Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, November 30, 2010

Gari kutoa moshi

Mtoto mmoja aliporudi nyumbani toka shuleni akawa anamsimulia baba yake, ''baba leo tumepelekwa jumba la makumbusho tumejifunza mengi''

Baba akanena, ''safi sana mwanangu.''
Mtoto: Pia nimewaambia waje nyumbani kukuona.
Baba: Enh??!! Kuniona? Akina nani?
Mtoto: Si watu wa makumbusho:

Baba: Mimi wananifuata ili iweje.
Mtoto: Nimewaambia baba angu ana gari la zamani na linatoa sana moshi, na wao wanataka gari la zamani linalotoa moshi mwing kama lako.

Afrika kusini

Mama: Mume wangu safari bado haijaiva.
Baba: Najipanga mke wangu, South Africa maisha yapo juu kidogo.
Mtoto: Mhh! Baba, we si ulisema unaenda Afrika Kusini? Mbona mama unamdanganya unamuambia unaenda South Africa?

Maneno

Mwanaume mmoja alifuatwa na jirani mwema na kumuambia ''baba nanihi nimemuona mke wako yupo na mwanaume mwingine muda huu huu.''

Mwanaume aliefuatwa akajibu, ''ooh bora mwanaume maana nlishamkataza kukaa na wanawake umbea mwingi.''

Monday, November 29, 2010

Mke na mume

Mwanamke mmoja alikua amekaa sebuleni na mwanae, punde akachukua simu na kumpigia mumewe huku simu ikiwa katika sauti kubwa (loud speaker) ''mume wangu upo wapi? Mbona unachelewa kujibu''

Mume akawa anajibu kupitia simu, ''naja punde mke wangu nipo kwenye jam''
Kale katoto kakaenda jikoni na kurudi huku kakimuambia mama yake ''mama...mama... Baba muongo mbona hayupo humu kwenye chupa ya Jam'' (mithili ya siagi)

Unataka kusoma nini

Baba mmoja alikaa kibarazani na mwanae wa miaka minne akiongea nae, akamuuliza swali ''mwanangu ukikua mkubwa ungependa kusoma nini?''

Mtoto nae bila hiyana akamjibu Dad yake, ''mimi baba? Nikikua nataka nisome magazeti''

Mavituzi

Mwanamke mmoja wa kipemba alikuja Dar, siku moja akaopolewa na kidume. Alipewa malavidavi moto moto ikiwa kunyonywa kona zote.

Siku aliporudi kwa mumewe zanzibar wakati yupo na mumewe wakati wa malavidavi akamuambia ''mume wangu, Dar yaliwa hiyo''

Dogo

Dogo mmoja akimuambia ama kumuuliza baba yake, ''baba... nyumba ina dirisha, gari lina dirisha, ndege ina dirisha sasa mbona hamna dirisha kwenye baiskeli?''

Sunday, November 28, 2010

Chai time

Jamaa mmoja alikua anapita sehemu karibu na mgahawa, akaona mini-bus aina ya Coaster ina jeneza imepaki ikiashiria wasindikiza maiti wanapata kifungua kinywa.

Akamuita dereva wa ile bus na kumuuliza:
Jamaa: Samahani we ndi dereva?
Dereva: Ndio kaka, kulikoni?
Jamaa: Mbona mmesimama hapa?
Dereva: Mkuu tunapata chai kidogo safari ndefu.
Jamaa: Sasa mwenzenu kwenye jeneza mbona hamjamnunulia hata andazi?

Friday, November 26, 2010

Ajali kusimulia

Dogo mmoja akiwasimulia wenzake ''dah, baba angu si kapata ajali?''
Dogo wa pili, ''kagongwa na gari?''
Dogo wa kwanza, ''ndio! Yaani bora kagongwa na benz kuliko ingekuwa corolla''

Taratiibu

Jamaa mmoja alikua na mpenzi wake chumbani, alipotoka bafuni mchumba wake akamuambia ''ee chupi yako saafi''

Jamaa alipofika kitandani akawa anakaa taratiiiibu saaana, mpenziwe akamuuliza ''vipi misuli imekushika?''

