Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, October 9, 2012

Kambi ya jeshi

Jamaa alikatiza kambi ya jeshi. Akapewa adhabu ya kubeba tofali 1,000. Alipofikisha 900 akakumbuka mkuu wa kambi kasima nae, akaenda msemea aliempa adhabu: mkuu akanena "umeshabeba mangapi hadi sasa?" Jamaa akajibu "900" mkuu akanena "basi yarudishe halafu uendelee na safari yako."

Taxi na ofa

Jamaa kwenye taxi alimuona mke wake anaingia hotel na njemba akamuambia taxi driver "unataka tengeneza laki 2 sasa ivi?" Akajibu "ndio" akapewa kazi akamchukue mke wa jamaa amlete. Akarudi na mwanamke sie jamaa akanena "huyu sio mke wangu" taxi driver akanena "najua! Huyu ni mke wangu mshikilie namfuata wako sasa."

Monday, October 8, 2012

Dokta na mgonjwa wake

Daktari mmoja alienda wodini akamkuta mgonjwa wake amelala usingizi maongezi yakawa hivi baada ya kumuamsha "nimekuja kukuletea dawa ya usingizi hii hapa kunywa"