Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, June 30, 2011

Mchango wa harusi

Ofisi moja wakati wakati wanapitisha karatasi ya mchango wa harusi ya mfanyakazi mwenzao. Majina yalikua yameandikwa mpaka nyuma mmoja akauliza "haya majina mengine huku nyuma ni ya nini?"

Mwingine akajibu "haya ya mbele mchango wa harusi na haya ya nyuma mchango wa suti ya mwana harusi"

Kitambi

Jamaa mmoja alikua anamtania mwenzake mwenye umbo la kitambi mbele ya marafiki wengine, "ona huyu jamaa angu hata rangi ya mkanda haijui sababu ya kitambi, kama unabisha mwambie aangalie sasa hivi"

Dawa bandia

Jamaa: We kwa nini unapenda nunua dawa bandia bwana?
Mnunuaji: Mi ntajuaje kama bandia au sio sasa.
Jamaa: Si unauliza.
Mnunuaji: Bwana eeh mi nanunua ivo ivo Orijino bandia.

Tuesday, June 28, 2011

Wizi wa fedha

Jamaa watatu waliona gari inakuja mbele yao ina rangi ya bank fulani si wakaiteka. Wakati wanawauliza waliomo ndani "pesa ziko wapi! Pesa zikowapi" ndipo mmoja kati ya waliomo akajibu "jamani hii ni ambulance ya benk sio gari ya kubeba hela"

Monday, June 27, 2011

Uzunguni...

Jamaa mmoja alibandika tangazo lifuatalo "wife wanted" akimaanisha anamtafuta mke wake....
Siku ya pili alipokea barua za kutosha zikisema njoo umchukue wangu.

Huduma mbili

Jamaa mmoja alienda viti virefu, akanywa kinywaji chake kisha hali ikawa hivi:
Mteja: Bia nliyokunywa shilingi ngapi?
Mhudumu: Bia shilingi 300
Mteja: Enhe? Mbona bai rahisi ivo? Niitie boss wako.
Mhudumu: Jupo ghorofa ya juu na mke wangu...
Mteja: Anafanya nini na mkeo?
Mhudumu: Kama ninachofanya mimi kwenye biashara yake.

Saturday, June 25, 2011

Hesabu ya kichwa

Mtoto mmoja aliulizwa na baba ake "Dany kulikua na ndege watano ukampiga mmoja na bunduki watabaki wangapi?"
Dogo nae akajibu "hamna atakaebaki wataruka wote"

Kukosea email

Mwanaume mmoja alikosea email address wakati anamtumia mkewe bila ya yeye kujua akaituma ikaenda kwa mtu mwingine. Mwanamke mmoja mjane alipotoka kumzika mumewe akafika nyumbani na kwenda kusoma email za pole na rambi rambi alipofungua email akazimia! Mtoto wake kuja akawa anamnyanyua alipoisoma email akakuta imeandikwa hivi:
To: My Loving Wife
Subject: I’ve Reached Safely
Date: 21 st July, 2004.

Kuku wa kufuga

Dada mmoja kila alipoenda nunua kuku 100 siku mbili mbele anaenda kununua tena, mara ya tatu alipoenda akamuambia muuza vifaranga "itakua nakosea, nawapanda chini sana"
(Yaani akiwapanda kama mbegu za mahindi)

Siku mbaya

Jamaa mmoja alikua bar amekaa akiingalia glasi yake yenye kinywaji kwa zaidi ya nusu saa! Akatokea jamaa mmoja alikimuangalia akichofanya akaichukua na kunywa....
Mwenye bia akaanza kulia. Jamaa akamuambia "usijali takununulia bia ingine acha kulia"

Mwenye bia akaanza kunena "kazini leo nimefukuzwa, gari yangu pia imeibiwa, waleti nimeisahau kwenye taxi, nyumbanio mke wangu memfumania na house boy, na hapa umekunywa sumu yangu yote nliyotaka kuinywa......"

Mtoto wa nani?

Wakiiomba mahakama iamue nani anapaswa kuishi na mtoto.
MKE: Mtoto ni wangu nilibeba mimba miezi 9, nikajifungua na kumnyonyesha.
MUME: Akauliza; "hivi nikichomeka ATM card kwenye mashine ikatoa pesa, pesa ni za ATM au zangu niliyechomeka card?"
Hakim aliinama kwa aibu kisha mzee akapewa mtoto!.

Friday, June 24, 2011

Fundi kompyuta

Mteja: Fundi afadhali umekuja, laptop yangu inapata sana joto kupitiliza. Basi jamaa baada ya masaa kadhaa aliporudi akamuuliza fundi "enhe umelitatuaje tatizo?"
Fundi akajibu "nimeonelea niiweke kwenye friji ipoe kwanza"

Hesabu

Mama: Mkono mmoja nna machungwa 7 mwingine 8 je nna mangapi jumla?
Mtoto: Utakua una mikono mikubwa.

Glovu

Jamaa mmoja alivaa glovu (glove) mkono mmoja akaulizwa kulikoni nae akajibu, "kwenye utabiri wa hali ya hewa kwenye tv wamesema mkono wa kushoto kutakua na joto, mkono wa kulia kutakua na baridi"

Kwa umri huu....

Baba: We mtoto, Frank kwa umri wako alipata Fisrt Class degree. Wewe unasubiri nini?
Mtoto: Baba, Hitler katika umri wako alijiua wewe unasubiri nini?

Mlevi huyu mhh

Mlevi alipiga simu polisi: Gari yangu imeibiwa dashboard, gia, staring, accelerator hata break....
Polisi kabla hawajaanza kuja akapiga tena na kusema "ooh nimekosea kumbe nilikaa kiti cha nyuma"

Thursday, June 23, 2011

Mambo ya bafuni

Mtoto mmoja akimuambia mama yake, "mama mi naona unapataga shida, si umuambiage baba akusugue na dodoki mgongoni wakati wa kuoga kama baba anavyomsuguaga jirani yetu ukisafirigi"

Kutolewa mahari!

