Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Saturday, July 31, 2010

Alarm

Kuna jamaa mmoja alipoisikia alarm ya gari fulani inapiga kelele, akawa anatembea huku akipepesha mikono yake juu kama kwaya masta anapoongoza nyimbo fulani ya kwaya.

Vizee

Kulikuwa na vibibi viwili vizee wakiongea, mmoja akamuambia mwenzake "siku hizi nnasahau sana, jana nilisimama kwenye ngazi nikawa sikumbiki kama nilikuwa nataka kushuka au kupanda?"

Wa pili nae akamuambia mwenzake, "mimi nilikaa kwenye kitanda nkawa sikumbuki kama nataka kulala au ndio nimeamka"

Wa tatu akawaambia wenzake, "Loh, mimi ndio sijielewei kabisa, juzi nilikuwa bafuni na ndoo ya maji nikawa sikumbuki kuwa ndio nataka kuoga au ndio nimemaliza tayari"

Friday, July 30, 2010

Besdei

Vizee viwili mke na mume siku moja wakati wapo mezani, mke akamuambia muwewe.
''tutoe nguo zote tule chakula bila kubanwa banwa.

Wakati wanakula mke akalalamika ''mh! nimeanza sikia joto ghafla.''
Ndipo mume akajibu ''ni kwa sababu titi zipo kwenye bakuli la supu.''

Thursday, July 29, 2010

Siku ya harusi

Mwanaume mmoja alikuwa na ugonjwa wa kusahau sahau sana, siku moja wakati yupo nyumbani anafua nguo zake na usafi kwa ujumla, ghafla akaingia mwanamke akiwa amefyumu ile mbaya. Kumbe alikuwa ni bibi harusi ndani ya vazi lake tayari, na huyo aliemkuta akifanya usafi ndio mume mtarajiwa, hakuonekana kanisani.

Uelewa huu?

Jamaa mmoja alipofika maeneo fulani fulani ya uzunguni akakuta kibao kimeandikwa "Amri hairuhusiwi kutembea eneo hili" yule kaka pamoja si akaamua kutambaa mpaka alipolimaliza hilo eneo...

Ndege pori

Eti wale ndege pori wanaopenda kula mizoga baada ya simbana wengineo kumaliza kula, na wao walipata kamzoga mpaka mwisho wa siku wakatosheka na kuwepo tu pembeni palipo huo mzoga. Ndipo akaja ndege mwenzao na wakamuambia "usitulaumu kuchelewa kwako, sie tushakula ukikikuta cha baridi hilo halitu-husu"

Shoga

Shoga mmoja mwanajeshi wakati yupo vitani akawa anabishana na mwanajeshi mwenzake, "we vipi unazubaa zubaa nini m-shoot huyo adui anazidi kuja karibu yetu?"
Ndipo yule shoga akamjibu "we humuoni alivyo mzuri vile, mi siwezi"

Kwa dokta

Mama mmoja aliporudi nyumbani akawa anaongea mawili matatu na mumewe, kidogo anaingia mtoto wao wa kike. Wakamuuliza "enhe za hospitali? Daktari anasemaje?"
Mtoto kwa nafasi nae akawa anajibu, "majibu mazuri tu, ila nimesahau chupi yangu kwa dokta" wazazi walitizamana...

Kwenye computer

Kibosile mmoja alimpigia secretary wake simu "mbona hujanijibu e-mail yangu mpaka sasa?"
Secretary akajibu, "boss nimeisoma ila nimeshindwa kuijibu, nipo nyumbani bado na kibaya ni kwamba paka wangu ameimeza "mouse"

Tembo

Kijana mmoja alikuwa na tembo wake mdogo akimfuga, siku moja wakati wapo matembezini jamaa akafungua zipu yake na kujisaidia haja ndogo, nipo tembo wake akamuuliza "unawezaje kupumua na huo mkonga wako?"