Jamaa akajibu, ''naogopa ntaichafua chupi''

Mimba

Baba mmoja akifanya ishara kadha wa kadha mbele ya tumbo la mkewe ambae ni mjamzito.
Mkewe alimuangaliaa mwisho akashindwa vumilia akamuuliza ''kwani mbona sikuelewi mwenzangu?''

Mumewe bila hiyana akamjibu, ''we huoni kuwa namfundisha mwanangu tangu akiwa tumboni akitoka awe trafiki polisi?''

Kuonja

Mtoto: Mama hiyo unayotengeneza ni nini?
Mama: Natengeneza sumu nimuwekee baba yako ananiudhi sana.
Baada ya masaa kadhaa.
Mtoto: Mama nimeionja ile sumu taamu, baba atafaidi kweli leo.

Mtoto akisimulia jambo

Mtoto: Mama nikuambie kitu?
Mama: Niambie tu mwanangu.
Mtoto: Haya, kwani baba muoga eenhe?
Mama: Mh!! Kwa nini mwanangu?
Mtoto: Maana ukisafiri huwa anaogopa kulalia godoro anamlaliaga dada wa kazi tuuu.

Wednesday, November 24, 2010

TV

Mtoto mmoja alizoea kuona TV za kisasa tangu amezaliwa. Siku moja akaenda kutembelea ndugu zao alipofika akaona TV zile zenye kichogo nyuma akamuita baba yake na kumuuliza ''baba hii nini nyuma ya TV?''

Kwa dokta

Dokta mmoja wa kiume akimhudumia mama mjamzito.
Dokta: Hii ni mimba yako ya kwanza?
Mjamzito: Ndio, hivi huwa inauma wkati wa kujifungua?
Dokta akajibu, ''mimi mbona nlijifungua bila maumivu''

Bata

Kibosile mmoja alienda kuangalia sarakasi, mwanasakasi mmoja akawa amemuweka bata chini ya beseni amemfunika juu chini huku akiruka ruka na kucheza.

Yule kibosile akaongea na jamaa mpaka akamunua yule bata. Siku chache mbele akampigia simu yule aliemuuzia, ''halo... Mbona bata hachezi kama siku ile?

Jamaa akamjibu, ''ulikumbuka kumuwashia mshumaa?''

Tuesday, November 23, 2010

Hela iko wapi?

Mama akimuuliza mama yake.
Mama: Jesca mwanagu ile pesa yangu pale mezani ipo wapi?
Mtoto: Ooh! Nimeitumia mama ila niliitoa photocopy nimekuachia kopi.

Friday, November 19, 2010

Mtoto na mama yake

Mtoto mmoja akimuambia mama yake mjamzito alipomuona anakoroga chai. ''wee mama weewee! Shauri yako, utamuunguza mtoto tumboni''

Pesa bank

Jamaa mmoja alianza kuangua kiliobaada ya kusikia taharifa ya habari, kuulizwa kulikoni akajibu ''nimesikia kwenye taharifa ya habari bank ya cbn imeibiwa milioni mia tawi la mjini''

Jamaa akawa hajamuelewa, ''sasa wewe unalia nini?''
Anaelia akajibu, ''si jana tu nimeweka milioni mia tawi lile lilee'' (huku akifuta machozi)
Msimuliwaji alicheka mpaka akakaa chini na kumuambia ''hehehe imeibiwa bank au wewe? Hahahaha!''

Kituo cha polisi

Jamaa mmoja alienda mpaka kituo cha polisi akafika na kuuliza, ''nna tatizo nyumbani kwangu''
Polisi akamuuliza: Tatizo gani hilo lililokuleta?
Jamaa akajibu: Kuku wangu wawili wameibiwa na mbwa wenu.
Polisi: Mbwa wetu?
Jamaa: Si yule mbwa anaitwa polisi kwani sio wenu?

