Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, December 31, 2010

2011

Chekazone inawatakia wadau wake wote heri ya mwaka mpya na fanaka tele. Mungu awajaalie heri katika maisha yenu ya kila siku.

Wanandoa wakigombana

Wanandoa wawili baada ya majibizano yaliyogharimu takribani nusu saa yaliishia hivi:
Mwanamke: Nilikua mpumbavu kukubali kuolewa na wewe.
Mwanaume: Nili-fall in love ndio maana sikuliona hilo.

Mbwa

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake, "baba hivi kwa nini huyu mbwa wetu hapa nyumbani anapenda saaana kufukuza gari huku akibwaka kama avile anataka kuling'ata?"
Baba mtu akamjibu mwanae kwa kicheko "hehehe mwanagu unajua nini? Huyu mbwa anadhani atapewa gari aendeshe"

Apointiment

Dereva mmoja alikua akitafuta pa kupaki gari yake bila mafanikio,
Ikafika hatua akabandika kikaratasi kimeandikwa "nimezunguka jengo kwa dk 20 sijapata pa kuegesha gari. Hivyo nimeamua kuliegesha hapa nina apointment vinginevyo ntapoteza kazi yangu" akakiweka kwenye kioo na kukishikizia na wiper.

Aliporudi akakuta na yeye kikaratasi cha mkatisha ticket za parking kimeandikwa "nimefanya kazi hii kwa miaka 20 na hii ndio mara ya kwanza siwezi kukuachia vinginevyo ntapoteza kazi yangu"

Maua

Ndugu mmoja alimtembelea ndugu yake anaeishi mjini. Ikawa kila siku alfajiri anajituma kumuagilia maua ya ndugu yake mwenye nyumba mjini.

Siku moja akamuuliza ndugu yake ''nimekua nkimwagilia sana maua yako ya nje na ndani ila ya ndani sioni mabadiliko si uyatoe nje yakue vizuri?''

Ndipo ndugu yake akamjibu, ''ooh pole sana haya ya ndani ni ya plastik sio maua halisi''

Wednesday, December 29, 2010

Maji

Siku moja familia moja ilienda mikumi kuangalia wanyama. Sasa wakati wanaangalia angalia wakaona pundamilia wakiwa pembezoni mwa mto wakinywa maji.

Mtoto akamuuliza baba yake, ''sasa baba hawa pundamilia maji yao yamechemshwa kweli?''

Monday, December 27, 2010

Alarm system

Jamaa mmoja alibahatika kununua gari, sasa kwa vile mpaka anainunua gari yake mpaka inakaa barabarani akawa kama ameshaishiwa hela. na akihitaji kweli kuweka alarm system mapema awezavyo. Akapata wazo la ziada la kusogeza siku, si akallipaka pilipili gari lote. Halafu kichwani akiwaza "dah hapa itakua sijamkomesha mwizi ataejitokeza hasa kama ni mhindi"

Foleni ya magari

Siku moja jamaa wawili walikua wakitwanga stori za hapa na pale zikaingia mpaka zihusuzo foleni za barabarani. Jamaa mmoja akasema "dah foleni za dar bwana, jumapili zinaafadhali kidogo"

Mwenzake akadakia na kujibu "weeweee! Kitu ubungoooo. Pale foleni ni compulsory"
Yaani akimaanisha ni laziiimaa!

Kucha za kubandika

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake mzazi "mama mi nna swali"
Mama yake akamuambia "uliza tu mwanangu"
Ndipo mtoto akauliza "hivi kucha za kubandika ukikata zinakua?"

Saturday, December 25, 2010

Spea tairi

Mtoto mmoja akimuuliza baba yake "baba, hivi spea tairi huwa inapataga pancha?"

Xmas

Mtoto mmoja alimsumbua sana baba yake kuhusu sherehe za xmas!
Ilikua baba ninunulie hiki, baba ninunulie kie.
Baba yake akashindwa kuvumilia akamuambia
"Mwanangu mpenzi xmas imeahirishwa mpaka mwakani"

Friday, December 17, 2010

Sh 200

Jamaa mmoja alienda kununua sigara packti zima.
Alipofika akajikuta ata pungufu ya shilingi mia mbili. Muuza duka akakomaa bila mia mbili hatoi kitu. Jamaa akaenda nyumbani na kumchukua mwanae wa miaka minne na kumpa muuza duka.

Muuza duka akauliza, ''sasa huyu mtoto ndio wa nini mie?''
Jamaa akamjibu, ''ile mia mbili anayo huyo mtoto aliimeza ichukue''

Thursday, December 16, 2010

Mgonjwa kulazwa

Mgonjwa mmoja wa malaria alipoenda hospitali akaambiwa alazwe kulingana na hali aliyokua nayo. Bahati mbaya akaambiwa wodi na vitanda vyoote vimejaa, jamaa (mgonjwa) akadakia na kusema ''ina maana hata mochuari nako kumejaa? Nipelekeni huko''

Tuesday, December 14, 2010

Saprizi

Mwanamke mmoja aliporudi nyumbani mumewe akamfunika nakitambaa usoni.

Akampeleka mpaka kwenye meza ya chakula, sasa mkewe alikua anasumbuliwa na tumbo. Akawa anajinyanyua upande mmoja akijamba mara kama tatu.

Mumewe alipomfungua kile kitambaa ili akutane na hiyo sapraizi. Hamadi meza ya chakula imejaa wakwe wa pande zote mbili...

