Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, November 29, 2011

"siku zote napenda kutembea kwenye mvua kwa sababu hamna atakaeniina nikilia" nukuu toka kwa Charlie Champlin.

Sunday, November 27, 2011

Ndoa

Mtoto: Baba nikimaliza shule tu ya msingi namuoa bibi.
Baba: Utamuoaje mama yangu ambae ni bibi yako.
Mtoto: We mbona umemuoa mama angu nkakaushia tu?

Moto na maji

Mama: Mwanangu hebu turudi mara moja nyumbani sijazima jiko la gesi itaungua nyumba.
Mtoto: Mama hata mimi nimesahau kufunga bomba usijali maji yatazima moto ukiwaka.

Friday, November 25, 2011

Zumbukuku

Jamaa akimsimulia mwenzake "yaani nimezunguuka library leo sina hamu"
Rafiki akauliza "ukitafuta kitabu au kiti gani?"
Jamaa akampa jibu "si nikitafuta cheque-book maktaba nzima hamna"

Mchezo wa box

Kijana: Ume-enjoy kuangalia mchezo wa boxing?
Mtoto: Ndio, ila kulikua na baridi hadi mabondia walivaa gloves.

Buchani

Dada alienda buchani
Dada: Huyo kuku mkubwa ameshanunuliwa?
Buchani: Bado ila yupo mkubwa zaidi.

Jamaa ili amvutie zaidi akaenda nje na kumjazia jazia kuku mwingine aonekane mkubwa zaidi aliporudi ikawa hivi:

Buchani: Kuku mkubwa zaidi huyu hapa.
Dada: Sawa ntawanunua wote wawili.

Thursday, November 24, 2011

Mshamba wa ng'ombe

Jamaa alitoka nunua ng'ombe, njiani yule ng'ombe akaanza kukojoa. Jamaa baada ya hapo akageuza kurudi alipomnunua na kuwaambia "nibadilishieni huyu ng'ombe mlieniuzia ametoboka"

Mwanasheria

Mwanasheria alifanya mapenzi na mwanamke,kwenye gari, yule mwanamke akaisahau chupi. Mbele akamkuta mkewe na kumpakia.

Mke: Hee! Mume wangu umeanza tabia ya kutembea na chupi za watu kwenye gari. Akaitupa nje.
Mume (Mwanasheria): aah! Mke wangu ule ni ushahidi wa ile kesi ambayo ingetupatia milioni 30...

Wednesday, November 23, 2011

Nani ana akili

Vijana wawili walienda kuvua samaki wakapata wengi tu. Siku ya pili wakati wanaenda tena:
Kijana 1: Ulikumbuka kuweka alama pale tulipopata samaki wengi?
Kijana 2: Niliweka alama ya x chini ya ile boti tuliyokodi jana.
Kijana 1: We chizi kweli je wakitupatia boti tofauti na jana.

Gereji

Jamaa alipeleka gari yake kwa fundi:
Jamaa: Fundi gari yangu nkikata kushoto wakati inatembea inapiga kelele na kulia ivo ivo.
Fundi akaicheki huku na kule na baadae kudai chake.

Fundi: Gharama yake itakuwa elfu 20.
Jamaa: Tatizo lilikua nini?
Fundi: Tatizo bado lipo, ukifika kalishushe bakuli lipo kwenye buti ya gari yako.

Nikune

Mke alimuomba mumewe "mume wangu naomba nikune mgongoni sijifikii" mume akaanza kumkuna, punde mke akajibu "tayari mume wangu" mume nae akajibu "ngoja kwanza sijamaliza"
Mke: Khaa mgongo si wangu mie...

Tuesday, November 22, 2011

Kifo

"Ingekua kufa unakufa leo siku ya tatu unafufuka mtu akiniua tu nkifufuka siku ya tatu na mimi namuua" alisikika kijana akinena.

Monday, November 21, 2011

Kahawa

Mteja: Naomba nipatie kahawa bila maziwa tafadhali.
Mhudumu: Maziwa tumeishiwa labda nikupe kahawa bila sukari.

Hotelini na glass

Mteja: Naomba nletee glass safi, maana jana ulinipatia chafu.
Aliporudi mhudumu akaenda pale walipo wale wateja wawili na kunena.
Mhudumu: Nani kati yenu ameagiza glass safi?

Panya

Mteja: Hotelini kwenu mnajitahidi sijaona panya kabisa.
Mhudumu: Watatokea wapi na chakula chapikwa kibaya.

Sunday, November 20, 2011

Swali darasani

Mwalimu: Kuku ni jamii ya ndege je nyoka na samaki.
Mwanafunzi: Nyoka ni jamii ya treni na samaki jamii ya meli.

