Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, September 29, 2010

Mende

Kuna jamaa mmoja alienda kula kwa mama ntilie, kumega tu tonge la kwanza akakuta mende maongezi yao yakawa hivi:
Jamaa: Ebo nimekula mende kwenye chakula changu.
Mama ntilie: usijali, tutakutoza tu pesa ya chakula, huyo mende ni bure

Saturday, September 25, 2010

Eskot

Jamaa alienda kuomba escort ya polisi. Akaulizwa "umebeba billion ngapi au umetishiwa life?"
Akajibu "No napita na kitimoto msikitini".

Wednesday, September 22, 2010

Talaka

Mwanaume: Rafiki yangu mi nataka mpatia mke wangu talaka.
Rafiki: Kwa nini tena?
Mwanaume: Kila nkirudi nyumbani nakuta kaficha mwanaume kwenye kabati la nguo.
Rafiki: Oh! Hiyo mbaya sana.
Mwanaume: Yaani nakosa nafasi ya kutundika nguo zangu kabisa.

Kwenda ulaya

Mtoto: Mama mi niliwaomba tangu mdogo kwenda ulaya.
Mama: Usijali mwanangu ngoja ngoja kidogo.
Mtoto: Ningoje mpaka lini? Sa ivi tangu mdogo ningekua nimeshakaribia kwa kutembea kwa mguu.

Tuesday, September 21, 2010

Kichekesho

Mtoto akimuambia mama yake, "mama nikusimulie kichekesho ucheke?
Mama: Ndio mwanangu nisimulie nasikiliza.
Mtoto: Haya anza kucheka kwanza.

Airport

Rubani mmoja wa ndege alipotua ndege na kumuuliza mwenzake, "leo tumetua kiwanja gani mbona tambarare kubwa na hata nyasi hamna...?"

Rubani wa pili akamjibu, "kwa sababu tumetua juu ya bahari."

Airport

Rubani mmoja wa ndege alipotua ndege na kumuuliza mwenzake, "leo tumetua kiwanja gani mbona tambarare kubwa na hata nyasi hamna...?"

Rubani wa pili akamjibu, "kwa sababu tumetua juu ya bahari."

Picha ya thamani

Wakili mmoja alimfuata kingunge mmoja na kumuambia.
Wakili: Mzee nna habari nzuri na mbaya za kukupa.
Kingunge: Oh! Okey, anza na nzuri.
Wakili: Mke wako amepata picha yenye thamani ya milioni 10.
Kingunge: Oh! Safi sana. So nini tatizo?
Wakili: Ni picha yako upo na secretary.

Mchumba

Kijana mmoja alienda soma nje miaka mitano. Akaoa huko huko, siku aliyorudi Tanzania akaja na mkewe akamtambulishe kwa wazazi wake.

Siku aliyoenda alikuwa na rafiki zake watatu, wawili kati yao wasichana.
Akamuambia mama yake ajaribu mtambua yupi ndio mkwewe.

Mama akamnyooshe mlengwa.
Jamaa akauliza, "hee! Mama umemjuaje kama ndie huyu?"
Mama: Nimechukia tangu nlipomuona.

Adhabu!

Mtoto wa miaka mitano siku moja alimuona mama yake akiwa na baba yake kwenye majamboz, mtoto akamwambia mama yake "aanha! Kumbe mimi unaniadhibugi kwa kukinyonya kidole gumba changu."

Ngazi

Mama na mtoto wakipandisha ngazi kwenda ghorofa ya kumi kwenye apartment yao, lift ilikuwa mbovu siku hiyo.
Mtoto: Mama nikuambie kitu...
Mama: Embu nyamaza.
Mara ya pili ivoivo akajibu.
Ghorofa ya 10 huku wakiwa hoi kwa kuhema.
Mama: Enhe ulikuwa unasemaje?
Mtoto: Nlikua nataka kukuambia nimesahau ufunguo kwenye gari wa mlango.

Ujauzito

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake mjamzito "mama... mama... Asa we unafanyaje huyo mtoto tumboni akianza kulia?"

Kuhesabu.

Watoto wakihesabu mpaka kwa kidhungu mpaka 10.
Wa 1: Akishia 4.
Wa 2: Akafikia 6.
Wa 3: Akahesabu mpaka 10. Alipoona watu wanamuangalia kwa uwezo wake mzuri akaendelea ...prince, queen, king... Nk

Mtoto wa kike

Mtoto alikutana uso kwa uso na wazazi wake waki-do, baba akamwambia "oh! Mwanangu, tunamtengeneza mdogo wako wa kike"

Siku moja baba alirudi home na kukuta mwanae akilia akamuuliza, "unalia nini?"
Mtoto: Yule mdogo wangu uliekimtengeneza jirani yetu memuona akimla.