Jamaa mmoja alienda kwa wakwe kujitambulisha ili siku chache akatoe mahari.
Wakwe wakamuambia kwa mwanetu haina haja ya kutoa mahari uje tu umchukue.
Jamaa akawaambia "mmh! bure bure!? au mwanenu bomu lasubiri wa kumlipukia?"

Alfajiri mlangoni

Mwanamke mmoja alienda kufungua mlango, kumbe alikua mumewe ndio anarudi:
Mke: Haya alfajiri hii saa 12 ndio unarudi toka bar, umefuata nini?
Mume: Breakfast.

Mke mpenda zawadi

Mke alimuuliza mumewe,"Mbona siku hizi huninunulii zawadi kama pale kabla hujanioa?" Mume akamjibu "umeniona mimi kichaa? Tangu lini mtu akampa chakula samaki baada ya kumvua!"

Wednesday, June 22, 2011

Chuo

Mhadhiri mbele ya wanachuo darasani alinena "anaejiona yeye ni mjinga kuliko wote asimame" darasa likawa kimya kwa sekunde kadhaa punde mwanachuo mmoja akasimama. Mhadhiri akauliza "wewe ndio mjinga kuliko wote humu?"
Mwanachuo akajibu "hapana, nimeona umesimama peke yako muda wote"

Mtoto shuleni

Mtoto mmoja akimuambia mama yake "mama leo nimepewa adhabu kwa kitu ambacho sijakifanya" Mama yake akanena... "haiwezekani naenda huko huko shuleni... Kwanza umefanya nini shuleni?" Mtoto akajibu "sijafanya homework"

Kazi ni kazi

Unajua watu wanaishije mjini?
Watu wana kazi zinazowaweka mjini.
Kuna kikundi chenyewe kazi yao kukodiwa kwenye misiba kwa dhumuni moja tu nalo ni ''kulia tu'' huwa wanapata kwanza historia ya marehemu the rest yatafuata baada ya hapo...

Tuesday, June 21, 2011

Passport size

Jamaa mmoja alienda migration kufuatilia passport, moja ya swali aliloulizwa ni kama ana picha passport size mbili akajibu ''mimi nna moja'' akumgeukia rafiki yake na kumuambia ''aisee una picha moja uniazime niwe na mbili?''

Monday, June 20, 2011

Radio kwa fundi

Jamaa mmoja alipeleka radio kwa fundi, fundi akamuuliza ''nini tatizo la radio yako?''
Mwenye radio akajibu ''mtangazaji nimemsikia amesema ana mafua, itakua sijaipuliza vumbi muda mrefu kwa sababu.''

Saturday, June 18, 2011

Nasa kibao

Mwanamke mmoja alimnasa kibao jamaa.
Mwanaume alie karibu akauliza "mbona kukupiga kulikoni?"
Jamaa akajibu: Fulana yake usawa wa matiti imeandikwa gusa hapa. Ndio niligusa.

Jirani akichimba...

Jamaa alimkuta jirani yake anachimba shimo:
Jamaa: Vipi mbona umechimba shimo kwema?
Jirani: Samaki wangu wa kufuga amekufa.
Jamaa: Pole, sa shimo lote hilo kasamaki kale tu?
Jirani: Kubwa kwa sababu yumo ndani ya tumbo la paka wako.

Gari mbele mara nyuma

Gari lilikua linaendeshwa, ghafla likawa linaenda mbele mara nyuma, mpaka mtu mmoja akamuita trafic.
Dereva wa gari akanena: Doh afathali trafic umekuja. Nimeona mti mbele nkaogopa kuugonga, mbele kidogo nkaona mti mwingine. Nkaogopa kuugonga!
Trafik akanena: Mama sio mti ni hiyo Air Freshner yako hapo umeiweka kwenye dash board.

Manesi na utani kwa dokta

Manesi watatu walipanga kumtania dokta wanaefanya nae kazi.
Baadae wakakutana kila mmoja kumpa mwenzake mrejesho kila mmoja kamfanyia utani gani dokta:
Wa kwanza: Mi nliweka pamba kwenye kipimo cha kusikilizia mapigo ya moyo ili asisikie.
Wa pili: Mie yangu ndio kali, nimetoboa tundu condom zake zote.
Nesi wa tatu akazimia.

Jambazi kuvamia kanisa

Jambazi alivamia kanisani na bunduki akasema-haya wanaosema wanampenda Yesu wabaki humu ndani, wasiompenda watoke nje. Waumini wote kwa kuogopa kifo wakatoka nje. Ndani akabaki mchungaji na wazee wawili tu-Jambaz akamgeukia mchungaji akasema "mtumishi unaweza kuendelea na ibada, nlitaka kukuondolea wanafiki."

Kumsaidia mke

Jamaa::: Nashindwa kumsaidia mke wangu anakaa macho hadi saa 11 alfajiri kila siku. Mwenzake akamuuliza "anakua anafanya nini?" Ndipo jamaa akajibu "ananisubiri mimi nirudi toka bar"

Fundi na spana...

Chizi mmoja alichukua spana na kwenda benk mlangoni akakutana na mlinzi, akamuliza "unakwenda wapi na hiyo spana?" akajibu "nakwenda kufungua akaunti"

Friday, June 17, 2011

Usalama uwanja wa ndege

Jamaa mmoja alikua akikokota kitoroli cha 'airport akiwa na mabegi yake huku akiwa amevaa chupi, na singland yake, ikimaanisha mkanda, suruali na shati pamoja na viatu kavishikilia.

Askari mmoja akamuuliza "vipi mbona unatembea nusu uchi?"
Ndipo jamaa akajibu "ntavaa baada ya security check zote hapa airport, kuepuka usumbufu wa vua vaa vua vaa"

Mifupa mingapi?

