Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, December 27, 2011

Vitamin

Kitu cha Pharmacy:
Mama: Nimekuja nunua vitamin kwa ajili ya wanangu.
Muuzaji: Ipi sasa? Vitamin A, B, C?
Mama: We nipe iliopo hawajui kusoma bado.

Bondia aporwa

Bondia alienda kituo cha polisi:
Bondia: Nimeibiwa laki sita na kibaka hapo njiani.
Polisi: We si bondia imekuwaje umemuachia?
Bondio: Siwezi weka pambano kwa bei ndogo ivo.

Kipofu na gazeti

"unajua sikuelewi, umesema we ni kipofu na mbona unasoma gazeti hapo?" Mwanamke aliuliza.
Jamaa akajibu "hapana umeshindwa nielewa sisomi gazeti hapa naangalia picha tu."

Petroli

Mwanaume: Daktari mke wangu kanywa petroli ana kimbia kimbia tu ndani nifanyeje?
Dokta: Funga milango na madirisha yote petroli ikiiisha atasimama.

Duka la madawa

Dukani yanapouzwa madawa:
Mteja: aunauza hii dawa?
Muuzaji: Ndio.
Mteja: Ni feki hii na sumu.
Muuzaji: Lakini hamna alielalamika kabisa.
Mteja: Uliona wapi maiti inalalamika?

Monday, December 26, 2011

Mabox

Mzee mwenye nyumba asubuhi baada ya pombe za jana kuisha akinena kwake "we mama ibu na haya mabox meengi ivi nje ya nini kama sio uchafu?"
Mke akamjibu: Mume wangu leo si boxing day? Hivyo nimekusanya mabox yoote dukani kwa mangi.

Ndio kwaanza

Ndani ya chumba cha upasuaji:
Mgonjwa: Dokta tafadhali fanya upasuaji vizuri hii ndio operation yangu ya kwanza.
Dokta: Usijli hata mimi ni operation yangu ya kwanza.

Specialist

Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi nna homa.
Dokta: Oh, nenda nyumbani kalale kwenye maji ya baridi sana kesho uje.
Mgonjwa: Sasa si ntapata nimonia?
Dokta: Najua, na mimi ni Speshalisti wa nimonia.

Maongezi ya bar

Bar na maongezi:
Rafiki 1: Glass yako ipo tupu, nikuongezee ingine?
Rafiki 2: Glass tupu siitaki labda kama ina bia.

Stori ya kifo

Jamaa akimsimulia mwenzake kifo cha mtu wakiemfahamu wote wawili:
Kijana 1: Jamaa kafa akiwa usingizini dah.
Kijana 2: Sasa akiamka atajuaje kama keshakufa?

Sunday, December 25, 2011

Kwenda xmas

Mtoto: Mama! Baba si ameenda xmas?
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto: Mpigie simu muambie mbona xmas yeye amekuja huku?

Xmas

Chekazone inawatakia wadau wote Heri ya Krismas.
Kucheka ni moja ya kuwa na afya njema.
Mungu awatangulie kwa kila jambo.

Saturday, December 24, 2011

Washua nao...

Mshua mmoja akimuuliza mwenzake baada ya kukutana airport, "rafiki yangu unaenda wapi tena?"
Mshua nae akajibu "nna hisi nna ka-malaria naenda india kucheki."

Ombaomba tajiri

Ombaomba: Nimeandika njia 100 za kuwa tajiri.
Mpita njia: Sasa mbona unaomba bado?
Ombaomba: Hii ni njia mojawapo ya kuwa tajiri.

Masumbwi

Kwenye masumbwi:
Kocha: Kwa nini hauzuii ngumi za mpinzani wako?
Mpiganaji: We huoni nnkivyozizuia kwa uso wangu?

Mpenda bia

Jamaa: Ndugu yangu kwa nini unapenda sana bia?
Mlevi: We hujui? Bia ni tamu mno.
Jamaa: Tamu mno kama nini sasa?
Mlevi: Tamu kama bia.

Friday, December 23, 2011

Walevi bwana

Walevi wawili maongezini:
Mlevi 1: Nna mpango wa kuinunua Dunia.
Mlevi 2: Mhh! Huwezi...
Mlevi 1: Kwa nini siwezi?
Mlevi 2: Siiuzi tu.

Si kavunja cha kale

Mhusika wa jumba la mambo ya kale akilalamika "Umevunja seti ya vikombe vilivyotumika miaka 800 iliyopita."
Mgeni/mtalii: Oh asante Mungu mi nlijua ni vipya.

Fundi aje...

Rafiki: Ulisema ungemleta fundi kengele ya, mlangoni siku tatu zilizopita nkaona kimya.
Rafiki 2: Nlimtuma na alikuja akabonyeza kengele wee hamna aliemfungulia.

Tip...

