Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, March 29, 2012

Kisanga cha mke

Mwanamke akihojiwa na mumewe. "mbona umechelewa kufika na ulisema ungefika saa 7mchana" mwanamke akajibu "ohh mingefika mapema ila boss alinituma nimsaidie kutafuta condom tulizotumia mkewe asijue kama nimetembea nae tulipokuwa semina." Mwanaume "mke wangu una... Nje ya ndoa?" Mwanamke "hapana tukizitumia kufundishia, mkewe alimtegeshea tu."

Wednesday, March 28, 2012

Bangi bwana

Jamaa alivuta bangi akavua nguo zote akajicheki kwenye kioo akajiona kavaa suti. Akaenda kwa wenzake akawauliza "nimevaa suti nimependeza enh?" Wenzake wakajibu "umependeza kweli ila tai umekosea kuivalia chini."

Tuesday, March 27, 2012

Kizee hospitali

Dokta akimpa majibu mzee wa miaka 70.
Dokta: Nina habari nzuri na mbaya.
Mzee: Oh nipe nzuri kwanza.
Dokta: Vipimo vinaonyesha una saratani, una miaka miwili tu ya kuishi.
Mzee: Oh! Mbona miaka mingi hivo ntakua nshakufa tayari. Nipe habari mbaya sasa...
Dokta: Ndani ya miezi mitatu utakua umesahau yote nliyokuambia.

Sharobaro kanisani

Mchungaji mmoja akiwapa mikono wa waumini kabla ya ibada, akamkuta kijana sharobaro akamuhoji "kijana karibu ujiunge na jeshi la Mungu"
Kijana: Tayari nimejiunga jeshi la Mungu.
Mchungaji: Mbona nakuonaga kanisani krismas na pasaka tu sasa?
Sharobaro akajibu "Ohh, mimi ni secret service."

Sunday, March 25, 2012

Mpita njia aliuliza

Jamaa alikua anapita njia akaona nyumba moja watu wengi mno. Akauliza "kunani hapa?" Mtu mmoja akamjibu "mjukuu kamuua bibi yake"
Mpita njia akanena "ohh! Atakua na marafiki wengi kweli bibi"
Jamaa akamjibu "hapana hawa watu wanataka inunua hii nyumba."

Huduma ya dharura

Dokta mmoja akimsimulia mwenzake "baasi bwana, alikuja jamaa na dharura ohh mke wangu yupo kwenye taxi anakaribia kujifungua"

Dokta akaenedelea simulia "nkachukua vifaa husika mbio mpaka kwenye taxi, kufika nkamfunua nguo kuanza kumvua chupi, kuja kuhamaki sio mhusika nipo kwenye taxi sio zilikuwepo kama nne hivi."

Mkeo kajifungua...

Jamaa akiwa hospitali anapewa majibu na daktari "hongera sana, mkeo kajifungua mapacha wawili"
Jamaa akanena "sasa mbona sikununua vitanda viwili, nepi mbili mbili sijui itakuwaje sasa?"

Friday, March 23, 2012

Maasai gesti hausi

Mmasai alinde nyumba ya kulala wageni ugenini. Chumbani alikuta neti imeshashushwa. Asubuhi wakamkuta kalala chini kumuuliza akajibu "meona masai shamba enh alale kwenye tego nategeshea mimi?"

Enzi zilee

Mume alimuambia mkewe "tukumbushane enzi za uchumba wetu." Mke akasema ok.
Mume "kesho tukutane kijiweni petu saa 1 usiku"
Mke akajibu "okay sweetie" mume akasubiriaa mtu hakuja kabisa.
Mume akamuuliza baadae "mbona hukuja sasa?"
Mke: Mama alinikataza nisije.

Thursday, March 22, 2012

Baba na mwana

Baba: Jumaa...
Mtoto: Eeh baba.
Baba: Niletee kiberiti.
Mtoto: Cha sigara au bangi?
Baba: Shika adabu yako, cha sigara.
Mtoto: Cha baridi cha moto?
Baba: We leta kiberiti chochote.

Hausi geli mpya

Mzee alirudi nyumbani akakuta mkewe kaleta dada wa kazi za ndani (beki 3).
Mume: Mke wangu huyu nani?
Mke: Ni dada wa kazi za ndani.
Mume: Huyu nilimuona facebook akimsifia hausiboi wa jirani yetu huyu... Hapa kapajuaje?
Mke: Mimi nilimu-add kama rafiki humo humo facebook.

Wednesday, March 21, 2012

Bangi mbaya

Mzee mmoja alikataza vijana wasivute bangi pembeni ya nyumba yake. Vijana wakavuta wakavua mashati na kuanza kuisukuma nyumba.
Kibaka akapitia shati zao. Mmoja akageuka na kusema "tujitahidi kusukuma tumefika mbali hata mashati hayaonekani tena."

Tuesday, March 20, 2012

Habari ya msiba

Jamaa mmoja mila zao ni kuchoma maiti. Alitumiwa ujumbe kuwa mama yake mzazi amekufa na kumuuliza kama wauchome moto mwili au wamsubiri mpaka afike.
Jamaa akajibu ujumbe "uchomeni tu moto, halafu na majivu pia msisahau kuyachoma naja siku mbili hizi."

Mpaka kwa dokta

Jamaa alienda mpaka kwa daktari na kumuelezea "dokta ona nna karoti kwenye pua, na kipande cha pera kwenye sikio, ntakua na tatizo gani?"
Dokta akajibu "hauli inavyotakiwa"

Kasichana

Mtoto mmoja wa kike miaka 12 akimsimulia mama aliporudi toka kazini. "mama mi nadhani yule hausi boi wetu atakua shoga tu."
Mama kwa mshangao akauliza "hee kwa nini wasema hivyo?"
Mtoto akajibu "nimemshika naniliu weee hata haisimami."

