Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, June 14, 2011

Hii ya siku mingi

Wodi ya vichaa walichorewa kuku ukutani, wakaambiwa wamkamate! Woote wakaenda kasoro mmoja tu.
Wakamuuliza we vipi mbona hendi mkamata akajibu "shhhh nataga"

Adhabu

Mwanafunzi: Mwalimu unaweza niadhibu kwa kitu ambacho sijafanya?
Mwalimu: Hapana kabisa.
Mwanafunzi: Ohh! Basi sijafanya homework bado.

Kufiwa

Mwanaume mmoja aliefiwa na mke siku moja mbele mvua kuubwa ikanyesha sana. Basi alipoiona ile mvua akanena "Itakua ameshafika mbinguni"

Bifu la majirani

Jirani 1 akimuuliza jirani wa pili "huyu mbwa wako ananikera sana, anamfuata mbwa wangu kila kukicha"
Jirani wa pili akajibu "we shida yako nini, mie nampaga condom kila siku kabla hajamfuata mbwa wako"

Tangazo tata

Mwanaume mmoja alikua anamtafuta mke wake asijue yupo wapi?
Akakutana na jirani yake na kumuambia "nimemuona mkeo kaja chukuliwa na boss wako" jamaa mwenye mke akajibu "ooh basi nsije katwa mshahara bure atarudi baadae"

Denti wa kiinglish

Mwanafunzi mmoja aliekua akijifunza lugha ya kiingereza kama lugha ngeni, sasa akawa amemkuta mwalimu wake wa kiingereza kasimama kwenye kinjia alichotaka kupita, kuonyesha kama ameanza ku-masta kimombo akenena ili apishwe "excuse me can I pass away?"

Bomu

Vijana wawili waliokota mabomu mawili, wakashauriana wayabebe kuyapeleka ama kuyarudisha jeshini. Mmoja akauliza "je moja likilipuka?"
Mwenzake akajibu "tutadanganya tumeokota moja tu"

Ngumii

Katoto kamoja kalimkimbilia polisi na kunena:
Mtoto: Askari kuna watu wanapigana palee...
Askari: Baba yako nani?
Mtoto: Ndio wanapigania hicho hicho.

Trafik polisi

Jamaa wawili walipanda pikipiki mbele kidogo wakaona trafik akionyesha ishara ya kuwasimamisha. Jamaa aliepakiwa kwenye pikipiki akamuambia dereva "sasa sie tushajaa ye anataka kukaa wapi au labda hatujafunga mkanda?"

Monday, June 13, 2011

5 + 5 = ?

Mwalimu aliuliza 5+5 jibu ni ngapi?
Alikataza kuhesabu vidole, basi dogo mmoja wa kiume akaingiza vidole ndani ya pensi ili ahesabu kimya kimya mwisho wa siku akaibuka na jibu "mwalimu jibu ni 11"

Meseji...

Jamaa mmoja alituma meseji kwa rafiki zake kama ifuatavyo:
"Wishing you happy independence day.
Oh sorry, this massage is only for singles..
Married people, please ignore it.."

Nani chizi?

Jamaa mmoja alikua yupo bar na palikua na kelele kweli, akanyakua simu yake ya kiganjani na kumpigia rafiki yake fulani aliyekua yupo tu nyumbani. Maongezi ya jamaa yalikua hivi:

Aliepo Bar: Haloo! Haloo! Sikusikii vizuri sijui upo kwenye makelele sogea palipo na utulivu.
Aliepo nyumbani akajibu: Mimi au wewe ndio yupo penye kelele?

Ugonjwa wa kusahau

Mgonjwa: Dokta nna ugonjwa wa kusahau.
Dokta: Limekuanza lini hilo tatizo?
Mgonjwa: Tatizo gani?

Siendi shule

Mtoto: Mama mi kesho siendi shule bwana.
Mama: Kwa nini mwanangu?
Mtoto: Mwalimu mwenyewe hajui kitu juzi katufundisha 9-4=
5, Na jana tena katufundisha 6-1=5...

Mke akinena...

Mke: Nataka nikuambie kitu ila usininase kibao.
Mume: Sema tu uwe na amani.
Mke: Nina ujauzito.
Mume: Sasa ulikua unaogopa nini?
Mke: Nilisemaga kabla hujanioa kwa baba akaninasa kibao.

