Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, October 29, 2011

Mnyalukolo

Jamaa kwenye daladala pembeni kuma dada alianza kwa kumsalimia halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa google?" Dada akamjibu "hapana, n kwanini umedhani naitwa
hivyo?" Jamaa akamjibu "maana una kila kitu nnachokitafuta"

Toto hili nalo...

Mtoto aligoma kutumwa na beki tatu, Mgeni
aliyekuwepo sebuleni ikabidi aonyeshe
busara zake akamuuliza mtoto "humu ndani
mdogo nani? Mtoto akajibu "mama" Mgeni
akamuuliza "kwanini?" Mtoto akajibu "mama
kila siku anavuliwa chupi na dadii wakati mi yangu kila siku
navua mwenyewe"

Tv kubwa

Babu alienda mjini kwa mwanae. Sebuleni akakuta Tv ya inch 53 na kuishangaa ilivyo kubwa. Siku moja kabla hajaridi kijijini mwanae alikuta Tv imevunjwa kuuliza akajibiwa "ni mimi mwanangu nimejimegea nusu nkaangalie kijijini, rimoti ntatumia yangu"

Babu huyoo

Babu alifanyiwa opereshen ya kusafishwa
korodani na kuanikwa bahati mbaya yaliliwa
na paka dokta akaamua kumbandika viazi ili
asifukuzwe kazi baada ya mwezi dokta
alimuuliza mgonjwa wake vp mzee khali
yako? BABU."ah sijambo najiskia vizuri ila
kuna tatizo jengine" DOKTA" tatizo gani?"
BABU naona badala ya kuota nywele za huku naota
matembele."

Vipofu wawili

Vipofu wawili kwenye basi
wakisafiri ghafla
gari likapata ajali kipofu
mmoja wakati anamtafuta mwenzake katika
kupapasa akashika punje ya mahindi
akashtuka "hee haya meno nini?" katika
kuendelea bahati mbaya akaingiza mkono
kwenye bususu ya mwanamke akalia kwa
uchungu "maskini John meno yote
yameng'oka"

Kuku na sikukuu

Kuku wangejua kusoma na kuielewa kalenda
yaani kipindi cha sikukuu tusingewakuta
kwenye mabanda!

Friday, October 28, 2011

Simama ukaguliwe

jamaa alikuwa kwa mguu alipofika getini
kwenye kampaundi ya mshikaji wake akakuta
kibao "SIMAMA UKAGULIWE" kwakuwa
mlinzi hakuwepo jamaa akajisachi
mwenyewe then akaingia ndani, kabla
hajafika mlangoni mlinzi akamfuata na
kumuuliza kwanini umepita mlangoni bila
ukaguzi? Akajibu "nimefanya auto search"

Redio msalani

Mke mmoja alimpa mme wake radio aende
nayo chooni ili asiboreke kwa vile huwa
anakaa muda mrefu.
Basi alivyotoka akamuuliza: "enhe, mume
wangu, vipi ulienjoy?"
mume: "ah, wajinga hawa! Wameniwekea
wimbo wa taifa nimekunya huku
nimesimama!"

Mume anapobanwa

Mwanamke mmoja alimuona mumewe amevaa nguo ya ndani imevaliwa nje ndani. Kamuuliza "mume wangu mbona pichu umeivaa nje ndani kulikoni?" Mume nae akajibu "ooh nilipitia site nkaamua kuoga huko huko."

Tuesday, October 25, 2011

Mkulima mmoja alifungua akaunti sasa alipopata kadi akaenda ATM alipocheki balance akazimia. Siku ya pili tena akazimia, ya tatu akapata wa kumsomea salio kumbe mkulima akiona namba ya akaunti ndio akidhani fedha.

News

Jamaa walipokuwa bar akimsimulia jambo mwenzake:
Joseph: Umezisikia news mpya?
Ibrah: News gani tena?
Joseph: Fredy kaachwa na mkewe...
Ibrah: Ohh! Mhudumu niongeze konyagi.

Monday, October 24, 2011

Choo cha mbwa

Mtoto mmoja alimuuliza baba ake "baba yule jirani yetu kwa nini anatumia choo kimoja na mbwa wake?" Baba ake akamuuliza "kivipi mwanangu sijakuelewa?" Mtoto akaiju "namuonaga akienda kukojoa pale kwenye ule mti kila siku na mbwa pia hapo hapo."

Simu hospitalini

Ilipigwa simu hospitalini ilipopokelewa "halo hapo ni kk hospitali?" Akajibiwa ndio. Kisha yakaendelea "ooh sasa nilitaka kujua hali ya mgonjwa chumba namba 80."