Harusi

Siku ya harusi bibi harusi alipofika kanisani akiwa ameshavalia gauni la harusi nk, kidogo anamuona mumewe mtarajiwa anatoka na bibi harusi mwingine amevaa kama yeye wakiwa tayari wamefunga ndoa. Bibi harusi wa kwanza akabaki kwenye mshangao asielewe kinachoendelea, ndipo mumewe mtarajiwa akamuuliza huyu wa awali, "Hukupata e-mail yangu?"

Simu haionekani

Mwanaume mmoja siku moja wakati yupo kwake ghafla akawa anasikia simu inaita halafu haioni, akaanza mlaumu mkewe " muone kwanza ushaificha simu yangu, mbona siioni na inaita?"

Mke akamuangalia na kumjibu; "una uhakika?"
Mume: Ndio
Mke akaenda akamfunua kitambi jamaa akaiona simu imejificha katikati ya nyama.
Mume akawa mdogo kama amemwagiwa maji ya baridi.

Wednesday, July 28, 2010

Mtoto huyu

Mtoto wa miaka 6 wa kike alienda sebuleni alipomkuta mama yake ameketi na baba yake.

Akasema, ''baba kondom yangu imepasuka una ingine ya akiba?'' mtoto alinena.
Mama nae kimoyo moyo akanena (mungu wangu mtoto huyu ameanza lini?)

Mama akauliza vizuri, ''imepasuka!? Umeipata wapi?''
Mtoto: Meipata kwenye suruali ya baba, nilikua naichezea...

Tuesday, July 27, 2010

Pancha

Baba mmoja alimuacha mwanae kwenye gari kwa muda. Punde kidogo mtoto akasikia kama gari inatikisika, kuchungulia akamuona kibaka ameinama kwenye tairi.

Mtoto akamuuliza yule kibaka, ''unafanya nini kwenye gari ya baba?''
Kibaka kujihami akajibu, ''baba yako kanituma nije kuziba pancha.'' Mtoto akasema 'oh okey'

Baba aliporudi akauliza, ''imekuwaje hamna matairi?'' mtoto ndipo akajibu, 'alikuja mtu akasema anaenda kuziba pancha ndo nkamuambia achukue yote manne akazibe asichelewe sana.''

Pancha

Baba mmoja alimuacha mwanae kwenye gari kwa muda. Punde kidogo mtoto akasikia kama gari inatikisika, kuchungulia akamuona kibaka ameinama kwenye tairi.

Mtoto akamuuliza yule kibaka, ''unafanya nini kwenye gari ya baba?''
Kibaka kujihami akajibu, ''baba yako kanituma nije kuziba pancha.'' Mtoto akasema 'oh okey'

Baba aliporudi akauliza, ''imekuwaje hamna matairi?'' mtoto ndipo akajibu, 'alikuja mtu akasema anaenda kuziba pancha ndo nkamuambia achukue yote manne akazibe asichelewe sana.''

Iki...

Mtoto mmoja alikua akimsikia baba yake usiku mara kwa mara akimwambia mama yake, ''ikisimama panda''

Siku moja akamuuliza mama yake, ''mama humu ndani kwetu kuna daladala usiku? Nasikiaga baba anakuambiaga ikisimama panda.''

Juice

Kijana mmoja alitengeneza juice ya mananasi. Alipomaliza kuitengeneza akagundua kuwa maji aliyotumia hakuyachemsha. Akawasha jiko na kuiweka juice yote kwenye sufuria na kuanza kuichemsha.

Monday, July 26, 2010

Ufugaji kisasa

Jamaa mmoja mfugaji aliamua kuwa mfugaji wa kisasa. Hivyo basi akanunua mashine ya kukamulia maziwa ya ng'ombe.

Siku moja mkewe alipotoka akaenda kuijaribu kwa kuchomeka uume wake pale, akaiwasha ikampa matokeo ya kuridhisha.

