Jamaa alimkuta jirani yake anachimba shimo:
Jamaa: Vipi mbona umechimba shimo kwema?
Jirani: Samaki wangu wa kufuga amekufa.
Jamaa: Pole, sa shimo lote hilo kasamaki kale tu?
Jirani: Kubwa kwa sababu yumo ndani ya tumbo la paka wako.
Karibu Sana.
Cheka Unenepe
Saturday, June 18, 2011
Gari mbele mara nyuma
Gari lilikua linaendeshwa, ghafla likawa linaenda mbele mara nyuma, mpaka mtu mmoja akamuita trafic.
Dereva wa gari akanena: Doh afathali trafic umekuja. Nimeona mti mbele nkaogopa kuugonga, mbele kidogo nkaona mti mwingine. Nkaogopa kuugonga!
Trafik akanena: Mama sio mti ni hiyo Air Freshner yako hapo umeiweka kwenye dash board.

Manesi na utani kwa dokta
Manesi watatu walipanga kumtania dokta wanaefanya nae kazi.
Baadae wakakutana kila mmoja kumpa mwenzake mrejesho kila mmoja kamfanyia utani gani dokta:
Wa kwanza: Mi nliweka pamba kwenye kipimo cha kusikilizia mapigo ya moyo ili asisikie.
Wa pili: Mie yangu ndio kali, nimetoboa tundu condom zake zote.
Nesi wa tatu akazimia.

Jambazi kuvamia kanisa
Jambazi alivamia kanisani na bunduki akasema-haya wanaosema wanampenda Yesu wabaki humu ndani, wasiompenda watoke nje. Waumini wote kwa kuogopa kifo wakatoka nje. Ndani akabaki mchungaji na wazee wawili tu-Jambaz akamgeukia mchungaji akasema "mtumishi unaweza kuendelea na ibada, nlitaka kukuondolea wanafiki."
Kumsaidia mke
Jamaa::: Nashindwa kumsaidia mke wangu anakaa macho hadi saa 11 alfajiri kila siku. Mwenzake akamuuliza "anakua anafanya nini?" Ndipo jamaa akajibu "ananisubiri mimi nirudi toka bar"
Fundi na spana...
Chizi mmoja alichukua spana na kwenda benk mlangoni akakutana na mlinzi, akamuliza "unakwenda wapi na hiyo spana?" akajibu "nakwenda kufungua akaunti"
Friday, June 17, 2011
Usalama uwanja wa ndege
Jamaa mmoja alikua akikokota kitoroli cha 'airport akiwa na mabegi yake huku akiwa amevaa chupi, na singland yake, ikimaanisha mkanda, suruali na shati pamoja na viatu kavishikilia.
Askari mmoja akamuuliza "vipi mbona unatembea nusu uchi?"
Ndipo jamaa akajibu "ntavaa baada ya security check zote hapa airport, kuepuka usumbufu wa vua vaa vua vaa"
Askari mmoja akamuuliza "vipi mbona unatembea nusu uchi?"
Ndipo jamaa akajibu "ntavaa baada ya security check zote hapa airport, kuepuka usumbufu wa vua vaa vua vaa"
Mifupa mingapi?
Daktari mmoja akimuelekeza jambo mtu chumba cha daktari.
Dokta: Unajua kwenye mwili wa binadamu kuna mifupa zaidi ya 500.
Jamaa: Dokta! Shhhhh! Taratibukuna mbwa wawili wapo na wazungu hapo mapokezi....
Dokta: Unajua kwenye mwili wa binadamu kuna mifupa zaidi ya 500.
Jamaa: Dokta! Shhhhh! Taratibukuna mbwa wawili wapo na wazungu hapo mapokezi....
Kukata roho
Mwanaume mmoja kabla hajakata roho akawa anamuambia mkewe "mke wangu nikuambie kweli kabla sijafa, nimetembea na wanawake wengi, nilikudanganya nitachelewa kurudi kumbe nilikua na wanawake....."
Mkewe nae akajibu "we unadhani kwa nini nimekuwekea sumu?"
Mkewe nae akajibu "we unadhani kwa nini nimekuwekea sumu?"
Malavi davi
Mwanaume mmoja akimuandikia mpenzi wake email walieachana miezi kadhaa kama ifuatavyo "mpenzi wangu nakubali kosa nlilolifanya, naomba turudiane, nitakupa raha ya moyo, mawazo hayaniishi juu yako mapenzi kwako hayana mfano. Nakupenda sana na Hongera kwa kushinda mchezo wa bingo milioni 100"
Matatizo kwa Dokta
Mgonjwa: Dokta nahitaji unisaidie, nna stress, hasira hovyo na watu hata sijielewi nna nini?
Dokta: Haya nielezee tatizo linalokusumbua.
Mgonjwa: Dokta we mzima? Si nshaelezea kila kitu?
