Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, August 5, 2011

Mtishia mtoto

NILIKUWA kwenye basi natoka kazini narudi nyumbani, kwenye viti vya pembeni yangu kulikuwa na mama mwenye mtoto.

Wakati tunaendelea na safari yule mama alitaka kumnyonyesha mwanawe, mtoto akagoma, mama akamwambia nyonya, kama utaki nampa anko anyonye!"
 
Anko ni abiria kijana mwanaume aliyekaa na huyo mama.

Mtoto akanyonya kidogo akaacha, mama yake akamtishia tena kumpa anko.
Yule kaka kwa hamaki akasema,"mama uwe na msimamo, nimepitiliza vituo vinne kwa ajili hiyo!

No comments:

Post a Comment