Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, September 30, 2011

Kwa kinyozi

Njemba ilienda kwa kinyozi na kuuliza "kinyozi ndevu shilingi ngapi?" Kinyozi akamjibu "400Tsh tu"
Njemba ikajibu "ok nifungie za 800Tsh"

Thursday, September 29, 2011

Kipofu kanusa

Kipofu aliingia mgahawa mmoja na kumuambia mwenye mgahawa, "nipe uma iliyotumika ntainusa na kutoa oda kilicholiwa kwa uma hiyo"

Akaletewa na kuinusa kisha akasema "niletee viazi mviringo vya nyama ya kuku" mwenye mgahawa alichoka kwa uwezo ule.

Wiki mbili mbele akarudi, mwenye mgahawa akachukua una na kumuambia mkewe ajifutie ukeni, kisha akampa jamaa aliponusa akajibu "kumbe Nancy nae yupo hapa?"
Mwenye mke alichanganyikiwa mpk jina analijua...nye mgahawa, "nipe uma iliyotumika ntainusa na kutoa oda kilicholiwa kwa uma hiyo"

Akaletewa na kuinusa kisha akasema "niletee viazi mviringo vya nyama ya kuku" mwenye mgahawa alichoka kwa uwezo ule.

Wiki mbili mbele akarudi, mwenye mgahawa akachukua una na kumuambia mkewe ajifutie ukeni, kisha akampa jamaa aliponusa akajibu "kumbe Nancy nae yupo hapa?"
Mwenye mke alichanganyikiwa mpk jina analijua...

Ufafanuziiii

Nini tofauti kati ya Stress, Tension na Panic?
Stress: Mkeo akiwa na mimba.
Tension: Msichana wako akiwa na mimba.
Panic: Both wakiwa na mimba.

Wednesday, September 28, 2011

Wachina Part II

Wachina wawili Dar es Salaam walipata mtoto mweusi!
Mume wa kichina akauliza "mbona mtoto mweusi?"
Mke wa kichina akajibu tunaishi Tanzania, hamna umeme, mimi wa moto, wewe wa moto, mapenzi moto moto... Mtoto kaungua joto...

Wachina

Familia ya Kichina iliamua kwenda marekani majina yao ni Chu, Bu, Hu, Su and Fu. Sasa ilibidi wafanane fanane kidogo majina na ua-merika... Ikawa hivi

Chu akaitwa Chuck.
Bu akaitwa Buck.
Hu akaitwa Huck.
Su and Fu wakaamua kubaki China

Madenge

Madenge alimwambia babake kuwa haendi shule tena Baba akamulizaa "kwanini?"
Madenge: Inaelekea walimu hawana uhakika na majibu yao, juzi wamesema 5+2=7, jana 4+3=7, leo 6+1=7, na kesho huenda watesema 7+0=7, sasa huo siubabaishaji?wamesema 5+2=7, jana 4+3=7, leo 6+1=7, na kesho huenda watesema 7+0=7, sasa huo siubabaishaji?

Saturday, September 24, 2011

Mume wa mtu

Mwanamume alimuangalia msichana aliepita, mkewe akamuambia "acha kuwakodolea wasichana umeshaoa wewe" Mume nae akamjibu "hata kama nipo kwenye diet ndio nsiangalie menu?"

Wednesday, September 21, 2011

Ujinga ni...?

Ujinga ni kutongoza demu kanisani alafu ukamwambie "leo its on me;wacha nikulipie sadaka"

Tuesday, September 20, 2011

Ushindani

Wikipedia: Najua kila kitu!
Google: Nina kila kitu!
Facebook: Najua kila mtu.
Internet: Bila mimi hamna kitu.
Umeme: Endeleeni kuongea....

Kwenye simu

Msichana alipokea simu akaongea nusu saa nzima, alipokata mama akamuuliza "nashangaa leo umetumia muda mfupi hewani" mtoto wake akajibu "ilikua wrong number"

Monday, September 19, 2011

Mlevi na mkojo

Jamaa alilewa, baadae aliposhtuka akahisi amebanwa na mkojo na alivyokua anakojoa huku anajamba mlevi mwenzie akumuliza "mbona unakojoa na kujamba jamba? naye akamjibu kuwa "uliona wapi mvua ikinyesha bila radi kupiga?? We mwendawazimu nini?"

