Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, January 28, 2012

Bafuni kwetu

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake swali "baba kwanini kila mtu hapa nyumbani akiingia bafuni tu anaanza kuimba?"
Baba akajibu "sababu ni kitasa cha mlango kimekufa mwanangu"

Tuesday, January 24, 2012

Mipango ya wezi

Wezi waluenda kuiba duka la sonara, wakagawana na kuondoka. Baada ya muda polisi wakaja na kumkuta mmoja wapo wakamuuliza nae akajibu, "tumepanga na wenzangu tugawane mie nimechukua duka"

Friday, January 20, 2012

Chai

Mzee mwenye nyumba alipopelekewa chai:
Mzee "hii chai mie nimesema nataka ya maziwa si rangi!"
Dada "maziwa yameisha tangu jana"
Mzee "kwani mama Issa si ananyonyesha mwambieni anikamulie japo robo kikombe..."

Mtoko...

Wachawai wakiwa katika maongezi yao:
Mchawi 1: Leo si ijumaa hatutoki?
Mchawi 2: Dah! Bahati mbaya ungo wangu umeisha inshuarensi so nikipata ajali imekula kwangu.
Mchawi 1: Basi kamuazime mbuggu wa kwake.
Mchawi 2: Wa kwake juzi tu umepigwa pasi ivo upo gereji.

Ndoto zingine...

Ally: Jana usiku meota nipo Japan.
Saidi: Mimi nimeota nina party nyumbani.
Ally: Sa mbona hukunialika?
Saidi: Mi nlijua bado upo Japan.

Mayai ya kuku

Muuza chips alivunja mayai takribani matatu yote matupu kilichofuata akanena "inaelekea hadi kuku wanatumia condom

Thursday, January 19, 2012

Imekuwaje tena?

Mwanamke mmoja alimnasa kibao cha uhakika mwanaume mmoja, jamaa wa pembeni akasogea kuuliza "vipi kaka mbona makofi hadharani?"
Jamaa aliepigwa akajibu "si fulana yake imeandikwa maeneo ya kifuani "gusa taratibu" ndio yaliyonisibu baada ya kugusa"

Gazeti

Dada mmoja aliketi kwenye kiti cha bustani, alikua,amekalia gazeti asichafue sketi yake nyeupe. Akatokea kijana mmoja akamuuliza "unasoma gazeti hapo?"

Dada kuepusha maongezi yasiendelee akajibu "ndio" kisha akainuka na kufunua ukurasa unaofuata kisha akaendelea kukalia.

Changudoa

Jamaa alizidiwa ikabidi akaopoe malaya wanaojiuza.
Jamaa: Enhe biashara inakuwaje?
Malaya: Short time elfu 15, mpaka asubuhi elfu 30.
Jamaa: Ok hamna shida si mnatoa na risiti lakini?
Malaya: We bwege nini umesikia hapa kibaruani kwako.
Jamaa: Sasa mie ntajuaje kama nakatwa VAT kihalali?

Monday, January 16, 2012

Kitu cha mbagala

Wakati watu wanagombania kupanda kwenye basi la mbagala kama kawaida yao, bibi mmoja alipanda bila shida akapata siti. Baada ya muda konda akamuuliza "bibi unalia nini sasa?"
Bibi akajibu "miaka yote 25 nliyoishi Mbagala sijawahi pata siti" konda akanena baada "bibi pisha siti hapo umekaa ya dereva."

Chenchede

Kidume: Haloo, naongea na Rehema?
Rehema: Ndio mie.
Kidume: Rehema yule nliekua nae tukalewa sana?
Rehema: Ndio mie, ukanisifia nna kiuno kitamu.
Kidume: Ohh! Safi za tangu siku ile?
Rehema: Nzuri tu, na nna mimba yako.
Kidume: Enh! Wrong namba.

