Sunday, January 4, 2015

Mama akimuambia mwanae jambo, "Steve tafadhali kuwa makini na hiyo nyundo, utajiponda vidole." Steve nae akajibu, "Usijali mama, Emma ndio atashikilia msumari."
Baba: Juma umeliona gazeti langu? Juma: Ndio, mama kalivurugavuruga na kulitupa. Baba: Agghh! Nilikua nataka yaliyomo kabla hajalitupa. Juma: Nikusimulie, kulikuwa na maganda ya nyanya, vitunguu na karoti.
Baba: Mwanangu, nina habari nzuri. Umepata mdogo wako wa kike sasa. Mtoto: Oh! Kweli baba? Mama ana hizi taharifa?
Sauti toka kwenye simu: Halo, mama ako yupo nyumbani? Msichana kakajibu: Ndio yupo Sauti kwenye simu: Unaweza kumuita aje niongee nae tafadhani? Msichana: Sawa, inabidi niende mtaa wa pili kumuita. Sauti kwenye simu: Nilidhani umesema yupo nyumbani lakini? Msichana: Ndio yupo. Hii simu ni nyumbani kwa rafiki yangu, sie tunaishi mtaa wa pili.