Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, August 30, 2011

RamliRamli

Jamaa mmoja alienda kwa mganga sasa ile kupiga ramli nk mganga akamuuliza sema shida yako, jamaa akanena "mekuja nna shida ya kulondoa giza la tanesco"

Mganga akamuambia baada ya kupiga ramli "kanunue jenereta shida yote itaisha, lisipowaka leta kuku watatu"

Monday, August 29, 2011

Story za kuku

Kuku A akimsimulia kuku B jambo kama ifuatavyo "wenzako Xmas iliyopita tulikula nyama ya kuku

Gari ngeni...

Baba akisimuliwa na mwanae "baba ukiondokaga kuna gari inakujaga, basi akiingia tu mama kwenye hiyo gari iiinaneesaa hiyoo mbona akipanda yako hainesi?"

Mke apokea simu

M'ke mmoja alipokea simu toka kwa mumewe (namba ngeni) akawa anajibu hivi (huku wote wakiwa ndani ya nyumba) "nipigie baadae hili fala lipo ndani saa hizi"

Mzee kwa dokta

Mzee: Dokta mkono wangu wa kushoto unauma sana!
Dokta: Usihofu ni hali ya uzee tu hiyo.
Mzee: Kama ndio hivyo mbona na wa kulia pia unauma?

Sunday, August 28, 2011

Lofa

Dogo mmoja aliingia saloon, kinyozi akawaambia wateja oneni huyu dogo ndio lofa kweli. Akachukua noti ya elfu 10 na 200Tsh. Dogo akachukua 200Tsh.

Kinyozi akanena, mnaona niliwaambia. Baadae mmoja wa wateja alikutana na dogo akamuuliza mbona hukuchukua ile elfu 10? Dogo akajibu "nikiichukua.tu mchezo utaisha"

Wiki 1 kuolewa

Msichana: Naolewa wiki ijayo, party itakua ya wachache na maalumu.
Mvulana: Ok! Utapendelea zawadi gani muhimu?
Msichana: Niletee mtu atakaenioa.

Kuwa nani maishani?

Mwanaume mmoja aliulizwa katika maisha yako unatamani kuwa kama nani? Akajibu "mende"
Alieuliza akashangaa na kuuliza kwanini?
Mwanaume akajibu "mke wangu anamuogopa sana mende kuliko mimi"

Nauli

Kwenye daladala jamaa alilipa nauli kwa kondakta. Kisha baada ya muda akamuambia konda "hehehe leo siku ya wajinga nlishalipa ticket hii hapa"

Saturday, August 27, 2011

Ratiba

Mpita njia: Haina haja ya kuwa na ratiba ya treni wakati kila mara inachelewa!
Injinia: Tutajuaje kama inachelewa kama tusingekua na ratiba sasa?

Samaki

Kijana mmoja alinunua samaki wawili wa kufuga akawapa majina mmoja A mwingine B. Rafiki ake akamuuliza "sa kwa nini umewapa majina hayo?" Akajibiwa "ili akifa A bado ntabaki na B"

Ujinga Ni...

1. Kujiita romantic na uko single.
2. Kukaa mbele kwa daladala alafu unaturn kwambia konda 'shusha' na umekaa na driver
3. Kutumia cursor kuscare mosquito itoke kwa screen ya comp.
4. Kureduce volume ya radio usome sms.
5. Kuruka line Angaza.
6.Kupigiwa simu halafu unaangalia balance yako after the call.
7. Kutafuta remote ya TV for 10 min, na tv iko a step away
8. KuDELETE namba ya ex wako na unaijua off head
9. Kubargain kitu kutoka 1000 hadi 500 alafu bado unapea muuzaji 5000 akupatie change
10. Kubuy beer ingine moja ukitegea fare ishuke hadi 200 ucku mkali
Jamaa na familia yake walienda kutoa mahari mida ya saa moja moja hivi kagiza kameanza kuingia, ghafla umeme ukakatika, mkwe akatamka kwa waliokuja kutoa mahari "pia tulisahau kujumuisha kwenye list ya mahari, jenereta pia linahitajika..."

Plastic Surgery

Dada mmoja mguu kwa mguu mpaka hospitali moja ya kukarabati sehemu za mwili ikiwepo sura yaani "plastic surgery" alipofika ikawa hivi:
Dada: Kufanya Plastic Surgery Shilingi ngapi?
Daktari: Inagharibu Laki moja taslimu.
Dada: Je, nkija na plastic langu bei itapoa?