Daktari mmoja akimuelekeza jambo mtu chumba cha daktari.
Dokta: Unajua kwenye mwili wa binadamu kuna mifupa zaidi ya 500.
Jamaa: Dokta! Shhhhh! Taratibukuna mbwa wawili wapo na wazungu hapo mapokezi....

Kukata roho

Mwanaume mmoja kabla hajakata roho akawa anamuambia mkewe "mke wangu nikuambie kweli kabla sijafa, nimetembea na wanawake wengi, nilikudanganya nitachelewa kurudi kumbe nilikua na wanawake....."
Mkewe nae akajibu "we unadhani kwa nini nimekuwekea sumu?"

Malavi davi

Mwanaume mmoja akimuandikia mpenzi wake email walieachana miezi kadhaa kama ifuatavyo "mpenzi wangu nakubali kosa nlilolifanya, naomba turudiane, nitakupa raha ya moyo, mawazo hayaniishi juu yako mapenzi kwako hayana mfano. Nakupenda sana na Hongera kwa kushinda mchezo wa bingo milioni 100"

Matatizo kwa Dokta

Mgonjwa: Dokta nahitaji unisaidie, nna stress, hasira hovyo na watu hata sijielewi nna nini?
Dokta: Haya nielezee tatizo linalokusumbua.
Mgonjwa: Dokta we mzima? Si nshaelezea kila kitu?

Mwanamke kwa dokta wa meno

Mwanamke mmoja kwa daktari wa meno wakati anang'oa jino yale maumivu ikabidi apeleka mkono wake kwenye korodani za daktari. Dokta akanena "mama samahani mkono wako umenishikilia ikulu" mwanamke nae akajibu "maumivu nnayoyapata hapa sasa tutaenda sawa"

Thursday, June 16, 2011

Nyoka

Mwalimu akiwaambia watoto kwenye darasa moja la english medium, "In this box, I have a 10-foot snake" bila kuchelewa katoto kamoja kakanyoosha mkono na kujibu "teacher, You can't fool me, Teacher... snakes don't have feet."

Huko jela...

Jamaa mmoja aliulizwa na mwenzake wakiwa jela:
Mfungwa: Imekuwaje umeletwa humu?
Mfungwa mgeni: Nilimpata farasi.
Mfungwa: Farasi ndio uletwe jela?
Mfungwa mgeni: Ndio, nilimpata kabla mmiliki hajampoteza!

He he he...

Kijana mmoja akimsimulia mwenzake jambo: "nilipokua mdogo nilikua nikisali nipate baiskeli, baadae nkaja gundua Mungu hajaniwezesha kupata. Hivyo basi nikaiba baiskeli na kusali ili nisamehewe"

Dawa ya kichwa

Mama mmoja mwanae alimuambia kua kichwa chamuuma sana hali ikawa hivi:
Mama: Mwanangu pole, kunywa dawa hii kitapoa tu.
Mtoto: Asante mama, dawa gani hiyo?
Mama: Hii panadol itakusaidia.
Mtoto: Itanisaidiaje wakati nikimeza inaeda tumboni badala ya kichwani sasa?

Mlevi kubatizwa

Mlevi mmoja alikua akipita eneo akaona watu wanabatizwa mtoni, akaenda mpaka eneo husika mchungaji akamuita ili ambatize. Akazamishwa mara moja na kutolewa:

Mchungaji: Kaka umemuona Yesu?
Mlevi: Bado.
Akazamishwa tena mara ya pili jibu likawa lile lile, mara ya tatu akaulizwa.

Mchungaji: Umemuona Yesu sasa?
Mlevi: Hapana, una uhakika kweli kaingia humu?

Wednesday, June 15, 2011

Kisiwa

Mwalimu aliuliza darasani "nani anaweza kuniambia kisiwa ni nini?"
Mwanafunzi mmoja akajitolea kujibu "kisiwa ni ardhi iliyozungukwa na maji pande zote kasoro moja tu"
Mwalimu akauliza "pande moja? ipi?"
Mwanafunzi akajibu "upande wa juu tu"

Siku ya kwanza shule

Mama: Umeionaje siku yako ya kwanza shuleni leo?
Mtoto: Ina maana na kesho naenda tena?

Vijiti (toothpick)

Jamaa mmoja mgeni mjini alitengewa chakula ugenini (uzunguni), meza ilipendeza msosi.
Baada ya kumaliza kula mwenyeji wake akamuuliza "kuna vijiti (toothpick) viliwepo hapa viko wapi?"

Jamaa akauliza "vile kwenye kichupa cha plastic?"
Mwenyeji akajibu "ndio ivo ivo"
Jamaa akajibu "mi nilijua vinaliwa na vyenyewe nimekula vyote"

Fluu

Askari mmoja alipiga chafya tatu mfululizo, boss mwenye nyumba anayolinda akamuambia "aisee taratibu usije wapatia vim-mbwa vyangu mafua"

Biashara matangazo

Mfanya biashara mmoja alienda kwenye mgahawa mmoja kupata mlo hali ilikuwa hivi:
Mfanya biashara: Juzi nilikuka nikapata pande kubwa la nyama, mbona leo kadogo hivi?
Mhudumu: Kwani ulikaa meza gani ulipokuja?
Mfanya biashara: Nilikaa pale penye lile dirisha kuubwa...
Mhudumu: Oh! Kawaida tunampatia mteja anaekaa pale ni sehemu nzuri ya kujitangaza mgahawa wetu.

Tuesday, June 14, 2011

Lift au kutembea?

Askari polisi wa barabarani wawili walikua wanaenda kazini:Askari wa kwanza: So tunapanda Basi au tunatembea kwenda job?Askari wa pili: Tusubiri tuone gari ya kwanza kufika....

