Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, May 26, 2011

Kila kitu Kipya

Jamaa kaoa mke kutoka kijijini,baada ya harusi kafungua nyumba yake mpya,kazindua gari lake jipya na wakati wa kumuingia bwana kavaa condom, yule mke akatuma sms kwao kwamba mume ana kila kitu kipya mpaka ile kitu bado mpya iko ndani ya plastiki haijafunguliwa!!

Mmasai kwa fundi

M-masai alipeleka radio kutengeneza fundi alipoifunguwa wakatoka mende wengi masai alipowaona akamwambia fundi
"kamata watangasaji wanatoroka!!"

Monday, May 23, 2011

Padre akiomba mchango

Padre mmoja aliwaomba waumini wake mchango kuzungushia ukuta eneo la makaburi. Mlevi mmoja akauliza papo hapo, ''kuna marehemu aliyewahi kutoroka?''

Saturday, May 21, 2011

Ngozi Bibi kizee

Bibi kizee mmoha alienda kuogelea kwenye bwawa maalumu la kuogelea. Alikutana na watoto wadogo na wakiogoelea.

Sasa alipozamia wakati anaibuka akawa anaelea mgongo ukiwa wa kwanza kuonekana, wale watoto walipomuona wanamuita mama yao ''mama... mama... Njoo uone kuna mamba humu kaingia...''

Thursday, May 19, 2011

Uaminifu

Mume: Mke wangu niambie ukweli hivi ushavunja uaminifu mara ngapi?
Mke: Siku moja nililala na mwenye nyumba sababu alikua anatudai kodi.
Mume: Si mbaya sana.

Mke: Mara ya pili, ulipofanyiwa operation hatukuwa na pesa ikabidi nilale na daktari.
Mume: Kweli unanijali mke wangu.

Mke: Mara ya tatu ni kile kipindi cha uchaguzi ulipokuwa unaomba kura za ubunge ikabidi nitembee na wapiga kura wako wote ili upite ndio maana ukashinda.

Yebo yebo

Mtoto mmoja alikua analia kapoteza yeboyebo zake, mtumishi wa Mungu akamkuta akilia akamuuliza.
Mtumishi: Unalia nini mtoto mzuri?
Mtoto: Natafuta yebo yebo zangu zimepotea.
Mtumishi: Basi usilie mwachie Mungu tu.
Mtoto: Mungu hazimtoshi zilikuwa ndogo sana.

Swali kwa mwanafunzi

Mwalimu: Mfano nikikupatia paka wawili, na wengine wawili na mwingine tena wawili je utakua na wangapi?

Mwanafunzi: Saba mwalimu.
Mwalimu: Hapana, sikiliza tena... (Mwl. Aliuliza vile vile)

Mwanafunzi: Saba Mwalimu.
Mwalimu: Ngoja nikupe mfano mwingine, mikikupa maembe mawili, na mengine mawili na mawili tena je ni mangapi ntakua nimekupa?

Mwanafunzi: Sita.
Mwalimu: Saaafi sana.

Mwalimu: Haya marudia lile swali la awali (Mwalimu akauliza vile vile tena).
Mwanafunzi: Saba.

Mwalimu akanena kwa hasira, ''shut up hiyo saba unaipata wapi sasa?''
Mwanafunzi akajibu, '' kwa sababu tayari ninae paka mmoja nyumbani!''

Wednesday, May 18, 2011

Ugeni wa mambo

Mwanamke mmoja alilowa na alikua hajui mapenzi yaani hajawahi kufanya mapenzi kabisa. Siku moja mumewe kabla hajasafiri alimuonyesha naniliu yake na kumuambia ''hii naniliu yangu inaitwa popoo, ninayo mimi tu sawa enhe''

Mume aliporudi toka safarini mke akanena ''mume wangu mbona Issa nae anayo popoo na we ulisema unayo wewe tu peke yako?''

Mume akajibu; ''ooh nilisahau kukuambia nilikua nazo mbili ingine mempatia Issa''
Mke akanena na yeye ''sa mbona Issa umempa kubwa na tamu we umejibakizia ndogo kama penseli?''