Birthday.

Katoto ka miaka mitano siku ya kusherekea tarehe ya kuzaliwa kwake aliulizwa na baba ake anapendelea zawadi gani akajibu "nimezunguka sana sijapata size yangu, wewe ukipata ninunulie condom nne tu"

Bi. Kizee na uzee wake

Bi. Kizee mmoja alienda hospitali, akamkuta mwanadada mjamzito akamuuliza "mbona tumbo lako kubwa?"
Mjamzito akajibu "nina mimba"
Kizee: Ooh una mimba? Unamaanisha una mtoto?
Mjamzito: Ndio.
Kizee: Sasa kwa nini umem-meza?

Friday, August 26, 2011

Hii ya msalani

Ndani ya vyoo vya hoteli mlango mmoja kuna mtu na unaofuata una mtu wakikata gogo, jamaa mlango wa pili alianzisha maongezi ifuatavyo:

Mlango wa 1: Habari yako?
Mlango wa 2 akajibu bila kujielewa kinachoendelea "nzuri tu"
Mlango 1: Unafanya nini sasa hivi?
Mlango 2 bado akawa haelewi elewi akajibu "nipo nafanya kama wewe.."
Mlango 1: Naweza kuja?
Mlango 2 baado akazidi shangaa huku akijibu "hapana usije nipo bize"

Baada ya hapo Mlango 1 akasikika akisema "ngoja nitakupigia simu tena kuna mtu naona anajibu maswali sio yake"

Njemba hizi...?

Njemba mbili zilienza kwenye Pub, wakaagiza vinywaji kisha kila mmoja akafungua mfuko na kutoa burger na kuanza kula. Mhudumu akaja na kuwaambie "samahani hairuhusiwi kula burger yako hapa"
Njemba zikaangaliana wakatikisa bega na kubadilishana burger zao na kuendelea kula.

Karanga

Kizee kimoja kwenye daladala alimpa kondakta karanga, baada ya mda akampa tena zingine. Konda akauliza "we mbona huli?"
Kizee akajibu "sina meno" Konda akauliza "sa umenunua za nini?"
Kizee kikajibu "mi napenda chocolate iliopo juu ya karanga tu"

Darasani

Mwalimu akifundisha darasani:
Mwalimu: Wee Kelvin kwa nini unaongea darasani wakati nafundisha?
Mwanafunzi: Na wewe kwanini unafundisha wakati sijamaliza maongezi?

Kijana na mapenzi

Kijana mmoja alikua anampenda msichana mmoja ila akishindwa kumuambia. Siku moja akamtumia email na kumuambia "nakupenda sana" kisha akaituma. Punde akasikia kama kuna email imeingia. Akasamua asiisome aje aisome asubuhi iwe kama 'surprise' kwake.

Ilipofika asubuhi akaenda ili alisome akakuta ujembe umeandikwa hivi "Message sending failed due to insufficient balance! Please recharge your Account."

Thursday, August 25, 2011

Blackberry

Jamaa mmoja akitumia simu ya blackberry aliwatumia ujumbe wenzake kwenye mfumo wa kucha kama ifuatavyo "Warning: don't accept request from Muammar Gaddafi (218DE940) he is looking for a place to stay!"

Ubishi ubishi

Walikua wanabishana bwana, njemba moja ikanena "mi nlirudi usiku mkubwa wife akafungua mlango na nyodo, kumkomoa nikaamua kusimama mlangoni mpaka asubuhi na mpaka leo hatugusani"

Rafiki akamuuliza, "haiwezekani? Sa mtoto mmpempatia wapi?" Njemba ikajibu "mi nshasema simgusi mtoto itakua aliiba mimba ya mtu tu si bure"
Jamaa na rafiki zake wawili aleinda nao kwao, alipofika mlangoni mwenyeji akachomoa ufunguo wa mlango alipoificha rafiki zake wakimuangalia huku akinena "hapa ndio nafichaga ufunguo ila kesho nautoa hapa"

Tuesday, August 23, 2011

Ulevi noma

Mlevi mmoja mchana wa jua kali alikua tayari pombe mtu, akapanda daladala sasa lile joto na hewa nzito si akazomea ardhi (kutapika), baada ya hapo akamuambie kondakta "konda njoo udeki" punde kwenye foleni akaona bajaj nje ipo kwenye foleni mlevi akanena "wee dereva wa bajaj una ufagio?"

