Karibu Sana.
Cheka Unenepe
Thursday, June 9, 2011
Mtoto mdadisi
Mtoto mmoja akimsimulia mama yake, "mama mtafutie baba kopo ka kutemea mate" Mama akiuliza kwa mshangao "koopo?" Mtoto akajibu "ndio mama maana kila ukisafiri. lazima atatema tu mate kwenye maputo kati ya mawili au matatu nayakutaga chini ya uvungu"
Msaada wa mmaasai
Mmaasai alikua akimuangalia driver wa bus akicheza na gear wkt wote wa safari. Abiria na dreva waliporudi toka lunch katikati ya safari wakakuta mmaasai kaichomoa gear yote kuulizwa na driver akajibu "mekusaidia kuing'oa meona saa nyingi we naangaika kuitoa"
Wagonjwa wa akili
Wagonjwa wa akili wawili walisimamishwa ghorofani kisha wakaambiwa wakojoe kuelekea chini.
Wa kwanza akasema "dokta parefu bwana mkojo wangu utaumia"
Wa pili akasema "naogopa wataudaka wapita njia na kunivuta chini bure nikafa"
Wa kwanza akasema "dokta parefu bwana mkojo wangu utaumia"
Wa pili akasema "naogopa wataudaka wapita njia na kunivuta chini bure nikafa"
Mlevi wodini
Mlevi mmoja alishikwa na homa kali ghafla, akapelekwa hospitali. Alipofikishwa wodini ili apewe mapumziko akakutana na walevi wenzake wanne nao wamelazwa jamaa akafurahi sana na kumuambia nesi aliyewepo zamu muda huo "nesi zungusha round ya tatu bill kwangu"
Mbu
Mbu mmoja alimkuta mwenzake amekaa kwa masikitiko akamuuliza mwenzake "vipi mbona huingii mzigoni leo?"
Mbu mwenzake akamjibu "dah nasikitika sana, nilijua leo nimepata mzungu kumbe mdoli bwana na sindano yangu imevinjikia"
Mbu mwenzake akamjibu "dah nasikitika sana, nilijua leo nimepata mzungu kumbe mdoli bwana na sindano yangu imevinjikia"
Wednesday, June 8, 2011
Mume na mkewe
MUME: Vipi mpenzi leo umekula nini maana sikuacha hela ya mlo.
MKE: Tumeshindia mapera na shemeji yangu mpenzi, mimi ndio nilipanda juu ya mti.
MUME: Inamana shemeji yako alibaki chini ya mti.
MKE: Ndiyo.
MUME: Alitaka kuangalia chupi yako mi namjua mdogo wangu.
MKE: Unafikiri mi mjinga nilimshtukia nikaivua nikapanda uchi

Ka-herufi kamooja tu...
Jamaa mmoja ilimtokea hii, alisahau kuweka herufi moja tu "e" mwishoni mwa sentensi wakati akimomuarifu mke wake kwa sms akiwa safarini kikazi. Aliandika sms kwa mkewe kama ifuatavyo "I am having such a wonderful time! I wish you were her..."
Jamaa aliopoa....
Jamaa mmoja aliopoa na mabo yalikua hivi:
Msichana: Naomba nikuambie ukweli, mimi ni malaya najiuza usiku ili nipate hela.
Jamaa akanena na yeye: Usijali nitakupatia 15,000Tsh tukimaliza...
Baada ya kumaliza hali ikawa hivi:
Jamaa: Naomba nikuambie ukweli, mimi ni dereva taxi na nitakuchaji 15,000Tsh kukurudisha nilipokutoa.

