Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, February 29, 2012

Gari mupya

Jamaa alinunua benz automatic gia. Akaendesha vizuri lakini usiku uligoma kabisa kwenda. Kuita fundi akawa anaelezea baada ya kuhojiwa ni vipi imemgomea kwenda akajibu "ni hivi... Mchana nikiweka D inaenda vizuri, ila usiku haiendi nkiweka N. Au N sio for "Night and D for Day?"

Jina kwenye simu

Msichana mmoja alichukua simu ya mpenzi wake akaandika namba yake ili ajipigie aone jamaa amesave jina gani. Alipofanikiwa akakuta imeandikwa "fundi tiles"

Darasa la kimombo

Mwalimu aliuliza: Do you undestand the importance of period?
Mwanafunzi mmoja akajibu mdogo kwa umri "yes i know, siku moja my sister alisema amekosa period mama akazimia na baba akachanganyikiwa."

Kipi bora?

Mwalimu: Kwa nini wanasema mapenzi bora kuliko vita?
Mwanafunzi mmoja akajibu "kwa sababu condom ni bei rahisi kuliko bunduki."

Kibaka

Raia walifukuza mwizi akakimbilia makaburini usiku. Punde akavua nguo zote na kuelekea walipo raia wenye hasira. "tunamtafuta mtu kapita hapa na kifurushi" jamaa akajibu "sijamuona, mi mwenyewe mgeni hapa nimezikwa jana ngoja niwaulize wenyeji wangu"
Raia hamna aliebaki baada ya hapo.

Posa

Jamaa alienda kutoa posa akaambiwa "mtoto yupo shule bado anasoma" njemba nayo ikajibu "sawa ntakuja wakati wapo mapumziko "break time"

Tuesday, February 28, 2012

Askari mnarani

Jamaa mmoja alipofika mjini pale posta mpya kwenye askari (mnara) akanena, "hee kipindi kile nlipokuja dar huyu askari alikua bado mdoogo, leo amekua hivi."

Wednesday, February 22, 2012

Mawazo ya mtoto

Mtoto: Baba na mama nimemleta fundi yupo hapo nje anawaaubiri"
Baba akadakia "mimi nimekuagiza au mama yako?"
Mtoto: Hamna alieagiza, mimi nimemleta awatengenezee kitanda chenu kina kelele sana usiku kulala shida."

Mtoto mzuri

Mtoto alimuona dada mja mzito.
Mtoto: Humo tumboni una nini?
Dada: Kuna mtoto.
Mtoto: Mzuri enh kama wewe?
Dada: Ndio.
Mtoto: Sasa mbona umem-meza?

Disco

Marafiki wawili walienda disco maongezi yao yalikua hivi.
Mshkaji 1: Ee we vipi tangu umekuja hauchezi hata nyimbo moja vipi?
Mshkaji 2: Kuna nyimbo naipenda sana halafu haichezwi mpaka muda huu...
Mshkaji 1: Mwimbo gani huo?
Mshkaji 2: Si wimbo wa taifa.

Ugeni wa mambo

Mwananchi mmoja alietoka nyumbani kwake na kuelekea duka la dawa. Alipofika yakawa hivi "dada samahani nimerudi tena, hivi ulisema zile plasta nimeze mara ngapi kwa siku? Nimepitiwa kidogo."

Simu zina mambo

Mvulana: Mambo? Upo wapi mpenzi?
Msichana: Nipo chumbani nasikiliza mziki. Wewe je?
Mvulana: Mimi nipo nyuma yako humu club, geuka utaniona.

Kimombo.com

Mtoto wa miaka 11 alikua ameketi na baba ake. Kwa mbali akamuona msichana wake anakuja. Dingi hataki mwanae kujihusisha na mapenzi mapema, kuua soo msichana alipofika akaamua kumuongelesha kimombo.

Mvulana: Ohh umekuja fuata kile kitabu "speak english my father doesn't speak?"
Msichana: Yah na kile cha "where should i wait for u"
Mvulana: Hicho hakipo labda kile "wait for me under coconut tree"
Msichana: Sawa kama kipo cha "i give you 5min" njoo nacho kesho shule.

Baba akajua mwanangu anapenda shule sana.