Nesi akijibu "oh yule mgonjwa yupo anaendelea vizuri, bp imeshuka na sukari pia unatengemaa vyema mpaka sasa. Kwani wewe ni nani mwwnzangu?"

Toka kwenye simu ikajibiwa "mimi mgonjwa chumba namba 80 nikiuliza maana hamna alieniambia hivyo."

Misemo ya mitaani

Niliidaka sehemu msemo huu "mwanaume u-handsome mwisho form six baada ya hapo inaangaliwa pesa tu."

Mume na mke wakigombana

Mke: Pumbafu... X%;?0++$.. Na ndiio maana si mzuri kitandani.
Mume akakaa kimya tu. Mke akauliza, "si naongea na wewe mbona kimya?"
Mume akajibu: Nipo kitandani namaliza usingizi ili niwe mzuri kitandani.

Saturday, October 22, 2011

Kisanga mahakamani

Jamaa alipopewa nafasi kujitetea kwa kosa la kubaka mbwa alinena ivi "mheshimiwa hakimu mbwa mwenyewe ndio alitaka akawa anajipitisha pitisha kila mara..."

Mayai kwa mtoto

Katoto kamoja kaliulizwa na baba ake,"mwanangu sasa mbona hujala mkate na mayai?" Kale katoto kakajibu "sa takulaje mayai wakati hayajachinjwa kuku walio ndani yake?"

Thursday, October 20, 2011

Mtoto kwenda shule

Mtoto mmoja akimuambia mama yake kabla ya kwenda kulala, "mama mi kesho ntakua naumwa mkono sitaenda shule" asubuhi alipoamshwa akakumbushia "mama si nlikuambia ntakua naumwa mkono jamani?"

Monday, October 17, 2011

Aliuliza jamaa

Jamaa mmoja alitoa ya moyoni kama ifuatavyo:
"nimepanda ndege, basi, pikipiki, helikopta, treni na boti. Bado kitu kimoja tu "ungo" je mnapaki wapi nijue naanzia wapi?"

Hesabu

Mwanafunzi aliandikiwa hesabu ubaoni atafute jawabu tokanalo na herufi x. Mwanafunzi akamjibu "sa mwalimu ntatafutaje x wakati hiyo hapo naiona?"

Kamchezo

Jamaa alipaka gundi kwenye benchi akimvizia dada,mmoja akae ili atapoinuka akiinuka nguo ichanike mtegaji aone makalio ya dada. Bahati nzuri dada mmoja alikaa punde akahisi tofauti alipoinuka akainuka na benchi zima na si nguo kuchanika.

Kuibiwa baiskeli

Jamaa alienda Tanga akaibiwa baiskeli, kuulizia hakuipata. Basi akanena "inshallah ntafanya kama alivyofanys babu"

Vijana waliposikia wakamrudishia na kumuuliza "babu yako alifanya nini?" Jamaa akajibu "alishukuru Mungu akanunua ingine"

Saturday, October 15, 2011

Hii ya kitambo kilee

Mttoto alitumwa akanunue gazeti la tarehe 10.
Akalikosa, aliporudi kwa baba yake akamjibu
"baba nimekosa la terehe 10, ila menunua ya tarehe 5 mawili"

Friday, October 14, 2011

Vijana na mabishano

Kulikua na vijana watatu, wa kwanz akaangusha saa yake toka ghorofa moja hadi chini ikabomoka, wa pili na e ivo ivo. Aliporusha wa tatu haikubomoka wakamuuliza "imekuwaje?" Jamaa akawajibu "saa yangu iko nyuma dakika 5"

Wednesday, October 12, 2011

Simu ilipopigwa

Mwanaume alipiga simu nyumbani akapokea mwanamke si sauti anayoifahamu. Ikawa hivi:
Mwanaume: We ni nani?
Mwanamke: Mimi ni house girl.
Mwanaume: Mbona sijaajiri house girl kwangu.
Mwanamke: Nimeajiliwa asubuhi hii...

Mwanaume: Huyo mwanamke alekuajiri yu wapi?
Mwanamke: Yupo chumbani na mume wake.
Mwanaume: Enhe? Nani? Mi ndio mumewe. Sasa sikiliza unataka kupata milioni 4?
Mwanamke: Ndio baba.

Mwanaume: Nenda kachukue pisto ipo... Kisha uwatungue wote pumbavu zao.
Mwanamke alipofanya akarudi kwenye simu "enhe sasa mzee miili yao naiweka wapi?
Mwanaume akajibu "itupe kwenye swimming pool.
Mwanamke akajibu "lakini hamna swimming hapa nyumbani"
Mwanaume akanena "ngoja kwanza hapo ni nyumba plot. No. 811?"

Monday, October 10, 2011

Hii mimba...