Mapenzi yanapoisha...

Mwanaume akimuambia mkewe
Mume: Nikiondoka sidhani kama utapata mwanaume kama mimi tena maishani?
Mke: Nani kakuambia nataka mwanaume kama wewe?

Wapi hela?

Babu mmoja alikua anaishi peke yake, nyumba ya nyumba yake alitamani kulima viazi ila uzee ndio shida. Mwanae pekee yupo jela angemsaidia. Hivyo basi mwanae alimuandikia barua baba ake imeandikwa hivi "Baba zile hela nimezifukia numa ya nyumba, usifukue mpaka nitoke"

Siku ya pili askari walifurika eneo kufukua fukua bila kukuta kitu, mwanae akamuandikia baba yake barua ingine akiwa jela, "baba huo ndio msaada pekee nimekupatia haya panda sasa viazi"

Dogo akiomba msaada baada ya...

Katoto kavulana: Njoo haraka haraka kuna mwanaume anampiga baba angu zaidi ya dakika 20 sasa!
Polisi: Kwa nini hukuniambia awali?
Katoto: Kwa sababu baba ndio alikua anamdunda dakika chache zilizopita.

Happy Birthday Chekazone

CHEKAZONE IMETIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUANZA KWAKE.
NAWASHUKURU NYOOTE TULIO PAMOJA KIPINDI CHOTE HIKO.
TUENDELEZE MCHAKATO WA KUTABASAMU NA KUCHEKA.
CHEKA UNENEPE MAISHA NI MAFUPI SANA.

Wanaume Vs wanawake

Mwanamke mmoja aliwauliza wanaume wawili "intakuwaje mwanamke akitawala dunia?"
Mwanaume mmoja kwenye group akajibu "kutakua hamna vita, ila wivu utakua mwingi na baadhi ya nchi hazitaongeleshana"

Polisi na Dereva

Jamaa mmoja alisimamishwa na askari wa usalama barabarani:
Askari: Mzee unatambua kuwa ulikua spidi sana?
Jamaa: Ndio askari.
Askari: Unaharakia wapi?
Jamaa: Unajua nini! Mke wangu ametoroka na askari kama wewe. Sasa nikadhani ndio wewe unamrudisha.

Saprize

Mume mmoja alipanga kumfanyia mkewe Surprise!
Akanyoa nywele za kifuani zote, kufika home akaunganisha kitandani alipolala mkewe. Mke kumgusa akanena "oh shemeji umekuja saa ngapi?".

Hii ya siku mingi

Wodi ya vichaa walichorewa kuku ukutani, wakaambiwa wamkamate! Woote wakaenda kasoro mmoja tu.
Wakamuuliza we vipi mbona hendi mkamata akajibu "shhhh nataga"

Adhabu

Mwanafunzi: Mwalimu unaweza niadhibu kwa kitu ambacho sijafanya?
Mwalimu: Hapana kabisa.
Mwanafunzi: Ohh! Basi sijafanya homework bado.

Kufiwa

Mwanaume mmoja aliefiwa na mke siku moja mbele mvua kuubwa ikanyesha sana. Basi alipoiona ile mvua akanena "Itakua ameshafika mbinguni"

Bifu la majirani

Jirani 1 akimuuliza jirani wa pili "huyu mbwa wako ananikera sana, anamfuata mbwa wangu kila kukicha"
Jirani wa pili akajibu "we shida yako nini, mie nampaga condom kila siku kabla hajamfuata mbwa wako"

Tangazo tata

Mwanaume mmoja alikua anamtafuta mke wake asijue yupo wapi?
Akakutana na jirani yake na kumuambia "nimemuona mkeo kaja chukuliwa na boss wako" jamaa mwenye mke akajibu "ooh basi nsije katwa mshahara bure atarudi baadae"

Denti wa kiinglish

Mwanafunzi mmoja aliekua akijifunza lugha ya kiingereza kama lugha ngeni, sasa akawa amemkuta mwalimu wake wa kiingereza kasimama kwenye kinjia alichotaka kupita, kuonyesha kama ameanza ku-masta kimombo akenena ili apishwe "excuse me can I pass away?"

Bomu

Vijana wawili waliokota mabomu mawili, wakashauriana wayabebe kuyapeleka ama kuyarudisha jeshini. Mmoja akauliza "je moja likilipuka?"
Mwenzake akajibu "tutadanganya tumeokota moja tu"

Ngumii

Katoto kamoja kalimkimbilia polisi na kunena:
Mtoto: Askari kuna watu wanapigana palee...
Askari: Baba yako nani?
Mtoto: Ndio wanapigania hicho hicho.

Trafik polisi

Jamaa wawili walipanda pikipiki mbele kidogo wakaona trafik akionyesha ishara ya kuwasimamisha. Jamaa aliepakiwa kwenye pikipiki akamuambia dereva "sasa sie tushajaa ye anataka kukaa wapi au labda hatujafunga mkanda?"

Monday, June 13, 2011

5 + 5 = ?

Mwalimu aliuliza 5+5 jibu ni ngapi?
Alikataza kuhesabu vidole, basi dogo mmoja wa kiume akaingiza vidole ndani ya pensi ili ahesabu kimya kimya mwisho wa siku akaibuka na jibu "mwalimu jibu ni 11"

Meseji...

Jamaa mmoja alituma meseji kwa rafiki zake kama ifuatavyo:
"Wishing you happy independence day.
Oh sorry, this massage is only for singles..
Married people, please ignore it.."

Nani chizi?

Jamaa mmoja alikua yupo bar na palikua na kelele kweli, akanyakua simu yake ya kiganjani na kumpigia rafiki yake fulani aliyekua yupo tu nyumbani. Maongezi ya jamaa yalikua hivi:

Aliepo Bar: Haloo! Haloo! Sikusikii vizuri sijui upo kwenye makelele sogea palipo na utulivu.
Aliepo nyumbani akajibu: Mimi au wewe ndio yupo penye kelele?

