambia mwenzake, "naumwa leo kichwa."

Mwenzake akamjibu, "we unaumwa? Nenda pale mapokezi Muhimbili uone wagonjwa."

Mchaga.

Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza "nipo wapi hapa?"

Nesi akajibu,"umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono."
Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex?
Ipo mzee, nesi alijibu.

Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji.
Mgonjwa: Yeuwi... Wamefunga duka?

Sunday, August 29, 2010

Maneno mengi

Wakati jamaa mmoja anakula akawa anamsimulia mwenzake, "nimekutana na huyu mmoja asubuhi hii, mara moja alianza nitukana na kunitishia nk nk"

Msimuliwaji akauliza, "kwani mmekutanaje na huyo mtu?"
Akajibiwa "nimekutana nae kwenye ajali, nilimgonga na gari bahati mbaya"

Afande

Afande: Pw Conso yuko wapi?
Kuruta: Kaenda Air-port afande.
Afande: Pumbafu si ni nimerituma uwanja wa ndege Air-port rimeenda kufanya nini, rikija ni fatiki tu.

Vifaranga

Jamaa mmoja alienda kudai vifaranga kwa jirani, kisa jogoo wake ndio baba wa vifaranga.

Kidole gumba

Jamaa kidole gumba kilikua kinamsumbua, akaenda kwa dokta. Alipofika nesi akamuambia avue nguo kisha aingie chumba cha kusubiria kumuona daktari.

Jamaa akasema "yani kidole gumba tu ndo nivue nguo zote?"
Nesi akajibu, "hiyo ndio sera ya hospitali yetu."

Jamaa chumba cha pili akadakia, "hiyo sio kitu mi nimekuja kutengeneza simu."

Tongoza

Mwanaume mmoja akimtongoza Mwanamke.
Mwanaume: Nipo tayari ku-share kila kitu nawe...
Mwanamke: Tuanze na bank akaunti yako.

Saturday, August 28, 2010

Kijiti

Kwenye sherehe moja ya kuwapongeza maharusi, bwana harusi alitangaza kumkabidhi kijiti rafiki yake mmoja nae aoe siku za usoni.

Jamaa mmoja toka kwa washiriki wa sherehe hiyo akatamka "atakipoteza huyo."

Talaka

Mke na mume walienda mahakamani kuomba sheria iwasaidie watengane, jaji akawauliza "sasa mtagawanaje? Mna watoto watatu"

Mume mtu akajibu "ohh basi tutakuja tena mwakani"

Polisi

Polisi mkuu: Umefanikiwa mkamata mtuhumiwa?
Polisi mdogo: Hapana, ila ameniachia alama za kumtafuta...
Polisi mkuu: Nini?
Polisi mdogo: Alama za vidole.
Polisi mkuu: Wapi?
Polisi mdogo: Kwenye mashavu yangu.

Meli kuzama

Meli moja ilikuwa inazama, watu wakaanza kupiga kelele "meli inazama... meli inazama..."
Jamaa mmoja akasema "kwani ni umbali gani toka hapa mpaka kwenye ardhi?"

Akajibiwa, "kilomita 2"
Jamaa akasema, "sasa hao wanapiga kelele za nini kumbe ni hapo tu?"
Akajitosa kuanza kuogelea kidogo akauliza huku akiwa kwenye maji, "ni upande gani ilipo ardhi?"

Akajibiwa, "kwenda chini" (chini ya maji).

ATM|Password

Dada mmoja wakati anatoa hela kwenye ATM, wa nyuma yake akasema "hahaha nimeiona password yako ina nne-nne. Jamaa akajibu "haha umekosea, ni 1382."

Bia ya mwisho

Mume: Tufanye tuondoke.
Mke: Mume wangu niongezee bia moja ya mwisho.
Mume: Hapana utakojoa kitandani usiku.

Dokta | Mifugo

Jamaa mmoja alimpeleka ndama wa ng'ombe wake kwa dokta. Dokta akamuuliza ana shida gani?
Akajibu "mekuja umpime ndama wangu DNA nijue kama ni wa kwangu!"

Lini besdei

"Mama... Mama... Kwani birthday yangu mbona haifiki tu?"
Mama: Kwani unaijua tarehe?
Mtoto: Ndio si tarehe 32 Mei?

Mwanamziki kwenye TV

Jamaa mmoja alimuona mwanamziki kwenye tv moja akiimba. Baada ya masaa kadhaa akatoka na rafiki yake wakaenda kumtembelea mtu.

Walipofika kwenye tv channel ingine tofauti na home kwake akamuona mwanamziki yule yule akamuuliza mwenzake kwa kunong'ona "huyu mwanamziki huku kafika saa ngapi? Me si nlimuacha kwenye tv ya home."

Besdei

Mke siku moja akimuambia mumewe kwenye simu, "mume wangu usije sema sijakukumbusha, kesho ni birthday yangu."

Mume akamjibu, "sidanganyiiiki."

Mimba

Siku moja mama mmoja akimuasa mwanae wa kike pekee na dunia ya leo. "mwanangu Jesca, usiongee na mwanaume utapata mimba na mengineyo kama ukimwi nk"

Baadae usiku baba yake aliporudi akawa anamsalimia mwanae huyo wa kike, mtoto nae akajibu "mama kaniambia nisiongee na mwanaume ntapata mimba"

Viagra

Siku moja mzee mmoja alimpigia simu daktari wake, mambo yakawa hivi... "dokta... dokta... Mke wangu kameza viagra zangu nifanyeje?"

Tanzanite

Marafiki wawili wakiongea.
J: Hatujaonana siku nyingi sana.
H: Kweli kabisa, unashughulika wapi siku hizi?
J: Nipo na mradi wa Tanzanite. Wewe je?
Mwenzake ili aonekane yupo juu kimaisha akajibu.
H: Ooh! Mimi nipo kwenye mradi wa Mbeyanite.

English only

Shule moja ya dotcom mwanafunzi mmoja alikuwa amejiegesha kitandani na mwenzake, sasa huyo mwenzake anaitwa Kassim akawa anauvutia kwake mto.

Jamaa ikawa inamkera sasa kizungu kwake kidogo shida ikabidi amuambie "katelefone katelefone pliz don't smoke my river"

Tafsiri: Kassim Kassim acha kuvuta mto wangu.

Sinema

Mzee mmoja aliulizwa, "mzee ni sinema gani unaipenda sana?"
Mzee akakaa kimya sekunde kadhaa huku akivuta kumbukumbu kisha akajibu "ile ya kipaimara ya mjukuu wangu"

Namba ya simu

Juma: Jamaa amekupa namba?
Ali: Ndio na nsham-beep.
Juma: Hebu ni hiyo namba.
Baada ya kupewa akanena.
Juma: Wee! Ume-beep landline?

Dawa

House girl mmoja aliulizwa "umempa dawa mtoto?"
Akajibu "amekataa kumeza, nimemsaidia kuzimeza mimi ili zisipotee bure"

Friday, August 27, 2010

Mkia

Mdada mmoja alienda kwa daktari wa wanyama, safari hii alienda na mbwa wake akamuambia dokta "dokta naomba umkate mkia mbwa wangu"
Dokta: Kwanini jamani?
Dada: Bibi anakuja kesho sitaki amtikisie mkia"

Dawa ya...

Jamaa mmoja mweupe wa ngozi alienda kwa dokta. Akamuambia dokta "dokta nna kiji-alama kekundu kwenye ngozi, sivi ni nini?

Dokta akampa dawa akapake nyumbani.
Kesho yake aliporudi akamuambia dokta, "kile kidoa kimeishia kabisa, ni dawa gani umenipa?"

