Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, September 7, 2010

Mama na mtoto

Mtoto: Mama kwani dada wa kazi hajakua tu?
Mama: Kwa nini mwanangu?
Mtoto: Ananyonya mpaka leo!
Mama: Mhh! Mwanaaangu...
Mtoto: Kweli mama, mi nlimuona kapiga magoti huku baba anamnyonyesha.

Headphones II

Jamaa alifika duka la vyombo vya mziki akaona headphones, akaulizia kazi yake akajibiwa. Kisha akauliza "inachukua mda gani mziki kufika masikioni?"

Headphones

Jamaa alinunua discman kwa mara ya kwanza, sasa wakati ameweka headphones masikioni akisikiliza mziki, rafiki yake akawa anaushika waya wa headphones huku akisema "hee! Huu waya wake mzuri"

Jamaa mwenye discman akamuambia kwa ukali "wee usiushike utazuia mziki usifike masikioni"

Gazeti

Mtoto katumwa gazeti la tarehe 10. Alipokosa na kurudi... "baba nimekosa gazeti la tarehe 10. Nimenunua ya tarehe 5 mawili"

Kikaoni

Mtendaji mmoja kwenye kikao alimuuliza mwenzake.
Mtendaji: Ndugu yangu mbona hatuonani?
Mtendaji ii akajibu "samahani mkuu, hatuonani wapi?"

Monday, September 6, 2010

Jirani mpya

"mama nikuambie yule dada jirani yetu anaitwa nani?" mtoto akimuuliza mama yake.
Mama akauliza, "we umejuaje mwanangu?"
Mtoto: Si baba alimuita nkasikia.
Mama: Enhe alimuitaje?
Mtoto: Si Honey! Tena ukiondokaga baaba muoogaa peke yake basi anaendaga kulala kwa huyo dada.

Watoto je?

Jamaa mmoja akiongea na rafiki yake "mke wangu hapendagi kabisa nimguse miaka yote tangu tumeoana."
Rafiki yake akanena "sasa hao watoto mmewapataje?"

Don't drink & Drive

Jamaa mmoja alirudi kwake, mkewe akamuuliza "vipi mume wangu mbona... Kwa miguu?"
Mume akajibu "nimekuta kibao kimeandikwa don't drink and drive ivo nlipokunywa tu maji nkaiacha pale pale gari"

Njoo nje

Katoto kamoja ka-kiume kalirudi ndani mbio mbio huku kakimuambia mama yake "mama mama njoo haraka haraka umuone mama frank kasimama pale nje sketi yake inapeperuka na upepo... njoo umuone kavaa ya blue kama yako"

Watoto wa mtaani

Bibi mmoja kasikika akilalama, ''kila siku wanasema watoto wa mitaani wanaongezeka! Si wamfundishe huyo mitaani uzazi wa mpango?"

Sunday, September 5, 2010

Thermos

Jamaa aliona kifaa dukani, akauliza "hii nini?"
akajibiwa "hii ni thermos, kazi yake kufanya cha moto kubaki moto na baridi kuwa baridi."

Siku yupo kazini boss akamuuliza nae akamjibu kama alivyojibiwa.
Boss akauliza tena, "sasa umeweka nini ndani?"
Jamaa akajibu, "chai na maji ya baridi ya kunywa baadae."

Kuchelewa

Jamaa aliamka haraka haraka akiwa amechelewa. Mbio mbio akiwahi anapoenda.
Baada ya mda akarudi.
Mama: Vipi mbona umerudi?
Jamaa: Nimechelewa mekuta mlango washafunga kanisani.
Mama: We umeenda kanisa gani?
Jamaa: Hapo konani karibu na...
Mama: Khaa! Pale msikitini jamani kanisa lipo kwa mbele zaidi.

Mwanga wa tochi

Kaka mmoja na mchumba wake walienda tembea kwenye garden. Kaka akavuka daraja la mbao, alipomaliza likavunjika.

Mchumba wake akasema, "ntavukaje sasa?"
Kaka akajibu, "subiri giza liingie, ntawasha tochi kisha utavuka kupitia juu ya mwanga wa tochi."
Mchumba: "Haa! Hapana nkifika katikati ya mto we utazima tochi halafu ntaanguka."

Punguza uzito

Dokta alimshauri jamaa akimbie kwa siku 30 ili apungue uzito.
Siku 30 baadae jamaa kwenye simu, "dokta asante sana nimepungua, ila sasa ntarudije nipo mile 300 toka nyumbani?"

Punguza uzito

Dokta alimshauri jamaa akimbie kwa siku 30 ili apungue uzito.
Siku 30 baadae jamaa kwenye simu, "dokta asante sana nimepungua, ila sasa ntarudije nipo mile 300 toka nyumbani?"

Hii nini?

