Monday, June 14, 2010

Kupokea simu

Wanaume kadhaa walikuwa kwenye chumba kimoja cha kubadilisha nguo za michezo ghafla simu ikaita. Mwanaume mmoja akawaambia wale wote wakae kimya akaipokea simu:
Mwanaume: Halo?
Mwanamke: Halo honey, upo club?
Mwanaume: Ndio.

Mwanamke: Nipo mlimani city nimeona suti ya laki 6 ni sawa nikiinunua?
Mwanaume: Ndio mpenzi inunue tu.
Mwana ke: Pia nimeona Lexus ya 2008 mpya kwa $ 55,000 nimeipenda sana.
Mwanaume: Oh! Kwa pesa hiyo bila shaka.

Mwanamke: La mwisho mpenzi kuna nyumba masaki kwa Milioni 150 ipo full loaded.
Mwanaume: Consider it done.

Baada ya maongezi kuisha jamaa akatabasamu na kuiweka simu pale alipoikuta na kuuliza
''yeyote anaemjua mwenye simu hii nani?''

No comments:

Post a Comment