Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, May 30, 2012

Ajali ilivyotokea

Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika." Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"
Mwanaume kwenye simu "dokta, mke wangu ameanza kuwa anafikira kama sungura...." Dokta akajibu "ihh mlete hospitali nimcheki. Mume akanena "dokta vyovyote itavyokuwa usimpe tiba lakini.

Dawa yake

Mume alizoea kila mara akirudi usiku ananyimwa unyumba na mkewe kwa kisa anaumwa kichwa. Siku mume akarudi na moja kwa moja akampelekea panadol mbili na maji, mkewe akanena "nani kakuambia naumwa kichwa?" Mume akajibu "yes nimekukamata leo"

Mshtuko wa moyo

Mume karudi akasikia sauti asiyoielewa toka chumbani kwake, akaenda na kukuta mkewe analalamika amepata mshtuko wa moyo. Mbio anaenda sebuleni kupiga simu kuomba msaada. Punde mwanae akaja "baba anko Jose kajificha kabatini kwako uchi" mzee mbio mpaka chumbani. Fungua kabati akamkuta ndio na kumuambia "wee mke wangu anapata mshtuko wa moyo we umejificha tu uchi humu unawatisha watoto, njoo tumpe msaada haraka."

4WD

Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"

Ya leo mgonjwa

Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliepata ajali. Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?" Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh? Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.

Sunday, May 27, 2012

Pombe basi

Cha pombe alikunywa sana pombe akataka ongeza mhudumu akamjibu "hapana imetosha sasa umekunywa saaana." Mlevi akajibu "nimeanza kunywa miaka 36 ilopita sijawahi jua kama metosheka wewe umejuaje?"

Kwa mama lishe

Jamaa kwa mama lishe baada ya kula wali nyama akaletewa vijiti vya kutolea nyama kwenye meno. Vilipofika tu mezani kwake akahoji "vimechemshwa hivi? Maana kipindupindu nje nje."

Saturday, May 26, 2012

Wasiwasi

Dogo akimuongelesha mama yake aliepo sebuleni yeye akiwa jikoni "mama!" Mama nae akaitikia "ooh mwanangu" Mtoto: Unaikumbuka ile sahani inayokupa wasiwasi isije niteleza ikavunjika siku moja. Mama: Ndio mwanangu. Mtoto: Basi wasi wasi wako umeisha leo.

Swali jibu tofauti

Mwalimu aliuliza wanafunzi wa darasa la 3 wakike kwa kiume "mlikuwaje hapo awali kabla hamjawa hivi mlivyo leo wanafunzi?" Mwali akisubiria jibu akitaraji watajibu "walikua wadogo" wanafunzi wao wakajibu "tulikua na furaha, wengine wakilia nk"

Home work

Mwalimu: Haya James iko wapi homework yako? Mtoto: Mwalimu ilmeliwa na mbwa wetu nyumbani. Mwalimu: Nimefundisha kwa miaka 18 sasa, unadhani nitaamini hilo? Mtoto: Ni kweli mwalimu nimemlazimisha mpaka kaila.

Friday, May 25, 2012

Mbio za ushindi

Baba: Wewe Japhet hiyo saa umeipata wapi? Mtoto: Neshinda mbio ndio nkaipata. Baba: Hizo mbio mlikua na akina nani? Mtoto: Alikuwepo polisi, mwenye saa na mimi.

Fala wa kwanza

Mume: Unaniambia walikutongoza wanaume wanne ili wakuoe? Mke: Ndio hivo hivo kama ulivyosikia. Mume: Bora hata ungeolewa huyo fala wa kwanza kati ya wote waliokutongoza. Mke: Ndio nlivyofanya hivyo.

Thursday, May 24, 2012

Mwizi wa atm

Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu"

Kifamilia zaidi

Mke na mume wakiongelea suala la fedha kifamilia: Mwanaume: Sikiliza isingekua fedha hii nyumba isingewepo. Mwanamke: Na wewe sikiliza isingekua fedha zako nisingewepo hapa.