Sumu!

Jamaa alipiga simu kwa daktari:
Jamaa: Dokta mke wangu amekunywa sumu yangu yote halafu anajidai amelala, nisaidie nifamnyeje aamke?

Mooo!

Ng'ombe wakiongea.
Ng'ombe 1: Ng'ombe wenzako wote tunalia mooo! Wewe mwenzetu unalia meee!
Ng'ombe 2: Nlisahau waambia, najifunza lugha mpya.

Toothpick

Mteja kaingia bar.
Mteja: Mhudumu njoo. Habari yako?
Mhudumu: Nzuri tu karibu.
Mteja: Mna toothpick?
Mhudumu: Unataka ya baridi au moto?
Mteja: Namaana vijiti.

Vichaa ndegeni.

Ndege moja ilibeba vichaa, sasa walikuwa na kelele. Baada ya muda kidogo msimamizi wao akatokea kwa rubani na kumuuliza mmoja.
Msimamizi/mwangalizi: Wewe! Wenzako wakwapi?
Kichaa akajibu, wanakelele sana wapo hapo nje nimewatoa kidogo.

Monday, September 20, 2010

Ajali

Ilitokea ajali, jamaa mmoja alikatika mkono akawa analia.
Mwingine akasema, "we mkono tu unalia, mbona huya aliekatika shingo halii?"

Mjusi

Mjusi mmoja alikuwa amesimama kwenye siling board. Ghafla akapiga chafya... Punde akapiga chafya... Alipokaribia kupiga ya tatu si akaacha kujishika azibe pua, akaanguka.

Jino na ganzi!

Jamaa alienda kung'oa jino, sasa ganzi haikuingia vzuri.
Wakati daktari anamng'oa si jamaa na yeye ananyanyuka nalo. Mchezo ulikuwa huo bwana mpaka kumaliza hoi.

Sunday, September 19, 2010

Kama siafu

Mental mmoja alikua ghorofa ya 50, chini kulikua na mwanamke mnene. Alikua akimuona mdogo kama siafu.
Akashuka ghorofa kadhaa kwa awamu uku akizidi muona mkubwa. Alipofika chini akaenda mkumbatia.
Mdada mnene: We ni nani?
Mental: Nimekufahamu tangu mdogo kama siafu.

Ze fumanizi

Mwarabu mmoja alimfumania mke wake aki-do na mkewe.
Rafiki: Sasa ukamfanya nini?
Mwarabu: Sa ningefanya nini na sijui english.

Sumu

Mume alienda pharmacy.
Mume: Mke wangu anataka kujiua.
Pharmacy: Vipi nikuitie ambulance?
Mume: Nahitaji sumu nkampatie.

Mke|Ajali

Dokta: Mkeo ameumia sana kwa ajali, itabidi umlishe, umuogeshe, msalani.
Mume: Maskiini.
Dokta: Usijali, nkikutania. Amesha kufa

Mapacha bar

Mapacha wawili walienda bar, pembeni kulikuwa na mlevi kalewa akasema alipowaangalia "holly shit i think i see everthing double!"

Ku-do

Wanandoa wawili walisahau funga mlango wakati wana-do. Mtoto wao akaingia, baba akasema "oh, mwanangu najaza upepo kwenye mapafu ya mama yako"

Mtoto akajibu, "haja jana yule mbaba jirani alisahau kufunga wakati anamjaza upepo mama mdomoni."

Inzi

Inzi karibu kumi walikuwa wamekizonga kinyesi cha mbwa. Ghafla mmoja akajamba, mwingine akasema "we huoni ka tunakula hapa?"

Jogoo mfupi

Jamaa: Dokta nimekuja, Jogoo wangu mfupi, kwa nini hafiki mpaka miguuni.
Siku iliyofuata akaamka akajikuta hana miguu.

Kuungama

Kijana alipoenda kwa Padre, "nimekuja kumuungamia dhambi rafiki yangu."
Padiri akauliza, "kwa nini asije mwenyewe?
Kijana akajibu, "aah Rashidi ni muislamu."

Kuungama

Kijana alipoenda kwa Padre, "nimekuja kumuungamia dhambi rafiki yangu."
Padiri akauliza, "kwa nini asije mwenyewe?
Kijana akajibu, "aah Rashidi ni muislamu."

Dokta.