Mke na Mume

Mume alipanda kitandani akiwa tayari tayari kula tunda la ndoa na mkewe.
Mke alipokuja akanena "mie naumwa kichwa leo siwezi."
Mume akaenda jikoni kurudi naniliu yake ilikua kama ina unga unga mke akauliza "nini iyo?"
Mume akajibu "nimeipakaza asprini na panadol haya njoo."

Kwenye harusi

Mwalimu: Kwanini hujaja shule jana.
Mtoto: Nilienda kwenye harusi ya anko wangu.
Mwalimu: Amemuoa nani?
Mtoto: Amemuoa mke wake.

Malavi davi

Jamaa aliandika sms kwa mchuchu wake ifuatavyo.

Kama unatabasamu ntumie tabasamu lako.
Kama umelala ntumie ndoto uiotayo.
Kama unalia nitumie machozi yako.

Mwanadada akajibu ifuatavyo:
"nipo chooni je nitume chochote"

Sunday, January 15, 2012

Vichaa wakiwa beach

Vichaa kadhaa walipelekwa beach kupunga upepo, mmoja akawa kajitenga na wenzake. Nesi akamuuliza "mbona umejitenga na wenzako vipi?"
Kichaa akajibu "najiuliza hii bahari ingakua supu ningekula chapati ngapi?"

Talaka je?

Mwanaume: Kwa nini sasa usumuombe talaka mumeo kama humpendi na kumchukia?
Mwanamke: Yaani namchukia sana kiasi kwamba akinipa talaka ntampa wakati wa kuwa na furaha sana ndio sitaki.

Mie naumwa

Mfanyakazi alimtumia sms/msg boss wake...
Mf'kaz: Boss leo siwezi kuja kazini naumwa.
Boss: Mi nikiumwa nambusu mke wangu kisha napona na nakuja kazini.
Baada ya masaa mawili mfanyakazi akatuma tena sms "boss nakuja kazini nimeshambusu mkeo"

Swali kwa studentiii

Mwalimu: Haya nani anaweza kuniambia njia rahisi ya kuwa milionea?
Mwanafunzi mmoja: "Ni kuolewa na millionea."

Afadhali sija...

Jamaa akitembea njiani ghafla aliona asichokielewa akasimama na kugusa na kidole akalamba kupata testi. Akagundua kua ni poo (haja) ya mbwa kisha akanena "doh afadhali sijakikanyaga" ...lakini amekionja...

Saturday, January 14, 2012

Swali

Jamaa mmoja aliuliza swali hili "mbona tukikutana petrol stations hatupeani ofa ya mafuta kama bia tukiwa bar?" Jibu unalo.

Wapi leseni?

Askari (trafik) alimsimamisha dereva mmoja kwa spidi kubwa na kumuambia "unakimbiza sana gari, hebu nipe leseni yako"
Dereva akajibu "jana tu umeichukua leseni yangu, sa nikuonyeshe passport au?"

Kitu 100mil

Bibi kizee alishinda milioni 100, akapewa mtu ampe utayari kisaikolojia kuzipokea hizo pesa zisije muua kwa presha.

Mwanasaikolojia: Bibi ukipata 10mil utafanya nini?
Bibi: Ntanunua ng'ombe wa kulimia mashamba yangu.
Mwanasaikolojia: Ok, je 20?
Bibi: Ntanunua trekta niendeleze kilimo.
Mwanasaikolojia: Sasa je ukipata 100mil?
Bibi: Ntakupa wewe mimi ntashindwa pa kuziweka.
Mwanasaikolojia presha ikapanda na kumuua.

Friday, January 13, 2012

Dah aibu kusema

Njemba moja ilikua na korodani 3 alipofika kwa dokta kwa aibu ilimbidi aongee hivi:
Njemba: Dokta, kwa mfano mimi na wewe jumla tuwe na korodani 5...
Kabla hajamalizia dokta akadakia
Dokta: Usiniambie wewe unazo nne jumla?

Dawa

Kwenye simu...
Mama: We Daudi umempaka mdogo wako ile dawa ya kuchua mkononi?
Daudi: Ndio mama nime-mnywesha asubuhi na mchana...

Opena...