Mtoto akimjibu mama ake "mama kamimba kenyewe kadoogo tu nlikokapata, shule ntaendelea"

Sunday, October 9, 2011

Mchungaji atoa neno

Mchungaji kwenye msiba alinena "ndugu zangu acheni sigara, acheni pombe, starehe na ugolo tupeni kule."
Bibi mmoja akajibu "wee mchungaji nani atupe ugolo?"

Saturday, October 8, 2011

Toto hili?

Mama unajua housgel wetu ni malaika? Mama: Kwanini wasema hivyo?
Mtoto: Jana nilimuona ameshikilia ukuta akiwa uchi na mikono ameinua juu anaongea na Yesu akisema ooh! Yesu wangu nakuja... oooh! Yesu wangu nakuja jaman! yaan isingekuwa baba kumshikilia kwa nyuma naye akiwa uchi, saa hizi dada angekuwa mbinguni!

Mahakamani

Mtuhumiwa: Mheshimiwa hakimu, ilibidi nikagonge ukuta kuliko kumgonga ng'ombe.
Hakimu: Ng'ombe alikua jike au dume?
Mshtakiwa akajibu "sikumuangalia plate namba"

Mgao umeme

Mtoto aliulizwa "mbwa wako alikua wapi wakati umeme unakatika?"
Mtoto akajibu "alikua kwenye giza"

Kasuku anauzwa

Jamaa: Nauza huyu kasuku na anaongea.
Mteja: Sidhani kama anaongea mhh!
Punde kasuku akaanza kuongea kwa masikitiko "tafadhali ninunue, huyu hanipagi chakula, hanitoi nje kwenye hewa, hanipi nachohitaji"

Mteja: Sa why unamuuza wakati na kuongea anajua?
Muuzaji: Nimemchoka na tabia yake ya uongo.

Dunia ya kisasa

Maongezi ya vijana wawili yalikua hivi...
Msela: Dah leo nataka kupika ugali kwa sukumawiki ila sijui...
Mwenzake akamjibu.
Msela wa pili: Ingia google tu andika ugali...

Tuesday, October 4, 2011

Bahiri

BAHILI: Ndizi moja sh.ngapi ?
MUUZAJI: Ndizi moja sh. 100.
BAHILI: Nipe kwa sh. 60.
MUUZAJI: Kwa sh.60 utapata maganda tu.
BAHILI: Shika hii sh.40 nipe ndizi hayo maganda ya sh.60 yatoe siyataki!

Monday, October 3, 2011

Mke kabla...

Mke kabla hajafa alimtuma mumewe chumbani chini ya uvungu. Akakuta mayai3 na milioni 6. Kuuliza akajibiwa "yale mayai nimekua niyaweka kila tukifanya mapenzi sivyo" Mume akafikiria na kusema "sio mbaya matatu tu kwa miaka 26 ya ndoa." Kisha akauliza "na zile milioni 6?" Mke akajibu "nimekua nikiyauza mayai kila yalipokua yanajaa"

Mkubwa

Jamaa alichora mstari akamwambia mke wa mpangaji mwenzie "ukivuka tu nakubaka"" Kumbe mama yule alikua na nyege akavuka makusudi jamaa akamvutia geto kumpa tamu. Kumbe mtoto wake alikua akishuhudia yote hayo. Mume karudi tu, mtoto akamwambia "usivuke huo mstari utabakwa kama mama"

Sunday, October 2, 2011

Maasai

Mmasai aliingia mjini na PUNDA wake, kufika town akashangaa magari yanavyo toka kasi, akaamua kumuuliza jamaa mmoja... Mmasai: "Aisee rafiki, kwanini hisi gari nakwenda mbio sana?!" Jamaai: "Gari zinatumia Petrol/Diesel ndio maana zinakwenda sana..." Kesho yake jamaa akaenda SHELI na punda wake, kufika akamnyanyua PUNDA mkia. Akaomba Punda wake atiwe lita 5 za Petrol.... Baada ya dakika chache petrol si ikaanza kumuwasha yule Punda, akatoka mbio akaingia mitini.... Mmmasai akamfukuza, wapi hakumpata... Daaah, yero akaamua karudi Sheli, akafungua mkanda, akavua shuka lake, akainama. Akamwambia muuza mafuta, "Weka lita 10, 5 diseli, 5 petroli.... si nataka masindano na mimi, lazima onesa yeye nani saidi leo...."

Ualimu kazi

Kwel ualimu kazi Mwalimu kajamba darasan kwa aibu ikabidi achukue likizo ya mwezi 1. Baada ya kurudi kawauliza wanafunzi tumeishia wapi? wakamwambia pale ulipojamba...