Fundi bomba alikuja tatua tatizo moja kwenye nyumba moja.
Fundi: Shughuli nzima itagharibu laki mbili.
Mama: Haa! Mume wangu tu ni dokta hatengenezi hiyo pesa kwa saa.
Fundi: hata mimi nlikuwa napata kidogo wakati nlipokuwa dokta pia.

Boxing

Jamaa mmoja alienda kuangalia boxing (ndondi). Alikaa pembeni mwa kocha mmoja wa ndondi, kocha akamuambia jamaa "unaonaje ukijiunga na boxing? Utatengeneza pesa nzuri sana."

Jamaa akajibu, "haina shida, umejuaje kama mi ni dokta wa meno?"

Pikipiki | Gari

Mmiliki gari: Natumia pesa mingi kwa ajili ya mafuta ya gari. Wewe je mwenzangu?
Mmiliki pikpik: Natumia pesa mingi ku-repear kati ya mimi au pikpik.

Alama barabarani.

Traffick polisi alimsimamisha dereva alievuka kibao cha kuonye asimame.
Polisi: Hujakiona kile kibao usimame?
Dereva: Nilikiona, isipokuwa sikukuona wewe.

Nimesahau bukta

Jamaa mmoja alienda nyumba moja kugonga. Mlango ulipofunguliwa akaulizwa na mwanaume aliemfungulia mlango, "nikusaidie nini kijana?"

Kijana akajibu, "samahani kwa usumbufu ila nimekuja nimesahau bukta yangu ya ndani chumbani kwa mkeo?"

Saturday, September 18, 2010

Bado mna?

Frank: James hivi bado unam-date Lily?
James: Hapana.
Frank: Oh! Nlitaka nkuambiage zamani bora umemuacha maana ni mbaya hana mpango kabisa.
James: Hatu-date tena kwani nimemuoa tayari.

Inzi

Jamaa alishikwa na hasira alipokuta inzi kwenye supu yake akamuita mhudumu.
Mteja: Unaona nini hii?
Mhudumu: Oh! Usijali ameshakufa nimewapulizia dawa wote jikoni.

Siafu

Kwenye ndege kwa mara ya kwanza alipanda. Akaangalia nje.
Ima: Ona ona binadamu wadogo kama siafu.
Doto: Wee hao ni siafu kweli bado hatujapaa

Funga mkanda

True story:
Siku moja traffic polisi alipewa lift. Lilipofika suala la kufunga mkanda sasa... Mara aupitishe nyuma ya shingo, mara mgongo... Ilihitajika msaada maana ni aibu.
Kumbe wapo wasiojua kazi kuagiza/kuuliza tu.

Na bibi.

Baba mmoja karudi home kakuta mwanae anafanya mapenzi na bibi yake, "we mtoto umekosa adabu kabisa..."
Mtoto: Kumbe inauma enhe! We unavyofanyaga na mama yangu je?"

Toothpick

Jamaa mmoja restaurant baada ya kumaliza mlo. Akatafuta toothpick atoe nyama kwenye meno, hakufanikiwa. Meza ya pili jamaa alikuwa anacho kimoja anatakitumia akamuambia "kaka samahani ukimaliza hicho niazime pia"

Mimba

Mtoto alimuuliza mama yake?
Mtoto: Eti mama, kwani baba atajifungua lini?
Mama: Kwa nini umeuliza mwanangu?
Mtoto: We huoni tumbo lake kama hili la kwako?

Fumanizi

Jamaa alimuuliza rafiki yake, "utafanya nini ukimfumania mkeo na njemba?"
Jamaa akajibu, "ntamnyoa kwa chupa, na kuivunja vioo ile gari yake nyekundu."

Maiti

Ndege ilikuwa inasafirisha maiti. Bahati mbaya ilianguka na waliomo ndani wote wakafa. Jamaa mmoja kwa masikitiko aliposikia hiyo taharifa akasema, "maskiini, sasa maiti si imekufa tena?"

Kuchelewa kazini

Bosi: Imekuwaje leo unafika muda huu kazini? Umechelewa sana! Ni nini foleni au?
Mwajiriwa: Bosi nisame, yule jogoo anaewika kila siku alfajiri ameuzwa.

Friday, September 17, 2010

Ya leo ndogo

Mtalii alienda restaurant, meza ya jirani akaona jamaa anakula mlo akauli ile nini akajibiwa ni korodani za ng'ombe.

Akaomba aletewe akaambiwa ziliwepo hizo mpaki wiki ijayo kwenye mashindano ya ng'ombe dume na binadamu.

Siku ikafika mtalii akaenda ili awahi oda yake, alipoletewa akauliza "mbona za leo ndogo sio kama za siku ile?"
Mhudumu akajibu, "leo ng'ombe dume ndio kashinda."