Dokta: Haya nielezee tatizo linalokusumbua.
Mgonjwa: Dokta we mzima? Si nshaelezea kila kitu?
Mwanamke kwa dokta wa meno
Mwanamke mmoja kwa daktari wa meno wakati anang'oa jino yale maumivu ikabidi apeleka mkono wake kwenye korodani za daktari. Dokta akanena "mama samahani mkono wako umenishikilia ikulu" mwanamke nae akajibu "maumivu nnayoyapata hapa sasa tutaenda sawa"
Thursday, June 16, 2011
Nyoka
Mwalimu akiwaambia watoto kwenye darasa moja la english medium, "In this box, I have a 10-foot snake" bila kuchelewa katoto kamoja kakanyoosha mkono na kujibu "teacher, You can't fool me, Teacher... snakes don't have feet."
Huko jela...
Jamaa mmoja aliulizwa na mwenzake wakiwa jela:
Mfungwa: Imekuwaje umeletwa humu?
Mfungwa mgeni: Nilimpata farasi.
Mfungwa: Farasi ndio uletwe jela?
Mfungwa mgeni: Ndio, nilimpata kabla mmiliki hajampoteza!
Mfungwa: Imekuwaje umeletwa humu?
Mfungwa mgeni: Nilimpata farasi.
Mfungwa: Farasi ndio uletwe jela?
Mfungwa mgeni: Ndio, nilimpata kabla mmiliki hajampoteza!
He he he...
Kijana mmoja akimsimulia mwenzake jambo: "nilipokua mdogo nilikua nikisali nipate baiskeli, baadae nkaja gundua Mungu hajaniwezesha kupata. Hivyo basi nikaiba baiskeli na kusali ili nisamehewe"
Dawa ya kichwa
Mama mmoja mwanae alimuambia kua kichwa chamuuma sana hali ikawa hivi:
Mama: Mwanangu pole, kunywa dawa hii kitapoa tu.
Mtoto: Asante mama, dawa gani hiyo?
Mama: Hii panadol itakusaidia.
Mtoto: Itanisaidiaje wakati nikimeza inaeda tumboni badala ya kichwani sasa?
Mama: Mwanangu pole, kunywa dawa hii kitapoa tu.
Mtoto: Asante mama, dawa gani hiyo?
Mama: Hii panadol itakusaidia.
Mtoto: Itanisaidiaje wakati nikimeza inaeda tumboni badala ya kichwani sasa?
Mlevi kubatizwa
Mlevi mmoja alikua akipita eneo akaona watu wanabatizwa mtoni, akaenda mpaka eneo husika mchungaji akamuita ili ambatize. Akazamishwa mara moja na kutolewa:
Mchungaji: Kaka umemuona Yesu?
Mlevi: Bado.
Akazamishwa tena mara ya pili jibu likawa lile lile, mara ya tatu akaulizwa.
Mchungaji: Umemuona Yesu sasa?
Mlevi: Hapana, una uhakika kweli kaingia humu?
Mchungaji: Kaka umemuona Yesu?
Mlevi: Bado.
Akazamishwa tena mara ya pili jibu likawa lile lile, mara ya tatu akaulizwa.
Mchungaji: Umemuona Yesu sasa?
Mlevi: Hapana, una uhakika kweli kaingia humu?
Wednesday, June 15, 2011
Kisiwa
Mwalimu aliuliza darasani "nani anaweza kuniambia kisiwa ni nini?"
Mwanafunzi mmoja akajitolea kujibu "kisiwa ni ardhi iliyozungukwa na maji pande zote kasoro moja tu"
Mwalimu akauliza "pande moja? ipi?"
Mwanafunzi akajibu "upande wa juu tu"
Mwanafunzi mmoja akajitolea kujibu "kisiwa ni ardhi iliyozungukwa na maji pande zote kasoro moja tu"
Mwalimu akauliza "pande moja? ipi?"
Mwanafunzi akajibu "upande wa juu tu"
Siku ya kwanza shule
Mama: Umeionaje siku yako ya kwanza shuleni leo?
Mtoto: Ina maana na kesho naenda tena?
Mtoto: Ina maana na kesho naenda tena?
Vijiti (toothpick)
Jamaa mmoja mgeni mjini alitengewa chakula ugenini (uzunguni), meza ilipendeza msosi.
Baada ya kumaliza kula mwenyeji wake akamuuliza "kuna vijiti (toothpick) viliwepo hapa viko wapi?"
Jamaa akauliza "vile kwenye kichupa cha plastic?"
Mwenyeji akajibu "ndio ivo ivo"
Jamaa akajibu "mi nilijua vinaliwa na vyenyewe nimekula vyote"

Fluu
Askari mmoja alipiga chafya tatu mfululizo, boss mwenye nyumba anayolinda akamuambia "aisee taratibu usije wapatia vim-mbwa vyangu mafua"
Biashara matangazo
Mfanya biashara mmoja alienda kwenye mgahawa mmoja kupata mlo hali ilikuwa hivi:
Mfanya biashara: Juzi nilikuka nikapata pande kubwa la nyama, mbona leo kadogo hivi?