Alipomaliza akawa anataka kuizima, kila akitafuta hapaoni. Akapiga simu kwa supplier kuomba msaada. ''halo... nimeunua mashine.... ni nzuri sana... je unaichomoaje toka kwenye chuchu za ng'ombe?''

Supplier akamjibu, ''oh, hiyo ipo automatic inajizima baada ya kupata galoni mbili za maziwa.''

Mama kujifungua

Dokta mmoja alipata dharura. Akaenda alipopigiwa simu, kufika akakuta mama mjamzito akikaribia kujifungua.

Hapakuwa na mtu hapo nyumbani zaidi ya huyo mama na mtoto, na umeme ulikatika. Dokta wakati anashughulika kuzalisha akamuomba yule mtoto wa miaka 6 amsaidie kumulika na tochi.

Baada ya mama kujifungua dokta akamuuliza mtoto, ''unasemaje kuhusu mtoto?''
Kale katoto ka miaka 6 kakajibu, ''mfinye akome, aliingia kufanya nini humo?''

Mtoto alipoona

Siku moja mtoto alimuona mama yake akiwa karibu kujifungua. Alipoona nywele akauliza.

Mtoto: Mama, nini hiyo katikati ya miguu yako?
(Akimaanisha nywele)
Mama: (Akamjibu kwa mshangao) ni brush ya kufulia nguo.

Baada ya muda dokta alizinyoa zote.
Mtoto aliporudi akauliza tena, ''brush imeenda wapi mama?''
Mama akajibu, ''nimeipoteza mwanangu.

Siku chache mtoto akamfuata mama yake, ''mama.. mama njoo, nimeiona brush yako anayo house girl anamsafishia baba uso..."

Baada ya shughuli

Mwanaume mmoja baada ya shughuli na mwanamke aliemuopoa, aliangalia mule chumbani kwa yule mwanamke akaona picha. Akauliza:

Mwanaume: Huyu mumeo kwenye picha? (huku akiwa na woga).
Mwanamke: Hapana.
Mwanaume: Je, ni mchumba wako?
Mwanamke: Hapana.
Mwanaume: Sasa ni nani huyu kwenye picha?
Mwanamke: Ni mimi kabla sijafanyiwa upasuaji (operation).

Sunday, July 25, 2010

Duma

Jamaa mmoja alikua anaangalia kipindi cha wanyama. Akamuona Duma (chetah) anamfukuza swala akasema ''khaa, huyu myama ana kiiimbia. Mi akinifukuza wala sikimbii, maana atanikamata tu ya nini nijichoshe wakati kifo kipo palepale.''

Fumanizi

Mwanamke mmoja wakati yupo na kibwana cha nje. Ghafla mumewe akarudi. Hivyo akamua kumpaka unga yule bwana wa nje. Halafu akamwambia agande kama sanamu.

Mume alipoingia akauliza, ''hii sanamu ya uchu umeitoa wapi?'' mke akajibu 'nimeletewa na rafiki yangu.'
Mume akauliza tena, 'mbona naniliu yake kama ina...' (huku akinama kuichungulia)
ndipo jamaa (sanamu akasema) ''oya tuheshmiane''

Maktaba

Dada mmoja alienda maktaba alipofika akamuuliza mhusika pale maktaba 'nimekuja kumuonda daktari.'

Mhusika wa maktaba akajibu huku akimshangaa kimoyo moyo ''dada hapa ni maktaba''
Ndipo yule dada akauliza kwa kunong'ona ''oh, samahani, nimekuja kumuona daktari.''

Nimemfundisha

Mwanamke mmoja akimusimulia shoga yake ''mwenzangu si nimemfundisha mume wangu kuchoma mishkak pale nyumbani chini ya mti?''

Rafiki akauliza, 'kulikoni?'
Manamke akajibu, ''si mishkaki yote inaishia kumpa yule mwanamke upande wa pili.''
Rafiki: Mishkaki ijayo ipakae chroloqin...