Dokta akajibu " ni lipstic remover"

Hela

Babu alimuona mjukuu wake akifungua mlango bila kuugusa.
Babu akampa elfu kumi, mtoto akajibu "hapana babu, kaa nayo tu nimedanganya nimejifunga uzi.

Asubuhi ilipofika babu akampa elfu kumi tena, mtoto akasema "babu lakini umenipa jana."
Babu akajibu, "ile ya jana ya bibi yako"

Ndevu

Mtoto akimuambia Baba yake "baba... Yule mkata majani wetu ana ndevu kama zako?"
Baba: Ndevu?
Mtoto: Ndio ndevu kwa chini ya kitovu.
Baba: We umeonaje?
Mtoto: Nilimuona mama akimnyoa...

Thursday, August 26, 2010

Wamama watatu

1: Jana si nlifungua pochi ya mwanangu, nkakuta bangi. Nlikua sijui kama anavuta.

2: Hiyo mbona afadhali mi nlikuta Kitambulisho feki, sikuweza amini.

3: Hizo zenu hamna kitu, me nlikuta condom kwenye pochi ya mwanangu, nlikua sijui kama ana uume.

Matumizi ya kondom

Jamaa alifundishwa matumizi ya condom, kwa vile mfundishaji hakuwa na zana ilimbidi atumie chupa ndogo ya maji kama mfano wa uume.

Jamaa alikua chumbani aki-do na mwanamke akaivisha chupa condom huku akido pembeni mwa ilipo chupa, huku akijua yupo sahihi.

Gari

Jamaa mmoja wakati wanasafiri gari ndogo mbili zikawapita (overtakin) akasema "ile gari ya nyuma itachoka kumfuata ile ya mbele."

Wednesday, August 25, 2010

Redioni

Jamaa mmoja alikuwa anahojiwa redioni, akaambiwa achague mwimbo wa kumburudisha si akachagua wimbo wa taifa.

Maongezi

Jesca: Za masiku my dia?
Hilda: Njema, nimekumiss shosti.
Jesca: Hata mie shosti. Hivi babu yako bado yupo?
Hilder: Enhe yupo bwana, anazeeka tu.
Jesca: Hivi ana miaka mingapi sasa?
Hilder: 98 sasa.
Jesca: Mh! Bado mdogo kumbe.

Condom

Jamaa mmoja alienda pharmacy kununua condom, alipofika akamkuta dada ndio mhusika kisha akasema "...nahitaji condom..."

Muuza madawa akajibu "unahitaji size gani?"
Mteja akajibu "sijui habari ya size"
Muuza madawa akajibu "vua suruali tuone."

Sumu

Baba alikua ana wivu kwa mwanae mchanga anavyonyonya hivyo akaweka sumu kwenye chuchu za mke wake. Siku iliyofuata wakakuta dereva wao akafa kwa sumu.

Tuesday, August 24, 2010

Window 7

Jamaa mmoja alinunua laptop, sasa siku moja fundi akawa anamuelekeza jambo "open window 7 kwanza!"
Jamaa akajibu "nyumba yangu haina madirisha saba fundi."

Bar | Maegesho

Kaka mmoja aliingia bar. Akaenda mpaka kaunta, akaagiza bia kwa kuinyooshea kidole. Mhudumu akakataa kumpatia bia.

Jamaa akauliza kwa nini?
Mhudumu akajibu, "ukitoka hapa utaenda ku-drive"
Jamaa akauliza "sasa mbona nje kuna parking za magari?"

Simu|Pesa

Mama: Jamani simu zinakula heela khaa! Hadi nachukia.
Mtoto anasikiliza tu. Siku moja anko ake akaja akawa anaweka simu ya mkononi mezani. Mtoto akamwambia "anko usiweke pesa karibu na simu italiiwa hee!"

Pesa inaongea

Mtoto: Baba, eti pesa inaonge?
Baba: Ndio mwanangu.
Mtoto: Sasa mbona naisemesha haijibu?

Swaumu

Dokta wa meno alipomaliza mng'oa jino mgonjwa wake akamuambia "unaweza piga kelele kwa sauti kubwa uwezavyo?"

Mgonjwa akauliza, "kwa nini mbona umening'oa vizuri tu."
Dokta akajibu, "nje pana foleni kubwa sana, na swaumu imekolea nataka wapungue."

Maji

Mtoto mmoja asubuhi moja alimsikia dad yake akimuambia kaka yake mkubwa akajaze maji kwenye gari.

Basi muda ulipofika baba kufika kwenye gari akauliza "nani amejaza maji kwenye gari?"
Katoto kakajibu "ni mimi baba"

Baba: Niliposema kaka yako akajaze maji sikumaanisha ndani ya gari, ona viti, kapeti vyote maji tupu.

Lift

Jamaa mmoja alipewa lift. Nje mvua ikaanza kunyesha kwa vile lift alopewa ina vuja ikabidi amuulize mwenye gari "mbona gari yako inavuja kama mti wa maembe?"

Tafuta gari

Mlevi mmoja alilewa chakari, akawa yupo yalipopaki magari. Akawa anatafuta gari lake huku akigusagusa ama kupapasa karibu kila gari asilitambue la kwake.

Jamaa mmoja akamkuta na kumuuliza "unafanya nini?"
Mlevi: Natafuta gari langu.
Jamaa: Sasa ndo utalijuaje kama ndio lako?
Mlevi: Lenyewe ambulance.

Msafiri|Mpokeaji

Jamaa mmoja alikuwa anasafiri toka mkoani kuelekea Dar. Mwenyeji wake akamtumia meseji "unakuja na basi gani?" Msafiri akajibu "nipo kwenye Sumry Air-line" Mpokeaji akajibu "oh, na mimi nasogea sogea ubungo air port kukusubiri."

Mbegu

Jamaa mmoja alienda kwenye party. Baada ya kula keki kwa jinsi ilivyotamu akauliza kwa jamaa wa pembeni yake "aisee hamna mbegu ya hii..."

Raia

Kijana mmoja alikaa chini ya mti akiwaza "ili kujua mie ni raia wa nchi yangu au la! Ntajaribu gombea ubunge."

Mswaki

Mzee mmoja wakati wa kula mezani na familia yake aliuliza "nani kapika mboga leo?"
Mtoto mmoja akajibu "Jesca baba"
Baba akanena "Oh! Hajapiga mswaki"
Mama akauliza "why?"
Baba: Chumvi nyingi.

Monday, August 23, 2010

Moshi

Jamaa mmoja alizoe maisha yake yote kijijini, kupika kwa kutumia kuni nk nk...
Alipofika mjini siku moja akaona gari linatoa moshi ile mbaya akauliza "ile gari inatumia kuni?"

Maongezi|Watoto

Mtoto mmoja akiongea kwenye simu na mtoto mwenzake, "mesikia baba na mama yako wamefunga pingu, sasa unaishi na nani?"

Sms

Mwanamke: Mpenzi wangu mbona hujibu sms zangu jamaani?
Mwanaume: Nasubiri zifike 25 nikurudishie zilizoshika top 10.

Chura

Mtoto mmoja.. "mama.. mama.. Njoo haraka baba anakufa huku amemeza chura njoo haraka."
Mama kufika anakuta baba kalala huku anakoroma.

Bahati nasibu

Jamaa alishinda bahati nasibu.
Mshindi: Nimeshinda milioni 30, nipatie pesa yangu.
Mchezeshaji b.nasibu: Haiwi hivyo, huwa unapatiwa milioni moja leo halafu zingine baada ya wiki mbili.

Mshindi: Mi sielewi, nipeni pesa yangu.
Jamaa mchezeshaji akamjibu vile vile.

Mshindi: Basi nipe elfu moja yangu nliochezeshea.