Saturday, November 19, 2011

Msiba wapi

Bibi alipotea asijue msiba wapi akauliza vijana pale kijiweni. Wakamteka na kwenda kumla uroda. Walipomaliza bibi akawauliza wale vijana "haya na arobaini lini nije tena?"

Wednesday, November 16, 2011

Tv na kochi

Jamaa: ...wameniibia kila kitu kasoro Tv na kochi.
Polisi: Imekuwaje waibe vyote waacha ivo tu?
Jamaa: Wakati wanaiba nlikua naangalia Tv kwenye kochi.

Monday, November 14, 2011

Yuupi?

Jamaa akimsimulia jambo mwenzake "nataka kuoa mwanamke anaejua kupika, anaejiheshimu na alie na mvuto pia."

Rafiki akajibu "enhe! Sasa utamuoa yupi kati ya hao watatu?"

Vioja msibani

Mh. Mmoja alipopewa nafasi ya kuongea neno,alipokuwa msibani ambae ni mwana siasa wa siku nyingi alianza kwa kusema "msiba oyee"

Ugomvi mke na mume

Mke akifoka kwa sauti "ushukuru baba yangu ndio katoa pesa ukanunua flat screen, gari na furniture vinginevyo usingekuwa na jeuri #$€$$%*+=."

Mume nae akajibu "ushukuru baba ako katoa hizo pesa vinginevyo nsingekuwa hapa... #€*+"

Kero za mke

Mwanamke: Kama mumeo anakukera kila siku si uachane nae unde zako tu.
Mke: Sitaki kufanya kitu chochote kitachompa furaha kikiwemo icho.

Machinga complex

G: Hiivi kwa nini Mbeya na Tabora wasiwajengee machinga complex yao?
P: Aah wale wawatolee fotokopi halafu wawapelekee tu.

Sunday, November 13, 2011

Video library

Mteja alienda video library kuazima sinema ya kuangalia ikawa hivi:
Mteja: Nimekuja kuchukua Batman forever si ipo?
Mhudumu: Ipo ndio ila yapaswa kurudishwa sio kuichukua forever.

Kwa dentist

Dokta: Embu acha hizo kelele sijaanza hata kung'oa jino lenyewe.
Mgonjwa: Ndio najua, toa mguu wako umenikanyaga vidole vyangu vyote.

Urithi saluni

Mzee mmoja kutokana na umri aliamua kumpa mwanae saluni yake aiendeshe. Akampa maneno yafuatayo "mwanangu hii kazi inabidi uwe makini sana, wateja wengine wakali na wanatabia ya kugeuka ghafla hivyo angalia usijikate na wembe"

Saturday, November 12, 2011

Kesi ya mke na mume

Mwanamke aliulizwa "nini alisema kwako mumeo mpaka yakawa haya ya kumtwanga na kiti?" Mwanamke akajibu "jina langu naitwa Irene sio Judith, sa muulizeni Judith ni nani?"

Mifupa ya binadamu

Jamaa akipewa majibu na daktari wake baada ya uchunguzi "inaonekana mifupa ya miguuni mwako imekua laini sana saasa..." Akamkatisha na kumuambia "shhh taratibu dokta hapo nje kuna mbwa wanne watasikia"

Kitu cha heshma

Mtoto aliona nyeti za baba ake kuuliza akajibiwa "hii ni heshima mwanangu." Siku ya pilivwakaja wageni mtoto akaambiwa awape heshima si akafungua na kutoa nyeti kisha akanena "mnashangaa hizi baba, ana heshima kubwa zaidi"

Friday, November 11, 2011

Swali la mtego

Mwalimu: Uliona wapi bahari isiyokua na maji au dunia isiyo na watu?
Mwanafunzi: Si kwenye ramani au atlas.

Uzurulaji

Askari wa doria: Wewe kijana unafanya shughuli gani hapa mjini?
Kijana 1: Sina nnachofanya sina ajira kabisa.
Polisi: Na wewe mwingine unafanya shughuli gani?
Kijana 2: Mie ni boss wake.

Jumba la makumbusho

Jamaa bahati mbaya aliangusha bakuli la kuvunjika likavunjika ndani ya jumba la makumbusho. Askari akaja na kusema "mungu wangu hicho ulichovunja ni cha miaka 2000 iliyopita"

Aliyeangusha akajibu "ohh afadhali mi nilidhani kipya"

Baridi kali

Juma: We vipi mbona unatetemeka mikono.
China: We huhisi baridi kama mimi?
Juma: Sa si ingiza mikono mfukoni mwa suruali.
China: Mifuko imejaa nimeweka gloves.

Swali na jibu

Kijana alimuuliza maswali ya chemsha bongo mtoto:
Kijana: Kwa mfano baba kakupa shilingi 500 na mama kakupa shilingi mia 500 utakua na shilingi ngapi?