Sunday, August 21, 2011

Mbakaji

Polisi huku kamshikilia njemba moja wakiwa mbele ya jimama moja, polisi akamuuliza yule mama "huyu ndio kijana aliekubaka?"
Yule mama akajibu "Sijui labda arudie tena ndio ntamjua"

Mziki kwenye simu

Jamaa mmoja alienda kwenye party! Kuna mziki ambao upo kwenye simu yake ukapigwa na Dj kwenye hiyo party, akamuambia Dj "zima mziki mara moja" sekunde kadhaa 1 au 2 zikapita akasema "basi endelea kumbe anabeep tu"

Ikajirudia hivyo kama mara 3 hivi mwisho wa siku kumbe alikuja gundua kumbe ni mziki kwenye party na sio simu yake ikiita.

Saturday, August 20, 2011

Trafiki polisi alimsimamisha dereva mmoja mahojiano yakawa hivi:
Dereva: Afande nini shida na leo?
Trafik: Ohh wewe ndio nlikukamata jana enhe?
Dereva: Ndio mimi.
Trafiki: Na umelewa tena kama jana?
Dereva: Askari hii bado ni ile ile pombe ya jana nlikua sijaimalizia kwenye gari.

Friday, August 19, 2011

Mafuta darasani

Mwalimu akifundisha, kamuona mwanafunzi anapaka mafuta kichwani.
Mwalimu: Wee kwanini unapaka mafuta kichwani?
Mwanafunzi: Jana usiku nlisikia baba akimuambia mama paka mafuta kichwa kama haiingii. Napaka ili somo liingie.

Thursday, August 18, 2011

Mfanyakazi wa Mochuari

Mfanyakazi wa mochwari alikata dudu ya maiti moja ili akamuoneshe mkewe jinsi ulivyo mkubwa. MME: "hebu angalia dudu hii ilivyo mkubwa"MKE: "heeh zuberi amefariki"

Hii kali

Kijana mmoja alikuta ameweka kitu chenye rangi ya blue mdomoni alipoulizwa akajibu "we huoni vizuri? Si bluetooth"

Toroli

Jamaa mmoja alipata kazi ya kusafisha jiji na maeneo yake! Sasa kwa vile ni mgeni kazini, siku ile ile ya kwanza wakati anakokota toroli lake la kuzolea taka akalibandika ile stika yenye herufi "L" akimaanisha "Learner kama kwenye magari"

Cheka unenepe!

Wednesday, August 17, 2011

Siku ya siku

Baba alimkuta mwanae anachemsha maji kuuliza akajibiwa "baba mi mesoma havipandi hapa nachemsha madaftari ninywe maji yake tu, kesho mtihani"

Tuesday, August 16, 2011

Kazi ipo

Jamaa alimuuliza rafiki yake ampe ushauri kabla hajaingia kwenye dimbwi la kuitwa mwana-ndoa "eti kaka kitu gani cha kufanya mwanamke awe na furaha maisha ya ndoa"
Rafiki akamjibu "mpende sana mkeo na usijaribu kumu-elewa kuhusu wanawawake"

Miguu ya kuku

Mteja alipofika mgahawani akamuita mhudumu na kumuuliza;
Mteja: Una miguu ya kuku?
Mhudumu: Hapana ninayo hii hii yangu tu.

Girlfriend na Boyfriend

Boyfriend: Unataka niku-kiss?
Girlfriend: Hapana.
Boyfriend: Unakumbuka swali nlokuuliza.
Girlfriend: Unataka niku-kiss?
Boyfriend: Ndio, usisitizapo tu.

Monday, August 15, 2011

Mtihani ulivyokawa...

Msichana mmoja akimsimulia boyfriend wake;
Msichana: Ule mtihani ni kama girlfriend?
Mvulana: Unamaanisha nini kufananisha na girlfriend?
Msichana: Ngumu kumuelewa, complication, maswali mengi na majubu yake sasa huwa mhh!