Pombe bwana

Mwanaume mmoja aliopoa mwanamke huku akiwa amelewa, na huyo mwanamke kalewa pia.

Walipofika nyumbani kwa jamaa, mwanamke akachukua kioo na kujiangalia kisha akasema "huyu kwenye frame ya picha ni mkeo? Mbona anarembua kama kalewa pombe?"

Jamaa akakichukua kioo, kuangalia akajibu "yupi huyu? Frame hii ni mimi enhe chukua uangalie tena..."

Uchoyo

Mwanaume mmoja alipomfumania mkewe akiwa na njemba uchi wa nyama, "...yaani una thubutu kunivunjia heshima yangu? Unaleta mwanaume mpaka chumbani kwangu...."

Mke akajibu, "sasa mume wangu me ntamnyimaje mtu kitu ngali nnacho?"

Shabaha

Mijamaa miwili ilikuwa inatoka kuwinda, mmoja akamwambia mwenzake "aisee naiona nyumba yako tokea hapa nlipo, halafu mkeo yupo na njemba ndani." (kwa darubini ya bunduki).

Mwenye mke akajibu "enh!!? Mshuti mke wangu kichwani, na hilo lijamaa sehemu za siri."
Jamaa akajibu "ooh, hiyo rahisi. Risasi moja tu itapiga sehemu zote hizo."

Talaka

Mama, baba na mtoto walikuwa wamekaa sebuleni. Baba akatoa laptop kwenye begi ili aiwashe. Kabla hajawasha mtoto akadakia "baba.. baba.. Naijua password yako."

Baba kwa mshangao akauliza "umeijuaje we mtoto?"
Mama nae yupo anasikiliza.
Mtoto akadakia "naijua si 'talaka'? Au unabisha?"

Maua...

Mama mmoja alipanda maua yake mazuri nyumbani nje.
Siku moja house girl wake alikuwa anatongozwa na kijana wa mtaani tu. Kuja kuhamaki baada ya kutongozwa yale maua kayavunja vunja...

Sunday, August 22, 2010

Mbu

Mbu mmoja alimuambia mwenzake "sijui nna malaria?"
Mwenzake akamjibu "tatizo lako hutumii neti."

Mbu

Mbu mmoja alimuambia mwenzake "sijui nna malaria?"
Mwenzake akamjibu "tatizo lako hutumii neti."

Sumu ya panya

Mtoto mmoja alimuambia mama yake, "mama leo sijawasikia panya kabisa wakigonga gonga masufuria"

Mama akajibu, "enhe kweli kabisa mwanangu"
Mtoto: Unajua kwa nini mama?
Mama: Enhe kwa nini mwanangu?
Mtoto: Nimewaekea ile sumu ya panya kwenye mboga tuliyokula jioni hii...."

Ukuta

Katika wodi ya wagonjwa wa akili, walichorewa ukuta wakaambiwa waruke waende zao.

Wootee wakakimbilia wakabaki wawili wanawaangalia wenzao. Wakaulizwa na daktari wao.

"Nyie mbona hamfanyi kama wenzenu?"
Wa kwanza akajibu, "ukuta wenyewe si haujakauka bado"
Wa pili akajibu, "ona, ona tayari umeshaweka ufa ukuta wenyewe"

Na mama yake

Mtoto: Mama kwa nini mmeachana na baba?
Mama: Mwanangu hilo sipendi lizungumzia....

Siku chache baadae katoto baada ya pekua pekua akaona taharifa kadhaa kwenye kitambulisho cha mama yake. Siku ya pili akamfuata mama yake.

Mtoto: Mama najua kwa nini umeachana na baba?
Mama: Ee!! Umejuaje?
Mtoto: Kwa sababu una F kwenye Sex nimeona kwenye kitambulisho.

Swali tamu

Mwalimu aliuliza swali wanafunzi wa chekechea wakawa wanajibu.

Mwalimu: Sehemu gani ya mwili mtu akifa inaenda mbinguni?
Mwanafunzi 1: Roho ndio inaenda.
Mwanafunzi 2: Moyo.
Mwanafunzi 3: Miguu.

Mh! Mwalimu alistuka akauliza "enhe kwa nini miguu?"

Mwanafunzi wa 3 akajibu "jana nliona mama kanyoosha miguu juu uku akisema "oh God am coming... Huku baba kamlalia juu asiende"

Saturday, August 21, 2010

Siku ya hukumu

Mchunga alikuwa anahubiri kanisani akasema 'siku ya mwisho (hukumu) watu watalia na kusaga meno ndipo walipoinuka kibogoyo na bubu wakasema sisi tumesevu kwenye hukumu.

Bafu|Singo

Jamaa anajulikana kabisa amepanga chumba single yaana hamna bafu wala choo ndani. Siku moja rafiki yake wakati anamuita huku nje akajibu ''nakuja nipo bafuni naoga kabisa!''

Kuoa

Mtoto mmoja alikua anamuona jirani yao kwa miaka takribani miwili wakiishi na mchumba wake nyumba moja.
Siku moja hao majirani walitangaza nia ya kuoana, mtoto alipozidaka nyepesi hizo akaenda mwambia mama yake, "mama! mama, yule jirani yetu anataka kumuoa mke wake."

Mwizi|Mwalimu|M'sheria

Mwizi, Mwalimu na Mwanasheria wote walikufa ghafla kwenye ajali mbaya.

Walipofika peponi wakaambiwa nako kumejaa ila atakaepatia jibu la swali ndio ataingia...

Mwalimu aliulizwa "ni meli gani ilizama Tanzania?" akajibu MV. Bukoba.
Akaambiwa amepatia aingie.

Mwizi akaulizwa "ni watu wangapi walipoteza maisha kwenye hiyo ajali?" mwizi akajibu 150.
Akaambiwa amepatia na aingie.

Mwanasheria akaambiwa kulingana na jibu alilotoa mwizi "wataje majina?"

Aje...

Askari polisi mmoja akiwapa maagizo askari walio chini yake "Mkamtafute mtuhumiwa aje akiwa HAI au MAiTi aje ajibu Tuhuma zinazomkabili"

Makaburini

Mama mmoja na mwanae wakipita pembezoni mwa makaburi, mama akasoma maandishi kwenye kaburi moja kisha akajisemea kwa masikitiko "maskini alikuwa DAKTARI na MUWAZI tu.

Mtoto nae akasoma kisha akamuuliza mama yake "mama kwanini wamewazika wawili sasa?"

Dharura|Ndege

Rubani alitangaza watu wote wakae vitini ndege imeleta shida wanatakiwa watue kwa dharura.
Pilot akamuliza mhudumu wa ndege "watu wote wamekaa?"
Mhudumu akajibu "ndio kasoro mwanasheria mmoja anapita pita kuchukua biznez cards"

Vekesheni

Jamaa alienda vekeshe na mkewe. Bahati mbaya akafia wakati wapo vekesheni Jerusalem.

Akaambiwa kumsafirisha mpaka nchini mwao ni dola 3000, wakimzika Jerusalem ni dola 300 tu.

Jamaa akakataa kumzika pale pa dola 300 huku akisema "hapo zamani sana alikufa akafufuka baadae, mi sipo tayari mke wangu afufuke."

Kibosile akifa

Boss mmoja hospitalini hoi kitandani, alimuita mwanasheria wake, daktari na mchungaji.
Akawaambia "hapa nna dola elfu90 chini ya mto. Nimeziweka kwenye bahasha dola elfu 30 tatu. Nataka nikifa kabla hawajatupia udongu mzirushie kaburini."

Wakaitikia "sawa, haina shida"

Baada ya mazishi:
Mchungaji: Acha niseme ukweli nimechukua dola elfu10 tu kwa ajili ya ujezi wa kanisa ingine kama marehemu alivyoagiza.