Wednesday, November 17, 2010

Siku ya kwanza shuleni

Mama alimuuliza mwanae baada ya kurudi kutoka shule siku ya kwanza, ''enhe mwanangu umejifunza nini leo shuleni?''
Mtoto akamjibu mama yake ''bado sijajifunza vya kutosha itabidi nirudi tena kesho''

Kojoleo

Mtoto mmoja wa kike alimuambia baba yake ''baba na mimi ninunulie kojoleo kama la dereva''

Tuesday, November 16, 2010

Dawa ya usingizi

Jamaa: Dokta zile dawa ulizonipa jana mbona ni za usingizi?
Dokta: Ndio, si ndio ulizotaka nikupatie?
Jamaa: aah mi nlitaka za kulala sio za usingizi.

Teja

Teja moja (bwia unga) alikuwa kituo cha daladala akiitia/piga debe daladala ''tandika tandika gari...'' huku anasinzia na ule ulevi wao wa kubwia unga.
Kuja kuhamaki ''kumbe daladala ishatimua kitaambo kama dakika tano zilizopita''

Sunday, November 14, 2010

Moto

Mtoto mmoja akimuambia baba yake kwenye simu wakati nyumba yao inaungua moto, ''baba... baba... Heee wahi uone nyumba yetu inaungua kaaama kwenye sinema ya James Bond vile gadi raha''

Mswaki

Jamaa mmoja alienda kwa rafiki yake na kumuambia nna bidhaa nauza ikiwemo miswaki!
Jamaa anae uziwa akanunua.

Kesho yake jamaa akapita tena ''aisee mswaki ulioniuzia mzuri nimeupenda sana.''
Jamaa akamjibu ''asante sana ipo mingine kama unataka yote used kama nliokuuzia''

Saturday, November 13, 2010

Maongezi ya vijana

Vijana watatu wa kiume na msichana mmoja wakiongea mara akapita msichana mrembo mmoja kati ya wale vijana akasema ''dah mrembo yule mtamu'' mwingine akasema ''si mchezo''

Ikafika muda wa yule dada kati ya vijana watatu akamuuliza kijana mmoja wa tatu ''Iddi wewe je?''
Iddi akajibu ''aanh mimi niko period''

Kipofu kwa daktari

Kipofu alipelekwa hospitali na ndugu yake kufika hospitali nesi akawaambia ''kumuona daktari ni shilingi elfu kumi''

Yule aliempeleka hospitali kipofu akajibu, ''tumekuelewa ila huyu mwenzangu ni kipofu hawezi kumuona daktari''

Friday, November 12, 2010

Mmassai na mzigo

Mmasai mmoja alipewa lifti kwenye kenta alikuwa amejibebesha mzigo kichwani. Alipopanda kwenye kenta akawa bado mzigo wake upo kichwani. Wakamuambia aushushe tu si yupo kwenye gari mmasai yule akakataa katu katu.

Thursday, November 11, 2010

Headphone

Jamaa mmoja alimuuliza mwenzake swali lifuatalo, ''kwani hizi headphones ni za kupitishia sauti?''
Mwenzake akamjibu ''ndio maana ake''
Akauliza tena ''hazichakachui unachokisikia kweli?''

Jiografia

Mtoto: Mama nikuulize swali?
Mama: Enhe mwanangu uliza tu.
Mtoto: Hivi Arusha na Tanzania ipi kubwa?

Treni

Mtoto mmoja wa kiarabu alipelekwa kusoma Ujerumani. Siku moja akamuandikia barua baba yake kama ifuatavyo:

Dear Dad,
Huku Berlin-German hali ya hewa nzuri!
Wanafunzi na walimu wananishangaa mimi nakuja na Ferrari shule wengine wote wanakuja na treni.
Wako Mwanao.