Mlangoni

Mtu: We mtoto mama yako yupo nyumbani?
Mtoto: ndio. Jamaa akagonga sana hamna aliefungua.
Mtu: We mtoto si umesema mama ako yupo nyumbani?
Mtoto: Ndio yupo, hapa sio tunapoishi.

Inzi kwenye supu

Mteja: Mhudumu! Hii supu kuna inzi wawili wameingia...
Mhudumu: Usijali hawajui kuogelea watakufa tu.

Uoga huu....?

Mwanaume mmoja alisikika akisema "Mke wangu muoga kweli, hadi maji eti anaogopa" Mwenzake akamuuliza "kivipi?"
Njemba akajibu: Si kila nikirudi namkuta akioga na mlinzi wetu.

Kasichana & Kavulana

Ka-sichana: Unafikiri kwa nini Mungu alimuumba msichana kabla ya Mwanaume?
Ka-vulana: Alitaka kutengeneza copy ya mwanamke kabla ya final copy.

Sekunde 55

Mgonjwa: Daktari nina sekunde 55 tu kabla sijaaga dunia, nisaidie nisife.
Dokta: Nakuja nisubirie kwa dakika 1 tu.

Mvua.

Boss: Ally nenda kamuagilie maua muda umefika.
Ally: Boss lakini kuna mvua inanyesha nje.
Boss: Chukua mwavuli.

Sunday, August 14, 2011

India

Mvuta bangi anamuliza mlevi, "Eti, India iko mbali?"
Mlevi: "Sidhani, kwa sababu tuko na Muhindi mmoja kazini. Huwa anakuja kwa baiskeli kila siku!"

Meneja na Sekretari

Boss wa kampuni kamkuta meneja anampa mabusu motomoto sekretari wake akauliza kwa ukali "wewee nakulipa kufanya huu ujinga au?"
Meneja akajibu "hapana boss hii ni for free tu."

Mshahara oyee

Mzee aliporudi nyumbani mwisho wa mwezi swali la kwanza aliloulizwa na mkewe "haya mshahara uko wapi?"
Mume: Nimeshautumia wote, nimenunua kwa ajili ya hapa nyumbani!
Mke: Umenunua nini cha kumaliza laki tano yote?
Mume: Nimenunua raundi kumi za bia tuburudike...

Vimbwanga

Mlevi mmoja aliingia choo cha kike, akawa anakojoa huku amekaa chini mtu akamkuta na kumuuliza "vipi?" Mlevi bila hiyana akajibu "wee huoni tangazo limeandikwa kaa chini wakati wa kukojoa" (choo ni kile kukaa).

Saturday, August 13, 2011

Nani zaidi...

Mama alimuuliza mwanae. "Obama ni nani?"
Mtoto akasema "sijui".
Mama akasema "zingatia masomo."

Mtoto nae akamuuliza mama yake unajua "Jenifer ni nani?"
Mama akajibu "Sijui"
Mtoto akamjibu "Mzingatie sana mumeo!"

Friday, August 12, 2011

Pombe bwana

Jamaa mmoja baada ya ku-pombeka vya kutosha ugenini mkoa fulani nchini Tanzania alipangisha kwenye hoteli moja ya ghorofa kadhaa. Sasa baada ya kulewa chakari akapanda Bajaj na kumuambia dereva wa bajaj "nipeleke ghorofa ya tano"

Kizee kwa Daktari

Kizee kimoja kilienda kwa daktari wake na mkewe wote wazee. Dokta baada ya kumfanyia uchunguzi wa mwanzo dokta akamuambia babu "nahitaji mkojo wako, haja kubwa kidogo, na mbegu za kiume tufanyie uchunguzi"

Babu akamgeukia mkewe (bibi) nae bibi akamuuliza "nini?"
Babu akauliza "amesemaje dokta?"
Bibi akajibu: Anataka chupi yako.