Mhudumu akipewa tip baada ya kumpokea mgeni hadi kwenye chumba cha hotel.
Mhudumu: Mh mh! Mzee tip kidogo.

Mzee akampatia 100Tsh.
Mhudumu: Mzee hapa kama unanitukana angalau ingekua 200Tsh.
Mzee: Siwezi kukutukana mara mbili.

Nani anachapwa?

Kijana: Kwanini ukifanya kosa baba ako anamchapa kaka ako?
Kijana: Tuko mapacha

Mtoto wa nani?

Mwanamke 1: Nna wasi wasi mume wangu anani-cheat.
Mwanamke 2: Unahisi nini haswaa?
Mwanamke 1: Watoto wawili wa mwisho nlowazaa hajafanana nae.

Jumba la makumbusho

Walipoeenda kusoma vikaratasi vya maoni ya wageni watembeleao jumba la makumbusho, walikuta kikaratasi kimeandikwa hivi:

"Kulikua na mvua kubwa nje, ndio maana nkaingia humu. Asanten kwa hifadhi"

Tangazo mume

Mwanamke 1: Nliona tangazo gazetini umetanga kumchoka mumeo ?
Mwanamke 2: Nimepata barua 200 zikisema nichukue waume zao.

Thursday, December 22, 2011

Kupima damu

Jamaa alienda pima malaria, nesi akamtoboa damu ikawa haitoki, akatoboa tena ikawa vile vile. Nesi akaamua kunyonya kidole ili itoke.
Jamaa kuona vile akanena "nesi na mkojo hautoki"

Msosi fasta

Jamaa akimsimulia jambo mwenzake "aisee dah! Ile hotel iko fasta kukuandalia msosi sijawahi ona."
Mwenzake akamjibu "hehe we hujui? Mwenye hotel anafuga simba wawili jikoni"

Wezi wawili

Mwizi 1: Tumesahau kuhesabu pesa kiasi gani tumeiba.
Mwizi 2: Ondoa shaka kesho magazeti yatasema ni Tsh ngapi?

Ndani ya lecture

Mwanafunzi 1: Ukweli sielewi kabisa Prof. Anachotufundisha.
Mwanafunzi 2: Prof. Mwenyewe anasemaga hajui anachotufundisha.

Huyu nae

Mpita njia: umesema umepoteza pochi ndani sasa mbona upo nje unaitafuta?
Mpoteza pochi amajibu: Ndani kuna giza siwezi iona.

Walevi wawili

Walevi wawili walikiongea njiani kurudi makwao:
Mlevi 1: Hiivi nani wanakua wasikilizaji pande zote mke na mume wakipayukiana?
Mlevi 2: Aah iyo simpoo si majirani...

Hakimu na mtuhumiwa

Hakimu: Mara ya mwisho nlikuonya usirudi tena hapa mahakamani hujanisikia.
Mtuhumiwa: Mh. Hakimu niliwaambia hawa polisi ila hawakunisikiliza.

"Diet"

Jamaa akipewa ushauri na dokta "sasa uanze diet, pata yai 1 tu na nusu kikombe cha maziwa"
Mpewa ushauri akauliza "sawa dokta, nifanye ivyo kabla au baada ya lunch?"

Liniumezaliwa?

Mwalimu: Fred umezaliwa tarehe ngapi?
Fred: Tarehe 26 Septemba.
Mwalimu: Mwaka gani?
Fred: Kila mwaka.

Wednesday, December 21, 2011

Mtu na mdeni wake

Jamaa alikua anamdai rafiki yake hela yake siku nyingi na kupeana kalenda tuu juu ya kulipana kila wakutanapo. Siku 1 wakati wapo bar...

Ghafla majambazi hao mara kusanyeni wallet, simu nk... Jamaa akatoa bahasha na kumpa rafiki yake.
Rafiki akauliza "hiki nini wanipatia?"
Akajibu "si ile pesa yakl unayonidai"

Ujumbe wa dokta

Jamaa aliamka asubuhi na kukuta ujumbe toka kwa dokta aliemfanyia upasuaji siku mbili zilizopita ukisema hivi:

"Tafadhali fika hospitalini mara moja, nimeshindwa nunua gazeti leo kuna sarafu yangu ya 100Tsh ilidondokea tumboni wakati nakufanyia upasuaji"

Mume wa 3

Mwanamke: Mungu wangu unaonekana kama mume wangu wa tatu.
Mwanaume: Kwani una wanaume wangapi waliokuoa?
Mwanamke: Wawili tu mpaka sasa.

Kuungama kanisani

Kijana alienda kuungama kwa paroko:
Kijana: Baba paroko nimekuja kuungama...
Paroko akajibu: Haina haja nimesoma blog yako yote.