Monday, May 16, 2011

Mpakistan

Familia moja ya wapakistan ilienda kuishi marekani.
Mtoto wao wakamuanzisha shule. Alipofika shuleni hali ilikua hivi:

Mwalimu: Unaitwa nani?
Mwanafunzi: Ahmad.
Mwalimu: Oh! Hapa marekani kuanzia leo utaitwa George sawa.

Aliporudi home akawasimulia wazazi wake, wakamchapa sana. Aliporudi shule kesho yake ikawa hivi:

Mwalimu: Kulikoni mbona umevimba vimba?
Mwanafunzi: Jana usiku nyumbani nimeshambuliwa na wa-pakistan wawili (wazazi wake).

Kutoa Mahari

Jamaa mmoja alienda kutoa mahari, ulipofika muda muafaka sasa mbele ya wakwe watarajiwa akawauliza, ''je naweza kutoa mahari kwa njia ya M-pesa au tiGo pesa sasa ivi?''

Ujanja

Jamaa mmoja alikua anaugonjwa wa kusahau. Kila akiweka password kwenye computer anaisahau, siku moja akaamua kuandika password mpya inaitwa ''incorrect'' baada ya hapo kila akiikosea au kuisahau kompyuta inamkumbusha kwa kuandika ''password you enter in incorrect''

Saturday, May 14, 2011

Pombe

Jamaa mmoja alikua bar na mkewe akalewa chakari. Mkewe akawa anamsaidia kumkokota mpaka nyumbani, walipofika housegirl akawafungulia mume akanena ''vyumba vipo au vimejaa?''

Tuesday, May 10, 2011

Mlevi chakari

Mlevi mmoja alikuwa kalewa chakari, sasa punde akakutana na rafiki yake mmoja pale bar akamfuata na kumuongelesha sauti ya kilevi levi "Aisee ndugu yangu ninunulie bia mbili tu akili yangu ikae sawa"

Cheka Unenepe

Misemo tofauti tofauti: Kitanda cha zamani, ndoto mpyaa!
Unatema Big G kwa karanga za kuonjeshwa.

Mwizi mgeni

Mwizi mzoefu na mgeni walienda kuiba waliporuka ukuta mwizi mzoefu akalia "nyauuu" walizi wakapotezea wakijua ni paka. Aliporuka mwizi mgeni akalia "nyauu wa pili".

Kuvaa Msuli

Jamaa (mwanaume) alivaa msuli ndani hakuvaa chupi, kwa mbele kulikua na paka. Si yule paka akazirukia naniliu akijua ni panya.

Monday, May 9, 2011

Voda Vs Zantel

Mtoto kamuuliza Mama yake: "Mama wewe unatumia Voda na Baba Zantel, mbona usiku nilisikia Baba anakuomba Tigo ukamwambia asugue taratibu, nani ana Line Mbili?!"

Kibabu kizee

Mzee wa miaka 85 alimnyonya mkewe wa miaka 80 matiti kimapenzi.Mzee akafa. Kwenye Post mortem yake waliandika: DIED OF DRINKING EXPIRED MILK. BEST BEFORE 1955.

Misa ya maziko

Jamaa mmoja alimwomba Padri amfanyie misa ya maziko mbwa wake. Padri akamjibu, Hapana hatufanyi misa hizo labda ujaribu sehemu nyingine. Jamaa akamuuliza sehemu gani wanafanya hizo misa maana nina shs millioni tatu ya sadaka? Padri akadakia "Wewe hukusema mbwa wako alikuwa mkristo ,mlete mlete nintamfanyia misa hamna shida"

Neno

Jamaa alimpa lift mwanamke, basi ikawa kila akibadilisha gia mkono unagusa paja la yule binti,basi yule mwanamke akawa analalamika na kusema "kasome Mathayo 7:7"Jamaa akaogopa na kuacha kumshika! ile kufika home tu jamaa akakimbilia biblia. Kufungua akakuta imeandikwa"OMBENI NANYI MTAPEWA"

Kitendawili

Mwanafunzi: kitendawili...
Wanafinzi: Tegaa.
Mwanafunzi: nivue nguo nikupe utamu.
Mwalimu: Mshenzi wewe acha kutukana!
Mwanafunzi: mwalimu hata wewe hujui, jibu lake ni NDIZI!