Zama za ukoloni

Mwalilimu aliuliza swali darasani "tulitawaliwa toka wapi hadi wapi na wakoloni?" Mwanafunzi mmoja akajibu "enhe sina uhakika sana ila nnadhani ukurasa wa 60 mpaka wa 65"

Plani za ndoa

Msichana: Darling wangu tuki-oana nataka kushea nawe shida na matatizo yote na wewe.
Mvulana: Oh! Sawa lakina mimi sina shida wala matatizo yoyote ya kushea na wewe.
Msichana: Kwasababu hatujaona bado...

Nyumba ya watatu

Mke: Mume wangu ile nyuma tuliyopata tutaishi watatu badala ya wawili. Mume akajibu "ooh imekua baraka enhe safi sana"
Mke akamalizia "nakushukuru sana kwa kukubali, kuanzia kesho mama yangu ataishi nasi"

Tajiri wa wake

Tajiri mmoja alikuwa na wake wengi. Kudhibiti wafanyakazi wake akawawekea tego kwa wakeze ili mwanaume akitembea na mkewe naniliu inaliwa.

Aliporudi safari akafanya ukaguzi kwa wafanyakazi wake akiwafunua, kila aliyemfunua imeliwa. Wa mwisho akamkuta ipo safi basi akamsifu na kumwambia yeye ndie wa kuigwa.

Akamuuliza jina yule kijana akanyamaza na kujifanya kuongea kama bubu. Kumfungua mdomo kumbe ulimi umeliwa!

Sapraizi

Dokta akiaonge na mteja wake:
Dokta: Dah hongera umekua baba sasa.
Mteja: Tafadhali usimuambie mtu nataka kum-surprise mke wangu!

Ndoto ya panya

Dada: Baba tangu juzi naota panya anacheza tebo tenesi.
Baba: Usiogope ni kawaida tu.
Dada: Je nifanyeje nimeze dawa au?
Baba: Ya nini wakati leo ndio Fainali.

Darasa kuhama

Mwalimu: Haya wanafunzi kesho darasa litaenda kwenye juani..
Mwanafunzi mmoja akaonge: Mwalimu mi sitakuja.
Mwalimu akauliza "kwa nini?"
Mwanafunzi: Mama yangu hawezi niruhusu kwenda mbali kote huko.

Kaazi kweli kweli

Jamaa alipokua kwa daktari wa meno:
Mgonjwa: Dokta fasta nikatoe viatu vyoote sebuleni rafiki yangu anakuja leo home.
Dokta: Kwanini? Rafiki yako ni mwizi?
Mgonjwa: Hapana asije akavitambua viatu vyake.

Inzi kwenye supu

Mteja mmoja alimuita mhudumu ande alipo kwenye meza aliokaa!
Mteja: Hii supu uliyoileta kuna inzi amefia humu.
Weita: Yaah hawa hawajui kuogelea usijali

Kula kucha

Jamaa: Dokta mie nashindwa kuacha kula kucha je nifanyeje?
Dokta: Njoo nikusaidie, ning'oe meno yako yote itasaidia sana.

Kwenda Outing

Mume na mke walienda hotelini, punde mwanamke mmoja akamsalimia mume. Mke aka-mind na kuuliza "nani yule?"
Mume akamjibu: Tafadhali usini-disturb yule nae ataniuliza swali hilo hilo."

Watu wawili baa

Maongezi ya watu wawili wanaume:
Jimmy: "Umesema una mtoto wa kiume sio?
Hussein: Ndio.
Jimmy: Anavuta sigara?
Hussein: Hapana.
Jimmy: Anakunywa pombe?
Hussein: Hapana.
Jimmy: Anarudi usiku?
Hussein: hapana
Jimmy: Basi mwanao mtulivu sana, ana umri gani sasa?
Hussein: Ametimiza miezi sita sasa

6 x 7 = ?

Mwalimu: Haya nani anijibu 7x6 jibu ngapi?
Mwanafunzi: Jibu lake 42
Mwalimu: Haya je 6x7 jibu ni?
Mwanafunzi: jibu ni 24

Mhudumu na Mteja

Mteja kwenye restaurant moja akiongea na mhudumu "mhudumu, huyu kuku siwezi kumla niitie meneja wako"
Mhudumu nae akajibu "hata yeye akija hawezi kula huyo kuku"

Gazeti...

Mwanamke akimuuliza mumewe "kwa nini unaweka magazeti kwenye friji?" Mume akajibu: Yote yamejaa Hot News tuu.