Ajali hii mhh!

Trafic polisi: Unatambua kua umeua watu 10 kwenye ajali hii?
Dereva: Breki ziligoma, kushoto kuna mtu mmoja kulia wawili ungekua wewe ungeelekezea wapi gari?
Trafic polisi: Ningeelekea upanda wa mtu mmoja.
Dereva: Unaona, ndio nlifanya ivo ivo ila yeye alikua anakimbilia kwenye watu wengi mi nkamfuata huko huko.

Kosa lingine

Mwanafunzi: Mwalimu nimekosa sitorudia ten a, nipo chini ya miguu yako.
Mwalimu: Yaani umeongeza kosa huko chini ya miguu yangu unachungulia nini?

Mlokole na mlevi

Mlokole alipanda daladala akakaa pembeni mwa mlevi. Maongezi yao yakawa hivi:
Mlokole: Unajua wewe unaenda motoni?
Mlevi: Oh! Kumbe, wee konda nishushe bwana mi nlidhani unaenda mjini.

Saturday, March 17, 2012

Mwizi wa wallet

Mlevi mmoja aliibiwa wallet kwenye bus, "jamani kuna mtu kaniibia wallet yangu, naomba airudishe. Isije yakatokea yaliotokea mwaka jana."

Baada ya muda mwizi akairudisha, jamaa akapekua kila kitu kipo poa. Mwanamke mmoja akamuuliza "kwani mwaka jana kilitokea nini?"
Mlevi akajibu "niliibiwa wallet hivi hivi ikabidi nitembee mpaka nyumbani."

Friday, March 16, 2012

Pombe bwana

Walevi wawili walikua chakali wamelewa. Wakawa wanabishana "ule mwezi ni wa kijani" mwingine anasema mwekundu.
Mbele wakamkuta mtu wakamuuliza "eti, samahani ule mwezi ni kijani au mwekundu?"
Alieuliza aliangalia juu kisha akanena "upi sasa wa kushoto au kulia?"

Boss na masikio

Kwenye usahili boss asiekua sikio hata moja alikua anahoji ili apate mfanyakazi mwenye sifa.
Boss: Hii kazi inahitaji ufanisi, ni kwanza nini umekiona toka kwangu?
Mtu wa kwanza: Huna masikio kabisa.
Boss kwa hasira "toka nje"

Wa pili ivo ivo akatotelewa, mlangoni akamuonya mtu wa tatu. Alipoingia wa tatu nae akajibu "haujavaa miwani leo"
Boss: Umejuaje?
Mtu wa tatu: Kwa sababu huna masikio.

Thursday, March 15, 2012

Vituko vya dereva

Jamaa mmoja alidakwa na polisi akapaki pembeni. Gari ina vioo vyeusi aliekua anaendesha ni mmoja, akahamia kiti cha abiria mbele. Polisi alipofika akauliza "dereva wa hii gari yupo wapi?"
Jamaa akajibu "alikuwepo hapa sekunde chache zilizopita."

Spidi kali

Njemba moja ilisimamishwa na trafic polisi:
Polisi: Nimekusimamisha unakimbiza sana gari, spidi 90 sehemu ya kupita spidi 50.
Njemba: Afande embu angalia kwanza gari si hii hapa imesimama hiyo spidi unayosema mbona siioni?

Kutoka gesti hausi

Mke: Mume wangu nimepata news zako umetoka gesti na leo.
Mume: Mke wangu si kweli kabisa kama huamini kaangalie kitabu cha wageni ameandika mwanamke mie nlijua utaenda angalia tu.

Mwizi wa dhahabu

Mwizi mmoja alidakwa akikwapua moja ya saa kwenye duka la dhahabu, alipodakwa akasema "mkuu najua hutopenda vurugu, tufanye hivi niinunue hii saa yaishe hapa hapa."
Mwenye duka akakubali alipoanza kuandikia risiti bei ya hiyo saa kibaka alipoiona bei akanena "enh samahani naona bei yake kubwa kidogo hamna ingine ya bei rahisi?"

Gari zavutana

Mtoto mmoja alikua amegeuka akaona gari zinavutana akamuuliza baba ake "baba zile gari zinavutana?" Baba akajibu "ndio mwanangu"
Mtoto akanena tena "sasa ile inayovutwa si imu-over_take anaemvuta?"

Toka usingizini

Jamaa alikua ametoka kulala na sura yake ya usingizi usingizi... "oya vipi umetoka kulala nini?" Jamaa akajibu "ndio" alueuliza akanena tena "ndio maana unanukia ndoto ndoto bado."

Wednesday, March 14, 2012

Kitu cha dokta

Jamaa aliulizwa "mbona una picha kubwa ya daktari unataka kuwa dokta baadae nini?"
Jamaa akajibu "nimeambiwa maumivu yakizidi muone daktari."

Darasa la dini

Kwenye kipindi cha dini darasa liliulizwa "nani anataka enda mbinguni?" Darasa zima likanyoosha. Mmoja hakunyoosha, akaulizwa kulikoni wewe hujanyoosha kidole akajibu "mama kaniambia nikitoka shule nsipitie popote ninyooshe nyumbani."

Pochi mpya

Jamaa mmoja alimnunulia mkewe pochi mpya. Alipofika nyumbani kumpa mkewe nae akajibu "hee hii pochi si ndio alitaka ninunulia Rashid nkamuambia hainitoshi."