Kwenye simu maongezi...
Mwanaume: Dokta mtoto wangu amemeza opena.
Dokta: Usiwe na wasi wasi atakua salama tu.
Mwanaume: Sasa ntawafunguliaje soda wageni?

Tangazo kwa abiria

Wakiwa angani tangazo kwenye ndege lilitolewa kama ifuatavyo "mabibi na mabwana tunaomba radhi safari yetu leo itachelewa dakika 7 zaidi, hii ni kulingana na rubani tulie nae leo ni mgeni wa njia pia ni kipofu..."

Kisanga cha...

Jamaa ambae mke wake nesi alikua akimsimulia jambo mkewe, "si unamjua dokta shabani? Kanyang'anywa leseni ya udokta kisa alikua ana fanya mapenzi na wagojwa wake."

Mtoto wa jamaa akiemsimulia mkewe akadakia na kusema "sasa baba hapa nyumbani utamfukuza mama au houseboy wetu?"

Mzee wa miaka 90

Mzee mmoja wa miaka 90 alitaka kumuoa msichana wa miaka 30, akaenda kwa dokta wake kwanza.
Dokta akamuambia "ohh okay sasa toa vitendea kazi vyako nikague kama utaweza mzalisha huyo msichana" mzee akatoa ulimi na kidole cha kati.

Faida za maziwa ya mama

Kijana alikua kwenye mtihani, moja ya swali aliuliza faida 3 za maziwa ya mama akajibu:
a) Yana rutuba kwa afya ya mtoto.
b) Hayapatwi na bacteria.
c) Yapo kwenye kibebeo kinachovutia wanaume.

Thursday, January 12, 2012

Bar na watu wachache

Jamaa mmoja aliingia bar ilikua ya ndani hivi na watu wachache. Akapita kila meza, kila alipomaliza kuongea neno meza husika walitoka nje. Mpaka akabaki mhudumu wa kaunta tu. Alipomaliza akatoka nje ma kuwaambia warudi ndani.

Walikuta bia zao zote jamaa kanywa, mmoja akatoka mbio na kumfukuza. Kila akijaribu kumuacha jamaa huyu hapa nyuma akauliza "we unanifukuzia nini?" Jamaa akajibu "umekunywa bia yangu niliweka sumu, naitaka."

Ndoa ijayo

Ofisini kulikua hivi:
Mfanyakazi: Boss naomba off kesho nisije nna party ya kumvisha pete mchumba wangu.
Boss: Mwanamke gani chizi atakukubali wewe?
Mfanyakazi: Ni mwanao Jesca boss.

Mgonjwa wa akili

Mgonjwa wa akili alikua akikojoa ghorofani kuelekea chini. Alipomuona nesi akaahirisha. Baadae kumuuliza mbona ulipomuona nesi ui liacha akajibu "angenivuta je si ningeanguka!"

Wednesday, January 11, 2012

Mwizi a.k.a kibaka

Mwizi aliamua kumteka mtoto mmoja wa miaka 10 akikatisha nae sehemu yenye giza nene...
Mtoto: Naogopa...
Mwizi: Sa unafikiri ntakatisha na nani hapa?

Bangi zime...

Jamaa alipiga polisi simu "haloo, jirani yangu ameficha bangi kwenye kuni nyumbani kwake"
Kesho yake polisi walifika na kupekua pamoja na kupasua pasua kuni bila kuona bangi.

Jirani akampigia simu jirani yake "vipi polisi walikuja?" Jamaa akajibu "ndio"
Jirani akaendelea "unaona nlikuambia watakusaidia kupasua kuni, sasa zamu yako wapigie waambie nimefukia cocain kwenye bustani yangu."

Mgojwa hasira

Mgonjwa: Dokta nnasumbuliwa sana na hasira za mara kwa mara hata jambo dogo tu mi ni hasira.
Dokta: Tatizo haswa ni nini?
Mgonjwa: Si nimeshakuambia pumbavu zako unakua kama mwehu bwana.