Ugonjwa wa kusahau

Mgonjwa: Dokta nna ugonjwa wa kusahau.
Dokta: Limekuanza lini hilo tatizo?
Mgonjwa: Tatizo gani?

Siendi shule

Mtoto: Mama mi kesho siendi shule bwana.
Mama: Kwa nini mwanangu?
Mtoto: Mwalimu mwenyewe hajui kitu juzi katufundisha 9-4=
5, Na jana tena katufundisha 6-1=5...

Mke akinena...

Mke: Nataka nikuambie kitu ila usininase kibao.
Mume: Sema tu uwe na amani.
Mke: Nina ujauzito.
Mume: Sasa ulikua unaogopa nini?
Mke: Nilisemaga kabla hujanioa kwa baba akaninasa kibao.

Zama za ukoloni

Mwalilimu aliuliza swali darasani "tulitawaliwa toka wapi hadi wapi na wakoloni?" Mwanafunzi mmoja akajibu "enhe sina uhakika sana ila nnadhani ukurasa wa 60 mpaka wa 65"

Plani za ndoa

Msichana: Darling wangu tuki-oana nataka kushea nawe shida na matatizo yote na wewe.
Mvulana: Oh! Sawa lakina mimi sina shida wala matatizo yoyote ya kushea na wewe.
Msichana: Kwasababu hatujaona bado...

Nyumba ya watatu

Mke: Mume wangu ile nyuma tuliyopata tutaishi watatu badala ya wawili. Mume akajibu "ooh imekua baraka enhe safi sana"
Mke akamalizia "nakushukuru sana kwa kukubali, kuanzia kesho mama yangu ataishi nasi"

Tajiri wa wake

Tajiri mmoja alikuwa na wake wengi. Kudhibiti wafanyakazi wake akawawekea tego kwa wakeze ili mwanaume akitembea na mkewe naniliu inaliwa.

Aliporudi safari akafanya ukaguzi kwa wafanyakazi wake akiwafunua, kila aliyemfunua imeliwa. Wa mwisho akamkuta ipo safi basi akamsifu na kumwambia yeye ndie wa kuigwa.

Akamuuliza jina yule kijana akanyamaza na kujifanya kuongea kama bubu. Kumfungua mdomo kumbe ulimi umeliwa!

Sapraizi

Dokta akiaonge na mteja wake:
Dokta: Dah hongera umekua baba sasa.
Mteja: Tafadhali usimuambie mtu nataka kum-surprise mke wangu!

Ndoto ya panya

Dada: Baba tangu juzi naota panya anacheza tebo tenesi.
Baba: Usiogope ni kawaida tu.
Dada: Je nifanyeje nimeze dawa au?
Baba: Ya nini wakati leo ndio Fainali.

Darasa kuhama

Mwalimu: Haya wanafunzi kesho darasa litaenda kwenye juani..
Mwanafunzi mmoja akaonge: Mwalimu mi sitakuja.
Mwalimu akauliza "kwa nini?"
Mwanafunzi: Mama yangu hawezi niruhusu kwenda mbali kote huko.

Kaazi kweli kweli

Jamaa alipokua kwa daktari wa meno:
Mgonjwa: Dokta fasta nikatoe viatu vyoote sebuleni rafiki yangu anakuja leo home.
Dokta: Kwanini? Rafiki yako ni mwizi?
Mgonjwa: Hapana asije akavitambua viatu vyake.

Inzi kwenye supu

Mteja mmoja alimuita mhudumu ande alipo kwenye meza aliokaa!
Mteja: Hii supu uliyoileta kuna inzi amefia humu.
Weita: Yaah hawa hawajui kuogelea usijali

Kula kucha

Jamaa: Dokta mie nashindwa kuacha kula kucha je nifanyeje?
Dokta: Njoo nikusaidie, ning'oe meno yako yote itasaidia sana.

Kwenda Outing

Mume na mke walienda hotelini, punde mwanamke mmoja akamsalimia mume. Mke aka-mind na kuuliza "nani yule?"
Mume akamjibu: Tafadhali usini-disturb yule nae ataniuliza swali hilo hilo."

Watu wawili baa

Maongezi ya watu wawili wanaume:
Jimmy: "Umesema una mtoto wa kiume sio?
Hussein: Ndio.
Jimmy: Anavuta sigara?
Hussein: Hapana.
Jimmy: Anakunywa pombe?
Hussein: Hapana.
Jimmy: Anarudi usiku?
Hussein: hapana
Jimmy: Basi mwanao mtulivu sana, ana umri gani sasa?
Hussein: Ametimiza miezi sita sasa

6 x 7 = ?

Mwalimu: Haya nani anijibu 7x6 jibu ngapi?
Mwanafunzi: Jibu lake 42
Mwalimu: Haya je 6x7 jibu ni?
Mwanafunzi: jibu ni 24

Mhudumu na Mteja

Mteja kwenye restaurant moja akiongea na mhudumu "mhudumu, huyu kuku siwezi kumla niitie meneja wako"
Mhudumu nae akajibu "hata yeye akija hawezi kula huyo kuku"

Gazeti...

Mwanamke akimuuliza mumewe "kwa nini unaweka magazeti kwenye friji?" Mume akajibu: Yote yamejaa Hot News tuu.

Unataka kuwa?

Mwanaume mmoja aliulizwa " unataka kuwa nani?"
Nae akajibu "nataka kuwa mende"
Jamaa akamuuliza "mende? Kwa nini?"
Mwanaume akajibu "ili mke wangu aniogope

Kibweka

Girlfriend: Navyokupenda, nitakufa kwa ajili yako?
Boyfriend: How soon?

Ramani...