Tafuta mke

Jamaa wawili waligongana supamaketi bahati mbaya.
Wa1: Samahani kaka.
Wa2: Bila samahani, namtafuta mke wangu!
Wa1: Mimi pia vivyo hivyo.

Wa2: Mke wako yupoje?
Wa1: Mwembamba, mrefu hivi. Wa kwako je?
Wa2: Agh! Tuache tu, tumtafute wako kwanza.

Spidi ndogo na kubwa

Gari moja ilikuwa spidi ya 50kph, ingine ikapita kwa spidi ya 150kph. Mwisho wa siku wote wakajikuta Majerui hospitali.
Wa 50kph: Vipi tena?
Wa 150kph: Ajali bwana. Je, wewe si ulikuwa slow mbona upo hapa!?
Wa 50kph: Ulivopita nkajua injini yangu imezima nkashuka nkaangalie kumbe inatembea.

Ndege itilafu

Ndege angani ilianza sumbua | itilafu, ma-pilot (Rubani) wakavaa parashuti kujiandaa kuruka wakawaambia abiria "tunakuja tunaenda omba msaada kidogo."

Swali

Josh: Rafiki yangu nna swali nataka kukuuliza!
Sam: Uliza tu mi na wewe tena.
Josh: Hivi lile kovu kwenye paja la mkeo aliumiaga?

Mvuto

Aliingia bar mwanamke mzuri. Jamaa mmoja akamuambia mwenzake "aisee nimemfuatilia yule dada mwaka sasa na zaidi"

Mwenzake akajibu "mh" lakini wewe si ni shoga?"
Akamjibu tena "ndio najua, nataka aniunganishie kaka yake."

Wednesday, September 15, 2010

Baba!

Mtoto: Mama eti ni kweli Mungu ndio anatupatia maji na chakula?
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto: Sasa baba wa nini tena?

Gari usiku

Juma: Mi nashangaa watu wanawezaje endesha gari usiku.
George: Unamaana gani?
Juma: Najiuliza wanawezaje kujua|kuingiza gia kwenye giza?

Mapenzi

Mume: Mke wangu leo tujaribu kitu mupya.
Mke: Kweli mume wangu, twende kwenye garden park leo tuka-do.

Mume akakubali, walipofika eneo polisi nae akatokea kabla hata hawajaanza. Polisi akawadai faini Mume laki moja, mke laki tatu.

Mume: Haiwezekani, kwa nini mke wangu adaiwe zaidi?
Polisi: Kwa sababu huyu mwanamke ni mara ya tatu namnasa hapa akifanya ngono.

Tuesday, September 14, 2010

Museum

Mwanamke mmoja alienda museum, punde akaona taswira siyo. Akamuita mhusika wa pale "kaka haiwezekani, unataka kuniambia hii art?"

Mwanamke: Mbona hata hamna mvuto.
Mtu wa museum akajibu kwa upole, "mama hiki kinaitwa kioo"

Mke kupotea

Mtu na mchumba walienda kariako, punde jamaa akawa hamuoni mchumba wake. Akajaribu mtafuta bila kumpata.

Akamfuata mdada mwingine mrembo, "dada unaweza ukaongea na mimi kidogo?"
Dada akajibu "hapana, kwanini?"

Jamaa: Namtafuta mchumba wangu, akiniona naongea na msichana mzuri kama wewe atakuja tu."

Mapacha

Mwanamke mmoja alipanda daladala na watoto wawili.
Dereva: Hawa ni mapacha?
Mwanamke: Hapana, kwa nini?
Dereva: Siamini tu kama hujatumia condom mara mbili.

Mapacha

Mwanamke mmoja alipanda daladala na watoto wawili.
Dereva: Hawa ni mapacha?
Mwanamke: Hapana, kwa nini?
Dereva: Siamini tu kama hujatumia condom mara mbili.

Monday, September 13, 2010

Jino

Jamaa alienda kwa dokta, "dokta nimekuja na jino la ng'ombe u-replace pale uliponing'oa jana."

Sunday, September 12, 2010

Pikipiki

Idd: Kaka nimenunua pikipiki jana bwana.
Ali: Oh hongera sana. Je ni left hand au right hand?

Supu

Mzee mmoja alienda pata mlo restaurant.
Mzee: Hii supu mbona sio nzuri kama ya jana.
Mhudumu: Mh! Muongo mbona ndio ile ile ilobaki jana?