Mtoto alimuliza mamake.
Mtoto: Hiki nini?
Mama: Mapulizo (matiti)
Mtoto: Nilimuona baba jikoni akiyapuliza ya dada mfanyakazi

Kanisani

Jamaa alikutana na wenzake wanatoka kanisani akawauliza, "leo sijaja kanisani, vipi wameita majina?"

Mtekanyara

Jamaa mmoja alimteka mtoto wa tajiri akaandika barua "nimemteka mwanenu, nataka dola elfu5. Nimemruhusu mara 1 tu aje achukue nguo za kuvaa kesho."

Mtekanyara

Jamaa mmoja alimteka mtoto wa tajiri akaandika barua "nimemteka mwanenu, nataka dola elfu5. Nimemruhusu mara 1 tu aje achukue nguo za kuvaa kesho."

Soda | 500

Mmasai kaenda dukani kauliza "soda bei gani?" Kaambiwa "mia 5."
Katoa kibuyu, "weka ya mia nampa mtoto."

Ibada

Jamaa alikua anaangalia ibada kwenye tv sebuleni. Punde akajibu sms iliyoingia "siwezi chat now padre ataniona"

Makaburini

Dogo mmoja na wenzake wawili walipita njia moja karibu na makaburi. Sasa wakawa wanaona wengine wamekufa na umri mkubwa mfano 95, 101 nk nk.
Aliporudi nyumbani akamuambia mama yake, "mama mi nikifa niandikeni nimeishi miaka 200"

Mama kwa mshangao akauliza, "hee! We mtoto nani uliwahi msikia...?"
Mtoto: We niandikieni ivo ivo?
Mama: Kwa nini wasema hivyo mwanangu?
Mtoto: Nataka niwashinde wote waliokufa.

Makunyanzi

Mtoto mmoja alimuona bibi yake walioenda kijijini. Baada ya kuona ngozi ya bibi yake ina makunyanzi ya uzee sana akamnong'oneza mama yake, "mama... kwani bibi si aipige pasi tu ngozi yake imejikunja sana!?"

Mnyama gani?

Siku moja mama mmoja alienda mbuga za wanyama na mwanae mdogo wa miaka miwili. Wakati wakiangalia wanyama yule mtoto akaona tembo akamuulima mama yake "mama huyu mnyama gani? Mbona ana mkia mbele na nyuma?"

Friday, September 3, 2010

Msiba

Dada mmoja alipata taharifa kafiwa na mama yake. Boss akamuambia aende tu nyumbani. Dada akasihi aendelee wepo eneo la kazi.

Baadae boss akaenda muangalia akakuta analia akamuuliza "vipi tena kulikoni?"
Dada akajibu "dada yangu anaenifuata amenipigia na yeye amefiwa na mama yake."

Kuchelewa rudi

Jamaa alinunua gari akaenda chalinze. Wakati anarudi mkewe akamuuliza "mbona umechelewa rudi?"
Mume "hii gari wameeka gia 4 kwenda mbele tu, kurudi nyuma eti 1 tu"
(alirudi kinyume nyume)

Mapacha

Mwanaume mmoja alienda hospitali, akakuta mkewe kajifungua mapacha akamuliza mkewe "huyu mtoto mwingine wa nani?"

Risasi

Mama mjamzito wa mapacha watatu alienda supermarket akapigwa risasi 3 tumboni.
Alipoenda kwa daktari akaambiwa "...usiwe na wasi wasi risasi zitatoka zenyewe"

Baada ya miaka 16 wale mapacha baada ya kuzaliwa siku moja ikawa hivi.
Wa kwanza: Mama.. Mama.. Nilienda chooni risasi ikatoka.
Wa pili nae siku moja akamuambia hivyo hivyo.

Wa tatu kabla hajasema mama akadakia "enh na wewe risasi imetoka?"
Mwanae akajibu "ndio imetoka wakati na... Ikampata baba kaanguka"

Thursday, September 2, 2010

Kutabiri mbele

Mwalimu aliuliza darasani, "inawezekana kutabiri jambo la mbele?"
Mtoto mmoja akajibu, "ndio! Mama huwa akiangalia daftari langu la hesabu huniambia, subiri baba yako arudi uone."

Wednesday, September 1, 2010

Makumbusho

Jamaa mmoja akipiga simu ofisi ya Makumbusho ya Taifa: "Haloo, hapo ni Makumbusho ya Taifa?"
OFISI: "Ndio, tukusaidie nini?"
JAMAA: "Ok, naomba mnikumbushe mwaka juzi saa yangu niliipoteza wapi?"
OFISI: "Pumbavu! Hiyo sio kazi yetu..!"
JAMAA: "Sasa makumbusho mnakumbusha nini?" OFISI: "Tunahifadhi mambo ya zamani." JAMAA: "Ahaa... kumbe saa yangu mtakuwa nayo..!"