Kitu msikitini

Msikiti mmoja wakati wa swala ya ijumaa, sheikh alitoa mawaidha muda mrefu saana. Waumini wakaanza ondoka mmoja mmoja.

Mmoja akabaki, sheikh akanena "bora wewe umebaki hao wengine wamekosa heshma"
Muumini akajibu "mi mwenyewe nasubiria mkeka wangu uliokalia."

Mwizi

Jamaa alikua akiandika meseji kwa boss wake akiwa katika daladala kuwa atachelewa kidogo kazini. Ghafla alipomaliza kuandika mwizi akaikwapua jamaa badala ya kuita mwizi... Mwizii akamuambia "bonyeza send, bonyeza send..."

Unyumba

Mwanamke akiwa mbele ya wazazi wake, yaani,wakwe wa mumewe.
Mwanamke: Wazazi wangu nimewaita mume wangu hanipi unyumba kabisa wiki sasa.
Mzazi: Mkwe wetu haya tuambie nini shida?
Mume: Dokta kaniambia nisipendelee vitu vitamu kwa sababu nna kisukari.

Kila kitu kikubwa

Kipofu aliagiza bia wakamletea kwenye jagi kubwa. Akanena "hee mbona kubwa hivi?"

Wa pembeni akajibu "Dar kila kitu kikubwa"
Kipofu akaomba kwenda chooni, akaingie mlango wa pili kushoto.

Kipofu akaingia mlango wa 3.
...akatumbukia kwenye bwawa la kuogelea akijua katumbukia kwenye choo akawa anapayuka kwa sauti "usiflash... Usiflash..."

Tuesday, January 10, 2012

Taxi driver mpya

Abiria kwenye taxi siti alimgusa bega dereva, alistuka mpaka kugonga ukuta wa watu.
Dereva: Dah kaka usifanye hivyo tena.
Abiria: Hamna shida nilikua nakuita tu.
Dereva: Ndio, leo ndio nimeanza hii kazi ya taxi kabla ya hapo nikiendesha gari la kubeba maiti.

Mteka nyara

Njaa ilimbana jamaa akaamua kumteka nyara mtoto wa miaka 6. Akamuandikia kikaratasi kimeandikwa hivi:
"nimemteka mwanao, anakuja kukupatia hiki kikaratasi na kesho uweke milioni 10 kwenye kona pale jalalani"

Mwenye mtoto nae akaandika kikaratasi na kumtuma mtoto kimeandikwa hivi:
"Kivo huu si mwandiko wako asa inakuwaje unamteka mwanangu?"

Maandazi 6

Mwalimu: Joseph nikikupa maandazi 6 nkatoa mawili yatabaki mangapi?
Joseph: Kama ukinipa na mchuzi halibaki hata moja.

Monday, January 9, 2012

Nyoka na panya

Nyoka: Oya vipi mbona unaniangalia sana?
Panya: Mbona unajistukia?
Nyoka: Muone ndo maana una ndevu...
Panya: Bora mie, we kubwa zima watambaa hadi leo.

Sunday, January 8, 2012

Darasa la hisabati

Mama: Mbona umenuna mwanangu?
Mtoto: Mwalimu wa hesabu hajaja leo.
Mama akajua mwanae kichwa kwenye hesabu na kupenda.
Mama: Usijali mwanangu ntamuambia aje kukufundisha hapa hapa nyumbani.
Mtoto: Tatizo yeye pekee ndio anauza ubuyu ndio maana.

Sumu ya panya

Jamaa aliwategea sumu ya panya kwwnye nyama ya nguruwe nyumbani kwake. Asubuhi alipoamka akakuta kikaratasi kimeandikwa "hatuli nguruwe, we samaki kesho uone."

Utambulisho

Walipofika mbeya kikazi wakati wa kujitambulisha.
Wa mimi naitwa Mwakasitu.
Wa pili: Mimi naitwa Mwakasege.
Wa tatu anaitwa Juma nae akanena "mimi naitwa Mwajuma"

Friday, January 6, 2012

Ombaomba

Mwanamke alikaa kwenye viti vya bustani za katikati ya mji. Punde akaja ombaomba wa kiume.