Mwendo wa ringtone

Jamaa mmoja aliweka ringtone kwenye simu yake mlio wa kifaranga. Siku simu ikaita si kunguru akaikwapua. Jamaa akabaki ananena "oyaa rudisha simu yangu"

Tuesday, February 21, 2012

Mwindaji na mchunaji

Mwindaji alishuka na kwenda kuwinda, ghafla akawa anarudi mbio "fungua fungua mlango simba ananifukuza" kabla hajaingia akaanguka hatimae simba akaingia garini jamaa yupo nje. Akainuka na kumuambia mchunaji "anza kumchuna huyo naenda kumleta mwingine."

Kengele

Mtoto mmoja alikua akijaribu bonyeza kengele kwa vile mfupi hakuifikia, kaka,mpita njia akaenda na kumsaidia kubonyeza. Kisha akamuuliza "nini kingine nkusaidie mtoto?"
Mtoto akajibu "tukimbie tukajifiche mwenyewe asituone"

Mzigo wetu

Mke: Mbona upo ivo umefukuzwa kazi?
Mume: Hapana sio hilo.
Mke: Sasa nini? Shida yako yetu sote mume wangu.
Mume: Oh afadhali... Sekretari wangu ana mimba yangu.

Vizee viwili

Babu: Mke wangu hujisikii wivu mimi kuvizia visichana?
Bibi: Hata mbwa wanakimbizaga magari na kuendesha hawajui.

Peteee!

Mke kwenye simu kwa ukali: Uko wapi mpaka muda huu?
Mume: Mke wangu unakumbuka lile duka la pete ile tuliyoiona nkakuambia naipenda sana na sikuwa na pesa wakati ule?

Mke akajibu huku akiona haya kidogo "ndio mume wangu naikumbuka sana."
Mume: Basi nipo bar jirani na hilo duka.

Monday, February 20, 2012

Kwenye tuta

Jamaa walikua kwenye gari, kwenye tuta likagusa. Ulipofika tuta la pili halikugusa mmoja kati yao akanena "nimenyanyua miguu ndio maana halijagusa asa ivi"

Saturday, February 18, 2012

Mtoto wa nje

Mwanamke mmoja alijifungua mtoto, si mume wake wa ndoa. Mume alikubaliana na hali halisi. Akapaka sumu kwenye chuchu ili mtoto afe, siku iliyofuata alipigiwa simu arudi nyumbani kuna msiba.

Akiwa njiani huku akitabasamu kutimia kwa lengo lake alipofika nyumbani akapewa taarifa kuwa, aliefariki ni "house boy" na si mtoto.

Kusali kabla...

Mwalimu wa hesabu na mwanafunzi wa darasa la tatu.
Mwalimu: Fredy mbona una sali saa hizi?
Mwanafunzi: Mama aliniambia niwe nasali kabla ya kulala.

Wednesday, February 15, 2012

Wivu

Mwanamke mmoja alikua akiangalia tv, alikua akiangalia mahojiano ya mchumba wake akihojiwa na mtangazaji mzuri wa kike. Wakati wanamaliza kipindi mtangazaji akamkumbatia mchumba wa huyu dada.

Wivu wa mapenzi dada akainuka kwenda kuchukua mwiko aje kumpiga mtangazaji. Aliporudi akakuta kipindi kimeisha na kuna matangazo, akanena "bahati yako umekimbia ungenitambua leo..."

Majibu...

Nesi alitoka leba na kumpa majibu mume wa mama aliepo leba.
Nesi: Hongera sana mkeo kajifungua watoto watatu wenye afya nzuri.
Mume: Nilijua tu ona sasa hao watoto wa ziada wawili ni wa nani?

Masikio vipi?

Jamaa alienda kazini masikio yote yakiwa yamefungwa plasta.
Boss: Vipi masikio mbona ivo?
Jamaa: Nlikua napiga pasi then simu ikaita, nkapokea kumbe ilikuwa pasi.
Boss: Na hilo sikio la pili je?
Jamaa: Nilikua nataka mpigia dokta, pasi tena ikanichoma.