Mwalimu: Hellen shika atlas onyesha India iko wapi?
Mwanafunzi akaonyesha na kupatia.
Mwalimu akauliza darasa "nani kagundua India"
Wanafunzi wakajibu "Hellen"

Kengere ya mlango

Mwanamke mmoja alikua anamsubiri fundi aje kumtengenezea kengele ya mlango wa nyumba yake. Zikapita siku 4 bila fundi kutokeza, akampigia simu kujua tatizo fundi kwenye simu akajibu "nimekuja kwako siku 4 mfululiza nabonyeza kengele hamna anafungua mlango."

Utofauti kati ya....

Dada na jamaa mmoja walikua katika maongezi yao kama ifuatavyo:
Dada: Eti mwanamke akitembea na wanaume 3 wanamuita malaya. Ila mwanaume akitembea na wana wake 10 wanamuita mwanaume rijali.

Jamaa nae akanena: Kufuli ikifunguliwa na funguo tatu todauti wanaiita mbovu. Ila Funguo moja ikifungua kufuli 10 tofauti wanaiita master key.

Mzungu mgahawani

Mzungu mmoja alishindwa kula kwenye mgahawa mmoja na kumuambia mhudumu "waiter this food test funny" Mhudumu nae kimombo kinapanda kidogo akajibu "test funny? Why you are not laughing?"

Kwa Dokta

Mgonjwa: Dokta nna tatizo moja.
Dokta: Tatizo gani?
Mgonjwa: Nikionge na mtu simuoni.
Dokta: Imekutokea lini?
Mgonjwa: Kwenye simu.

Sunday, June 12, 2011

Dogo na maswali

Mtoto: Baba mbona tumbo la anti kubwa?
Baba: We nawe wajua kila kitu?
Mtoto: Hapana baba sijui kabisa.
Baba: Ok! Ni limejaa tu maji si kingine.
Mtoto: Hee! Sa mtoto si atazama kwenye maji?

Mchaga hospitalini

Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza "nipo wapi hapa?"

Nesi akajibu,"umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono."
Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex?
Ipo mzee, nesi alijibu.

Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji.
Mgonjwa: Yeuwi... Wamefunga duka?

Mchaga hospitalini

Mchaga alipata ajali alipozinduka pale hospitali akauliza "nipo wapi hapa?"

Nesi akajibu,"umepata ajali, hapa upo hospitali. Bahati mbaya umekatika mkono."
Mgonjwa: Na je saa yangu ipo wapi ya Rolex?
Ipo mzee, nesi alijibu.

Nesi: Mkeo na watoto wapo hapa kukufariji.
Mgonjwa: Yeuwi... Wamefunga duka?

Kichaa kapewa mimba

Jamaa alimpa mimba binti wa kichaga, Baba mtu akapanga kumuua jamaa.
Mwanye mimba akamfata mzee na kumwambia "Mzee punguza jazba, ni kweli mi ndiye nimempa mimba binti yako na kusema kweli sitamwoa ila akizaa mwanaume nitakupa Bilioni 1, akizaa mwanamke nitakupa milioni 58 na duka kariakoo"

Mwenye mimba akanena tena: "Je ikitokea bahati mbaya mimba ikaharibika itakuwaje ?"
Mzee akajibu: Aisee baba angu itabidi umpatie nyingine hamna jinsi!

Malavidavi

Katikati ya maongezi kati ya wapendanao wawili mwanaume akamuambia mchumba wake "Nitaenda mpaka mwisho wa dunia kwa ajili yako" ndipo mwenza nae akajibu "utakaa huko huko au utarudi?"

Kazi

Boss mmoja akiongea na mmoja wa wafanyakazi wake kama ifuatavyo:
Boss: Tunahitaji mtu atakaefaa kwenye hii nafasi ambae ni responsible.
Mfanyakazi: Boss unaemtafuta ushampata, nikipofanya kazi mwanzoni kitu kikienda hovyo tu wananiambia mie ndio responsible...

Maneno ya wapendanao

Mwanamke mmoja akimuambia mpenzi wake "njoo ndani ya moyo wangu wewe ndio wangu"
Mwanaume akajibu "nije na malapa au niyavue?"

Zoezi Darasani

Ndani ya darasa moja mwalimu alitoa zoezi waandike Insha kuhusu kiwanja cha mpira wa miguu anachokifahamu... Bahati mbaya ama nzuri mwanafunzi mmoja alikua kakaa tuu hafanyi lolote mwalimu akamuuliza "we vipi mbona huandiki chochote"

Ndipo mwanafunzi akajibu "kulikua na mvua kiwanja kimejaa maji talowesha karatasi yangu."

Gari na Gia

Baba alishindwa vumilia akamuuliza mwanae.
Baba: Khalid kwa nini ukienda kwa Hussein unatumia saa moja kufika ila kurudi watumia masaa manne?
Mtoto: Unajua nini? Kwenda gia ziko mpaka nne, wakati wa kurudi ipo gia moja tu.

Nani kaanza...?

Baba na mwanae wakiambia jambo:
Baba: Mwanangu safari hii upate japo maksi zifike 97%
Mtoto: Nitapata 100% kabisa nini 97%?
Baba: Embu acha utani kwanza....
Mtoto: Nani ameanza kwanza?

Kitabu kipi?

Mwanamke mmoja wakati anahojiwa aliulizwa swali lifuatalo "je! Unapendelea kitabu gani hasa katika maisha yako?"
Mwanamke akajibu: Cheque book cha mume wangu.

Gelfrendi na boifrendi

Gelfrendi: Nataka tuachane, nakurudishia vitu vyoote ulinipatia...
Boifrend: Ok! Anza na kisses zoote...

Gari au mwanamke?

Katika maongezi vijana fulani walikua wanaongelea kati ya gari au mkeo nani wampenda zaidi, jamaa mmoja akadakia "weweee gari ndio nalipenda, maana gari ndio litaleta mke (mwanamke)... si kinyume chake" wenzake walicheka sana.

