Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, June 21, 2012

Baba na Bintie

Binti: Hi Baba Baba: Hi binti yangu? Binti: Nimempenda huyu mlinzi wa hapa nyumbani na nimeamua kutoroka nikaolewe nae Baba: Pumbavu kweli wewe unadhani nitashtuka? Safari njema na nisione sura yako tena hapa! Binti: Samahani baba... Nilikuwa nakusomea barua aliyoacha mama Baba: Umesema.????.!

Monday, June 18, 2012

Mlinziiii

Binti: Hi Baba Baba: Hi binti yangu? Binti: Nimempenda huyu mlinzi wa hapa nyumbani na nimeamua kutoroka nikaolewe nae Baba: Pumbavu kweli wewe unadhani nitashtuka? Safari njema na nisione sura yako tena hapa! Binti: Samahani baba... Nilikuwa nakusomea barua aliyoacha mama Baba: Umesema.????.!!

Mpenda mpira

Jamaa mpenda mpira kajichora tattoo mwilini mwake majina ya vifaa vya michezo, demu wake akawa anayasoma. kifuani NIKE pajani REEBOK, mgongoni PUMA kiunoni UMBRO matakoni FIFA, kwenye uume AIDS, msichana akashtuka kwa nini umeandika hapa AIDS jamaa akamwambia usiogope imelala tuu ikisimama patasomeka ADIDAS!

Jogoo

Jogoo alimkimbiza jike huku akiwaza nikimpata ataipata nikimkosa nitazuga nafanya zoezi, jike aliwaza nikisimama nitaonekana malaya nikikimbia nitalala na hamu ya kufanya.

Friday, June 15, 2012

Swali gumu

Mtoto alimuuliza baba ake aliporudi nyumbani akamuuliza "eti baba na wewe una nywele huku karibu na kitovu?" Baba kwa mshangao "wee mtoto umeona wapi hizo nywele?" Mtoto akajibu bila wasi wasi "baba mi meuliza tu maana yule anko anaekuja kwa mama ukiwa haupo nlimuona anazo"

Wazo la mtoto

Mtoto akimuambia baba yake pale sebuleni kwao palipokuwa na tanki dogo la kioo la kufugia samaki. Mtoto "baba mi naona kama hao samaki wana kiu si uwaekee maji ya kunywa!"

Tuesday, June 12, 2012

Kipigo icho

Mwanaume alienda kwa daktari wake ikawa hivi: Mwanaume: Dokta, mke wangu ananitwanga mangumi mno. Dokta: Kivipi na kwa nini haswa? Mwanaume: Mara zote anikutapo chumbani kwa house girl.

Semea mbovu

Mwanamke akimsemea mbovu bwana ake kwenye simu "mtu mwenyewe huna ishu, kwanza sio type yangu..." Mwanaume akajibu: Mpenzi wangu kwani vipi? Nipo bank kwa sasa... Mwanamke kusikia ivyo akanena "ohh mpenzi basi uje na laki moja nimeishiwa kitu..."

Sunday, June 10, 2012

Wazaramu

Wazaramu walimkamata mwizi wakamuweka mtu kati wakamsema weee mpaka mwizi akafa.

Wednesday, June 6, 2012

Faini ya kukojoa

Polisi alimdaka jamaa anakojoa pembezoni mwa ukuta. Polisi: Wewe unajua panakatazwa kukojoa hapa? Jamaa: Sasa nimebanwa nifanyaje? Polisi: Faini yake elfu tano. Jamaa akatoa noti ya elfu 10. Polisi: Sasa chenji tunaipataje? Jamaa: Tafuta chenji unipe changu. Polisi: Basi kojoa tena...