Mbele ya kioo

Mwanamke mmoja alimkuta mumewe yupo mbele ya kioo kikubwa akila chakula akiwa hajavaa nguo kabisa.

Mkewe akamuuliza kulikoni? Jamaa akajibu ''naangalia kama napungua, nimepunguza kiwango cha kula''

Malalamiko

Mwanamke: Mume wangu kila nnachompikia anasema sio kizuri.
Rafiki: Umewahi jaribu kitabu cha mapishi?
Mwanamke: Hapana sijajaribu je kinapikwa kwani?

Kasuku wawili

Kasuku wawili kwenye kitabu cha hadithi wakiongea. ''Nimechoka kuishi kwenye hiki kitabu'' mmoja alimwambia mwenzake.

Kasuku mwenzake akamjibu ''mimi nasubiri leo akifika ukurasa nliopo napaa zangu.''

Baba, mama, mtoto

Baba, Mama na mtoto wakiwa mezani wanakula chakula cha jioni. Ndipo mtoto aliponena jambn, ''baba, baba... kitanda chenu kina sifa.''

Baba: Kwanini unasema hivyo mwanangu?
Mtoto: Baba wewe ukisafiri kinapiga kelele usiku kucha.

Mshahara

Jamaa mmoja akimuambia rafiki yake. ''Ndugu yangu... Mimi nadhani mshahara wangu upitie tbl tu moja kwa moja, maana wife ananinyima raha kabsaaa!''

Haraka haraka

Mfanyakazi mmoja alipokuwa ana mtayarishia mlo wa mchana bosi wake. Kwa vile mda ulikuwa umeenda sana akaamua kuwasha jiko la mkaa, ili ukolee haraka akachukua fani ya stand akaiwasha kuelekezea kwenye jiko la mkaa.

Saturday, July 24, 2010

hospitali

mlevi mmoja alilazwa, alipomuona daktari wa zamu anapita akamuita na kumuuliza ''eti dokta hamna dripu ya bia au whisky hii mlioweka haina fleva kabisa''

Friday, July 23, 2010

Swali darasani...

Mwalimu mmoja darasani wakati anafundisha aliuliza swali ''Nani alihusika kwenye ule mlipuko wa ubalozi wa marekani Tanzania?''

Mwanafunzi mmoja akajibu, ''sio mimi mwalimu, kweli kabisa.''

Hewa

Mtoto: Mama, kwa nini unapenda kupanda kwenye tumbo la baba usiku?
Mama: Ni kwa ajili ya kutoa hewa tumboni ili kuipunguza tumboni mwanangu.
Mtoto: Enhee! Lakini yule mama jirani huwa anaijaza tena kupitia mdomoni kwa baba.

Namba ya baba

Mzee: We mtoto baba yako yupo ndani?
Mtoto: Hayupo katoka.
Mzee: Hebu nipe namba yake nimtafute.
Mtoto: Haya andika T 331...
Mzee: Wee mtoto wee huo ndio mtandao gani?

Kung'oa jino

Jamaa mmoja alienda kung'oa jino. Dokta akamuambia 'lakini nimeishiwa ganzi!'
Kwa vile jamaa jino lilikuwa linamuuma sana akasema, ''bwana ningoe ivo ivo mi silali usiku kabisa.'

Basi dokta akafanya vitu vyake. Baada ya kumaliza akamuambia jamaa ''oh, pole na maumivu, kibaya zaidi nimeng'oa jino silo.'

Mlango dirisha

...alilewa mno, kufika kwake akajisachi mno funguo bila mafanikio ya kuuona.

Akaamua kufanya utundu akaingilia dirishani. Alipofika ndani akaiona funguo ilikuwa kwenye mfuko wa koti.
Si akatoka tena nje kupitia dirishani akaenda mlangoni kufungua na kuingia.