Muokoaji

Meli moja ya watalii moja wakati inapita walimuo mtu anahangaika kwenye maji yenye kina. Kila mtu akawa anaogopa kujitosa akamuokoe.

Ghafla jamaa mmoja akajitosa na boya la kuogelea akamuokoa.
Walipopandishwa kwenye meli akapewa kipaza sauti aongee kwa ujasiri alioufanya. Akashika kipaza sauti na kusema "namtaka alienisukumia kwenye maji"

Mwizi

Mwizi: Dokta malaria bado nnayo.
Dokta: Dawa nlizokupa ulimeza zote?
Mwizi: Zile ulizonipa nimeziiba, labda unipe zingine.

Karata

Wacheza karata:
Wa 1: Mambo gani ya kulowesha lowesha karata na mimate sasa. wa 2: Si umenipa jokeri ukasema nilambe karata tano!

Saturday, September 11, 2010

Chai

Jamaa mmoja mgahawani akinywa chai ghafla akaja jamaa mbabe mmoja na kuinywa chai yake, akanena "kaka sio vizuri hivyo."

Kisha akaendelea kusema, "leo nimefukuzwa kazi, wiki iliyopita mama yangu kafa, nimemfumania mke wangu na mwanaume, leo nataka kujiua umekunywa sumu yangu kwenye chai."

Vibonge

Kulikuwa na vibonge wakiongea.
Kibonge 1: Unene wangu mpaka mlangoni nashindwa kupita.
Kibonge 2: Unene wangu mpaka nashindwa panda daladala.
Kibongo 3: Unene wangu nilikuwa naanika chupi jirani yangu akaniuliza "unaanika tent?"

Walevi|Simba

Walevi wakitoka kulewa huko kijijini walimuona simba, mmoja akapanda mti. Wa pili akauzunguka mara kadhaa halafu akamuambia mwenzake "usiogope nipo mbali sana nshauzungu mti mara 6 nipo mbali sasa hawezi nifikia."

Zawadi ya besdei

Mke alimletea mumewe chuka kama zawadi kwenye birthday yake.
Mume akaduwaa, hii nini sasa...
Mke akamuambia "usishangae mume wangu hiyo ni zawadi nzuri sana"

Usiku wakati amelala akastuka akakuta chura nanyonya kwa ustadi naniliu ya jamaa.

Asubuhi alipoenda jikoni huku amemshikilia chura mkono mmoja, mkono wa pili kitabu cha mapishi. Mke akamuuliza, "enhe imekuwaje usiku? Zawadi nzuri?"

Mume akajibu, "namfundisha chura jinsi ya kupika, wewe paki nguo zako uondoke"

Picha ukutani.

Jamaa mmoja alikuwa chumbani kwake akitafuta pa kuweka picha ukutani. Alipopata wakati ana-drill ukuta ghafla akasikia kelele toka kwa jirani yao.

Akamtuma mwanae akaangalie kuna nini. Aliporudi akamuuliza mwanae, "enhe kuna nini?"
Mtoto: Umemtoboa mkono.

Goroli

Jamaa mmoja alienda kwa dokta:

Jamaa: Dokta golori yangu moja kubwa ingine ndogo mpaka marafiki zangu wanicheka.
Dokta: Ebu tuone.
Jamaa akashusha zipu kusha suruali...
Golori ya jamaa moja ikagusa mpaka chini.
Dokta akaanza kucheeka mpaka akagalagala.

Jamaa akamuambia dokta "sasa dokta hapo hujaiona kubwa yake"

Ombaomba

Omba omba mmoja alimuomba hela jamaa njiani.
Jamaa: Samahani huwa sitoagi hela mitaani.
Ombaomba akajibu, "sasa nifanyeje? Nifungue ofisi?"

Kadi ya ATM

Jamaa alipoteza atm kadi: "Nimepoteza ATM kadi yangu, kizuri ni kwamba huyo mwizi hatotumia pesa nyingi kama mke wangu."

Wallet

Restaurant
Ali: Jamani nimedondosha wallet ina laki tatu. Atakaeiona ntampatia elfu hamsini.
Jamaa mwingine humo humo restaurant akasema, "Yeyote atakaeileta kwangu ntampa laki moja."

Vidonda vya tumbo

Dokta: Mama inaonekana una vidonda vya tumbo.
Mume: Sasa dokta tusaidie, je plasta tutabandikaje? Au atakiwa aimeze?

Pipi utaoza meno

Chumba cha kupanga kimoja:
Mama: Mwanangu usile pipi meno yataoza.
Mtoto: Mbona mama we usiku unamnyonyaga baba mpaka anatoa gundi, huogopi?

