Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, July 10, 2013

Swali kwa wanafunzi

Mwalimu akiwa darasani akauliza swali: Haya naomba mniambie, utamuitaje mtu ambae anaongea na mtu au watu wakati huo huo wanaomsikiliza hawana mvuto wa kusikiliza akiyoyasema? Mwanafunzi mmoja akanyoosha kidole na kujibu: Jibu ni Mwalimu.

Ma-lavi-davi

Msichana: Nakupenda sana na nitakufa kwa ajili yako. Mvulana akajibu: Lini haswa utakufa sasa?

Jibu la mpenzi

Mvulana na msichana wapenzi wakiwa matembezini Mvulana: Naweza kukushika mkono wako? Msichana: Hapana usijali, sio mzito.

Mhudumu na mteja

Mhudumu: Nikuletee black coffee? Mteje: Kwani mna coffee ya rangi gani ingine?

Swali kwa chekechea

Mwalimu aliuliza swali kwa wanafunzi wa chekechea kama ifuatavyo: Mwalimu: Haya mninjibu swali hili, kati ya Jua na Mwezi kipi muhimu? Mtoto mmoja akanyoosha kidole na kujibu. Mtoto: Bora mwezi Mwalimu: Kwa nini umechagua mwezi? Mtoto: Kwa sababu mwezi unatupa mwanga usiku wakati tuna uhitaji, lakini jua linatupatia mwanga mchana wakati hata hatuuhitaji.