Ndege na msafiri

Jamaa mmoja alikuwa anategemea kupanda ndege kwa mara kwanza. Alikuwa na rafiki yake akamuambia, ''eti Joseph kwani kuna haja ya kwenda mpaka airport? Si zinapitaga hapa juu? Tutapandia hapa hapa si lazima mpaka kule.''

Ugenini

Jamaa mmoja wa kazi za ndani almaarufu house boy, alipoambiwa asisahau kumpa chakula mbwa hali ilikuwa hivi baada ya bosi wake kurudi, ''...nimemtengea mbwa chakula ameshakula ila matunda mpaka sasa hajayala.''

Nido

Mtoto mmoja alizoea sana chai ya maziwa ya unga jioni. Siku moja yalikuwa yameisha wakati alipotaka chai.

Aliambiwa yameisha wala hakuelewa somo, akauliza 'kwani mama yupo wapi?'
Wakamuambia anamnyonyesha mdogo wake.

Mtoto akaenda kwa mama yake, 'mama naomba nikamulie na mimi kidogo nikayaanike nje ninywe chai.'

Mhudumu na mteja

Mteja mmoja kwenye mgahawa alimuita mhudumu na kumuambia akawashe air condition, baada ya mda akamuita akaizime. Kwa muda wa dakika 15 mhudumu alisumbuliwa.

Mteja mwingine akamuliza 'mbona huyo mteja anakusumbua hivyo?'
Mhudumu akajibu, 'usijali hatuna hata hiyo air condition.'

Kwenda hotel

Jamaa mmoja alienda saloon ya kiume, akamkuta mwanamke mzuri na watu wengine wengine.

Akamwambia yule mwanamke 'we dada mzuri unaonaje tuka-enjoy hotel pamoja siku moja'

Mwanamke: Nimeolewa mie.
Jamaa: Si unamwambia mumeo utaenda over time.
Mwanamke: Labda umuambie wewe huyo hapo anaenyoa.

Thursday, July 22, 2010

Mapenzi, Faraja na Imani

Mtoto: Baba, nini tofauti kati ya MAPENZI, FARAJA na IMANI?
Baba: Labda nikujibu kwa mifano utaelewa zaidi....
Mama yako ni mke wangu MPENZI, huyu msichana wetu wa kazi ni FARAJA yangu, halafu nina IMANI kwamba mimi ni baba yako mzazi...!

Maumimivu

Mgonjwa alienda kwa daktari wa meno kung'oa jino.
Mgonjwa: Sh ngapi kung'oa jino?
Dokta: Na maumivu inakuwa 20,000/=. Bila maumivu itakuwa 10,000/=.
Mgonjwa: Oh, ng'oa bila maumivu.

Wakati shughuli ya kung'oa ilipoanza mambo yakawa hivi:

Mgonjwa: Aaagghh...
Dokta: Kumbuka, na maumivu inakuwa 20,000/=

Kazi ngumu

NIMEGUNDUA kaz 5 ngumu ktk dunia;

1-Kumpaka LIPSTIK KUKU

2-Kumpakata TEMBO

3-Kumpenda MENDE

4-Kumvalisha nguo MBU

5-LA MWISHO KUKUSAHAU.

Mke anatafutwa

Jamaa mmoja alibandika tangazo sehemu limeandikwa 'mke anatafutwa.'
Kesho yake alikuta barua nyingi zimeandikwa 'njo umchukue wangu.'

Jamaa na Nyoka wake

Kaka mmoja alikuwa na nyoka wake anae mfuga siku nyingi, siku moja alikuwa amekaa juu ya mti akipunga upepo na nyoka wake. Bahati mbaya tawi alilokalia likakatika.
Sasa wakati anaporomoka amakuambia nyoka wake "nidake... nidake"
Nyoka wake akanijibu "nikudakaje sasa mi nna mikono?"