Dokta: Mie nimechukua dola elfu15 tu ingine kama marehemu alivyosema.

Mwanasheria: Mie niliziweka kwenye akaunti yangu, nikaandika cheque na kuiweka kwenye bahasha nkafanya kama marehemu alivyosema...

Za nyuma

Unaikumbuka hii?
Nyoka m1 asked the atha "ivi sisi tuna sumu?" Mwenzake akajibu "ndio, why?" AKAMJIBU "nimejing'ata bahati mbaya!"

Ndio|Hapana

Kwenye mtihani wenye majibu Ndio|Hapana
Msimamizi mmoja alimfuata mwanafunzi wakati anasimamia mtihani akamuuliza "mbona unarusha rusha hiyo sarafu ya sh 100?"
M'funzi: Nahakiki kama majibu nlojaza ni sahii.

Mboga za majani

Mama mwenye nyumba aliporudi akauliza "mbona sebule ipo hivi leo?"
House girl akajibu "nimesahau kupanga vizuri, nilichukua hiyo mboga ndo naipika"
Mama akanena "weewe!! Hayo uliochukua ni urembo sio majani halisi (artificial mimea)

Akon

Unaujue wimbo wa AKON "lonely" basi nausikiliza hapa, AKON anauimba kanyong'onyeaa sijui "swaumu imemkolea?"

Kipindi cha tv

Mtoto mmoja wakati anaangalia kipindi kizuri kwenye televisheni akamuita mama yake "mama... mama njoo haraka uone"

Bahati mbaya mama yake akakosa hiyo sehemu, mwanae akasema "aaahh umecheleewa"

Mama nae akajibu "tv ya chumbani si unajua ipo dakika 4 nyuma itakuwa haijaonyesha ngoja nikaangalizie huko."

Ndoto tatu

Vijana watatu wakisimuliana ndoto ya jana usiku:
Wa 1: Aisee jana nimeota namiliki BMW new model.
Wa 2: Mie ndo funika, nimeota namiliki PPF Tower.
Wa 3: Mie yangu jana si nimeota namiliki wake zenu.

Mke na mume

Mwanamke mmoja alimpigia simu mumewe akiwa mbali nae.
M'ke: Umeamkaje m'me wangu?
M'me: Nimeamka na hang-ova leo mpenzi wangu.
M'ke: (kwa ukali alisema) nilijua tu nikisafiri utamleta tena huyo mwanamke wako.

Toto tundu ii

Mama mmoja wakati anamfokea mwanae mdogo alieharibu jambo alimalizia kwa kumuambia...
"...muone kwanza, sura mfuko wa jeans"
Mtoto akauliza "wa mbele, wa nyuma?"

Toto tundu

Mtoto mmoja alikua anaitwa Happy, na dada wa kazi za ndani nae anaitwa Happy. Sasa siku moja mama yake mtoto akamuambia mwanae Happy amuite dada aje...

Kwa vile alikuwa mbali kidogo yule mtoto ilimbidi aite kwa sauti kubwa kidogo "H.a.p.p.y!... Haaappy..." kituko ni pale alipokua akiita na yeye muitaji anaitika.

Mama yake akamuuliza "sasa mbona unaitika we mwenyewe tena?"
Mtoto akajibu "kwani na mimi si jina langu Happy?"

Friday, August 20, 2010

Mtoto kupotea

Mtoto mmoja alipoteana na dad yake mlimani city. Akakutana na askari akamuambia "nimepoteana na baba yangu namtafuta"

Askari akauliza "huwa anapenda nini haswa?"
Mtoto akajibu "bia na wanawake wenye nyonyo kubwa"

Pampus

Mtoto mmoja wakati anavishwa pampus huku baba wa toto akiwa pembeni.
Alikuwa anaangalia mwanae akivishwa pampus akamuuliza mkewe "hivi hizo kitu (pampus) huwa zina mifuko?"

Mke anapaki

Jamaa alirudi nyumbani akakuta mkewe anapakia nguo kwenye begi lake la safari.

Mume akauliza, "unapaki nguo unaenda wapi mke wangu?"
Mke akajibu, "naenda Daslam, nasikia wanawalipa dola 300 malaya. Bora niende huko kuliko kukupa tu bure."

Mchumba

Katoto kamoja siku moja alimuuliza bibi yake wa miaka 94.
"bibi... kwani we kuna mchumba?"

Bibi akajibu "mjukuu wangu, mchumba wangu ni tv, ndio anaenipa furaha na kuniondolea mawazo"

Sasa siku moja tv ilikuwa inaonyesha chenga chenga... Bibi akawa anaipiga piga/gonga gonga ionyeshe vizuri.

Kidogo mtoto akasikia mlango unagongwa akaenda fungua.
Kumbe alikuwa mchungaji kaja kumuona bibi.

Mchungaji: Hujambo...? Bibi yupo?
Mtoto: Yupo chumbani anampet pet mchumba wake.

Kupima damu

Mtoto mmoja alimkuta rafiki yake hospitali analia, akamuuliza "unalia nini?"
Dogo mwenzake akajibu "nimekuja kupima damu wamenikata kidole.''

Rafiki yake nae akaanza kulia. Mwenzake aliekuja kupima damu akamuuliza "unalia nini sasa na wewe?"
Mwenzake akajibu "mi nimekuja kupima mkojo"

Mgonjwa kwa dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja unibadilishie dawa.
Dokta: Dawa? Kivipi? Sijaelewa.
Mgonjwa: Mi naumwa kichwa ila dawa uliyonipa mbona nikimeza inaenda tumboni badala ya kichwani?

Naomba maji

Mtoto mmoja alipoenda kulala mara ghafla akaita... ''baabaa... naomba maji ya kunywa"

Baba akajibu, "lala bwana utakojoa kitandani."

Dakika chache baadae mtoto akasema vile vile tena. Baba nae akajibu vilele.

Awamu ya tatu mtoto akaomba tena na baba akajibu "sasa ntakuja na kiboko nikuchape, mbona hunielewi"
Mtoto akajibu "baba ukija na hiyo fimbo njoo na maji ya kunywa"

Kuchora mbwa

Kwenye kipindi cha sanaa wanafunzi waliambiwa wachore mbwa kafungwa kamba...

Baada ya muda mtoto mmoja akawa anatoka nje. Mwalimu akamuuliza "wapi unaenda?"
Mwanafunzi akajibu "namtafuta mbwa imebaki kamba tu nliyoichora, itakuwa amekata"

Bunduki

Jamaa alinunua bunduki, majaribio akam-shoot mwanae.
Alipokufa akasema ''aanha kumbe sio ya kichina"

Hii kutoka kwa...

Kichekesho hiki nlikisoma siku nyingi toka kwa cartoonist fadhil (jina la pili limenitoka)

Jamaa alienda kwa daktari wake alipofika akamuuliza dokta wake ''dokta! Hivi ile dawa ya kupaka uliniambia ninywe mara ngapi?"

Kuibiwa simu

Jamaa mmoja aliibiwa simu, sasa wakati anabishana ''simu yangu simu yangu.." akasema "kama unabisha tukapime DNA.

Thursday, August 19, 2010

Kupata mtoto

Katoto kamoja ka kike kalinyoosha mkono darasani kakauliza;
Mtoto: Mwalimu, bibi yangu anaweza kupata mtoto?
Mwalimu: Hapana ni mzee sana, hawezi.

Mtoto: Mama yangu je?
Mwalimu: Anaweza kupata, lakina na yeye amefikia uzee pia.
Mtoto: Mimi je?
Mwalimu: Ee! Hapana huwezi bado mdogo sana kupata mtoto.

