Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, August 31, 2012

Kitu cha posa...

Jamaa alienda kuposa kwa mzee mmoja.
Mzee: Umekuja kuposa huku unatafuna big g!!?
Jamaa: Natoa harufu ya sigara.
Mzee: Yani unavuta sigara!?
Jamaa: Vile nikitoka kilabu kulewa tu.
Mzee: Unalewa!?
Jamaa: Nilianza kulewa nilipokuwa jela.
Mzee: Yaani na kufungwa pia!?
Jamaa: Ah niliua mtu.
Mzee: Duh kumbe wewe muuaji!?
Jamaa: Ah, si kuna mzee nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, mimi nikamuulia mbali.
Mzee: Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, mke mkeo uyu! Na mahali utaleta ukipata haina shida.

No comments:

Post a Comment