Gari

Jamaa mmoja alinunua gari kwa mtu akiwa eneo la mteremkoni kidogo, sasa baada ya kukabidhiana kimanunuzi nakadhalika nakadhanika, alipoingia kwenye gari na kuanza kwenda akanenena "doh gari hili zuri kweli halina kelele kabisa"


Baada ya mteremko kuisha likawa haliendi tena, akamuita fundi kwa vile yeye hana mazoea sana na gari. Fundi alipokiuja akafunua boneti la gari kunako injini na kumjibu mwenye gari "unajua ulikuwa ukiendesha bila injini?"

Changudoa

Polisi wawili walitibuka siku hiyo wakaanza kamata kamata vyangudoa wanaouza miili yao kwa ngono. Walipofika kwa mmoja wao akawajibu hivi "mimi siuzi ngono... nauza kondom na naruhusu majaribio kwa atakaenunua kila kondom"

Chooni

Jamaa mmoja aliingia chooni (cha kike) ni choo cha kukaa na akukuta kakuta kuna karatasi kimeandikwa kaa chini ukojoe. Na yeye si akakaa chini kwenye sakafu kisha akanza kukojoa akilenga tundu la choo cha kukaa "huku akisema sasa haya masharti gani jamani kha!!?"

Kurudi toka shule

Mtoto mmoja aliulizwa na mama yake"
Mama: Mbona leo umerudi mapema sana toka shule?
Mtoto: Nilikuwa wa kwanza kujibu swali leo.
Mama: Swali gani hilo?
Mtoto: Nani amemrushia ufuti mwalimu mkuu?

Gazeti

Mtoto mmoja alitumwa kwenda kununua gazeti la tarehe kumi. Aliporudi akamuambia mjomba wake "mjomba nimekosa gazeti la tarehe kumi, hivyo nimenunua ya tarehe tano mawili"

Wednesday, July 21, 2010

Hii balaa

''Baba hivi kwa nini kila ukirudi nyumbani ghafla yule anko jirani yetu anatokea dirishani kwenu na sio mlangoni?'' mtoto alimuuliza baba yake.

Pistol

Mtoto alimkuta baba yake akisoma gazeti. Akitokea shule na kumkuta baba na kumuambia ''baba enhe chukua pistol yako nimeshamaliza kazi yake kuna mtoto alikua ananisumbua shule.''

Pizza

Jamaa alienda nunua pizza... Akaulizwa. ''je tukate kate vipande 6 au 12?''
Jamaa akajibu, ''nikatie vipande 6, 12 ntashindwa kumaliza.''

Samaki na mvua

Samaki mmoja akimuambia mwenzake baada ya mvua kuanza kunyesha, ''rafiki yangu twende tukajifiche kwenye pango tutalowa''

Mda wa kula

Mtoto alianza kuongea wakati anakula na mama yake.
Mama yake akamkatisha, ''Nyamaza usiongee wakati wa kula sio tabia njema mwanangu, utaongea baada ya kula.''

Baada ya kula mama yake akamuuliza, ''enh, ulikuwa unasemaje mwanangu?''
Mtoto akajibu, ''Usijali nilikua nataku kukuambia kuna mende kwenye chakula, ila umeshamla.''

Vegeterian

Jamaa alimuuliza mwenzake wakati wapo restaurant ''umekuwa vegeterian kwa sababu unawachukia wanyama?''
Mwenzake akamjibu, ''no, kwa sababu sipendi mimea.''

Babu

Mtoto mmoja akimuambia mama yake, ''mama kwani babu ananyonya mpk leo?"

''Hapana mwanangu vipi?'' mama aliuliza.
Mtoto akajibu ''nimemuona anamnyonya mziwa ya mama Jesca yule jirani yetu.''

Dokta wa meno

Dokta wa meno alimuuliza mgonjwa wake.
Dokta: Unaweza kunisaidia?
Mgonjwa: Kwa lepi dokta?
Dokta: Umeona hiyo foleni ya wagonjwa hapo nje? Nataka upige kelele za juu za maumivu mpaka wasikie...
Mgonjwa: Kwa nini?
Dokta: Nna kipindi saa nne asubuhi DStv sitaki kukikosa.