Mtoto akajibu: Ntakua na shilingi 500.
Kijana: Kw nini unasema hivyo?
Mtoto: Kw sababu mama hawezi kuipata hiyo 500.

Swali la mwalimu

Mwalimu aliuliza swali "enhe Juma, baba yako akikupa shilingi 150 na mama yako akikupa shilingi 150 utakua na shilingi ngapi?"

Mwanafunzi akajibu "ntapata kijoti"

Mabusu motomoto

Sam: Huwa nini m-kiss mke wangu kila siku kabla sijaenda kazini.
Ibra: Hata mimi namfanyia hivyo ukisha ondoka tu.

Macho mabovu

Mgonjwa: Dokta nasumbuliwa na macho sana siku hizi.
Mtu: Ni kweli unahitaji hapa ni mgahawani nenda,hospitali.

Wednesday, November 9, 2011

Ya usiku

Ilikuwa hivii:-
MTOTO: Eti baba unataka kuanza tena shule?
BABA: Kwa nini unauliza ivyo?
MTOTO: Jana ucku nlisikia mama anakwambia anataka muende la pili! Uthikubali baba utachekwa!

Chizi ajibu swali

Kijana: Nasikia mkeo anaongeaga mwenyewe akiwa peke yake.
Mtu mzima: Kwa kweli sijui, siwagi nae akiwa peke yake.

Mgonjwa huyu...

Mume: Daktari amekuja anataka kukuona.
Mke: Najisikia vibaya sitaki onana na mtu yeyote.

Gharama...

Mlala hoi alipoenda kwa daktari kupata huduma ya kiafya:
Dokta: Umeshawahi kuzimia?
Mgonjwa: Ndio, mara ya mwisho ulivyonitajia gharama zako.

Betri ya saa

Kimi: Kwa nini unatoa betri kwanye saa na kuzianika juani?"
Luko: Ili zipate kuwa na nguvu zaidi, nazirudishaga nkitaka angalia muda tu.

Tekinolojia

Dogo aliulizwa "wewe sasa mbona umebeba dvd juu chini na chini juu ndio nini?"
Dogo na akajibu "naogopa data zanaweza anguka njiani nlizozikopi humu."

Bar na maongezi

Jamaa 1: Mtoto wangu hasikii kitu nikimuambia jambo.
Jamaa 2: Anakukosea sana adabu.
Jamaa 1: Hapana ni kiziwi.

Mambo ya facebook

Baba aliingia facebook na kumuandikia mwanae wa kiume kwenye wall yake "Hi Son sio sote wazima, tumekumiss sana.HEBU SHUKA CHINI HARAKA CHAKULA KIPO TAYARI TUNAKUSUBIRI WEWE PUMBAFU.

Ugomvi baba na mama

Mtoto alikua analia nje jamaa mmoja akamkuta na kumuuliza "unalia nini mtoto?"
Katoto kakajibu "wazazi wangu wanapigana ndani?"
Jamaa: Baba yako ni nani?
Mtoto: Ndio icho wanachogombana ndani.

Hotelini india

Mtanzania alienda india, mgahawani:
M-tz: Nipatie Arul Jodi tafadhali?
Mhudumu: Umeona wapi iyo kitu mzee?
M-tz: Kwenye Menu.
Mhudumu: Hilo ni jina la mwenye hotel mzee.

Mke mgahawani

Mume akimuuliza mkewe: Siamini, yaani unakula mguu wa mbuzi wote wewe?
Mke akajibu: Hapana nimeagizia na juice.

Kitu hotelini

Wapendanao walifika mapokezi;
Mwanamke: Tafadhali tupe kitanda kimoja.
Mapokezi: Oh! Vimejaa kipo cha double.
Mwanamke: Nipe icho icho ntavisogeza karibu akikoroma tu nimtwange ngumi ya uso.

Kipofu barabarani

Ombaomba: Anti unaonekana kama malaika, niguse mkono wangu mie kipofu.
Mwanamke: Huyu atakua si kipofu.
Mume: Ni kipofu wala hadanganyi.
Mwanamke: We umejuaje?
Mume: Si amekuona upo kama malaika leo.

Tuesday, November 8, 2011

Kwa jirani...

Mwanamke: Mume wa huyo jirani yetu anambusu mkewe mara 3 kwa siku wewe kwa nini usifanye hivyo pia?
Mume akajibu: Ntafanya kama akiniruhusu kumbusu huyo mkewe.

Swali harusini

Mtoto: Mama kwa nini bibi harusi anavaa nyeupe?
Mama: Kwasababu ni siku yao ya furaha sana.
Mtoto: Mbona bwana harusi anavaa nyeusi?
Hakimu: Kwa nini umempiga mumeo na kiti?
Mshtakiwa: Mh. Hakimu meza ilikua nzito sana ndio nkachukua kiti.