Ombaomba: Oh mpenzi umekuja tu-enjoy.
Mwanamke: {kwa hasira} We umechanganyikiwa...!!?
Ombaomba: Sasa unafanya nini kitandani kwangu.

Mkojo ulibana

Jamaa alibanwa mkojo, akawa mbio mbio anakimbilia chooni kukojoa. Bahati mbaya akajikojolea njiani. Akaamua kurudi kwenye mkutano ivo ivo kwa vile ameshakojoa.

Majambazi

Majambazi waliingia benk kuiba, baada ya kubeba fedha za kutosha wakati wanaindoka mmoja wa majambazi waliovaa mpaka usoni; alimuandikia namba mrembo mmoja wa pale kauta namba ya simu vile amemzimikia.

Mchina kaibiwa

Mchina alipigwa mtama na kibaka akaibiwa simu. Mchina akaanza mfukuza kibaka, kibaka akaona isiwe tabu akaidondosha simu. Mchina akaiokota na kuendelea mfukuza.

Kibaka "we si nimekupa simu yako?"
Mchina akajibu "ndio umenipa bado mtama"

Tuesday, January 3, 2012

Mapacha

Mke alizaa mapacha, mume alipofika hosp. Akamuuliza mkewe "huyu mtoto m1 wangu na huyu mwingine utanieleza vizuri wa nani?"

Ndoa ikifungwa

Padre akiuliza umati kabla ya kufungisha ndoa kanisani "kuna yeyote mwenye kipingamizi ndoa hii isifungwe?"

Sauti ikasikika nyuma "padre subiri kidogo." Kisha jamaa akasogea mbele mbele.
Padre: Je, unapingamizi lolote ndugu?
Jamaa: Hapana kule nyuma nlikua sikusikii vizuri.

Maiti ikioshwa

Maiti ilikua inaoshwa, ngafla ikaanza kucheka waoshaji wakauliza "hii maiti inacheka nini?"
Maiti ikajibu "mnanitekenya bwana alahh!"

Mapadre na vekeshen

Ma-padre wawili walenda mbali kidogo kula starehe (bata). Ili wasijulikane wakanunua nguo na kupiga swaga za mtaani. Punde akapita dada mmoja wakammezea mate, dada akawasalimia "fatha mambo?"

Wasijue kawajuaje... Siku ya pili na ya tatu ivo ivo wakamuuliza: "we umetutambuaje...?"
Dada akajibu: Mi si Sister Rosa umenisahau?

Monday, January 2, 2012

Condom

Vijana wawili walienda mbiombio kwa dokta:
Kijana: Dokta nimemeza condom bahati mbaya nisaidie kuitoa.
Dokta: Huyu uliekuja nae yeye ni nani yako?
Kijana: Rafiki yangu ndio mwenye condom yake.

Nzuri na mbaya

Dokta: Mzee nna habari mbaya na nzuri, nianze ipi?
Mzee: Anza na mbaya ifuate nzuri.
Dokta: Mbaya mguu wako tumeukata kabisa. Na nzuri nitakununulia kiatu kwa bei rahisi tu.

Sunday, January 1, 2012

Alipobanwa mtihani

Mwanafunzi alibambwa kwenye mtihani:
Mwalimu: Uliiua unampigia simu nani akupe majibu?
Mwanafunzi: Mwalimu ile haikua cheating mtu nliempigia hajui jibu pia.

Jaza fomu

Jamaa mmoja alipokwama kujaza kwenye fomu.
Jamaa: Samahani sikumbuki jina la hospitali nlilozaliwa.
Mhudumu: Si lazima hospitali jaza mji uliozaliwa tu.
Jamaa: Nimejaza Kitandani, ndii sehemu nlipozaliwa.

Mwaka Mpya.

Heri ya Mwaka Mpya kwa wanablog hii wote.
Mwenyezi Mungu ashukuriwe.