Cha mwaka hiki...

Jamaa alienda kwenye party, pale mezani zikaletwa "tissue" wakati meza inaandaliwa si akazifakamia na kuanza kuzila akijua mkate mweupe, walipomuuliza akajibu mi niliona mikate yenyewe kidogo nkasema nianze kula haraka haraka...

Usichana unapoanza

Dada mmoja akimsimulia msichana mwenzake umri unafana fanana kidogo aliekianza usichana na urembo "napenda lipstick, ni nzuri na zina-test nzuri sana"

Siku iliyofuata yule mwenzake akarudi na kumuambia mwenzake...
"We ni muongo, nimenunua lipstick 10 na kula zote sio tamu"

Maisha ya ndoa

Mtoto mmoja alimuuliza baba ake, "baba nini siri ya ndoa yenye furaha?"
Baba nae bila hiyana akamjibu mwanae "bado ni siri mwanangu"

Za hospitali

Jamaa akimsimulia mwenzake jambo "tulipokuwa hospitali marafiki walikuja kuniona na kuniuliza 'how are you?"
Jamaa akaendelea kuonge tena "Walipokuja washkaji zangu wa karibu wakaniuliza 'vipi nesi wa ukweli?"

Saturday, June 11, 2011

Muchumba wa zamani

Mwanamke: Mume wangu unamuona yule pale alielewa mno?
Mume: Ndio, ni nani?
Mwanamke: Alikuwaga mpenzi wangu zamani, alikataa ndoa mi na yeye..
Mume: Ohh! Ndio maana anasherekea hadi leo...

Peni na Dokta

Mzee mmoja alimpigia simu daktari na kumuambia "dokta! Mwanangu kameza peni"
Dokta akajibu "tumia penseli wakati nakuja"

Baba mkwe na mkwewe

Jamaa alikwenda kwa ba mkwe wake kumpa shukran na ilikuwa hivii,
" baba nashukuru sana yaani umenipa mtoto mzuri, mtamu kitu yake ni swaafi kabisa!!"

Mzee akamjibu "sasa ungeonja ya mama ake ungechanganyikiwa."

Friday, June 10, 2011

Mkwe na Mkwewe

MAMA MKWE: "Binti samahani, ukweli mtoto hafanani na Kijana wangu kabisa"
BINTI: Mama bila samahani,huku chini nina njia ya Uzazi na sio Machine ya Photocopy.

Thursday, June 9, 2011

Kuoda vinywaji

Kulikuwa na akina kaka watatu pale bar:
Wa kwanza: Mhudumu niletee juice na glass.
Wa pili: Mhudumu mie naomba fanta na tissue.
Huyu wa tatu alikua mgeni kidogo mjini hali ikawa ivi....
Wa tatu: Mhudumu mie naomba niletee tissue ya baridi na glass.

Maasai

Mmaasai alinunua gari "manual gear" sasa akawa anamsimulia mwenzake wa umasaini kwenye simu "asee eloroi mekwisa nunua gari mekuta na rungu ingine ndani"

Mtoto mdadisi

Mtoto mmoja akimsimulia mama yake, "mama mtafutie baba kopo ka kutemea mate" Mama akiuliza kwa mshangao "koopo?" Mtoto akajibu "ndio mama maana kila ukisafiri. lazima atatema tu mate kwenye maputo kati ya mawili au matatu nayakutaga chini ya uvungu"

Msaada wa mmaasai

Mmaasai alikua akimuangalia driver wa bus akicheza na gear wkt wote wa safari. Abiria na dreva waliporudi toka lunch katikati ya safari wakakuta mmaasai kaichomoa gear yote kuulizwa na driver akajibu "mekusaidia kuing'oa meona saa nyingi we naangaika kuitoa"

Wagonjwa wa akili

Wagonjwa wa akili wawili walisimamishwa ghorofani kisha wakaambiwa wakojoe kuelekea chini.
Wa kwanza akasema "dokta parefu bwana mkojo wangu utaumia"
Wa pili akasema "naogopa wataudaka wapita njia na kunivuta chini bure nikafa"

Mlevi wodini

Mlevi mmoja alishikwa na homa kali ghafla, akapelekwa hospitali. Alipofikishwa wodini ili apewe mapumziko akakutana na walevi wenzake wanne nao wamelazwa jamaa akafurahi sana na kumuambia nesi aliyewepo zamu muda huo "nesi zungusha round ya tatu bill kwangu"

Mbu

Mbu mmoja alimkuta mwenzake amekaa kwa masikitiko akamuuliza mwenzake "vipi mbona huingii mzigoni leo?"
Mbu mwenzake akamjibu "dah nasikitika sana, nilijua leo nimepata mzungu kumbe mdoli bwana na sindano yangu imevinjikia"

Wednesday, June 8, 2011

Mume na mkewe

MUME: Vipi mpenzi leo umekula nini maana sikuacha hela ya mlo.
MKE: Tumeshindia mapera na shemeji yangu mpenzi, mimi ndio nilipanda juu ya mti.
MUME: Inamana shemeji yako alibaki chini ya mti.
MKE: Ndiyo.
MUME: Alitaka kuangalia chupi yako mi namjua mdogo wangu.
MKE: Unafikiri mi mjinga nilimshtukia nikaivua nikapanda uchi

Ka-herufi kamooja tu...

Jamaa mmoja ilimtokea hii, alisahau kuweka herufi moja tu "e" mwishoni mwa sentensi wakati akimomuarifu mke wake kwa sms akiwa safarini kikazi. Aliandika sms kwa mkewe kama ifuatavyo "I am having such a wonderful time! I wish you were her..."

Jamaa aliopoa....