Friday, September 10, 2010

Kipofu

Kipofu mmoja aliingia supermarket na fimbo ya kumuongozea. Mule supermarket kulikuwa na tangazo kubwa limeandikwa '50% OFF'
Kipofu akasema "mbona lile tangazo mmebandika ndani sasa, halafu maandishi yake yanaumiza macho?"

Furaha

Mwanajeshi mmoja alipoze mkono mmoja vitani. Akawa anataka jiua. Wakati yupo tayari akaona mtu mwingine ana mkono mmoja akiruka ruka...

Akaenda muuliza, "mbona kama una mkono mmoja unaruka ruka kwa furaha?"
Jamaa akajibu "nani kakuambia nna furaha? Ni nyuki kaning'ata tako."

Zima moto

Askari mmoja wa zima moto alienda nyumbani kwake na kumuambia mkewe "mke wangu tuwashe moto nyumba yetu nifanye mazoezi ya kuzima moto, siku nyingi sijazima moto."

Kuogelea

Mtu na msichana wake walikuwa beach.
Mwanamke: Njoo tuogelee mpenzi.
Mwanaume: Nibebe na condom?

Mwandishi wa habari

Mwandishi mmoja wa habari alikwama kwenye foleni kubwa iliyosababisha hiyo foleni. Akaamua atumie muda huo kushuka akachukue habari ya kuifanyia kazi...

Basi akapenya penya kwenye umati wa watu ili aone na kufanya kazi ya uandishi akakuta aliegongwa ni ng'ombe.

Paka!

Jamaa mmoja alisikia mlango ukigongwa, alipofungua akakuta jamaa amembeba paka.
Akamueka chini, paka akawa anaruka ruka huku na huko akaangusha whisky na glass. Mwenye nyumba akamfuata jamaa aliekua akiondoka akamuambia "siku ingine usije na paka kwangu"

Jamaa akajibu, "sio wangu mi nimemkuta mlangoni kwako akitaka kuingia nkajua wako."

Thursday, September 9, 2010

Kisima

Mgeni rasmi alipoenda zindua kisima si akachungulia kisimani kisha akauliza, "hee mmeshaanza kufuga na mamba humu?"
Kumbe kajiona sura yake.

Kisima

Mgeni rasmi alipoenda zindua kisima si akachungulia kisimani kisha akauliza, "hee mmeshaanza kufuga na mamba humu?"
Kumbe kajiona sura yake.

Tofauti kati ya...

Mtoto aliulizwa, "tofauti kati ya baba na mama ni nini?"
Mtoto akajibu "baba ni mlevi mama ni mpole."

Wednesday, September 8, 2010

Funguo ya pingu

Mtoto mmoja baba yake askari magereza, alienda na kumuambia baba yake, "baba naomba ufunguo wa pingu?"
Baba kwa mshangao akauliza "enhe! Za nini?"
Mtoto akajibu, "si kuna wafungwa wawili wapo nje wametoroka jela."

Funguo ya pingu

Mtoto mmoja baba yake askari magereza, alienda na kumuambia baba yake, "baba naomba ufunguo wa pingu?"
Baba kwa mshangao akauliza "enhe! Za nini?"
Mtoto akajibu, "si kuna wafungwa wawili wapo nje wametoroka jela."

Open roof

Traffic mpya kazini siku moja aliona gari kwa mbaali inakuja akaisimamisha. Gari husika ilikuwa open-roof... Kwa vile ilikuwa mara ya kwanza kuliona akamuuliza dereva "...hii gari yako mbona imeng'oka paa?"

Tuesday, September 7, 2010

Jino

Jamaa alienda kwa mtaalamu wa meno, alipofika akafungua zipu ya suruali na kutoa naniliu... Dokta akasema "e-e-e! Mimi sio... Mimi ni dokta wa meno."
Jamaa akajibu, "najua, kuna jino limenasia kwenye naniliu yangu"

Juisi ya papai

Josh: Dokta kaniambia ninywe juisi ya papai baada ya maji ya moto ya kuoga.
Fred: Je imekusaidia?
Josh: Hata sijui, siwezi maliza maji ya moto ya kuoga aliyosema kwanza.

Mama na mtoto

Mtoto: Mama kwani dada wa kazi hajakua tu?
Mama: Kwa nini mwanangu?
Mtoto: Ananyonya mpaka leo!
Mama: Mhh! Mwanaaangu...
Mtoto: Kweli mama, mi nlimuona kapiga magoti huku baba anamnyonyesha.

Headphones II

Jamaa alifika duka la vyombo vya mziki akaona headphones, akaulizia kazi yake akajibiwa. Kisha akauliza "inachukua mda gani mziki kufika masikioni?"

