Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, April 27, 2012

Diet

"Kaka nasikia siku hizi unafanya diet" kijana mmoja akimuambia rafiki yake aliekua mnene mnene kidogo" Papo hapo jamaa mmoja mingine kati yao akadakia "mhh! Labda afanye diet ya kunywa bia"

Wednesday, April 25, 2012

Mkopo huo

Jamaa akimshushua mwenzake "mshkaji wangu we tatizo unakopa sana, chuupi unakopa, maji unakoopa, mwanamke ukienda nae gesti unakopa pia" Jamaa akajibu: Sasa hali tete mie nifanyeje?

Tuesday, April 24, 2012

Kibweka cha leo

Soma hii ucheke kidogo: KESHO KUNA MAANDAMANO YA WEZI WANATAKA WAONGEZEWE SIKU, BADALA YA SIKU ZA MWIZI NI 4O, SASA ZA MWIZI ZIWE 60. UKIPATA UJUMBE HUU WATUMIE NA WEZI WENZIO WOTE.

Friday, April 20, 2012

Mgonjwa na Dokta

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi nna umwa malaria na kifua. Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu? Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta. Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.

Wednesday, April 18, 2012

Pilau la bachela

Bachela mmoja aliekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza. Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.

Nani alaumiwe?

Mwanamke: Nilikubali kuolewa na wewe haraka haraka kwasababu nlikua nna hasira siku ile. Mwanaume: Ooh! Mie sikuliona hilo nlikua kwenye dimbwi la mapenzi juu yako.

Full tank

Kijana mmoja alinunua gari, akaenda mpaka petrol station akajaza mafuta full tank. Alipotoka pale akaenda kwa fundi na kumuambia "fundi nna shida kidogo" fundi nae bila hiyana akajibu "niambie shida yako tu mkuu" Mwenye gari akanena "nahitaji unibandikie huu mshale wa mafuta kwa gundi ubaki huku huku juu kwenye full, ili mafuta yasiishe"

Nani kaliwa?

Nani imekula kwake hapa???? Phone call Girl:hellow Boy:sweet mambo vp? Girl: poa Boy:utakuwa free weekend?nilikuwa nataka uje nyumbani....kwangu. Girl: oh sorry,sintoweza kuja coz kuna harusi ya aunt yangu na siku ya pili kutakuwa na wageni nyumbani. Boy:kama ni hivyo sawa just nilikuwa nataka nikufanyie suprise nimekununulia i phone. Girl: oh usijali mpenzi wangu nitakuja,hata ukitaka nilale huko huko nitalala. Boy:vp kuhusu harusi? Girl:harusi ipi?nilikuwa nakutania sweety! Boy: poa na mimi nilikuwa nakutania hny!!

Hodi hodi

Usiku mkubwa mara ngo ngo ngo mlangoni: Wenye nyumba: Nani? Aliepo nje: Mimi. Wenye nyumba: Ndio wewe naani? Aliepo nje: Mimi mwizi nimeshindwa fungua mlango nimukuja kuiba tv.

Tuesday, April 17, 2012

Cheka kispoti

Wakulima wawili walikua wanatoka shamban na zana zao za kilimo wakapita katika uchochoro mmoja gafla waka sikia sauti, " simameni wote wawili wakasimama bana, weka jembe chini jamaa akaweka, weka kisu chini mmoja akasema sina kisu-ok kama huna kisu weka mavi-jamaa akatusua bana mdimba, ok we lamba mavi hapo fasta-jamaa wapili akalamba bana gafla wakasikia game sindo imeisha sasa tuchangen tena karata.

Monday, April 16, 2012

Mtoto alipotea

Mtoto wa miaka miwili na nusu alipotea alipotea na alipokua anaulizwa ili apewe msaada. Msamaria akamuuliza "enhe mama yako anaitwa nani?" Mtoto akajibu "anaitwa mama" Akaulizwa na "baba yako je anaitwa nani?" Mtoto akajibu "baba yeye anaitwa baba pia"

Sunday, April 15, 2012

Kilo zilipozidi...

Jamaa alienda kupima uzito akajikuta ana kilo nyingi kuliko akivyotegemea akashangazwa na kunena kama ifuatavyo "haiwezekani mi ndio nna kilo nyingi hivi? Embu tupime kimoja kimoja anza na mkono... Tufuate kichwa..."

Mwizi na chizi

Mwizi kaiba tv na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.