Vimbwanga vya simu

Jamaa mmoja alimpa rafiki yake simu ili atume ujumbe mfupi maana alikua ana shida na hiyo huduma, jamaa alipompatia akampa na sharti "usiandike meseji ndefu sana wino umebaki kidogo sana"

Dawa ya kichwa

Kaka mmoja alienda kwa daktari, "dokta hiki kichwa chaniuma saaana karibu kila siku ipitayo" Dokta akamjibu ngona nikupe mfano, mimi kilinitokea miaka kadhaa nikamuomba mke wangu awe ananikanda kila siku halafu mwishoni nampa penzi murua kikaacha kabisa kuuma"

Wiki kadhaa mbele jamaa akarudi kwa dokta "aisee dokta umenisaidia sana, ile mbinu imenisaidia sana sana. Sasa nimepona" Dokta akajibu "safi sana"
Kabla mgonjwa wake hajaondoka akamuambia "...na dokta sebule kwako pazuri sana"

Monday, August 8, 2011

Nyani wa mzungu

Mzungu alipita na nyani wake mbele ya kigenge cha muuza ndizi, yule nyani akapora ndizi akala. Muuzaji akamkasirikia, mzungu akasema unakasirika nini wakati kala ndugu yako!

Mzungu akaondoka, aliporudi akuta nyani wake kafa. Akauliza kwa nini mmemuua nyani wangu? Muuzaji akajibu hayakuhusu haya mambo ya kifamilia!!

Sunday, August 7, 2011

Gari inaoshwa

Mzee mmoja alimuagiza mwanae mdogo wa kiume amuoshee gari yake akamuambia "itakate umesikia?" Baada ya muda baba mtu akatoka akamuona baba mwanae anaosha gari na maji ya moto kumuuliza dogo akajibu "si ili itakate baba"

Saturday, August 6, 2011

Mbwa mkali

Nyumba moja yenye geti na kibao kiliandikwa kama tangazo kuwa. "Mbwa mkali" usiku mmoja wezi waliingia kwenye hiyo nyumba wakamuiba na mbwa mwenyewe.
Jamaa alimuuliza mwenzake "ingekua vipi gari ukiipaki ndio unakula mafuta?"

Friday, August 5, 2011

USA waligundua mashine ya kukamata wezi:

USA ilikamata wezi 20 kwa siku.
UK ilikamata wezi 50 kwa masaa 10.
Germany ilikamata wezi 80 kwa masaa 6.
Sudan ilikamata wezi 200 kwa saa 1.
Nigeria ilikamata wezi 500 kwa dk 30.
Tanzania ndani ya dk 15 wakaiba na mashine yenyewe.

Mtishia mtoto

NILIKUWA kwenye basi natoka kazini narudi nyumbani, kwenye viti vya pembeni yangu kulikuwa na mama mwenye mtoto.

Wakati tunaendelea na safari yule mama alitaka kumnyonyesha mwanawe, mtoto akagoma, mama akamwambia nyonya, kama utaki nampa anko anyonye!"
 
Anko ni abiria kijana mwanaume aliyekaa na huyo mama.

Mtoto akanyonya kidogo akaacha, mama yake akamtishia tena kumpa anko.
Yule kaka kwa hamaki akasema,"mama uwe na msimamo, nimepitiliza vituo vinne kwa ajili hiyo!

Chabo

Jamaa wakipiga chabo! Ghafla polisi akatokea na kuwauliza "nyiee mnafanya nini hapo" wale masela wakageuka na kumuambia polisi "shhhhh...." Huku wakimuonyesha ishara ya aje na yeye kushuhudia, polisi nae akanogewa.

Wednesday, August 3, 2011

Bajaj - Kioo

Dereva mmoja wa bajaj niliona kioo cha bajaj yake cha mbele kimepasuka kwa pembeni mithili ya jiwe limevunja, kumuuliza kulikoni akajibu "wamenivunjia kioo wakaingia na kuiba laptop"

Wali nyama

Jamaa mmoja kila akienda kuagiza wali nyama anapewa nyama kidogo, siku ya pili akaenda na kuagiza nyama wali....

Monday, August 1, 2011

Umeme

Jamaa mmoja alimtumia msg rafiki "umeme wamekata"
Rafiki akajibu "sie tuna wiki sasa hawajakati"
Jamaa: Hata sie tangu wiki iliyopita.

Baada ya kama saa moja kupita yule aliemtumua msg rafiki ake akamuandikia msg nyingine tena "hee! Kumbe umeme luku umeisha!"

TV Set

Jamaa mmoja alienda nunua Tv baada ya kutajiwa bei akahoji "samahani hii si mnaiita Tv Set?" Muuza duka akajibu "ndio"
Mnunuzi akamalizia "sasa kama ni Tv Set mbona mwanuza moja?"