Friday, August 26, 2011

Hii ya msalani

Ndani ya vyoo vya hoteli mlango mmoja kuna mtu na unaofuata una mtu wakikata gogo, jamaa mlango wa pili alianzisha maongezi ifuatavyo:

Mlango wa 1: Habari yako?
Mlango wa 2 akajibu bila kujielewa kinachoendelea "nzuri tu"
Mlango 1: Unafanya nini sasa hivi?
Mlango 2 bado akawa haelewi elewi akajibu "nipo nafanya kama wewe.."
Mlango 1: Naweza kuja?
Mlango 2 baado akazidi shangaa huku akijibu "hapana usije nipo bize"

Baada ya hapo Mlango 1 akasikika akisema "ngoja nitakupigia simu tena kuna mtu naona anajibu maswali sio yake"

No comments:

Post a Comment