Tuesday, August 17, 2010

Viatu vya ngozi

Mtoto mmoja alikutywa na mama yake akiwa na viatu vya ngozi... Mama yake akamuuliza ''Jasmine mbona umekaa chini?''

Jasmine akajibu ''ninaviandaa viatu vyangu''
Mama: Ooh umekua mtoto mzuri siku hizi unajua mpaka kupaka kiwi viatu? Wow!
Jasmine: Mama!! Nikipaka kiwi viatu si vitaharibika?

Mama akajibu ''haapaana mwanangu kwani vipi?''
Jasmine: Me mevipaka losheni kwani si vya ngozi na vyenyewe? Kiwi itaharibuu...

No comments:

Post a Comment