Kavulana kamoja kakadakia na kusema mbele ya darasa zima ''unaonaa? Mi nlikuambia usiogope''

Nikifa

Jamaa alitishiwa kisu wakati wanataniana na rafiki yake, alietishiwa kisu wakati wa utani huo akasema ''weuwe, ooh, shauri yako. Nikifa utanitambua.''

Maelekezo

Jamaa akimuelekeza dereva aliekuwa nae vijijini wakati wa kuvuka daraja la kienyeji la magogo.

Kilichokua kinatakiwa kufanyika ni amuelekeze dereva akanyage kulenga magogo ili isije ikatelezea mtoni.

Mwongozaji akawa anamuelekeza ''njoo njoo njoo..." huku eti mkono mmoja kajiziba uso kwa uoga wa kushuhudia.

True story

Kuna siku wakati wa mizunguko ya ukaguzi vijijini tulifika kijiji kimoja, wananchi wawili watatu katika nyumba moja walitoka nje haraka haraka wakidhani askari. Kisa cha yote kwenye kijumba hiko kinauza podbe haramu ya Gongo.

Wednesday, August 18, 2010

Ujiko

Kijana mmoja wa makamo aliopoa mrembo. Sasa wakati wapo evening walk alipoona gari aina ya prado inakuja kwa mbele akajirusha mbio kwenye kichaka.

Yule mrembo akamshangaa na kujiuliza. Akamuuliza ''vipi?''
Kijana akajibu, ''umeiona ile prado?''
Dada akajibu ''ndio'' kaka akaendelea ''ni ya nyumbani ile sijui baba yule?''

Maongezi yalipoisha jamaa akamuambia yule mrembo ''samahani nisaidie kutoka miba zimezidi nikamata''

Kiti

Baba mmoja alipata wageni kwake nyumbani. Akamtuma mwanae aongeze viti pale sebuleni.

Mtoto kwa vile ilikuwa hamna namna tena ya kupata kiti kimoja cha ziada, akaenda kung'oa kiti kimoja toka kwenye gari ya baba yake.

Alipoulizwa na baba yake amekitoa wapi akajibu ''nimekiazima kwa jirani baba''
Baba akajibu ''ooh kumbe, kizuri, usikirudishe tutamuambia kiliibiwa.''

Kesho yake baba kutoka nje akaona gari yake haina kiti akaanza kufoka, mtoto akadakia "baba ni hivi jirani aliona nachelewa kurudisha akachukua cha gari yako, sasa wewe mkomeshe chukua hiki ufunge kwako."

Simenti

Jamaa mmoja alijikuta anakanyaka ciment. Na alikuwa amelewa. Alipofika nyumbani akalala hivyo hivyo na viatu.

Asubuhi alipoamka akakuta mwanae anamwagia maji miguuni ''wewe unafanya nini?'' aliuliza kwa ukali.

Mtoto akajibu ''mama kaniambia nimwagie maji ciment ishike vyema usiende kulewa.''

Nusu kwa nusu

Bibi na babu walienda best bite, wakaagiza burger moja babu akaanza ikata nusu ampatie bibi.

Kijana mmoja alikuwa akiwaangalia akawauliza "niwanunulie ingine?"
Babu akajibu ''hapana hii tutagawana nusu kwa nusu.''

Kijana akamuuliza bibi "bibi na wewe utaanza ila?''
Bibi akajibu ''nasubiri kwanza, sasa hivi ni zamu yake kutumia meno yetu.''
(sijui ya bandia...?)

Tuesday, August 17, 2010

Simu kwenye basi

Mtoto mmoja wa makamo siku moja mama yake alimnunulia chupi inafanana kabisa na baba yake.
Sasa siku moja wakati yupo kwenye daladala na mama yake mara simu ikaita ya mama yake.

Mama kabla hajaipokea akamuambia mwanae ''baba huyo anapiga simu''
yule mtoto kabla hata mama yake hajaipokoea kwa sauti ya kusikika mote kwenye daladala akasema ''mama kisha muulize kama amejisahau amevaa chupi yangu, mie sijaiona leo.''

Kijiti

Jamaa alipomaliza pata mlo kwenye retaurant moja na mrembo wake akamuuliza mrembo wake hivi ''nikuagizie toothpick?''
Yule mrembo akamjibu huku akiona ona aibu ''enhe! Asante nimeshiba sana''

Mwalimu darasani

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake...
''mama, kwani mwalimu haruhusiwi kuvaa chupi?''
Mama kwa shauku na mshangao akauliza ''...mh! kulikoni mwanangu umesikia wapi hiyo?...''

Mtoto akajibu ''mi nashangaa mama, labda atakua anasahau... Si mwalimu wetu wa darasa ndio havaagi''
Mama akauliza ''we umejuaje?''

Mtoto: Si namtegesheaga kioo chini ya miguu yake.

Viatu vya ngozi

Mtoto mmoja alikutywa na mama yake akiwa na viatu vya ngozi... Mama yake akamuuliza ''Jasmine mbona umekaa chini?''

Jasmine akajibu ''ninaviandaa viatu vyangu''
Mama: Ooh umekua mtoto mzuri siku hizi unajua mpaka kupaka kiwi viatu? Wow!
Jasmine: Mama!! Nikipaka kiwi viatu si vitaharibika?

Mama akajibu ''haapaana mwanangu kwani vipi?''
Jasmine: Me mevipaka losheni kwani si vya ngozi na vyenyewe? Kiwi itaharibuu...

Swaumu

Jamaa alimuona mwenzake ni kama anatafuta kitu alichokipoteza akamuuliza ''mwenzangu vipi mbona kama hueleweki umepoteza kitu nini?''

Ndipo jamaa akamjibu ''ndio, nimeshangaa njaa imeacha kuuma ghafla nlipofika maeneo haya, hivyo laziima ntakua nimeidondosha hapa swaumu yangu''

Babashop

Mahause girl wameenda town wakawa wanaona kila salon imeandikwa barber shop. Wakatiaje, huyo baba shop tajiri ana maduka mji mzima.

Monday, August 16, 2010

Uwanjani

Siku moja wakati tupo uwanjani twacheza mpira wa kikapu, jamaa yetu mmoja ana maneno mengi sana.

Moja kati ya wachezaji akapewa pasi ikamponyoka mikononi... Yule maneno mengi akasema kwa sauti ''wee viiipi weewe unashindwa daka mpira? Unaogea kopo nini?''

Siku moja nyingine akaja uwanjani akiwa amevaa fulana nyeupe, mwisho wa siku baada ya kucheza kikapu akagundua fulana yake imechafuka maeneo ya mabegani akauliza kwa sauti ''nani kanikanyaga jamani?''

Moto

Jamaa mmoja alipoingia nyumba moja na kuona moto kwa ajili ya kutoa joto sebuleni (fire place).
Akaanza kwa kusema ''moto moto... moto..." huku akitafuta ndoo ya maji akauzime.

Lift

Jamaa mmoja aliomba lifti, ikawa hivi:

Jamaa: Naomba lift ndugu yangu.
Dereva: Utapakia wapi sasa ndugu yangu?
Jamaa: Hata hapo mbele.
Dereva: Hapa mbele hairuhusiwi abiria.

Jamaa: Basi hata huku nyuma.
Dereva: We huoni kama hili ni karandinga (lori la kubebea mahabusu/wafungwa).
Jamaa: Sasa mbona hao jamaa nyuma umewapa lift (wafungwa/mahabusu)?

Sunday, August 15, 2010

Kumtembelea mchumba

Kijana mmoja alienda mtembelea msichana wake anaesoma nae chuo kimoja. Jamaa alipofika nyumba husika akawa anataka kuishia nje, mzee mwenye nyumba akamsihi mtoto wake huyo mgeni aingie tu ndani.