Sunday, September 18, 2011

Jamaa wakati anajitetea baada ya fumanizi.... "Nisameheni jamani shetani alinipitia" Wakamuuliza "alikupitia wakati unaenda wapi?"

Friday, September 16, 2011

Trafiki polisi

Jamaa aliazima gari! Trafiki akamzimamisha na kumuuliza hili na lile kama vipo sawa isipokua fire extinguisher hakuiona. Akatozwa faini... Alipoingia kwenye gari kabla hajaondoka akaiona ilipokuwa akarudi kwa trafic na kumuambia "nimeipata haya nirudishie pesa yangu"

Nsaidie kutoa...

Mwanamke mmoja alimuambia mwanaume "kaka unaweza kunisaidia kutoa kitu kwenye chuchu zangu?"
Yule mwanaume akafurahia kweli na kumuuliza "ni nini hicho cha kutoa?" Mwanamke akamjibu "hayo macho yako ndio uyatoe"
Njemba moja iliagiza supu, wakati anapata hiyo supu mhudumu akamletea na vijiti vya kutolea nyama akishamaliza supu. Mhudumu kabla hajaondoka akamrudisha na kumuambia "dada virudishe hivi kaniletee vya baridi"

Thursday, September 15, 2011

Bia noma

Bar moja mtaa mmoja karibu na makazi ya watu siku moja mwanamke mmoja alikua anakimbizwa na mumewe. Ishu ilikua ugomvi wao, mwelekeo ulikua karibu kbs na meza ya wanywaji fulani.

Yule mama huku akikimbia "nisaidie nisaidie ataniua..." Wale walevi wao walichowahi ni kushika chupa na glass za bie pale mezani ikitokea kajikwaa zisimwagike.

Wednesday, September 14, 2011

Elimu

Baba: Mwanangu elimu ni ufunguo wa maisha!
Mtoto nae akajibu.
Mtoto: Najua baba sema sijakiona kitasa chenyewe.

Monday, September 12, 2011

Porini

Jamaa wawili walipata shida ya gari porini ikabidi waombe hifadhi kijijini. Giza lilipoingia wakapewa kachumba walale kilikua na silaha. Asubuhi wakasikia maongezi ya mke na mume wenyeji wao...

Mume: Tuwachinje wote au mmoja?
Mke: tumchinje mmoja kwanza, mwingine baadae.
Mume: Sawa ngoja tumchinje mmoja.

Masaa mawili baadae wakagongewa mlango na kuletewa wali kwa nyama ya kuku.

Porini

Jamaa wawili walipata shida ya gari porini ikabidi waombe hifadhi kijijini. Giza lilipoingia wakapewa kachumba walale kilikua na silaha. Asubuhi wakasikia maongezi ya mke na mume wenyeji wao...

Mume: Tuwachinje wote au mmoja?
Mke: tumchinje mmoja kwanza, mwingine baadae.
Mume: Sawa ngoja tumchinje mmoja.

Masaa mawili baadae wakagongewa mlango na kuletewa wali kwa nyama ya kuku.

Mahakama ya kizungu

Jamaa alienda kwenye mahakama moja huko majuu, kwa vile kizungu hakikuwa sawa sawa kwake palitokea minong'ono mikubwa mahakamani, hakimu akanena kwa kizungu kupata utulivu "Order... Order.." Jamaa kusikia vile akanena kwa sauti "Burger moja na soda tafadhali".

Kwa kimada

Jamaa ilipfika mida ya swala ya jioni akamuaga mkewe anaenda msikitini, kumbe anaenda nyumba ndogo. Huko alipewa huduma haswaa mpk alipomaliza akapitiwa na usingizi umeme ulipokatika!

Kuja kuhamaki saa tano usiku na missed call za mkewe, akavaa fasta fasta awahi home. Kufika ghafla umeme ukawaka akajikuta kavaa dela la nyumba ndogo akijua kavaa kanzu yake mbele ya mkewe.
Jamaa mmoja alisahau funga zipu ya suruali, akakutana na dada mmoja njiani na kumuambia "kaka samahani umesahau kufunga mlango wa gereji"

Yule kaka akajibu "ooh asante sana, umeona Prado imepaki?" Dada akajibu "hapana nimeona ka-starlet tu kana pancha tairi zote."