Sunday, February 12, 2012

Msiba wa tembo

"Mbona unalia?" Mtoto aliulizwa.
Akajibu "tembo amekufa"
"alikua mnyama wako?"
Mtoto akajibu "hapana mimi ndio wa kumchimbia kaburi"

Mchumba wa...

Mtoto: Baba kesho birthday ya mchumba wangu sijui zawadi ganibya kumpa?
Baba: Yupoje kwani?
Mtoto: Mzuri, Mrefu ana Hips na nywele ndefu.
Baba: Ohh! Mpatie namba yangu.

Friday, February 10, 2012

55

Mwalimu aliwaambia wanafunzi wa chekechea waandike namba 55.
Mwanafunzi mmoja akaandika 5 akawa kaganda tu.
Mwalimu akamuuliza mbona huandiki ingine?
Mwanafunzi akajibu "mwalimu sijui niandike upande gani, kwa mbele au kwa nyuma?"

Mgahawani

Mteja: Nimeona kabisa kidole gumba chako kwenye supu wakati unaniletea...
Mhudumu: Ndio... Supu haikua ya moto sijaungua.

Kifungua kinywa

Jamaa: Kwa kukuangalia usoni najua kabisa umekula mkate na mayai.
Rafiki: Hehe hiyo ilikua jana leo kiporo na uji.

Hoja hii

Mtoto: Hawa wanakimbia nini?
Mzee: Wanashindania kombe.
Mtoto: Sijaelewa babu.
Mzee: Yaani mshindi "mmoja" ndio atapata kikombe.
Mtoto: Sasa hawa wengine wanakimbia nini?

Bibi kizee kwenye basi...

Bibi kizee kwenye daladala alikaa karibu kabisa na driver. Dereva akawa anaendesha mkono mmoja nje dirishani, kwa vile hapendi akamgusa bega na kumnong'oneza "endesha na mikono yote, mvua ikinyesha nje ntakuambia"

Chura kwenye...

Mteja: Mhudumuuu njoo kuna chura kwenye supu yangu.
Mhudumu: Ohh pole kaka, inzi wapo likizo.

Boss wako

Jamaa aliulizwa amzungumzie boss wake akawa anajibu "boss wangu mhh! Yupo yupo tu hajulikani hata kivuli chake kimekataa kumfuata"

Chimba dawa

Muhindi alipigwa faini ya 1,000Tsh kwa kukojoa kichochoroni. Yeye akalipa 1,500Tsh. Akaulizwa mbona kalipa zaidi akajibu "wakati makojoa iko jamba kodogo"

Thursday, February 9, 2012

Kitu msikitini

Jamaa aliingia na panga msikitini "nani muislamu hapa?" Msikitini kiimyaa. Akamchukua mmoja akatoka nae nje akamchinjie kuku. Akarudi msikitini na panga likiwa na damu akauliza tena "nani muislamu humu?" Waumini wakamuonyeshea imamu, imamu nae akajitetea "jamani mie kusalisha siku mbili tu ndio nshakua muislamu?" Jamaa mwenye panga akajibu "nataka ukanisaidie kumchuna ngozi mbuzi wangu"

Siku ya kwanza

Mama: Enhe mwanangu, ume-enjoy siku yako ya kwanza shuleni?
Mtoto: Siku ya kwanza? Ina maana kesho naenda tena?

Samaki wa kufuga

Samaki wawili wa kufungwa wakiwa kwenye chombo cha kioo:
Samaki wa kwanza: Unaamini Mungu yupo?
Samaki wa pili: Ndio, unadhani nani anaebadilisha maji yakichafuka?

Bidhaa gani?

Mwalimu: Ni bidhaa gani tunaipata kutoka mtibwa?
Mwanafunzi: Hata sijui mwalimu.
Mwalimu: Wewe ina maana hamnunui sukari?
Mwanafunzi: Hatununui tunaombaga kwa jirani

Mke anakufa

Mke akiwa hoi/mahututi hospitali "mume wangu kuna jambo nikuambie kabla sijafa niwe na amani niendako"

Mume: Usihangaike kila kitu kipo sawa mke wangu...
Mke: Mume wangu nililala na rafiki yako, jirani yako na boss wako... Hivyo naomba unisamehe.
Mume: Usijali najua yote hayo ndio maana nimekuwekea sumu.