Jamaa alipoingia si akakuta mzee anasafisha bunduki huku akiongea ''kijana... mambo ya shule huko huko shule... mmemaliza assignment zenu?''

Nyoka

''Dokta nadhani nna matatizo ya kuona siku hizi'' nyoka akimuambia daktari.
Daktari akamuambia ''ntakusaidia.''

Baada ya siku kadhaa nyoka akarudi tena, dokta akamuuliza ''vipi ile miwani niliyokupatia haijakusaidia?''

Nyoka akajibu ''dokta nimegundua kuwa kumbe kwa muda wa miaka mitatu nilikuwa nikiishi chini ya maji''

Mugongo mugongo

Baba mmoja na mama wakati wanajiandaa kufanya mapenzi mtoto wao mdogo wa miaka miwili na nusu aka-a-mka ''baba na mimi naomba nipande mgongonu'' mtoto aliomba.

Baba akawa anakataa, mama akasema ''muache tu hamna shida'' basi mtoto akapanda.
Wakati wanashughulika mama akawa amezidiwa na utamu kweli kweli mtoto akasema ''baba jishikilia jana kidogo tuanguke wakati wakati nimepanda mgongoni mwa yule mleta maziwa''

Saturday, August 14, 2010

Msibani

Mtoto mmoja alishuhudia kwa mara ya kwanza msiba mtu akizikwa akamuuliza mama yake ''mama... mama... Sasa nani atakua anambadilisha nguo huyo mtu wanaemfukia kwenye sanduku la mbao? Si zitachafuka haraka?''

Nguo ya mapenzi

Mwanamke mmoja alikuwa uchi wa nyama bibi yake akamuuliza pale sebuleni, ''mbona hivyo kulikoni?''
Mwanamke akajibu ''hii ni nguo ya mapenzi namsubiri muwe wangu.''

Baadae mume aliporudi akamkuta bibi yake mkewe nae hajavaa nguo ''bibi vipi leo una nini?"
Bibi akajibu, ''nimevaa nguo ya mapenzi namsubiri babu yenu''

Mume wa yule mwanamke akamjibu ''oh kumbe, sasa mbona hujainyoosha na pasi?"
(makunyanzi mwilini)

Biashara

Kaka mmoja akiitangaza biashara yake mbele ya mteja, ''kaka nauza vyombo vya plastic, vya udongo na miswaki used''

Kuchimba dawa

Mtoto mmoja alikuwa na anko ake wakitoka kijiji kimoja kwenda kingine, mara yule mtoto akabanwa na haja kubwa akamuomba anko yake amsubiri aingie kuchimba dawa.

Wakati yupo upande wa pili wa kichaka akamuuliza anko yake ''anko nachimba shimo kabla au baada?''

Friday, August 13, 2010

Mwalimu wa biology

Mwalimu mmoja wa baiolijia akifundisha darasani lile somo la viungo vya uzazi, akauliza "Kuna ambae hajaelewa mpaka nilipofikia sasa?"
Mwanafunzi mmoja akanyoosha kidole na kuuliza "Mwalimu mi umeniacha kidogo, labda ungevua suruali ukatuonyesha ndio tutaelewa vyema kwa mifano hai"

Bwenini

Mkufunzi mmoja wa chuo akiwaambia wanafunzi wa mwaka wa kwanza masharti "Bweni la wanaume ni la wanaume tu na la wanawake ni la wanawake tu" huku akiendelea kuongea "ukifumwa mara ya kwanza utalipa faini ya shilingi elfu 20, mara ya pili elfu 60, mara ya tatu laki mona na 80"

Mwanafunzi mmoja akauliza "Je kwa semester (Muhula) nzima ni shilingi ngapi?"

Wakili na Daktari

Mzee mmoja alipoona ana masaa 24 kabla hajafa pale hospitali. Akaagiza dokta na Mwanasheria wake waje.

Dokta akauliza ''hapa nafanya nini?'' mzee akajibu ''nothing, we simama tu hapo hapo.''

Mwanasheria nae akauliza ''hapa nafanya nini?'' mzee akajibu ''nothing, we simama tu hapo hapo.''

Baadae wakauliza tena pale waliposimama mzee akawajibu ''Kristo alikufa na wezi wawili, so na mimi nafanya vivyo hivyo''

Kuachana

Mwanamke mmoja alipovunja ukimya akamuambia mpenzi wake waachane. Mpenzi wake kwa vile alikuwa mji mwingine kabisa, akatuma picha 13 na kumuambia ''sikumbuki vizuri we ni yupi, chukua picha yako zingine nirudishie''

Thursday, August 12, 2010

Kabla ya kufa

Mume: Mke wangu nikifa utaolewa tena?
Mke: Ndio, itategemea.
Mume: Utampa gari yangu aendeshe.
Mke: Mh! Nadhani.
Mume: Utamuacha akae kwenye kiti changu sebuleni?
Mke: Labda.
Mume: Utamuacha avae suti yangu nzuri?
Mke: No, ye ni mfupi.

Wodini

Jamaa mmoja aliamka akiwa kitandani wodini baada ya kupata ajali mbaya. Akauliza ''dokta... dokta... Mbona siusikii kabisa mkono wangu wala mguu..."

Dokta akajibu, 'huwezi isikia kwa sababu nimeikata yote'

Huzurio kwa dokta

Mwanamke mmoja alienda kwa dokta kufanya check-up. Kwa vile alikuwa anaona aibu akamuambia dokta azime taa ili avue nguo. Alipomaliza akamuuliza ''dokta niweke wapi nguo zangu?''

Dokta akajibu ''weka kwa hapa karibu na zangu''

Ajali-pikipiki

Dereva mmoja wa pikipiki alivaa koti nyuma mbele, akapata ajali.

Wasamaria walipokuja kumsaidia wakajua shingo imegeuka wakaanza kuigeuza kugeukia usawa wa koti. Kumbe ndio kifo.

Wednesday, August 11, 2010

Kuibiwa

Mzee mmoja na mkewe wakati wanatoka supermarket na mkewe walikuta gari yao haipo walipoipaki. Wakaenda polisi kutoa taharifa.
Polisi akashauri waje nae sehemu ya tukia kutafuta ushahidi.

Wakalikuta gari lao limerudi na kuna kibahasha kimewekwa kwenye wiper kimeandikwa hivi ''samahani nilichukua gari lako, mke wangu alishikwa na uchungu nkaamua kumkimbiza hospitalini. Pole kwa usumbufu. Chukua tiketi mbili hizo mje kwenye tamasha kama zawadi yangu''

Siku walipoenda kwenye tamasha kurudi wakakuta nyumba imeibiwa vile vitu vya thamani vyooote na kukuta barua imeandikwa ''nina shida ya ada ya mwanangu hivyo nimekuja tena.....''

Maji ya kunywa

Jamaa mmoja aliomba majiya kunywa, alipopewa akanywa. Alipomaliza akauliza maji yako matamu kweli ya umeyahifadhi kwenye mtungi nini?

Mwenyeji wake akajibu, ''hapana atii, haya ya mferejini''
Jamaa akashtuka ''mferejini?''
Yule jamaa akamjibu ''yakhe si bomba la maji kule Zanzibar twaita mfereji atii.
Ndipo jamaa akasema ''aanhaa kumbe, duh!''

Ajali

Mtoto mmoja alimuambia mama yake alipopigiwa simu: ''hujambo mwanangu?''
Mtoto akajibu ''sijambo mama ila nimepata ajali, na polisi wananifukuza hivi nnavyoongea''

Mama akashtuka na kumuuliza vizuri, ''eenh!! Unasema??''
Mtoto akaendelea kujibu, ''ndio hapa nyumbani kwenye video game''

Tuesday, August 10, 2010

Ndoto isiyoeleweka

Jamaa: Dokta nna tatizo, nikilala nasikia kitu uvunguni mwa kitanda. Nikichungulia nasikia juu ya kitanda.
Dokta: Noo mara mbili kwa wiki ofisini kwangu ntakusaidia kulitatua.