Kutega shule

Simu ilipigwa:
Simu: Haloo naongea na mkuu wa shule?
Mkuu: Ndio, una shida gani?
Simu: Napenda kukutaharifu kuwa mwanangu leo hatoweza kuja shuleni.
Mkuu: Wewe una mahusiano gani huyo mtoto?
Simu: Hiyo ni sauti ya mama yangu inaongea.

Katoto shuleni

Mwalimu: Fredy jana ulitega darasani enhe?
Fredy: Sio sana mwalimu nlikua kantini tu.
Mwalimu: Kantini ukifanya nini?
Fredy: Nkitega kipindi chako.

Babu kwa dokta

Baba alipokua kwa dokta:
Dokta: Babu kwa afya yako utafikisha miaka 90.
Babu: Dokta mbona tayari nna miaka 90.
Dokta: Si unaona nlikuambia utafika 90.

Katika chumba cha upasuaji

Upo katika chumba cha upasuaji halafu kwa mbaali ganzi imepungua unasikia maneno ayaongeayo dokta:
I. Hili ni ini, na hii ni figo hiki kingine ni nini tena?
II. Hebu leta icho kitabu fungua ukurasa wa 4.
III. Hapana uko umepachana sipo rudi huku juu...

Uelewa muhimu

Mama mwenye nyumba alimpeleka mkwewe hospitali. Baada ya shughuli za hospitali alimuuliza mkwewe "mama ivi daktari alichukua na temperature?" Mkwe akajibu "kwa kweli sijui nilipaswa kuja nayo?"

Beki 3 na bosi wake

Beki tatu akimuambia bosi wake "mama mtoto ametumbukia kwenye kisima"
Mama mtoto: Enh! Ulimvisha pampers?
Dada: Ndio mama.
Mama mtoto: Bora maana angechafua maji.

Monday, November 7, 2011

Matamanio

Jamaa alienda saluni kunyoa, wakati ananyoa alomuona mwanamke pembeni akimuosha mteja akamuambia "dada leo unaonaje tukalale hotel?"
Dada akajibu "nimeolewa" jamaa akasisitiza "si unamuambia leo una over time, ntakulipa vizuri"
Mwanamke akamjibu "mwambie mwenyewe huyo hapo anaekunyoa nywele"

Mtoto na baba ake

Mtoto aliona korodani za baba ake akauliza "baba hizo nini?" Baba akajibu "mwanangu haya ni ma-apple" yakaishia hapo. Baada ya wiki akamuuliza mama ake "mama yale ma-apple mawili ndani ya suruali ya baba ni ya kienyeji au kizungu, maana ya mlinzi wetu ya kizungu.”

Taa ya gari

Dereva mmoja wa basi alimuambia kondakta "hebu toa kichwa nje uone indicator kama inawaka?" Konda alifanya hivyo na kumjibu "ndio, hapana, ndio, hapana..."

Swali la msingi

Kama kobe hana lile limfunikalo pale ni yupo uchi au hana nyumba?

Maongezi yao...

Vijana walikua wakiongea kama ifuatavyo:
Kijana 1: Tatizo lako we mbishi sana.
Kijana 2: Sio kubisha tu.
Kijana 1: Sa uliona wapi mbwa hana mguu mmoja.
Kinaja 2: Mie nimeona pahali alipouacha sasa.

Kunywa

Police wa barabarani alimsimamisha dereva mmoja na kumuhoji "mzee vipi umekunywa?"
Mzee akajibu "hapana" papo hapo mwanae akadakia "baba sema ukweli si ulikua unakunywa maji punde tu?"

Saturday, November 5, 2011

Ugenini

Jamaa ugenini alibanwa na haja kubwa. Alienda msalani aliporudi akamuuliza kwa kunong'ona mwenzake "msalani nimekuta toilet paper tatu, ya pinki, blue na nyeupe nkashindwa fahamu ipi nitumie na maji hamna."

Mwenzake akamuuliza "sasa umetumia ipi?"
Akajibu "sijatumia bado mekuja uliza kwanza kwako"

Cha pombe

Cha pombe mmoja alienda kwa daktari akipoulizwa akajibu shida yake "dokta nafikiri nna tatizo moja tu, mfumo wangu wa kilevi umejaa damu ndio sababu nashundwa pata bia nyingi. Nisaidie kupunguza..."

Wednesday, November 2, 2011

Babu kapata ajali

Babu aligongwa na baiskeli akaanguka chini jamaa mmoja akanena "mpeni maziwa fresh huyo atazinduka"

Babu nae akaibuka na kunena "na chapati tatu usisahau"