Jamaa mmoja aliopoa na mabo yalikua hivi:
Msichana: Naomba nikuambie ukweli, mimi ni malaya najiuza usiku ili nipate hela.
Jamaa akanena na yeye: Usijali nitakupatia 15,000Tsh tukimaliza...

Baada ya kumaliza hali ikawa hivi:
Jamaa: Naomba nikuambie ukweli, mimi ni dereva taxi na nitakuchaji 15,000Tsh kukurudisha nilipokutoa.

Teja

Teja mmoja alikuwa anavuta bangi, ghafla akasikia sauti ya ajabu akauliza "nani wewe?" Akajibiwa "ni mimi israel mtoa roho" Teja nalo likajibu "Dah... umenistua kweli mi nilijua polisi"

Chumba cha upasuaji

Ndani ya chumba cha upasuaji wakati mgonjwa keshapasuliwa eneo husika dokta akamuambia nesi mmoja wapo kati ya waliopo ndani ya chumba cha upasuaji "Nesi nenda kwenye internet fungua surgery.com halafu peleka mpaka chini ukanisome sehemu imeandikwa "are you totally lost?"

Daktari na Mgonjwa

Mgonjwa mmoja alienda kumuona daktari wake na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mgonjwa: Dokta mbona sipati nafuu?
Dokta: Ulifuata masharti ya dawa niliyokupatia?
Mgonjwa: Ndio, kwenye chupa yanasema "hakikisha chupa ya dawa umeifunga vizuri"
(Akimaanisha hajainywa kabisa).

Tuesday, June 7, 2011

Mende na binadamu

Mende mmoja alimuambia jamaa mmoja kabla hajamuua ''kabla hujaniua mie ndio nineweza mpigisha kelele mchumba ako kuliko wewe''

Mke na Mume

Mke alimuambia mumewe, ''niambie jambo moja litalonifurahisha na kuniudhi kwa wakati mmoja''
Mume naye kama utani akanena ''we ni mtamu zaidi kuliko wadogo zako wa kike''

Wagonjwa wa akili

Wagonjwa wa akili walipanga kutoroka hospitali.
Walipanga wamvamie mlinzi wampige watoroke.
Walipofika mlangoni wakakuta mlango wazi na mlinzi hayupo. Wakanena ''dah mpango wetu wa kutoroka ushafeli'' basi waka wakaghairi.

Password

Jamaa mmoja na mchumba wake walienda mtembelea rafiki yao. Ilipofika wakati wa kulala wakamuomba watumie simu ya mezani kupiga mwenyeji akawajibu ''ooh ina password''

Walipouliza kuhusu computer labda watume email wakajibiwa pia ina password. Mwenyeji akawauliza kama wataoga muda huo au la! Mgeni akanena ''hamna password bafuni?''

Mchaga mpirani

Mchaga mmoja mmoja kwa jina Masawe alikua anacheza nafasi ya goli kipa... Sasa wakati timu pinzani inakuja kushambulia Masawe si akamuona mtu anae mdai akaacha kuokoa goli lisiingie akakimbilia kumdai...

Bikini

Mtoto mmoja alimuona dada mmoja baharini amevaa vile vichupi nyenye asilima kubwa mfumo wa kamba ndipo mtoto akasema/akamuambia yule dada "dada makalio yako yanaitafuna chupi yako imeliwa yote nyuma"

Sunday, June 5, 2011

Nyonyo

Mama mmoja kwenye daladala mtoto wake wakati anakataa kunyonya akawa anamtishi mwanae akimuambia ''nyonya au sivyo ntampa huy baba pembeni'' mtoto ndio ananyonya.

Iliendelea hivyo kwa mara 3 ndipo yule baba nae akanena ''we mama make up your mind ilikua nishuke kituo cha pili kilichopita''

Saturday, June 4, 2011

Jela

Wafungwa watatu walipokutana jela hivi ndivyo kila mmoja alivyokua akimsimulia mwenzake:
Mfungwa wa kwanza: Nimefungwa kwa sababu niliua watu wanne.
Mfungwa wa pili: Nimefungwa kwa sababu niliiba bank.
Mfungwa wa tatu: Nimefungwa kwa sababu niliiba ghorofa. (ili aonekane na yeye sio wa kuja)

Kuchelewa shule

Mtoto akimjibu mwalimu "Mwalimu nimechelewa kwa sababu baba na mama walikua wanapigana, mama alikua anatumia kiatu changu kumpigia baba nilikua nasubiri wamalize nikivae nije."

Thursday, June 2, 2011

Mwalimu na mtoto

Mwalimu akimuuliza mtoto ''wewe jana ulisema mama yako anaumwa?''
Mtoto akajibu ''nilikosea kumbe alikua anaumwa mlinzi''

Babu na mjukuu

Babu akimuambia mjukuu wake ''jifiche mwalimu wako anakuja umetoroka shule leo''
Mjukuu nae akajibu, ''weewe ndio ujifiche nimemdanganya umekufa''

Wednesday, June 1, 2011

Parashuti

Ndege moja ndogo ilibeba watu wanne, punde rubani akatangaza "nasikitika ndege muda wowote inaanguka na tuna pashuti 3 tu sie tupo wanne". Jamaa mmoja mwalimu akawahi moja na kuruka nje ya ndege.

Wa pili kabla hajaruka akamuambia mtoto mmoja kati ya abiria, "chukua na wewe parashuti kabla rubani jakauwahi" ndipo yule mtoto akajibu "usijali wote tutapona, yule alieruka wa kwanza kachukua begi langu la mgongoni kasahau parashuti"

Pombe chakari

levi mmoja alipanda daladala usiku akielekea kwake, kwenye basi akakutana na mwanamke mcha mungu akamuambia yule mlevi "unaenda moja kwa moja motoni"
Yule mlevi akamuamrisha dereva "dereva simama nimepanda daladala sio..."