Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, March 14, 2016

Ndoa knisani

Wakati dnoa inafungwa kanisani, mchungaji akauliza "kwa yeyote mwenye pingamizi na aje mbele..." Ghafla kibabu kikasimama na kwenda mbele. Bi harusi akaanguka na akazimia. Mchungaji akamuuliza "haya babu tuambie pingamizi lako" Babu akajibu "nimeamua kuja mbele, kule nyuma sisikii vizuri."

Mlevi kaibiwa...

Mlevi mmoja alipoingia kwenye gari yake ikabidi apige simu kama ifuatavyo; Mlevi: Haloo, nimeibiwa usukani, dashboard, gia pia, na pedo za break" Polisi: Tukio limetokea eneo gani? Baada ya sekunde kadhaa mlevi akapiga simu tena polisi "Jamani msije tena kumbe niliingia mlango wa nyuma vyote vipo."

Wednesday, March 2, 2016

Picha ya mapacha

Mama mmoja alizaa mapacha, ugumu wa maisha watoto wake mmoja akaikabidhi familia moja wakamuita Kijo na mwingine familia ingine wakamuita Tulo. Siku moja mama mzazi wa mapacha akatumiwa picha ya Kijo amekua kua, akamuambia mumewe "natamani wanitumie picha ya Tulo pia." Mume akamjibu "ni mapacha kumbuka, ukimuona mmoja ni umemuona mwingine."

Walevi wawili

Walevi wawili walikua wanabishana: Mlevi 1: We umelewa, nakuambia ule ni mwezii unabisha. Mlevi 2: Sio mwezi bwana, si nyota kabisa zile we huoni? Akapita msamaria mmoja wakaona waulize "eti samahani, ule mweziii au nyota?" Msamaria akawajibu: Ile ni tubelight imefungwa kwenye mti imefunikwa funikwa na majani.
Dada mmoja alipotumiwa vocha na mpenzi wake, wakati anamshukuru maneno yalikua kama ifuatavyo: "Baby jamani asante, ila juanitumia ya kutolea."

Sahau matatizo

Jamaa mmoja alimuomba ushauri mwenzake juu ya matatizo yakiyomsonga, akamjibu kama ifuatavyo. "Namna rahisi ya kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) ni kuvaa viatu vinavyokubana."

Machizi wawili safarini

Kulikua na chizi watatu walipanda treni kuelekea Mbeya, maongezi yao kama ifuatavyo: chizi wa kwanza: Unaona vile miti inavyokimbia? Chizi wa pili akajibu: Eee! itabidi tupande miti tukirudi. Chizi wa tatu: Nauli yake ipo juu nilipieni...

Mtoto kaunguza picha

Mtoto mmoja alikua kwenye daladala na mama ake. Maongezi ya mtoto yakawa hivi kwa sauti ya kusikika kwenye daladala nzima, "kwani mama tunenda wapi wakati hatujaoga?"