Swali la leo

Tukikutana Bar twapeana ofa vinywaji... Petrol station mbona twachuniana? (naulisa)

Kikojozi

Mtoto akilalama kwa mama yake "mama unanionea tu, mbona baba usiku namsikia anakuuliza akojoe na unamruhusu?"

Kigugumizi

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake swali "mama kwanini baba kila siku anapenda kulala juu yako?"
Mama alikwama kutoa jibu.

Mbele ya kioo Part ii

Katoto ka miaka minne kalifuatwa na kuulizwa "wewe kusinzia mbele ya kioo kulikoni na unachelewa mafundisho?"

Dogo akamjibu baba ake "baba mie melala hapa ili ukifika muda mwenzangu kwenye kioo aniamshe kumbe na yeye kalala pia."

Mbele ya kioo

Mama mmoja alimkuta mwanae amelala huku akiwa,mbele ya kioo cha kujitazama. Mama akamuuilza "we Esther mbona umelala mbele ya kioo vipi?"

Mtoto nae bila hiyana toka usingizini akajibu "si nimelala hapa ili nijione nkiwa nimelala"
Akasisitiza "yaani nijue kweli nimelala au nipo macho."

Tuesday, December 20, 2011

Maskini kipato

Mama: Mwanangu mbona upo na huzunika sana.
Mtoto: Majirani zetu inaonekana maskini sana, mtoto wao kameza 100Tsh tu wamechanganyikiwa je angemeza elfu 10?

Saturday, December 17, 2011

Kiingereza

Jamaa mmoja wakati anapita sehemu alisikia mtu akiongea lugha ya kigeni kiinglishi. Papo hapo akanena kimya kimya akanena (kwa vile kizungu akichoongea ilikua kimobomoka bomoka mno)

"mmh huyu jamaa anaongea lugha inayofanana na kiingereza"

Friday, December 16, 2011

Hii kali

Mwanamke katikati ya ndoto akiweweseka "ondoka fasta fasta mume wangu amerudi" jamaa alie pembeni yake akatoka nje na nguo zake kujificha. Alipofika nje akagundua kuwa aliekua anaota ni mkewe na yeye alilala nyumbani kwake pia.

Walevi wawili.

Mlevi: Jana mke wangu alikua kwenye Tv
Mlevi 2: Aliingiaje sasa?
Mlevi 1: Sijui alichukua stuli maana Tv ipo ukutani.

Kengele

Mwenye nyumba wakati anatoka akakutana na mtu "wewe ni nani?" Jamaa akajibu "fundi wa kengele,nimekuja rengeneza"

Mwenye nyumba "sasa si ungekuja tangu jana fundi?"
Fundi "nipo mlangoni tangu jana nabonyeza tu kengele hamna anaekuja kufungua mlango"

Kituo cha polisi

Kijana alipofika kituo cha polisi.
Kijana: Nimekuja uliza, hao kwenye picha ukutani ni akina nani?
Polisi: Hawa watuhumiwa sugu wanatafutwa na polisi.
Kijana: Khaa! Nyie wazembe sa si mngewakamata wakati mnawapiga izo picha!?

Fundi kitandani

Mwanamke akimuambia fundi "bora umekuja yaani treni ikipita tu nje nyumba inatetema nusula nidongoke toka kitandani" akamuambia fundi apande kitandani ashuhudie mwenyewe.

Wakati fundi yupo kitandani mume akaingia "haya nini maana ya hii hali fundi yupo na wewe chumbani?"
Mke akajibu "utaamini kuwa alikua anaisubiria treni?"

Kilo mbili

Jamaa alienda kujiunga jeshi la polisi, alizidi kilo mbili akakataliwa. Akaenda saluni kunyoavna aliporudi kupima mzani akakutwa bado kilo moja.

Dogo akamjibu afande "afande hii kilo moja iliyobaki kupungua itapungua nkioga na kukojoa tu"

Wednesday, December 14, 2011

Matokeo mtihani

Dogo alipata 90 kwenye pepa. Mshua alipoona akamuambia "mwanangu sa si ungepata 100 kabisa"
Dogo akajibu "tatizo Juma aliandika mwandiko mbaya jibu la mwisho sikuona vizuri"

Joto

Abiria: Konda ondoeni gari bwana joto humu...
Konda: Oya usituzengue, shuka kapande friji.

Tuesday, December 13, 2011

Siti zipo

Abiria: Siti zipo humo ndani au imejaa?
Konda: We chizi nini kwani umesikia wamekalia ndoo humu ndani?

Hamnazo

Baba baada ya kupekua daftari za mwanae "wewe mbona madaftari yapo matupu?"
Mtoto: Niliandika labda nlisahau kupiga mistari maandishi yatakua yamedondokea kwenye begi.

Vioja daladala

Konda: Oya kamatia gari inaondoka hii...
Abiria: Siti zote zimejaa ivo ntakaa wapi?
Konda: Usinizengue, km vipi ungekuja na siti yako.