Jamaa: Itakuwa shingapi kwa kila nikija?
Dokta: Itakuwa elfu 30 tu.

siku chache baadae walipokutana mtaani.
Dokta: Mbona hukuja tena?
Jamaa: Nilipata mtu alinisaidia kumaliza tatizo lile.
Dokta: Alikusaidiaje sasa?
Jamaa: Aling'oa miguu yote ya kitanda kwa shilingi elfu 10 tu.

Monday, August 9, 2010

Nyama ya mbuzi

Kwenye sherehe ndogo nyumba fulani waliandaa party. Mzee mwenye nyumba akaagiza wachinje mbuzi.

Mwisho wa siku aliporudi nyumbani alipopita zizini akaona jambo... Akaanza kubwata alipoingia sebuleni, ''...mmeniudhi sana... Mi mesema mchinje mbuzi mmoja mmechinja wawili..." alifoka akafoka.

Mke: Mume wangu jamani ni mbuzi mmoja tu kachinjwa...
Mume: HAPANA SI KWELI...
Mke: Si kweli kivipi?
Mume: Si mmemchinja yule mbuzi wangu mjamzito...

Ajali na msaada

Gari moja lilipata ajali, mwanamke mmoja akawa wa kwanza kufika kutoa msaada.
Hata kabla hajaanza akatokea jamaa na kumsukuma yule mwanamke na kusema "pisha dada, nimesomea kutoa first aid.''

Yule mwanamke baada kama ya dakika 3 nae akanena ''ukifika muda wa kumuhitaji daktari nipo hapa''

Kwa mshauri

Mume na mke walienda kwa mshauri kuhusiana na matatizo ya ndoa yao. Walipofika, mwanamke akaanza elezea kwa muda wa dakika 15 kuhusu kero azipatazo.

Alipomaliza, mshauri akanyanyuka kwenye kiti akaenda akamshika yule mwanamke kwa kuonye anamjali, akambusu hapa na pale. Yule mwanamke akabaki kimya bila la kuongea.

Mume akauliza, ''umewezaje kumnyamazisha?''
Mshauri akajibu "unatakiwa umfanyie hivyo kila siku."
Mume akajibu "basi ntakua namleta kwako"

Sunday, August 8, 2010

Mitumbani

Kuna kaka mmoja alienda nunua nguo za mtumba akampatie mpenzi wake zawadi. Aliposagura sagura akakutana na kisketi kifupi.

Akauliza, ''khaa hii sketi mbona fupi sana...?
Akajibiwa na muuza mitumba ''aanha? Hicho si cha kuzimia tv tu nyumbani...''

MC

Lectural wetu alikuwa akikamata paper mbili mmedeseana (mmegezeana/cheat paper) alikuwa anaomba mje kuidentify the original..

Mtihani upi...?

Wakati nipo chuo siku moja lecture wetu wakati anasahisha mitihani, bahati nzuri/mbaya akakuta mitihani miwili inafanana majibu yake.

Akawaita wote wawili wenye mitihani husika, walipofika akawauliza ''upi original?''

Bar

Jamaa mmoja aliingia bar moja uko majuu. Alipofika akaagiza pale kaunta kichwaji kwenye glasi ndogo akanywa.

Alipomaliza akaambiwa bei yake ni sarafu (coin).
Kwa vile kaunta ni kubwa akaipiga na kidole sarafu moja mpaka mwisho wa kaunta upande wa kushoto, na nyingine upande wa kulia na ya mwisho akaiweka katikati ya kaunta (viti virefu). Kisha akatimua.

Mhudumu akamuangaliaa asijue la kumfanya.

Siku ya pili jamaa akaja tena akafanya vile vie.
Siku ya tatu pia... Akatoa noti wakati wa malipo na chenji inatakiwa zirudi Sarafu mbili.

Mhudumu akachukua sarafu ya kwanza akaiweka mwisho kabisa mwa kauta kushoto na ingine kulia. Ili tu ampe huyo jamaa usumbufu aliompatia siku mbili zilizopita.

Yule mteja alipoona vile akato sarafu na kuiweka katikati ya kaunta na kumuambia ''nipe glasi nyingine.''

Biashara

Jamaa mmoja nje ya duka lake aliandika tangazo dogo kwenye kibao. ''Mali mpya imeingia, Mali mpya imeingia... Wale wenye matatizo ya kutotabasamu wakiwa barabarani. Sasa tumewaletea tabasamu la kila aina toka China. Bei yetu ni nzuri. Karibuni sana.

Saturday, August 7, 2010

Mtoto ali...

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake, ''mama kuna siku chache kabla ya kunizaa nilisikia mdundo wa mziki mkubwa, ulikuwa umeenda disko au kwenye harusi?''

Friday, August 6, 2010

Mlevi mlemavu

Mlevi mmoja alikuwa hana mikono aleinda Bar, kwa vile hakuwa na mikono yote miwili alikua akimuomba mhudumu amsaidie kumnywesha bia, kumfuta mdomo na kumtolea pesa ya kichwaji toka mifukoni mwa huyu asie na mikono.

Ikafika kipindi jamaa asiye na mikono akamuuliza mhudumu ''samahani msalani/chooni ni wapi hapa bar?''

Mhudumu akajibu, ''sisi hatuna choo we toka nje halafu kuna jengo hili ilipo hii bar la kwanza, la pili halafu utakuta choo.''

Basi mpaka ubungo

Abiria mmoja alipanda basi toka Arusha mpaka Dar, alipofika ubungo akamuambia konda hivi: ''konda tukifika ubungo naomba unishushe mule ubongo ndani stand ya mabasi ya mkoa''

Maisha ya alfajiri Dsm

Jamaa mmoja kwa vile anaishi mbali na katikati ya mji wa Dar es Salaam, ilikuwa inambidi kuamka saa 10 usiku ili saa 11 awe barabarani, na kwa sababu jiji la Dar lina foleni za magari kila kona, anajikuta nyumbani anarudi saa 5 usiku.

Siku moja aliporudi alipoingia sebuleni mwanae kwa vile hamuonagi mara kwa mara akasema hivi... ''mama... Mama... Kuna mgeni sebuleni.''

Pa kushushwa

Jamaa mmoja alipanda basi toka mbeya, alipokaribia karibia ubungo akiwa maeneo ya kimara akanyanyuka kwenye kiti chake na kwenda mpaka kwa dereva, kisha akamuambia ''dereva! Samahani unaweza ukanishusha kwanza hapo sinza halafu uje zako ubungo?''

Sinema kwenye basi

Abiria mmoja wakati yupo kwenye basi toka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.
Aliangalia sinema waliyoekewa abiria wote alifika hatua akamsogelea dereva kwa vile alikuwa karibu nae akamuuliza.

''dereva, tangu tumetoka Mwanza na bado tupo njiani. Wenzio twaangalia sinema... Mbona wewe huangalii?''

Ajali

Marafiki wawili wa kiume walipata ajali, bahati nzuri hawakuumia kama ilivyo kwa gari.

Mmoja akamuambia mwenzake, ''kabla hatujalaumiana kosa la nani ngoja tushereke tumepona''
Mwenzake akajibu, ''kweli kabisa tufanye hivyo.''

Wakachukua chupa ya pombe kali kwenye gari haikuvunjika wa kwanza akanywa kisha akaifuta chupa na kumpa mwenzake nae anywe.."

Mwenzake akamjibu ''hapana ngoja kwanza mpaka trafiki polisi aje...''