Headphones

Jamaa alinunua discman kwa mara ya kwanza, sasa wakati ameweka headphones masikioni akisikiliza mziki, rafiki yake akawa anaushika waya wa headphones huku akisema "hee! Huu waya wake mzuri"

Jamaa mwenye discman akamuambia kwa ukali "wee usiushike utazuia mziki usifike masikioni"

Gazeti

Mtoto katumwa gazeti la tarehe 10. Alipokosa na kurudi... "baba nimekosa gazeti la tarehe 10. Nimenunua ya tarehe 5 mawili"

Kikaoni

Mtendaji mmoja kwenye kikao alimuuliza mwenzake.
Mtendaji: Ndugu yangu mbona hatuonani?
Mtendaji ii akajibu "samahani mkuu, hatuonani wapi?"

Monday, September 6, 2010

Jirani mpya

"mama nikuambie yule dada jirani yetu anaitwa nani?" mtoto akimuuliza mama yake.
Mama akauliza, "we umejuaje mwanangu?"
Mtoto: Si baba alimuita nkasikia.
Mama: Enhe alimuitaje?
Mtoto: Si Honey! Tena ukiondokaga baaba muoogaa peke yake basi anaendaga kulala kwa huyo dada.

Watoto je?

Jamaa mmoja akiongea na rafiki yake "mke wangu hapendagi kabisa nimguse miaka yote tangu tumeoana."
Rafiki yake akanena "sasa hao watoto mmewapataje?"

Don't drink & Drive

Jamaa mmoja alirudi kwake, mkewe akamuuliza "vipi mume wangu mbona... Kwa miguu?"
Mume akajibu "nimekuta kibao kimeandikwa don't drink and drive ivo nlipokunywa tu maji nkaiacha pale pale gari"

Njoo nje

Katoto kamoja ka-kiume kalirudi ndani mbio mbio huku kakimuambia mama yake "mama mama njoo haraka haraka umuone mama frank kasimama pale nje sketi yake inapeperuka na upepo... njoo umuone kavaa ya blue kama yako"

Watoto wa mtaani

Bibi mmoja kasikika akilalama, ''kila siku wanasema watoto wa mitaani wanaongezeka! Si wamfundishe huyo mitaani uzazi wa mpango?"

Sunday, September 5, 2010

Thermos

Jamaa aliona kifaa dukani, akauliza "hii nini?"
akajibiwa "hii ni thermos, kazi yake kufanya cha moto kubaki moto na baridi kuwa baridi."

Siku yupo kazini boss akamuuliza nae akamjibu kama alivyojibiwa.
Boss akauliza tena, "sasa umeweka nini ndani?"
Jamaa akajibu, "chai na maji ya baridi ya kunywa baadae."

Kuchelewa

Jamaa aliamka haraka haraka akiwa amechelewa. Mbio mbio akiwahi anapoenda.
Baada ya mda akarudi.
Mama: Vipi mbona umerudi?
Jamaa: Nimechelewa mekuta mlango washafunga kanisani.
Mama: We umeenda kanisa gani?
Jamaa: Hapo konani karibu na...
Mama: Khaa! Pale msikitini jamani kanisa lipo kwa mbele zaidi.

Mwanga wa tochi

Kaka mmoja na mchumba wake walienda tembea kwenye garden. Kaka akavuka daraja la mbao, alipomaliza likavunjika.

Mchumba wake akasema, "ntavukaje sasa?"
Kaka akajibu, "subiri giza liingie, ntawasha tochi kisha utavuka kupitia juu ya mwanga wa tochi."
Mchumba: "Haa! Hapana nkifika katikati ya mto we utazima tochi halafu ntaanguka."

Punguza uzito

Dokta alimshauri jamaa akimbie kwa siku 30 ili apungue uzito.
Siku 30 baadae jamaa kwenye simu, "dokta asante sana nimepungua, ila sasa ntarudije nipo mile 300 toka nyumbani?"

Punguza uzito

Dokta alimshauri jamaa akimbie kwa siku 30 ili apungue uzito.
Siku 30 baadae jamaa kwenye simu, "dokta asante sana nimepungua, ila sasa ntarudije nipo mile 300 toka nyumbani?"

Hii nini?

Mtoto alimuliza mamake.
Mtoto: Hiki nini?
Mama: Mapulizo (matiti)
Mtoto: Nilimuona baba jikoni akiyapuliza ya dada mfanyakazi

Kanisani

Jamaa alikutana na wenzake wanatoka kanisani akawauliza, "leo sijaja kanisani, vipi wameita majina?"

