Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, August 31, 2012

Kitu cha posa...

Jamaa alienda kuposa kwa mzee mmoja.
Mzee: Umekuja kuposa huku unatafuna big g!!?
Jamaa: Natoa harufu ya sigara.
Mzee: Yani unavuta sigara!?
Jamaa: Vile nikitoka kilabu kulewa tu.
Mzee: Unalewa!?
Jamaa: Nilianza kulewa nilipokuwa jela.
Mzee: Yaani na kufungwa pia!?
Jamaa: Ah niliua mtu.
Mzee: Duh kumbe wewe muuaji!?
Jamaa: Ah, si kuna mzee nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, mimi nikamuulia mbali.
Mzee: Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, mke mkeo uyu! Na mahali utaleta ukipata haina shida.

Thursday, August 30, 2012

Wizi Vs. mkwara

Jamaa mmoja alimuibia nauli mzee kwenye daladala..
Mzee: jamani alieniokotea nauli yangu airudishe kabla sijafanya nilichofanya mwaka 1947. Kijana kwa kutetemeka akarudisha hela ya babu alafu akauliza kwani babu ulifanya nini mwaka 1947 Mzee akajibu nilitembea kutoka mbagala mpaka posta.

Tuesday, August 28, 2012

Nani atupe...

Ndani ya meli,watu makabila tofauti walikua na mizigo,meli ilizidiwa ilibidi mizigo ipunguzwe,Mzungu akatupa computer, akasema"kwe2 zpo tele,Mchina akatupa box la cmu akasema"kwetu zipo tele" Muhindi Akamwaga kiroba cha tambuu akasema kwetu zipo kibao, Mmasai akatupa shanga.. Mchaga anahaha hajui atupe nini kila kitu chake anakionea uchungu ,ghafla alimtumbukiza Mmasai akasema"Yesu na maria hawa wapo tere ARUSHA"

Sunday, August 26, 2012

Kwa Dokta

JANE:"Daktari,kila mara baada ya kukojoa mwisho wa mkojo hutoka rangi ya brown." DAKTARI:"Mmmh,h uwa unafanya mapenzi mara ngapi kwa siku?" JANE:"Hee,ati siku! Mi hufanya mara mbili kwa mwaka dokta." DAKTARI:"Huo si ugonjwa ni kutu!"

Saturday, August 25, 2012

Mchungaji nae

MCHUNGAJI: Mgeukie jirani yako na umwambie Mungu yumwema, WAUMINI wote wakageukiana na kusema Mungu yumwema, MCHUNGAJI: Leo nitawaombea wale wote wasio zaa,mgeukie mwenzio na umwambie leo utapata mimba, mara likasikika bonge la kofi siti za nyuma! Kumbe mtoto 1 alimgeukia baba yake na kumwambia leo utapata mimba.

Wednesday, August 22, 2012

Pete ya dhahabu

Dada mmoja aliingia duka la urembo, akaona pete 1 ya dhahabu, wakati akiisogelea aione vizuri, bahati mbaya akajamba, akaangalia pande zote kama kuna mtu kamsikia, alipogeuka nyuma akakutana macho kwa macho na muuzaji. Kwa aibu akazuga akamuuliza muuzaji hii pete unauza shilingi ngapi? Muuzaji akamjibu "kuiona tu umejamba, je nikikutajia bei si utakunya hapa hapa?"

Tuesday, August 21, 2012

Mkristo na futari

Ivi unafaham... Mkristu kavamia futari vuuuupu. Baada ya kula Sheikh akamchagua asome dua ya kushukuru! Jamaa kataka kuingia mitini ila akajikaza kiume na kuanza kama ifuatavyo: Jamaa:Ya Tawfiq. Watu:Amin. Jamaa:Ya Habib. Watu:Amin. Jamaa:Ya Shabiby. Watu:Amin. Jamaa:Ya Abood. Watu:Amin. Jamaa:Ya Hood. Watu:Amin. Jamaa:Ya Scandnavia. Watu:kimya! Jamaa:Ya Ngorika. Watu:Mhhhhhhh! Jamaa:Ya Dar Express! Watu:Aaaaa, chezea sisi kamata tia bakora mwanaharamu huyu!

Utambulisho

Semina Ubungo Plaza... watu wakaanza kujitambulisha, Wa kwanza: Mimi naitwa John niko UDOM mwaka wa pili nasoma LAW. Wa pili: Mimi naitwa Stella niko UDSM mwaka wa 3 nasoma PUBLIC RELATION. Wa tatu: Kwa kusuasua sana huku akijishtukia, mimi naitwa Paul niko TANESCO mwaka wa4 nasoma MITA!!

Thursday, August 16, 2012

Kichaa juu ya mti

Siku kichaa mmoja alipopanda juu ya mwembe asubuhi akakaa huko mpaka jioni, kisha ilipofika jioni akajiangusha chini mzima mzima
Daktari wa wagonjwa akili akamuuliza "mbona umejiangusha?"
Yule Kichaa akajibu "Nimeiva tayari"

Tuesday, August 14, 2012

Simu ya nani?

Jamaa mmoja alipanda kwenye gari, wakati wapo safarini dereva wa ile gari akawasha redio, kwa vile ilikuwa na sauti ndogo na spika zake ndogo yule aliyepewa lifti akajikuta akipayuka bila kujua "simu ya nani hiyo inaita muda mrefu?" asijue kuwa ni mziki toka kwenye redio.

Baba mbali na familia

Mzee mmoja alikua anafanya kazi mbali na familia yake, siku moja alipata likizo akarudi kuwa karibu na familia yake. Alipoika mtoto wake akamuuliza mama yake "mama huyu nani?" mama nae bila hiyana akajibu "ni baba yako huyu" Mtoto akahoji tena "sasa na yule anaelalaga chumbani kwako kama baba hayupo sio ndio baba yule?"