Uuwii

MAMA:Mwanangu unamjua mkwawa? MTOTO:Cmjui MAMA: pumbav kuwa makin na masomo. MTOTO:Mama unamjua joyce MAMA:Hapana MTOTO:Mama kuwa makin na mumeo..

Saturday, April 14, 2012

Jino linauma

Mume akiumwa jino kweli kweli alifika kwa dentist na mkewe. Dokta akamuuliza "jino lipi linauma?" Mgonjwa akamgeukia mkewe na kumuambia "muonyeshe dokta jino linalouma"

Gongo no. 1

Njemba moja ilienda kwenye baa ya uswahilini akaagiza gongo ile namba moja. Wakati anakunywa mwenzake akamuambia "mzee jiangalie utalewa mpaka shati ukatufia hapa buuree, taratiiibu tafadhali" Njemba akajibu "kama nikifa nistue nilianzishe tifu hatakaa mtu hapa ma*#nin"}...".

Nani ajifiche

Majira ya saa moja usiku mtoto alimuona mama yake anarudi nyumbani akamuwahi na kumuambia "mama... mama usiende nyumbani kwanza baba yupo na mwanamke mwingine, ngoja nkamuulize nani ajifiche kati ya wewe au yeye?"

Live tv

Mtoto mmoja alikua anaangalia kipindi maalumu kilichokua kikirusha kwenye tv moja kwa moja toka eneo la tukio (kipindi cha mahojiano ya hoja). Baba aliporudi nyumbani akamuambia baba ake "baba mekuona kwenye tv, mekugusa hata husikii"

Friday, April 13, 2012

Swali la mwalimu na mwanafunzi

Mwalimu: Ema kulikua na ndege watano ukamtungua mmoja watabaki wangapi? Mwanafunzi: Wataruka wote hamna atakaebaki. Mwalimu: Watabaki wanne mmoja atakufa. Mwanafunzi: Mwalimu na mimi nna swali. Mwalimu: Uliza tu. Mwanafunzi: Kulikua na wanawake watatu wanakula koni wa kwanza anailamba, wa pili ana imega, wa tatu anainyonya yupi kati yao kaolewa? Mwalimu: Mhh! Wa tatu ndio kaolewa. Mwanafunzi: Umekosa alieolewa mwenye pete ya ndoa kidoleni.

Chemsha bongo

Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anaesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?" Mtoto akajibu "iyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"

Mume na mke kaazi...

Mwanamke: Mume wangu naomba hela nkanunua bra. Mwanaume: Mbona huna cha kuweka humo? Mwanamke: We mbona umevaa boxer wakati huna cha kukiifadhi humo?

Lipi bora

Mwanamke huki akimchapa mumewe "wee si ulisema umekoma kutembea na wanawake wa nje?" Mume: Mke wangu basi nisamehe sitarudia ntatembea na wanawake wa ndani tu.

Je umelewa?

Askari wa doria walimdaka mzee mmoja akiwa chakali kwa pombe huku akiendesha gari. Askari: Mzee unajua kwamba unaendesha ukiwa umelewa. Mzee: Hapana sijalewa afande kwani vipi (akiongea kilevi levi) Askari: Naomba leseni na kadi ya gari. Mzee: Ok, nishikie hii bia yangu nkutafutie hivo vitu.

Simu ya mke...

Mume wa mtu alikua yupo gesti hausi na nyumba ndogo yake. Punde simu ikaita mkewe akiwa anampigia "mume wangu nimekuja ofisini sijakukuta nimeambiwa umetoka upo wapi?" Mume nae bila hiyana "ohh my wife nimetoka nafanya kazi za nje leo"

Pombe hii?

Cha pombe mmoja akifokewa na mkewe "tatizo lako ukilewa huwa unaongea sana" njemba nayo haikukaa tu kimya akaamu kumjibu "mke wangu tatizo pombe nnazokunywa zinakua zisha-chacha ndio maana."

Wednesday, April 11, 2012

Hela

"Mzee umedondosha hela" kijana mmoja alimuambia. Mzee akapuuzia na kusema "okota tu hela yenyewe feki"

Tsunami

Taharifa ya Tsunami kutokea pwani ya maeneo ya Tanzania baada ya kupata tetesi kuwa haitatokea jamaa mmoja akanena "tsunami imeahirisha kuja Tanzania kisa umeme umekatika"

Tuesday, April 10, 2012

Mpenzi pombe

Jamaa akiiambia bia yake akiyokiinywa "wewe ndio mpz wngu! Huna wivu hata kdg hata mkiwa watatu meza moja. Tatizo lenu nikiondoka nashindwa kujua nani kati yenu kanilewesha sana"

Monday, April 9, 2012

Wapi ufunguo?