Malengo

Watoto wawili mapacha wakiwa bado tumboni mwa mama yao wakiongea:
Mtoto wa kwanza: Mimi nikitoka humu ndani lazima niwe fundi umeme, kwa sababu ya hili giza.

Mtoto wa pili: Mimi lazima niwe muwindaji.
mwenzake akamuuliza. ''Kwa nini?''
Akajibu: We humuoni yule nyoka anaeingia humu mara kwa mara.

Monday, December 13, 2010

Kigugumizi

Vijana watatu walikuwa wanasafiri toka Dar kwenda Morogoro na gari ndogo. Ghafla maeneoo ya kimara akakatisha jamaa na guta/mkokoteni wakamkosa kosa. Yule mwenye kigugumizi akawa anatukana sasa kile kigugumizi akaanza tangu eneo la tukio mpaka anafika Kibaha ndio akalipata tusi alilokilitamka...

Sunday, December 12, 2010

kutojua matumizi

Mtoto mmoja alikua hajui jeneza ni kitu gani siku moja akamfuata baba yake na kumuambia ''baba... baba... Ninunulie jeneza la kuchezeaa''

Dereva

Dereva mmoja alikamatwa na askari wa usalama barabarani akawa anaulizwa na kijibu kama ifuatavyo:
Trafiki: Una stika ya usalama barabarani?
Dereva: Ndio.
Trafiki: Fire Extinguisher?
Dereva: Ndio. Ila sina leseni tu...

Saturday, December 11, 2010

Mgao wa umeme

Jamaa mmoja wakati yupo kijiweni anatwanga stori na wenzake, mmoja akasema ''dah huu mgao wa umeme kero sana Dar, na hili joto mh''
Ndipo mwenzake akanena, ''ooohh ndio maana nyumbani nasikiaga kitu kama jenereta, kumbe kuna mgao siku hizi?''

Friday, December 10, 2010

Network

Jamaa mmoja alimuona dereva wa lori moja limechoka choka hivi likiwa barabarani. Akamuona dereva wa lori anaongea na simu huku akiendesha. Akamuuliza yule dereva ''samahani, hivi kumbe na humo network inapatikana?''

Thursday, December 9, 2010

Akili za darasani

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake ''eti baba inawezekana kukopa?''
Baba hakuelewa akamuuliza, ''sijakuelewa mwanangu''
Mtoto: Kesho kutwa kuna mtihani nataka nimkopeshe Raymond akili zake maana sijasoma kabisa''

Kuopoa bar

Jamaa mmoja alienda Bar, akamuona mrembo mmoja akamuomba wakae nae meza moja.
Wakati wanapiga stori. Jamaa akawa anamuambia yule mwanamke, ''onja basi bia kidogo''

M-dada akajibu ''ooh mimi sinywi bia kabisa''
Jamaa akasisitiza zaidi ''jaribu tu si kidogo tu''
Mwanamke, ''nna dozi bwana leo''
Jamaa: Yaani kidogo tu, dozi gani hiyo bwana?''
Mwanamke: Nipo kwenye dozi ya ARV kaka....

Wednesday, December 8, 2010

Dude

Wakina dada wawili wlimuona mmasai kakaa vibaya wa kiume! Wakawa wanamuona maeneo nyeti! Mmasai alipowashtukia akawaambia ''nyie mnaishangaa hii? Nnazo zingine tatu nyumbani''

Saturday, December 4, 2010

Umeme

Jamaa mmoja akimuuliza mwenzake, ''jana nlikuona na mrembo pale kibarazani''
Jamaa aliekua na mrembo, ''ndio bwana nilikua namtongoza''
Jamaa wa kwanza, ''enhe sasa ikawaje?''
Akajibu, ''nilishindwa kuongea''
Jamaa akamuuliza ''kwa nini ulishindwa?''
Aliekitongoza akajibu ''umeme ulikatika sikuweza kusoma kikaratasi maneno ya kuongea''

Kagera

Jamaa wakiongelea kazi, mmoja akamuuliza mwenzake, ''aisee hivi ulisema wamekupagia wapi kazi?''
Jamaa yake akamjibu, ''dah si Kagera ndugu yangu'' mwenzake akajibu ''duh! Si kuna kutekwa tekwa njiani kule?''
Jamaa akajibu, ''we acha tu, sijui ndio wamenitoa kafara au ndio wananipeleka mafunzoni''

Thursday, December 2, 2010

Kuendesha usiku

Dada mmoja akimuambia mpenzi wake amfuate alipoenda kwenye sherehe. ''Mpenzi wangu najua hupendi kuendesha gari usiku ila leo naomba uje kunichukua sherehe ikiisha''

Mchumba na akamjibu, ''mpenzi ntakuja kukufuata ila si unajua kuna mgao wa umeme, naogopa pia wasije kata umeme kwenye gari bure.''

Mlevi akiongea

Mlevi mmoja akiongea
''nikopeshe hela ndugu yangu, ntakulipa wiki ijayo nimekwama kwa kweli mwenzangu. Naahidi kesho tu ntakurudishia pesa yako.''
Akii-a-mbia ATM''

Mvua

Jamaa mmoja alimpigia simu jamaa yake simu na kumuuliza, ''aisee za masiku? Mvua vipi huko inanyesha?''
Jamaa ake akajibu ''nzuri tu, ila mvua ndio inanyesha!''
Alieuliza mwanzo akanena, ''dah! Hadi mvua ya mgao mbona huku hainyeshi!!?''