Baba nae akajibu,
Dear Son,
Nimefurahi kupata barua yako, kuhusu ferrari usijali basi na mimi ntakununulia Treni ya kwako.
Mimi baba yako.

Samaki wa kukaanga

Siku moja mtoto mmoja alienda kuogelea, aliporudi nyumbani akakuta wamepika ugali na samaki. Papo hapo akatamka ''hee!! Mama huyu samaki sio ameletwa na mzee idrisa?''

Mama akajibu ''ndio mwanangu, kwani vipo''
Mtoto akajibu tena, ''basi kama ndie aliemleta nilimuona huyu samaki alikuwa ana mimba''

Wednesday, November 10, 2010

Rubani wa ndege

Rubani mmoja wakati yupo angani baada ya muda mrefu hewani akamuita mhudumu na kumuambia ''tafuta mtu kati ya abiria akazibe pancha tairi moja kabla hatujatua...''

Gari

Jamaa wawili wakipiga stori zao za kawaida tu, mmoja akamuambia mwenzake ''ebwana si James kanunua gari bwana''
Mwenzake akanena ''aah gari yenyewe inatoa moshi utadhani inatumia kuni... Sio ishu''

Mgeni

Mtoto: Mama... Maaama!
Mama: Abee mwanangu unasemaje?
Mtoto: Eti mama, kwani baba amekuwa mgenisiku hizi?
Mama: Hapana kwani vipi mwanangu?
Mtoto: Si jana na leo memuona anaingia na mdada nyumba ya kulala wageni.

Tuesday, November 9, 2010

Ki-ndege

Jamaa alienda kuangakia sinema, alipoomba kukata ticket mbili za kuingia akaambiwa hawaruhusu kuingia na wanyama au ndege.

Akaenda pembeni akamfiche yule ndege kwenye suruali, kisha akafanikiwa kuingia ndani kuangalia sinema! Kwa vile joto lilizidi akafungua zipu ili kale kandege kapunge upepo. Humo sinema pana kigiza giza......

Dada mmoja akamnong'oneza mwenzake ''hii dudu ya huyu jamaa pembeni yangu inakula popcorn zangu''

Kukujoa hadharani

Jamaa mmoja alikua anakujoa kwenye eneo la wazi, ghafla polisi akatokea na kumuuliza '' wewe kwa nini unakojoa hadharani? Hebu fungazipo yako utoke hapo''

Yule jamaa akaanza kucheka sana baada ya kupandisha zipi yake, polisi akamuuliza ''kulikoni tena?''
Jamaa akajibu ''nimefunga zipu ila bado naendelea kukojoa ndani ya suruali.''

Sunday, November 7, 2010

Kifo cha mgonjwa

Jamaa walikua na mgonjwa wao aliekuwa amelazwa na hali mbaya! Wakaamua kumuita mchungaji aje kumuombea!

Yule mgonjwa akaomba peni na karatasi kwa vitendo, akaandika kitu akampa mchungaji. Mchungaji akakichukua na kukiweka mfukoni.

Alipokufa mgonjwa, baada ya kuzika akakumbuka ana kile kikaratasi, akakitoa na kukisoma mbele ya watu wasikie marehemu alichoandika kama ifuatavyo ''mchungaji umekanyaga paipu yangu ninayovutia oxygen''

Mjane

Mjane mmoja tajiri alibandika tangazo limeandikwa hivi ''nahitaji mwanaume mwenye sifa zifuatazo:
1. Asinipige
2. Asinikimbie
3. Awe mzima kitandani

Baada ya kupata maombi mengi siku moja akagongewa na mwanaume hana mikono wala mguu. Akamuuliza ''enhe sasa wewe ndio....''

Mwanaume akajibu, ''si unaona sina mikono so siwezi kukupiga, sina miguu siwezi kimbia''
Mjane: Na je kitandani je?
Mwanaume: We unadhani kengele nimegongaje?