Mhudumu: Kwani ulikaa meza gani ulipokuja?
Mfanya biashara: Nilikaa pale penye lile dirisha kuubwa...
Mhudumu: Oh! Kawaida tunampatia mteja anaekaa pale ni sehemu nzuri ya kujitangaza mgahawa wetu.

Tuesday, June 14, 2011
Lift au kutembea?
Askari polisi wa barabarani wawili walikua wanaenda kazini:Askari wa kwanza: So tunapanda Basi au tunatembea kwenda job?Askari wa pili: Tusubiri tuone gari ya kwanza kufika....
Mapenzi yanapoisha...
Mwanaume akimuambia mkewe
Mume: Nikiondoka sidhani kama utapata mwanaume kama mimi tena maishani?
Mke: Nani kakuambia nataka mwanaume kama wewe?
Mume: Nikiondoka sidhani kama utapata mwanaume kama mimi tena maishani?
Mke: Nani kakuambia nataka mwanaume kama wewe?
Wapi hela?
Babu mmoja alikua anaishi peke yake, nyumba ya nyumba yake alitamani kulima viazi ila uzee ndio shida. Mwanae pekee yupo jela angemsaidia. Hivyo basi mwanae alimuandikia barua baba ake imeandikwa hivi "Baba zile hela nimezifukia numa ya nyumba, usifukue mpaka nitoke"
Siku ya pili askari walifurika eneo kufukua fukua bila kukuta kitu, mwanae akamuandikia baba yake barua ingine akiwa jela, "baba huo ndio msaada pekee nimekupatia haya panda sasa viazi"
Siku ya pili askari walifurika eneo kufukua fukua bila kukuta kitu, mwanae akamuandikia baba yake barua ingine akiwa jela, "baba huo ndio msaada pekee nimekupatia haya panda sasa viazi"
Dogo akiomba msaada baada ya...
Katoto kavulana: Njoo haraka haraka kuna mwanaume anampiga baba angu zaidi ya dakika 20 sasa!
Polisi: Kwa nini hukuniambia awali?
Katoto: Kwa sababu baba ndio alikua anamdunda dakika chache zilizopita.
Polisi: Kwa nini hukuniambia awali?
Katoto: Kwa sababu baba ndio alikua anamdunda dakika chache zilizopita.
Happy Birthday Chekazone
CHEKAZONE IMETIMIZA MWAKA MMOJA TANGU KUANZA KWAKE.
NAWASHUKURU NYOOTE TULIO PAMOJA KIPINDI CHOTE HIKO.
TUENDELEZE MCHAKATO WA KUTABASAMU NA KUCHEKA.
CHEKA UNENEPE MAISHA NI MAFUPI SANA.
NAWASHUKURU NYOOTE TULIO PAMOJA KIPINDI CHOTE HIKO.
TUENDELEZE MCHAKATO WA KUTABASAMU NA KUCHEKA.
CHEKA UNENEPE MAISHA NI MAFUPI SANA.
Wanaume Vs wanawake
Mwanamke mmoja aliwauliza wanaume wawili "intakuwaje mwanamke akitawala dunia?"
Mwanaume mmoja kwenye group akajibu "kutakua hamna vita, ila wivu utakua mwingi na baadhi ya nchi hazitaongeleshana"
Mwanaume mmoja kwenye group akajibu "kutakua hamna vita, ila wivu utakua mwingi na baadhi ya nchi hazitaongeleshana"
Polisi na Dereva
Jamaa mmoja alisimamishwa na askari wa usalama barabarani:
Askari: Mzee unatambua kuwa ulikua spidi sana?
Jamaa: Ndio askari.
Askari: Unaharakia wapi?
Jamaa: Unajua nini! Mke wangu ametoroka na askari kama wewe. Sasa nikadhani ndio wewe unamrudisha.
Askari: Mzee unatambua kuwa ulikua spidi sana?
Jamaa: Ndio askari.
Askari: Unaharakia wapi?
Jamaa: Unajua nini! Mke wangu ametoroka na askari kama wewe. Sasa nikadhani ndio wewe unamrudisha.
Saprize
Mume mmoja alipanga kumfanyia mkewe Surprise!
Akanyoa nywele za kifuani zote, kufika home akaunganisha kitandani alipolala mkewe. Mke kumgusa akanena "oh shemeji umekuja saa ngapi?".
Akanyoa nywele za kifuani zote, kufika home akaunganisha kitandani alipolala mkewe. Mke kumgusa akanena "oh shemeji umekuja saa ngapi?".
Subscribe to:
Posts (Atom)