Teja
Teja mmoja alikuwa anavuta bangi, ghafla akasikia sauti ya ajabu akauliza "nani wewe?" Akajibiwa "ni mimi israel mtoa roho" Teja nalo likajibu "Dah... umenistua kweli mi nilijua polisi"
Chumba cha upasuaji
Ndani ya chumba cha upasuaji wakati mgonjwa keshapasuliwa eneo husika dokta akamuambia nesi mmoja wapo kati ya waliopo ndani ya chumba cha upasuaji "Nesi nenda kwenye internet fungua surgery.com halafu peleka mpaka chini ukanisome sehemu imeandikwa "are you totally lost?"
Daktari na Mgonjwa
Mgonjwa mmoja alienda kumuona daktari wake na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Mgonjwa: Dokta mbona sipati nafuu?
Dokta: Ulifuata masharti ya dawa niliyokupatia?
Mgonjwa: Ndio, kwenye chupa yanasema "hakikisha chupa ya dawa umeifunga vizuri"
(Akimaanisha hajainywa kabisa).
Mgonjwa: Dokta mbona sipati nafuu?
Dokta: Ulifuata masharti ya dawa niliyokupatia?
Mgonjwa: Ndio, kwenye chupa yanasema "hakikisha chupa ya dawa umeifunga vizuri"
(Akimaanisha hajainywa kabisa).
Tuesday, June 7, 2011
Mende na binadamu
Mende mmoja alimuambia jamaa mmoja kabla hajamuua ''kabla hujaniua mie ndio nineweza mpigisha kelele mchumba ako kuliko wewe''
Mke na Mume
Mke alimuambia mumewe, ''niambie jambo moja litalonifurahisha na kuniudhi kwa wakati mmoja''
Mume naye kama utani akanena ''we ni mtamu zaidi kuliko wadogo zako wa kike''
Mume naye kama utani akanena ''we ni mtamu zaidi kuliko wadogo zako wa kike''
Wagonjwa wa akili
Wagonjwa wa akili walipanga kutoroka hospitali.
Walipanga wamvamie mlinzi wampige watoroke.
Walipofika mlangoni wakakuta mlango wazi na mlinzi hayupo. Wakanena ''dah mpango wetu wa kutoroka ushafeli'' basi waka wakaghairi.
Walipanga wamvamie mlinzi wampige watoroke.
Walipofika mlangoni wakakuta mlango wazi na mlinzi hayupo. Wakanena ''dah mpango wetu wa kutoroka ushafeli'' basi waka wakaghairi.
Password
Jamaa mmoja na mchumba wake walienda mtembelea rafiki yao. Ilipofika wakati wa kulala wakamuomba watumie simu ya mezani kupiga mwenyeji akawajibu ''ooh ina password''
Walipouliza kuhusu computer labda watume email wakajibiwa pia ina password. Mwenyeji akawauliza kama wataoga muda huo au la! Mgeni akanena ''hamna password bafuni?''
Walipouliza kuhusu computer labda watume email wakajibiwa pia ina password. Mwenyeji akawauliza kama wataoga muda huo au la! Mgeni akanena ''hamna password bafuni?''
Mchaga mpirani
Mchaga mmoja mmoja kwa jina Masawe alikua anacheza nafasi ya goli kipa... Sasa wakati timu pinzani inakuja kushambulia Masawe si akamuona mtu anae mdai akaacha kuokoa goli lisiingie akakimbilia kumdai...
Bikini
Mtoto mmoja alimuona dada mmoja baharini amevaa vile vichupi nyenye asilima kubwa mfumo wa kamba ndipo mtoto akasema/akamuambia yule dada "dada makalio yako yanaitafuna chupi yako imeliwa yote nyuma"
Sunday, June 5, 2011
Nyonyo
Mama mmoja kwenye daladala mtoto wake wakati anakataa kunyonya akawa anamtishi mwanae akimuambia ''nyonya au sivyo ntampa huy baba pembeni'' mtoto ndio ananyonya.
Iliendelea hivyo kwa mara 3 ndipo yule baba nae akanena ''we mama make up your mind ilikua nishuke kituo cha pili kilichopita''
Iliendelea hivyo kwa mara 3 ndipo yule baba nae akanena ''we mama make up your mind ilikua nishuke kituo cha pili kilichopita''
Saturday, June 4, 2011
Jela
Wafungwa watatu walipokutana jela hivi ndivyo kila mmoja alivyokua akimsimulia mwenzake:
Mfungwa wa kwanza: Nimefungwa kwa sababu niliua watu wanne.
Mfungwa wa pili: Nimefungwa kwa sababu niliiba bank.
Mfungwa wa tatu: Nimefungwa kwa sababu niliiba ghorofa. (ili aonekane na yeye sio wa kuja)