Friday, November 5, 2010

Kipimo

Jamaa mmoja mlevi alienda kuomba kazi kiwanda cha wine wakam-test kwa kumpa mvinyi (wine)aonje na kufafanua ni kinywaji gani nk nk
Akapewa wine ya kwanza akaionja na kujibu, ''hii ina miaka 10, kilevi......'' nk nk
Akapewa ya pili pia akapatia vyema kabisa.

Wakaona kweli anafaa wakamuekea mkojo kwenye glass, yule jamaa alipoonja akajibu ''mkojo wa mtu mwenya miaka 21, na mjamzito wa miezi mitatu, na kama hamnipia kazi ntawatajia na baba wa huyo mtoto.''

Wednesday, November 3, 2010

Hotelini

Mr. na Mrs. Walienda hotel moja kusherekea miaka yao 50 ya ndoa. Punde kidogo wakarudi reception na mume akaanza kubwata ''hatukitaki kile chumba, hakina kiti, meza, dirisha wala choo''

Mzee wa watu akazidi bwatuka ''yaani mmetuona sie ndio wakuja sio, niitie meneja wenu haiwezekani kabisa.....''

Mhudumu akawa anajaribu kumkatisha mpaka akafanikiwa ''Mzee... Mzee... Mzee hile ni lift sio chumba mlichopewa''

Kununiana mke na mume

Mke na mume wakiwa safarini kwenye gari yao, takribani tangu waanze safari hamna alieongea neno na mwenzie. Baada ya muda mbele wakamuona nguruwe, mume akauliza ''huyo ni ndugu yenu upande gani?''

Mke nae bila hiyana akajibu, ''ndio ndugu yetu upande wa wakwe zangu.''

Neno mbadala

Mwanaume mmoja shule yake iliishia darasa la saba alienda kwa daktari na maongezi yao yakawa hivi:
M'ume: Dokta, mke wangu ni mvivu sana, nimekuja unisaidie.
Dokta: Enhe nikusaidiaje?
M'ume: Nataka unipe neno la kidaktari la kumaanisha kuwa yeye ni mvivu mnoo. Maana nkimuambia kavukavu atanijeruhi leo.

Utani huu

Mfanyakazi mmoja akiongea mbele ya wenzake chuo fulani, ''aisee mmemuona Mkuu wetu mpya alivyo na sura mbaya kama anang'oa jino?''

Mwanamke mmoja pale pembeni akadakia, ''unajua mimi ni nani?''
Mfanyakazi akajibu, ''hapana, we ni nani?''
mwanamke akajibu, ''mimi ni mke wa huyo unaemzungumzia''

Mfanyakazi: Ooh, na mimi unanifahamu ni nani?
Mwanamke akajibu: Hapana.
Mfanyakazi akanena, ''Ooh vizuri kumbe kibarua changu kipo salama.''

Monday, November 1, 2010

Kelele kwa mtoto

Mama mmoja mjamzito alipokuwa akiongea na kucheka kwa sauti na shoga yake ghafla mwanae mmoja wa miaka mitano akaja na kumuambia, ''mama usipige kelele utamwamsha mtoto tumboni.''

Kahawa

Dokta nna tatizo, kila nkinywa kahawa baada ya muda nasikia kama maumivu hivi kwenye koo.
Dokta baada ya kumfanyia X-ray nakadhalika akamuambia ''siku ingine kabla hujanywa chai hakikisha umetoa kijiko cha sukari kwenye kikombe kwanza.''

Jicho

Marafiki wawili wakiongea, mmoja akimuambia mwenzake jambo linalomsumbua!
Rashid: Ebwana mi jicho langu lanisumbua.
Ima: Linafanyaje kwani?
Rashid: Linakua kama lina kidoti hivi kwa mbele nakiona ona.
Ima: Umemuona Daktari?
Rashid: Hapana nakiona kidoti tu nlichokuambia.