Swali darasani

Mwalimu aliuliza swali darasani "kwa nini sokwe ana pua kubwa?" Mwanafunzi mmoja akajitokeza na kutoa jibu "mwalimu, kwa sababu ana vidole vikubwa."

Konda na Sharobaro

Kondakta: Oyaa ingia ukamate bomba tusepe.
Sharobaro: Siwezi men hamna siti naona full ndani.
Kondakta: Huna lolote si ungekuja na kiti chako sasa.

Konda na abiria

Kondakta: Dada ingia kuna kiti pale nyuma.
Dada: Siwezi kukaa siti za nyuma.
Kondakta: We si mwendaji kwani za nyuma zipo nje ya gari...

Tuesday, February 7, 2012

Nyimbo gani

Mtoto mmoja aliulizwa swali "ni mziki gani anaupenda sana kuusikiliza?"
Mtoto akajibu "kengele ya saa nane ya kwenda nyumbani"

Monday, February 6, 2012

Mtoto keshaanza

Mama mmoja alianza pata wasi wasi kua mwanae wa kike atakua ameanza mahusiano, kwa kuogopa asije akapata mimba akamuita na kumpa somo nk nk.

Mwisho wa siku akampa condom. Mtoto akacheka sana kisha akajibu "mama una wasi wasi ntapata mimba? Hapana mimi natembea na Lisa."

Sunday, February 5, 2012

Kupiga pasi

Jamaa mmoja aliambiwa akapige pasi shati:
Jamaa: Nisaidie kulinyoosha kwa pasi hilo shati hapo na pasi hiyo hapo ya mkaa.
Alieambiwa akajibu "hii pasi yako haipigi shoti, naogopakurushwa"

Saturday, February 4, 2012

Safari ya boti

Mzee mmoja alikua kwenye boti akielekea visiwani, bahati mbaya upepo ukavuma na msuli aliovaa ukapeperuka. Mzee muda wote huo aliwahi kikofia chake (baraka-sheikh).

Kumuuliza matokeo ya kuzuia kofia na kubaki uchi yeye akajibu "hizo nywele mzionazo na hiyo naniliu vyote vya zamanj, hii kofia bado mpyaa."

Kwa mchungaji

Mchungaji akitoa maombi... "waumini mkirudi nyumbani muinue matatizo yenu juu na Mungu atayatatua.

Muumini mmoja aliporudi nyumbani yeye akamnyanyua juu mkewe.

Friday, February 3, 2012

Maembe yakigawana

Jamaa wawili walinunua maembe sasa wakaamua wakayahifadhi kwenye chumba cha kuhifadhi maiti. Baadae mlinzi akasikia watu wakiongea "...we chukua hii nipe hiyo..." Mlinzi,akakimbia na kukutana na dokta akamuambia huku akihema "dokta... Hahh hahh... Mochuari maiti zinachukuliwa na shetani wanagawana"

Utaniii

Jamaa mmoja mrefu alilala kitandani, kwa vile kitanda ni kidogo miguu ilizidi nje. Rafiki zake walipokuja wakamfunga kitambaa chekundu wakimaanisha mzigo umezidi bodi kama kwenye gari ya mizigo.

Thursday, February 2, 2012

Kupanda na...

Jamaa mmoja alitoka kijijini akaja mjini Dar es Salaam. Siku moja wakati ameenda kupanda daladala kabla hajapanda akamuuliza konda "kondakta samahani naruhusiwa kupanda na viatu?"

Wednesday, February 1, 2012

Amemeza...

Jamaa: Mtoto wangu si alimeza condom yangu jana bwana...
Rafiki: Aah sasa ulipata ingine au ilikua iyo iyo tu?

Mtoto alichokiona

Mtoto mmoja akimsimulia mama ake, "mama leo nimemuona mwanamke kavaa sketi fupi huyoo kaama yule anaekuwaga na baba ukienda kazini"

Dereva alipoambiwa

Dereva mmoja alishuka kwenye gari haraka haraka baada ya kusimamishwa na mtu haraka haraka na kuhoji "vipi mbona umenisimamisha ghafla hivi kuna nini?"
Jamaa aliemshusha akanena "matairi yanazunguka huku nje ndio nkikuambia."