Mtekanyara

Jamaa mmoja alimteka mtoto wa tajiri akaandika barua "nimemteka mwanenu, nataka dola elfu5. Nimemruhusu mara 1 tu aje achukue nguo za kuvaa kesho."

Mtekanyara

Jamaa mmoja alimteka mtoto wa tajiri akaandika barua "nimemteka mwanenu, nataka dola elfu5. Nimemruhusu mara 1 tu aje achukue nguo za kuvaa kesho."

Soda | 500

Mmasai kaenda dukani kauliza "soda bei gani?" Kaambiwa "mia 5."
Katoa kibuyu, "weka ya mia nampa mtoto."

Ibada

Jamaa alikua anaangalia ibada kwenye tv sebuleni. Punde akajibu sms iliyoingia "siwezi chat now padre ataniona"

Makaburini

Dogo mmoja na wenzake wawili walipita njia moja karibu na makaburi. Sasa wakawa wanaona wengine wamekufa na umri mkubwa mfano 95, 101 nk nk.
Aliporudi nyumbani akamuambia mama yake, "mama mi nikifa niandikeni nimeishi miaka 200"

Mama kwa mshangao akauliza, "hee! We mtoto nani uliwahi msikia...?"
Mtoto: We niandikieni ivo ivo?
Mama: Kwa nini wasema hivyo mwanangu?
Mtoto: Nataka niwashinde wote waliokufa.

Makunyanzi

Mtoto mmoja alimuona bibi yake walioenda kijijini. Baada ya kuona ngozi ya bibi yake ina makunyanzi ya uzee sana akamnong'oneza mama yake, "mama... kwani bibi si aipige pasi tu ngozi yake imejikunja sana!?"

Mnyama gani?

Siku moja mama mmoja alienda mbuga za wanyama na mwanae mdogo wa miaka miwili. Wakati wakiangalia wanyama yule mtoto akaona tembo akamuulima mama yake "mama huyu mnyama gani? Mbona ana mkia mbele na nyuma?"

Friday, September 3, 2010

Msiba

Dada mmoja alipata taharifa kafiwa na mama yake. Boss akamuambia aende tu nyumbani. Dada akasihi aendelee wepo eneo la kazi.

Baadae boss akaenda muangalia akakuta analia akamuuliza "vipi tena kulikoni?"
Dada akajibu "dada yangu anaenifuata amenipigia na yeye amefiwa na mama yake."

Kuchelewa rudi

Jamaa alinunua gari akaenda chalinze. Wakati anarudi mkewe akamuuliza "mbona umechelewa rudi?"
Mume "hii gari wameeka gia 4 kwenda mbele tu, kurudi nyuma eti 1 tu"
(alirudi kinyume nyume)

Mapacha

Mwanaume mmoja alienda hospitali, akakuta mkewe kajifungua mapacha akamuliza mkewe "huyu mtoto mwingine wa nani?"

Risasi

Mama mjamzito wa mapacha watatu alienda supermarket akapigwa risasi 3 tumboni.
Alipoenda kwa daktari akaambiwa "...usiwe na wasi wasi risasi zitatoka zenyewe"

Baada ya miaka 16 wale mapacha baada ya kuzaliwa siku moja ikawa hivi.
Wa kwanza: Mama.. Mama.. Nilienda chooni risasi ikatoka.
Wa pili nae siku moja akamuambia hivyo hivyo.

Wa tatu kabla hajasema mama akadakia "enh na wewe risasi imetoka?"
Mwanae akajibu "ndio imetoka wakati na... Ikampata baba kaanguka"

Thursday, September 2, 2010

Kutabiri mbele

Mwalimu aliuliza darasani, "inawezekana kutabiri jambo la mbele?"
Mtoto mmoja akajibu, "ndio! Mama huwa akiangalia daftari langu la hesabu huniambia, subiri baba yako arudi uone."

Wednesday, September 1, 2010

Makumbusho

Jamaa mmoja akipiga simu ofisi ya Makumbusho ya Taifa: "Haloo, hapo ni Makumbusho ya Taifa?"
OFISI: "Ndio, tukusaidie nini?"
JAMAA: "Ok, naomba mnikumbushe mwaka juzi saa yangu niliipoteza wapi?"
OFISI: "Pumbavu! Hiyo sio kazi yetu..!"
JAMAA: "Sasa makumbusho mnakumbusha nini?" OFISI: "Tunahifadhi mambo ya zamani." JAMAA: "Ahaa... kumbe saa yangu mtakuwa nayo..!"