Kuchelewa shule
Mtoto akimjibu mwalimu "Mwalimu nimechelewa kwa sababu baba na mama walikua wanapigana, mama alikua anatumia kiatu changu kumpigia baba nilikua nasubiri wamalize nikivae nije."
Thursday, June 2, 2011
Mwalimu na mtoto
Mwalimu akimuuliza mtoto ''wewe jana ulisema mama yako anaumwa?''
Mtoto akajibu ''nilikosea kumbe alikua anaumwa mlinzi''
Mtoto akajibu ''nilikosea kumbe alikua anaumwa mlinzi''
Babu na mjukuu
Babu akimuambia mjukuu wake ''jifiche mwalimu wako anakuja umetoroka shule leo''
Mjukuu nae akajibu, ''weewe ndio ujifiche nimemdanganya umekufa''
Mjukuu nae akajibu, ''weewe ndio ujifiche nimemdanganya umekufa''
Wednesday, June 1, 2011
Parashuti
Ndege moja ndogo ilibeba watu wanne, punde rubani akatangaza "nasikitika ndege muda wowote inaanguka na tuna pashuti 3 tu sie tupo wanne". Jamaa mmoja mwalimu akawahi moja na kuruka nje ya ndege.
Wa pili kabla hajaruka akamuambia mtoto mmoja kati ya abiria, "chukua na wewe parashuti kabla rubani jakauwahi" ndipo yule mtoto akajibu "usijali wote tutapona, yule alieruka wa kwanza kachukua begi langu la mgongoni kasahau parashuti"

Pombe chakari
levi mmoja alipanda daladala usiku akielekea kwake, kwenye basi akakutana na mwanamke mcha mungu akamuambia yule mlevi "unaenda moja kwa moja motoni"
Yule mlevi akamuamrisha dereva "dereva simama nimepanda daladala sio..."
Yule mlevi akamuamrisha dereva "dereva simama nimepanda daladala sio..."
Thursday, May 26, 2011
Kila kitu Kipya
Jamaa kaoa mke kutoka kijijini,baada ya harusi kafungua nyumba yake mpya,kazindua gari lake jipya na wakati wa kumuingia bwana kavaa condom, yule mke akatuma sms kwao kwamba mume ana kila kitu kipya mpaka ile kitu bado mpya iko ndani ya plastiki haijafunguliwa!!
Mmasai kwa fundi
M-masai alipeleka radio kutengeneza fundi alipoifunguwa wakatoka mende wengi masai alipowaona akamwambia fundi
"kamata watangasaji wanatoroka!!"
"kamata watangasaji wanatoroka!!"
Monday, May 23, 2011
Padre akiomba mchango
Padre mmoja aliwaomba waumini wake mchango kuzungushia ukuta eneo la makaburi. Mlevi mmoja akauliza papo hapo, ''kuna marehemu aliyewahi kutoroka?''
Saturday, May 21, 2011
Ngozi Bibi kizee
Bibi kizee mmoha alienda kuogelea kwenye bwawa maalumu la kuogelea. Alikutana na watoto wadogo na wakiogoelea.
Sasa alipozamia wakati anaibuka akawa anaelea mgongo ukiwa wa kwanza kuonekana, wale watoto walipomuona wanamuita mama yao ''mama... mama... Njoo uone kuna mamba humu kaingia...''
Sasa alipozamia wakati anaibuka akawa anaelea mgongo ukiwa wa kwanza kuonekana, wale watoto walipomuona wanamuita mama yao ''mama... mama... Njoo uone kuna mamba humu kaingia...''
Thursday, May 19, 2011
Uaminifu
Mume: Mke wangu niambie ukweli hivi ushavunja uaminifu mara ngapi?
Mke: Siku moja nililala na mwenye nyumba sababu alikua anatudai kodi.
Mume: Si mbaya sana.
Mke: Mara ya pili, ulipofanyiwa operation hatukuwa na pesa ikabidi nilale na daktari.
Mume: Kweli unanijali mke wangu.
Mke: Mara ya tatu ni kile kipindi cha uchaguzi ulipokuwa unaomba kura za ubunge ikabidi nitembee na wapiga kura wako wote ili upite ndio maana ukashinda.

Yebo yebo
Mtoto mmoja alikua analia kapoteza yeboyebo zake, mtumishi wa Mungu akamkuta akilia akamuuliza.
Mtumishi: Unalia nini mtoto mzuri?
Mtoto: Natafuta yebo yebo zangu zimepotea.
Mtumishi: Basi usilie mwachie Mungu tu.
Mtoto: Mungu hazimtoshi zilikuwa ndogo sana.
Mtumishi: Unalia nini mtoto mzuri?
Mtoto: Natafuta yebo yebo zangu zimepotea.
Mtumishi: Basi usilie mwachie Mungu tu.
Mtoto: Mungu hazimtoshi zilikuwa ndogo sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)