Mwanamke mmoja alipoteza ufunguo wa nyumba maeneo ya nyumbani. Sasa wakati anautafuta mumewe aliporudi akauliza na kuambiwa ufunguo umepotea. Mume akatoa simu na kumuambia mkewe "hebu nipe namba niu-beep"

Sunday, April 8, 2012

Kibweka - Pasaka

Mtoto alienda uganini siku ya pasaka, kabla ya mlo wa mchana akamuuliza mama yake kwa kumnong'oneza "eti mama na hapa watapika na toothpick?" Mama akajibu "mwanangu hizo huwa hazipikwi" Mtoto: Mbona nyumba ya jirani house girl huwa anazipika na zenyewe?"

Saturday, April 7, 2012

Jina la kijiji utata...

Mkoa wa Ruvuma una kijiji kinaitwa SENGE. Rais alienda ktk kampeni za Uchaguzi 2010. Mambo yakawa hivi: M/kiti na Katibu WA SENGE. Ndugu wananchi WA SENGE, Vijana, Wazee Wenzangu, na Watoto Wooote Wa SENGE. Mabibi Na Mabwana Wa SENGE "Asalam aleykum". "Wa Senge Oyyeeee!" Wa Senge Kimyaaaaa!.

Friday, April 6, 2012

Shetani bar

Wakiwa bar wanakunywa ghafla aliingia shetani, bar nzima kila mtu akakimbia mlevi mmoja akabaki. Shetani: We mbona hujakimbia huogopi? Mlevi: Niogope nini wakati nimemuoa dada yako miaka 20 iliyopita.

Mazungumzo - madereva

Dereva wa kwanza: Mie nlikuwashia taa nkikuambia kuwa acha mimi niende wa kwanza. Derava wa pili: Na mimi nilikuwashia wiper nikikuambia hapana, hapana.

Hamna kisichowezekana

Mtoto mmoja akimuambia baba yake jambo "hamna kinachoshindikana katika hii dunia" Baba yake akajibu "okay! Itoe dawa ya mswaki kwenye chupa yake kisha uirudishie humo humo.".

Faini chuoni

Mkuu anaehusika na wanafunzi wa chuo akiwafafanulia jambo wanafunzi wapya chuoni "ndugu zangu... Bweni la wasichana ni wasichana tu na wanaume ni wanaume tu." Akiendelea kuwaasa "atakae kamatwa mara ya kwanza atalipishwa faini ya elfu 20, mara ya pili elfu 60, mara ya tatu elfu 180." Mwanafunzi mmoja akanyoosha mkono kuashiria anaomba kuuliza swali, aliuliza hivi "je? Ni shilingi ngapi kwa muhula mzima?"

Swali na jibu

Mwalimu: Nini kinakufanya uone? Mwanafunzi: Ni Macho, pua na masikio! Mwalimu: Pua na Masikio? Kivipi? Mwanafunzi: Pua na Masikio hushikilia miwani yangu.

Mlevi na Mkewe bar

Mlevi mmoja alitoka na mkewe kwenda pata baridi moto katikati ya kinywaji njemba ikanena "I love you so much" mkewe akamuuliza "unaongea na mimi au bia?" Jamaa akatoa jibu lake "naongea na bia sio wewe."

Kutengeneza keki

Mtoto aliona mbwa wakifanya mapenzi akauliza mama yake "mama wale wanafanya nini?" Mama akajibu "wanatengeneza keki." Siku ingine akaona mbuzi akajibiwa ivo ivo. Siku moja mbele baada akaenda kwa mama yake "mama wewe na baba jana mlitengeneza keki sebuleni?" Mama "wewe umejuaje?" Mtoto akajibu "si nimekuta juisi juisi imedondokea kwenye kapeti"

Thursday, April 5, 2012

Mke muoga

Njemba moja: Mke wangu muoga na anaogopa maji. Rafiki yake: Unamaanisha nini? Njemba: Kila nirudipo nyumbani namkuta kwenye sinki la kuoga na houseboy bafuni.