Sharobaro

Sharobaro ndani ya Kanisa baada ya kupokea divai akamwambia mchungaji " NAOMBA TISHU MEN!"

Mashine gani ya...

Jamaa alimuuliza gym instructor "Kuna demu mkali ajabu nataka kumfurahisha,nitumie machine gani?" Akajibiwa; "Bora utumie ATM!"

Mchaga alipoopoa

Mchaga mmoja alipata mtoto wa pwani, kwenda nae gesti mwanamke akavua nguo kiunoni akiwa na shanga tele za kutosha.Yule mchaga kuziona tu akanena "Yeeesu na Maria hisi rosari zimeibiwa parokia gani?"

Kutongoza

Jamaa mmoja wakati amemsimamisha dada mmoja na wakati akimtongoza bahati mbaya/nzuri naniliu yeke ndani ya zipu si ikasimama. Jamaa alichoamua baada ya hapo ni kuitoa nje na kuiambia "haya tongoza wewe mwenyewe na haraka zako"

Saturday, May 7, 2011

Gari ya zamani

Sokwe

Sokwe mmoja aliporudishwa porini toka kwenye eneo la maonyesho ya wanyama akawa anawasimulia wenzake, ''dah sokwe wa mjini ni ma-sharobaro balaa''

4x4

Jamaa mmoja ndio mara ya kwanza alinunua gari yenye 4WD wakamuambia inapita popote hii.
Jamaa alipoichukua si akaenda nayo baharini akitaka kupita njia ya mkato...

Bibi kizee

Bibi alikua anamhusia mjukuu wake ''kua uyaone mjukuu wangu'' nae mjukuu wake akamjibu ''nimeyaona ya mwalimu Chilebo yako kama vibuyu''

Friday, May 6, 2011

Waalimu - Loliondo

Walimu walienda kwa babu loliondo kupata kikombe cha babu, baada ya kupewa kikombe cha dawa kila mmoja babu akawaambia haya 500 yangu nipeni, waalimu si wakatoa kadi za bima ya afya....

Mchaga na vijimambo

Mchaga mmoja alitumbukia kwenye kisima cha maji akapiga kelele huku akitapa tapa, mkewe akaja na namba mpya akamtupia amuokoe.

Mume akauliza umeinunua sh ngapi?
Mke: nimenunua sh 1,000 tu.
Mume akajibu: Irudishe nenda kwa masawe anauza sh 500 fanya fasta ntazama.

Mc katika shughuli

Mc katika shughuli wakati akimpamba bi. Harusi akasema ''sasa nawapa sifa kubwa ya bi.harusi, mi namfahamu huwa havai nguo za ndani''

Watu ''haaa!''

Kuonyesha hajakosea kwa msisitizo akanena zaidi, ''bi.harusi huwa havai nguo za ndani yeye ni za kutoka nje, italy, england na USA hebu mshangilieni jamani....''

Watu khaa!

Tuesday, May 3, 2011

Mbwa

Mtoto alimuona mbwa wa jirani anajikuna mguu wake, kama ilivyokawa kwa mdomo wanavyojikuna. Dogo kuona vile akamuambia baba ake ''baba ona mbwa anajikata kucha mwenyewe''

Monday, May 2, 2011

Mtoto akioga na baba

Mtoto mmoja alipokua akioga na baba ake, bahati mbaya akateleza na kujishikilia kwenye naniliu ya baba ake.
Baba yake akamwambia, ''shukuru leo umeoga na mimi ungeoga na mama yako sijui ungejidakaje?''

Changudoa

Siku televisheni kadhaa zilipotangaza kuuwawa kwa Osama, changudoa mmoja akasikika akisema ''mmh! Jamaani sa ntapata wapi buzi kama lile nipate mafuta ya bure kwenye gari yangu?''

Sunday, May 1, 2011

Kwa jirani

Jamaa mmoja alisahau kuvaa pichu kwa sababu ya haraka akiwahi sehemu. Kwa vile alikua mbali na home tayari akaamua apite kwa jirani mbele kidogo.

Akagonga mlango, alipofunguliwa akafungua mwanaume na kumuambia, ''samahani leo nimesahau kuvaa pichu ivo naomba niazime ile ya kwako ya kijivu huwa mkeo ananiazimaga nikiwa nae.''