Sunday, September 11, 2011

Mbwa na Mke

Jamaa aliulizwa swali "mlango wa nyuma mbwa wako anabwaka, mlango wa mbele mkeo anapiga kelele ukamfungulie utamfungulia nani kwanza?"

Jamaa akajibu "mbwa" sababu ya msingi alinena "mbwa akishafunguliwa atanyamaza, mke wangu ataendelea na kelele.

Tawi

Jamaa mmoja alienda kwa rafiki yake kumuomba pesa kidogo alikua ana shida, maongezi yalikua hivi "ndugu yangu nna shida ya kwenda loliondo kwa babu hivyo senti kidogo nisaidie" mdau aliemfuata akamjibu "ohh! Tena kuna branch Namanga arusha umelisikia?

Friday, September 9, 2011

Story za hapa na pale

Vijana kadhaa wakati wanatwanga stories zinazohusiana na foleni jijini Dar es Salaam, mmoja akanena "jamani kama foleni zingekuwa zinapewa Award basi foleni ya Tazara ingechukua"

Thursday, September 8, 2011

Vibaka + Timing

Vibaka walishafanya mchakato wao woote kwenda kuiba vitu vya gari, walipofika eneo la tukio hawakuikuta hiyo gari waliyoivizia siku nyingi.
Walipoona bila bila wakaenda mpaka mlangoni kugonga, alipokuja mwenyewe mlangoni wakamuuliza "oya gari umepaki wapi? Umetupa usumbufu kubeba spana turudishie basi nauli yetu."

Gari imeibiwa

Mwanaume: Shenzi kabisa alieniibia gari yangu.
Mwanamke: Nani?
Mwanaume: Sijui nani? Hajaacha hata ki-note chochote.

Wednesday, September 7, 2011

Usahili

Jamaa mmoja alienda kwenye usahili (interview) inahusiana na computer, maswali yalianza kama ifuatavyo:
Msahili: Unaijua computer?
Msahiliwa: Ndio naijua.
Msahili: Unajua kuitumia?
Msahiliwa: Ndio na nna akaunti ya facebook na twitter.
Msahili: Ok, unajua ku-m-add mtu?
Msahiliwa: Ndio.
Msahili: Ukifika nyumbani uniadd na mimi.

Tuesday, September 6, 2011

Jinyonge...

Jamaa mmoja alienda porini kwa nia ya kujinyonga, akaifunga kamba yake vizuuri, ile anataka kutumbikiza kichwa kwenye kitanzi tu mtini hapo hapo akamuona nyoka... Kilichofuata alitimua mbio za kutosha.

Msaada kwa wakwe

Kijana mmoja alipelekwa na mchumba wake kwa wakwe! Kufika wakakuta baba anataka pelekwa hosptitali alikua amekabwa na chakula.
Kijana akanena naweza msaidia, akamuwekea vidole viwili puani na kumuambia akohoe kwa nguvu, mzee wa watu akapona.

Mke akanena "huyu kijana anafaa enhe?" Mume akamnong'oneza mkewe "laiti ungenusa vidole vyake tungemfungulia mashtaka dhidi ya mtoto wetu.".

Homework

Mwalimu aliwaachia wanafunzi zoezi la kufanya wakienda nyumbani aliwaambie "wakaangalie nini mama yao anafanya"
Kesho yake waliporudi dogo mmoja akaulizwa na akajibu "jana mama nilimuona nyonyeshwa na baba, hivi hadi wakubwa bado wananyonya?"

Monday, September 5, 2011

Radio ya gari

Walipanda watu watatu kwenye gari ya mwenzao, mmoja akamuambia aliekua anaendesha gari hiyo "kaka mbona radio haiwaki, tupo kimya sana" jamaa akajibu "tanesco bwana washakata umeme"

Sunday, September 4, 2011

Mswaki

Mke mmoja akimuambia mumewe jambo fulani kama ifuatavyo:
Mke: Mume wangu umepiga mswaki?
Mume: Bado, kwani lazima?
Mke: Sa si usafi wa kinywa jamani?
Mume: Haijaandikwa kwenye biblia lakini?

Thursday, September 1, 2011

Kituo cha polisi

Aliingia njemba kituo cha polisi na kusema "mkuu wa kituo wapi yupo? Na ndie anaemmendea mke wangu. Nimekuja kumshtaki kwa mkuu wa kituo".