Karibu Sana.
Cheka Unenepe
Monday, March 14, 2016
Ndoa knisani
Wakati dnoa inafungwa kanisani, mchungaji akauliza "kwa yeyote mwenye pingamizi na aje mbele..."
Ghafla kibabu kikasimama na kwenda mbele. Bi harusi akaanguka na akazimia. Mchungaji akamuuliza "haya babu tuambie pingamizi lako"
Babu akajibu "nimeamua kuja mbele, kule nyuma sisikii vizuri."
Mlevi kaibiwa...
Mlevi mmoja alipoingia kwenye gari yake ikabidi apige simu kama ifuatavyo;
Mlevi: Haloo, nimeibiwa usukani, dashboard, gia pia, na pedo za break"
Polisi: Tukio limetokea eneo gani?
Baada ya sekunde kadhaa mlevi akapiga simu tena polisi "Jamani msije tena kumbe niliingia mlango wa nyuma vyote vipo."
Wednesday, March 2, 2016
Picha ya mapacha
Mama mmoja alizaa mapacha, ugumu wa maisha watoto wake mmoja akaikabidhi familia moja wakamuita Kijo na mwingine familia ingine wakamuita Tulo.
Siku moja mama mzazi wa mapacha akatumiwa picha ya Kijo amekua kua, akamuambia mumewe "natamani wanitumie picha ya Tulo pia." Mume akamjibu "ni mapacha kumbuka, ukimuona mmoja ni umemuona mwingine."
Walevi wawili
Walevi wawili walikua wanabishana:
Mlevi 1: We umelewa, nakuambia ule ni mwezii unabisha.
Mlevi 2: Sio mwezi bwana, si nyota kabisa zile we huoni?
Akapita msamaria mmoja wakaona waulize "eti samahani, ule mweziii au nyota?"
Msamaria akawajibu: Ile ni tubelight imefungwa kwenye mti imefunikwa funikwa na majani.
Sahau matatizo
Jamaa mmoja alimuomba ushauri mwenzake juu ya matatizo yakiyomsonga, akamjibu kama ifuatavyo. "Namna rahisi ya kusahau matatizo yako (japo kwa muda mfupi) ni kuvaa viatu vinavyokubana."
Machizi wawili safarini
Kulikua na chizi watatu walipanda treni kuelekea Mbeya, maongezi yao kama ifuatavyo:
chizi wa kwanza: Unaona vile miti inavyokimbia?
Chizi wa pili akajibu: Eee! itabidi tupande miti tukirudi.
Chizi wa tatu: Nauli yake ipo juu nilipieni...
Mtoto kaunguza picha
Mtoto mmoja alikua kwenye daladala na mama ake. Maongezi ya mtoto yakawa hivi kwa sauti ya kusikika kwenye daladala nzima, "kwani mama tunenda wapi wakati hatujaoga?"
Sunday, January 4, 2015
Sauti toka kwenye simu: Halo, mama ako yupo nyumbani?
Msichana kakajibu: Ndio yupo
Sauti kwenye simu: Unaweza kumuita aje niongee nae tafadhani?
Msichana: Sawa, inabidi niende mtaa wa pili kumuita.
Sauti kwenye simu: Nilidhani umesema yupo nyumbani lakini?
Msichana: Ndio yupo. Hii simu ni nyumbani kwa rafiki yangu, sie tunaishi mtaa wa pili.
Wednesday, July 10, 2013
Swali kwa wanafunzi
Mwalimu akiwa darasani akauliza swali: Haya naomba mniambie, utamuitaje mtu ambae anaongea na mtu au watu wakati huo huo wanaomsikiliza hawana mvuto wa kusikiliza akiyoyasema?
Mwanafunzi mmoja akanyoosha kidole na kujibu: Jibu ni Mwalimu.
Ma-lavi-davi
Msichana: Nakupenda sana na nitakufa kwa ajili yako.
Mvulana akajibu: Lini haswa utakufa sasa?
Jibu la mpenzi
Mvulana na msichana wapenzi wakiwa matembezini
Mvulana: Naweza kukushika mkono wako?
Msichana: Hapana usijali, sio mzito.
Swali kwa chekechea
Mwalimu aliuliza swali kwa wanafunzi wa chekechea kama ifuatavyo:
Mwalimu: Haya mninjibu swali hili, kati ya Jua na Mwezi kipi muhimu?
Mtoto mmoja akanyoosha kidole na kujibu.
Mtoto: Bora mwezi
Mwalimu: Kwa nini umechagua mwezi?
Mtoto: Kwa sababu mwezi unatupa mwanga usiku wakati tuna uhitaji, lakini jua linatupatia mwanga mchana wakati hata hatuuhitaji.
Thursday, November 8, 2012
Mgeni huyu...
Wageni wengine noma...........!!!!!!!!
MWENYEJI: "Utakunywa soda au chai?"
MGENI: "Ntakunywa soda wakati nasubri chai ichemke!....."
Tuesday, October 9, 2012
Kambi ya jeshi
Jamaa alikatiza kambi ya jeshi. Akapewa adhabu ya kubeba tofali 1,000. Alipofikisha 900 akakumbuka mkuu wa kambi kasima nae, akaenda msemea aliempa adhabu: mkuu akanena "umeshabeba mangapi hadi sasa?" Jamaa akajibu "900" mkuu akanena "basi yarudishe halafu uendelee na safari yako."
Taxi na ofa
Jamaa kwenye taxi alimuona mke wake anaingia hotel na njemba akamuambia taxi driver "unataka tengeneza laki 2 sasa ivi?"
Akajibu "ndio" akapewa kazi akamchukue mke wa jamaa amlete. Akarudi na mwanamke sie jamaa akanena "huyu sio mke wangu" taxi driver akanena "najua! Huyu ni mke wangu mshikilie namfuata wako sasa."
Subscribe to:
Posts (Atom)