Wednesday, May 23, 2012

Hii nayo

Mvulana: Nilimuita boifrendi wako shoga, si akanipiga na pochi yake.

Bia

Mama akisimuliwa na mwanae wa miaka saba "mama tulienda bar na dada, akajisikia vibaya na kushindwa kunywa bia yake. Ikabidi mimi ndio niinywe."

Tuesday, May 22, 2012

Jamaa alinunua friji jipya la zamani akaliweka nje na kuandika "friji hili ni bure nalitoa" zikapita siku mbili hamna alieamini yale. Siku ya tatu akaandika "friji hili lauzwa laki mbili" usiku wake likaibiwa.

Monday, May 21, 2012

Msaidie mwenzako

Jamaa mmoja alikua anamrekodi mwenzake kutumia video camera huku mhusika akicheza na moto. Ghafla moto ukashika shati la jamaa... Mpita njia akamuambia mwenye camera "wewee acha kamera muokoe mwenzako..." Mwenye Camera akajibu "kaniambia nimrekodi tu sasa mi nifanyaje?"

Saturday, May 19, 2012

Cheka kidogo

Njia rahisi kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) vaa viatu vinavyokubana.

Wednesday, May 16, 2012

Mlizi mbio mbio

Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta, Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa Mzee: Umemtambua aliyeiba? Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.

Hakimu & hongo

Kesi imeanza hakimu kakaa kwenye kiti chake akatangaza; Hakimu: Mlalamikaji na mtuhumiwa wote mmeniletea hongo niwapendelee. Mlalamikaji umenipa laki moja, mtuhumiwa umenipa umenipa laki moja na hamsini. Sasa nawarudishia hii hamsini elfu ili nisiwe na sababu ya kumpendelea mtu. Tunaendelea...

13, 13...

Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anesema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,..... akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14......

Ushauri wa dokta

Jamaa alikuwa anaumwa sana mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho; Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa Jamaa: Sijafa bwana Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.

Mume anaenda kazini

Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini.........

Friday, May 11, 2012

Mama aliporudi

Mtoto "mama afadhali umerudi baba yupo nyumbani na anti, baba kamlalia anti kwa juu wote wanapiga kelel sijui wanaumwa nini mimi meshindwa wasaidia

Simu ya tochi

Jamaa mmoja alikua na simu yenye tochi Po. Kwenye kagiza giza rafiki yake akaiomba awashe kumulikia mwenye simu akamjibu "aahh usiiwashe itamaliza vocha yenyewe kimeo"

Wednesday, May 2, 2012

Kitana mapengo

Dukani: Nikusaidie nini kaka? Mteja: Kitana changu vile kichanio kimevunjika. Dukani: Sasa si kimoja tu vilivyobaki vingine si vipo. Mteja: Hapana kilichovunjika ndio cha mwisho kabisa.

Hasira za mtoto

Baba na mtoto: Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini? Mtoto: Naenda chooni. Baba: Chooni? Kufanya nini? Mtoto: Kusafisha. Baba: Halafu ndio hasira zinaisha? Mtoto: Ndio nasafisha choo kwa mswaki wako.

Duka la tai

Jamaa alienda nunua tai alipofika ikawa hivi: Muuza duka: Karibu, nikusaidie nini? Mteja: Natafuta tai iliyochanganyika na maziwa na kahawa hivi. Muuza duka: Sijajua na sukari je au hutoitaji?

Tangaza ndoa...

Njemba ilienda kutangaza ndoa: Njemba: Mzee mimi nataka kumuoa mwanao. Mzazi: Unafanya nini kusukuma siku? Njemba: Nakaba, kupora na kubaka. Mzazi: Mbona vyote na hasi huna hata moja chanya? Njema: Ohh! Chanya nina HIV +ve.