Ajali

Marafiki wawili wa kiume walipata ajali, bahati nzuri hawakuumia kama ilivyo kwa gari.

Mmoja akamuambia mwenzake, ''kabla hatujalaumiana kosa la nani ngoja tushereke tumepona''
Mwenzake akajibu, ''kweli kabisa tufanye hivyo.''

Wakachukua chupa ya pombe kali kwenye gari haikuvunjika wa kwanza akanywa kisha akaifuta chupa na kumpa mwenzake nae anywe.."

Mwenzake akamjibu ''hapana ngoja kwanza mpaka trafiki polisi aje...''

Njia nyembamba

Dereva mmoja wa lori akiwa barabari akiendesha. Mbele akaona alama ya barabarani ikionyesha njia nyembamba mbele, na daraja dogo.

Alipokuja kuhamaki tayari alikuwa ameshakwama. Askari alipokuja akamuuliza ''we hukuona alama za barabarani?''

Jamaa akajibu, ''niliiona ila nimeishiwa tu mafuta ndio maana nipo hapa.''

Thursday, August 5, 2010

Kwenye mtihani

Mwanafunzi mmoja baada ya mtihani aliitwa na mwalimu wa darasa. ''wewe kwanini umefanya mitihani miwili?''

Mwanafunzi akajibu, ''hapana mwalimu mi nimefanya mmoja''
kisha mwanafunzi aliendelea kuelezea ''mwanafunzi mmoja alikuwa ananigezea labda amegezea mpaka jina langu.''

Jina...

Wanafunzi kwenye mtihani walipoambiwa aanze kufanya mti mmoja akamuita mwalimu msimamizi wa mtihani na kumuuliza, ''Mwalimu samahani, nimesahau jina langu.. Hivi naitwa nani vile?

Wednesday, August 4, 2010

Kwenda msalani

''naomba kwenda msalani...'' aliwaomba enzake aliokua amekaa nao.
Baada ya muda mfupi sana akarudi ''wenzake wakamuuliza "vipi mbona umerudi fasta hivyo? Au chooni kuna mtu?''

Jamaa akajibu ''nimesahau kikojoleo changu hamjakiona hapa?''

Mwendo wa kasi

Siku moja jamaa mmoja wakati anamsimulia jambo mwenzake, ghafla ikapita gari spidi kweli kweli.

Jamaa aliekimsimulia jambo mwenzake akasema ''khaa, ile gari ikipata ajali hata mponda majiko hatohitaji lile body la gari.''

Tuesday, August 3, 2010

Chupi ya chuma

Mwanaume mmoja alimchongea kufuli ya chupi ya chuma. Ili akienda masomoni amkabidhi rafiki yake awe mlinzi...

Siku ilipofika akampa rafiki yake kipenzi akamuambia aitunze mpaka atakaporudi.

Jamaa akawa anamkimbilia mwenye mke mda mfupi baadae... Akaulizwa... ''vipi kuna tatizo?''
Aliepewa fungua akajibu ''samahani umenipa ufunguo sio wenyewe.''

Kama fumanizi.

Mwanaume mmoja akiongea ''nilimuandikia mke wangu email kuwa ntarudi siku moja kabla, nimefika nyumbani nimemkuta na mwanaume best yangu kitandani.''

Rafiki yake akamjibu, ''labda hakuiona email.''

Majaribio...

Jamaa mmoja alitengeneza sumu. Sasa akawa anatafuta pa kuijaribia. Akaenda kwa mbwa wake na kumuekea aionje kama ni kali au la...
Mbwa wake akamjibu ''we vipi? Mi naoa mwezi ujao allah.''

Rangi ya Harusi

Mtoto mmoja aihudhuria harusi kwa mara ya kwanza, akauliza "mama kwanini bi. harusi amevaa rangi nyeupe?" Mama yake akamjibu na kumuambia "rangi nyeupe ni rangi ya furaha na leo ni siku yake ya furaha"

Mtoto akakaa kimya kwa muda na kuuliza tena "Mbona bwana harusi kavaa rangi nyeusi?"

Sumu ya nyoka

Jamaa mmoja aligongwa na nyoka. Kwa vile palikuwa mbali kidogo na hospitali. Akachukua hatua ya kwenda uku anakimbia.
Alipofika hospitali akakuta dokta anazalisha.

"siwezi kuacha hii kazi kwanza. Fanya hivi, nenda kakate sehemu husika alama ya x halafu inyonye sumu yote itoke.'' Dokta alimuambia.

Jamaa mbio mbia mpaka eneo la tukio, alipofika yule mwenzake akuliza ''dokta amesemaje?''
Jamaa alieenda hospitali akamjibu, ''dokta kasema unakufa tu.''

Hewani

Kwenye ndege moja abiria wakiwemo iliruka na baadae rubani akawa anatangaza kuhusu hali ya hewa ilivyo njema nk nk. Baada ya kutangaza akasahau kuiweka off mic aliyokiitumia na kufanya maongezi yao wao ma-pilot kusikika kwa abiria wote ndegeni.

Maongezi yao yallikuwa hivi "aisee ingawa ni one hour tangu tumeacha ardhi nimegundua kuwa geji ipo karibu na emptyi ilikuwa full"
Mwenzake akamjibu: "si nilisahau kufunga mfuniko wa tank la mafuta baada ya kupiga chakachua (kuiba mafuta ya deal).
"Sasa tunafanyaje?" wa kwanza aliuliza. Wa pili akajibu "Ngoja tuwaulize abiria kama kuna mtu ana mafuta ya akiba?"

Ngo-ngo-ngo

Jamaa mmoja alisikia mlango unagongwa...
Alipoenda kufungua akakuta panya mlangoni. Akamchukua na kumtupia mbali.
Wiki moja baadae akasikia mlango unagongwa. Akaenda fungua akakuta panya tena. Yule panya akamuuliza ''za tangu siku ile?''

Ahera

Jamaa alikufa akaenda ahera, huko akakutana na shetani, akamuambia "huku kuna vyumba vitatu, unatakiwa kuchagua kimoja ndio kitakuwa unaishi humo"
Jamaa akakubali na kwenda:

Chumba cha kwanza: Akakuta watu wamelala juu ya kitanda cha miba. Akasema "hapana ngoja niangalia chumba kingine"
Chumba cha pili: Akakuta watu wanaogelea kwenye maji machafu. Jamaa akakataa tena.
Chumba cha tatu: Akakuta watu wamekaa wanapata kahawa. Akasema "hiki ndio kinanifaa" akaingia.

Baada ya dakika chache akaja mtu na kuwa tangazia "haya mapumziko ya kahawa yameisha "kila mtu arudi kwenye kiti chake nyoka mmoja mmoja anapita kuwagonga"

Monday, August 2, 2010

Pingu

Mtoto mmoja wa miaka mitano siku ya harusi ya wazazi wake aliposikia neno hili ''...pingu za maisha...''

Siku chache kabla ya harusi akamuuliza mama yake, "mama we na baba nnataka funga pingu za maisha?"
Mama yake akajibu ndio.
Mtoto akaendelea, "sasa mi ntabaki na nani mkifungwa pingu?''

Siku ya mtihani

Mwanafunzi mmoja baada ya zile dakika tano za mwanzo za mtihani, baada ya kuona hali ishakuwa tete akamuambia msimamizi huku akimnong'oneza ''samahani nimesahau ki-boom changu bwenini, naomba kwenda mara moja.''

Mwanafunzi na mwalimu

Mwalimu mmoja wakati akifundisha darasani alimuona mwanafunzi mmoja amesimama akamuuliza, ''wewe una matatizo gani? Mbona umesimama?''

Mwanafunzi akajibu, ''nimeona umesimama peke yako mda wote nakusaidia...''