Monday, December 12, 2011

Swali kwa padre

Kijana akimuuliza padre "fatha nauliza, hivi peponi kuna futball pia?"
Padre: Njoo kesho tafadhali ntakua nimepata jibu.
Siku ilofuata akaja.
Padre akajibu "...ndio kuna futball na una mechi ya kucheza alhamis hii"

Kwa wakili

Wakili: Inakuwaje unataka talaka kumpa mkeo mzuri kiasi hiki?
Mume: Ona kiatu changu kilivyo kizuri, lakini mvaaji pekee ndio anajua kiasi gani kinambana.

Nani kabla ya ndoa

Mwanaume: Nilikua Milionea kabla sijaoa.
Rafiki: Safi, sasa ivi si ndo mnahela zaidi?
Mwanaume: Hapana nilikua bilionea hapo awali.

Kwenye treni

Mkaguzi tiketi kwenye treni "vipi mzee mbona hofu? Usiogope mzee wangu hamna shida ya kukufanya uogope."
Mzee nae akajibu "ohh afadhali maana nimepanda na sijakata tiketi ya safari yangu."

Sunday, December 11, 2011

Kwenye daladala

Mlokole mmoja alipanda Daladala moja
ambayo ulikuwa inatwanga mziki Wa kidunia
kwa kwenda mbele,Mlokole: nyimbo gani mnapiga hizo, wekeni nyimbo
za Yesu"Kond a akamjibu... ..."Yesu bado
hajatoa albamu.... .."

Saturday, December 10, 2011

Dereva wa daladala

Dereva wa daladala alisimamisha basi akampisha bi.mkubwa mmoja kwenye kiti chake. Abiria wakauliza "dereva vipi nani ataendesha sasa?"
Dereva akajibu "mpaka mtu ajitolee mpisha bibi huyu ndio ntarudi kwenye kiti changu"

Kung'oa jino

Dokta meno: Ajabu kweli nimeng'oa meno matatu ya mbele hata damu haitoki!!
Mgonjwa: Aahh umeng'oa ya bandia sio yenyewe.

Kwa dokta

Dokta: Hizi dawa ili mumeo apate usingizi.
Mke: Ohh atakiwa ameze saa ngapi?
Dokta: Ni zako wewe ukameze sio yeye.

Wednesday, December 7, 2011

Kibweka kanisani

Jamaa mmoja alikua anampenda sana dada mmoja. Akamfuata mpaka kanisani, ilipofika wakati wa kutoa sadaka jamaa akamuwahi dada na kumuambia "ohh kuhusu sadaka acha tu ntakutolea"

Baada ya mtihani

Baada ya kutoka chumba cha mtihani, wanafunzi walikamatana na kudundana mingumi ya kutosha. Mwalimu alipowakuta na kuwauliza kwanini wanapigana, mmoja wao akajibu; 
"mwalimu mimi mtihani wa hesabu sijajibu kitu, nimeandika jina tu, sasa huyu b.w.e. g.e nazi naye kaniiga, hajajaza kitu, ameandika jina tu sasa si itaonekana mmoja wetu amekopi kwa mwenzie halafu tutafutiwa matokeo wote!"

Sunday, December 4, 2011

Kichaa kapewa rungu

Kijana alikua anafukuzwa na kichaa aliekua na rungu mkononi kwa umbali wa kilomita 1. Alipochoka akaamua kusimama. Kichaa alipomfikia akam-dalika kidali poo kisha akamuambia "kalale nacho"

Kibweka kitandani

mzee mmoja alikuwa amelala na mkewe,akawa
anajamba kwa sauti mbali mbali,mkewe ikabidi
amuulize kulikoni mume wangu? mzee
akajibu"Potezea bna,Natafuta ringtone ya
matako yangu!"

Friday, December 2, 2011

Somea mtihani

Madogo wawili wa shule ya msingi:
Dogo A: Mtihani keshokutwa sa tunafanyaje?
Dogo B: Kuchemsha daftari tu na kunywa maji.
Dogo A: Tatizo notice zangu nyingi tashindwa maliza hayo maji.

Msiba wa kipenzi

Mwanamke mmoja alifiwa na mumewe kipenzi, siku ya mazishi akaomba msaada mmoja akisema "naombeni mumzike na hii simu yake na chaja niwe nawasiliana nae." Kisha akakumbuka jambo "aahh umeme wa kuchajia hata kuwa nao."

Thursday, December 1, 2011

Mtoto wa nani?

Mtoto alizaliwa na tangu azaliwe hakuwahi ongea. Kwa mara ya kwanza siku akataja "bibi" siku moja mbele bibi ake akafa.

Akataja tena baada ya miezi "babu" ikawa vilevile. Miezi tena akataja "baba" ndipo baba alipoanza andika urithi nk. Kilichofuata akafariki dereva wao.