Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, July 31, 2010

Vizee

Kulikuwa na vibibi viwili vizee wakiongea, mmoja akamuambia mwenzake "siku hizi nnasahau sana, jana nilisimama kwenye ngazi nikawa sikumbiki kama nilikuwa nataka kushuka au kupanda?"

Wa pili nae akamuambia mwenzake, "mimi nilikaa kwenye kitanda nkawa sikumbuki kama nataka kulala au ndio nimeamka"

Wa tatu akawaambia wenzake, "Loh, mimi ndio sijielewei kabisa, juzi nilikuwa bafuni na ndoo ya maji nikawa sikumbuki kuwa ndio nataka kuoga au ndio nimemaliza tayari"

No comments:

Post a Comment