Wednesday, April 4, 2012

Msg kwa wife

Meseji kwa mke wake "darling nipo bar napata mbili tatu, nitarudi ndani ya dk 50 zijazo, ukiona kimya soma tena hii meseji"

Besdei ya mke

Jamaa akimuuliza rafiki yake jambo "aisee nisaidie namna ya kuweza ikumbuka siku ya kuzaliwa mke wangu maana..." Rafiki nae akamjibu "mbona rahisi tu, isahau mara moja tu utapata..."

Mtoto miaka 18

Baba: Mwanangu sasa umetimiza miaka 18, njoo tuongee masuala ya mapenzi, kuachwa nk nk Mtoto wake wa kike akajibu: Sawa baba njoo nisikilize matatizo yako. Haya wapi panakukwaza nikusaidie kutatua?

Gym...

Kijana alienda GYM kufanya mazoezi akamuuliza mkufunzi wa mazoezi "nataka kumvutia mchumba wangu mashine/kifaa gani nitumie sana?" Mkufunzi akamjibu "mi nadhani mashine nzuri ya kumvutia mchumba ako ni ATM"

Mvuto nk

Mvulana: Navutiwa sana, sura nzuri, mvuto, kucha nzuri miguu ndio usiseme. Naweza pata namba ya simu? Msichana akijibu kwa aibu: Enhhe! Asante. Namba ya simu ni... Mvulana akamkatisha: Aahh sio wewe ni yule rafiki yako.

Changanya changanya

Deo akimsimulia mshkaji wake "unajua nini? Duniani hapa wanaume kuna mambo mawili huwa wayaelewi." Juma akajibu "kipi hicho wasichokielewa?" Deo "kumuelewa mwanamke kabla na baada ya ndoa."

Majina ya mapacha

Injinia mmoja wa program za kompyuta alipigiwa simu na kuambiwa mkewe kajifungua mapacha, hivyo wamekwama kuwatafutia majina... Jamaa akafikiria ndani ya muda mfupi akapata jina akawaita copy mwingine paste.

Nani kapoteza muda

Mwanafunzi wa darasa la pili: Yule mvulana anapoteza sana muda. Mwalimu: Wewe umejuaje unasema hivyo? Mwanafunzi: Nilikua nimekaa tuu namuangalia muda wote.

Saa ya bei chee

Jamaa walienda kununua saa! Mmoja akanunua saa ya laki 2 mwingine akanunuasaa ya elfu 30. Jamaa wa kwanza akamuuliza mwenzake "utofauti wa bei je zote zinaonyesha muda sawa?" Jamaa wa pili akajibu "hapana yako inaonyesha muda wako yangu inaonyesha muda wangu."

Njiwa amekufa

Baba akiwa matembezini jioni na mwanae: Mtoto: Baba huyu sio njiwa amekufa? Baba: Amekufa ndio, keshaenda kwa Mungu. Mtoto: Sasa mbona Mungu kamrudisha hapa tena?

Tuesday, April 3, 2012

Samaki baada ya...

Mtoto mmoja akiwa na baba yake restaurant: Mtoto: Najua kwa nini watu wakila samaki hawanyi maji... Baba: Kwa nini unasema hivyo mwanangu? Mtoto: Kwa sababu wanaogopa samaki wataanza kuogelea.

Kwenye harusi

Mtoto: Kwa nini Bw. Harusi huwa anakua upande wa kulia na Bi. Harusi upande wa kushoto? Mhasibu akajibu: Kwa mujibu wa Profit and Loss kwenye accounting, upande wa kulia kunakaa Income na upande wa kushoto expenses.

Kazi ya mwalimu

Mkufunzi walimuuliza mwanafunzi wake mmoja "wenzako woote wamekusanya kazi nliyotoa wewe ya kwako sijaiona kwanini?" Mwanafunzi akajibu "mbona nime-i-upload muda mrefu facebook nikaku-tag pia, hujaiona?"

Kibweka cha leo

Jamaa walikua wanapiga stori za hapa na pale maongezi yalikuwa hivi: Jamaa A: Unajua pale ilala unapata vitu karibu vyote vya mtumba! Jamaa B: Aacha utani bwana. Jamaa A: Ndio nakuambia hivyo sijui nguo, ma-jagi ya umeme, mabegi nk Jamaa B: Chakula je kipo cha mtumba?