Tuesday, July 20, 2010

Mwanamke dukani

Mwanamke alipokuwa dukani akanena ''nisaidie mume wangu awe-attention nami, una perfume yenye harufu kati ya Tv au computer?''

Kwenye daladala

Mwanamke alipanda daladala driver akanena ''huyu mtoto uliembeba ni mbaya sijapata ona.''

Mwanamke akapanda na kwenda kukaa. Kisha akamuambia jirani yake kwenye basi ''dereva amenitukana. Jamaa akamuambia ''mlete huyu ngedere wako nkushikie ukamshughulikie.''

Ahadi

''Nilipofika nyumbani usiku wa jana mke wangu akaniambia nimpeleke sehemu expensive (ya gharama)'' jamaa akimuambia rafiki.

Rafiki: Ukampeleka wapi?
Jamaa: Nkampeleka petrol station...Baba mmoja alichelewa kumpeleka mwanae shule, hivyo akawa anaendesha gari kasi kidogo mpaka akavuka taa nyekundu.

Baba: Mungu wangu nimevuka taa nyekundu.
Mtoto: Usijali hata gari ya polisi nyuma yetu imevuka.

Hasira

''kwa nini kila nkikunasa kibao haukasiriki au kurudisha?'' Mume aliuliza.
Mke akajibu, ''nasafisha choo''
Mume: Mh! Ndio inaidiaje?
Mke: Natumia mswaki wako kusafisha choo.

Mlevi- Polisi

Mlevi mmoja alisimamishwa na polisi.
Polisi alipofungua jamaa akaanguka chini. Polisi akamuambia 'umelewa!?'
Mlevi akajibu, 'oh, thank God, nilidhani usukani umepotea...

Kuwahi shule

Baba mmoja alichelewa kumpeleka mwanae shule, hivyo akawa anaendesha gari kasi kidogo mpaka akavuka taa nyekundu.

Baba: Mungu wangu nimevuka taa nyekundu.
Mtoto: Usijali hata gari ya polisi nyuma yetu imevuka.

Chuo - lecture

Wanachuo wakiwa darasani, lecture akanena ''afta 10 Billion yearz jua litaunguza dunia na ndio itakuwa mwisho wa maisha...''

Mwanafunzi mmoja akauliza, ''excuse me Sir, umesema 10 Billions yearz or 10 billion?''
Lecture: 10 billion.
Mwanafunzi: Whew, nilikuwa nimeshakuwa worried.

Chuo - lecture

Wanachuo wakiwa darasani, lecture akanena ''afta 10 Billion yearz jua litaunguza dunia na ndio itakuwa mwisho wa maisha...''

Mwanafunzi mmoja akauliza, ''excuse me Sir, umesema 10 Billions yearz or 10 billion?''
Lecture: 10 billion.
Mwanafunzi: Whew, nilikuwa nimeshakuwa worried.

Chemsha bongo

Mtoto mmoja aliulizwa na mama yake:
Mama: Kama ukila samaki?
Mtoto: It's good for my eyes.
Mama: Kama usipokula samaki?
Mtoto: It's good for the fish.

Darasani

Mwalimu aliwauliza wanafunzi darasani, 'nina machungwa saba nikitoa manne yanabaki mangapi?'
Mwanafunzi mmoja akajibu, 'yapo wapi?'

Bia za bure

Mlevi mmoja baada ya kulewa akadaiwa hela ya bia akajibu 'nimeshakulipa'
Mhudumu akasema 'ok kama umelipa haina shida''

Mlevi alipotoka akamuambia mwingine. Nae alipotoka akamuambia mwingie akanywe za bure.

Huyu watatu alipoingia baada ya mda kidogo mhudumu akanena 'kuna jamaa wawili leo hawajanilipa, atakaeleta ujinga ule tena nampa ngumi ya uso.'

Yule jamaa watatu akamkatisha ''wasikuumize kichwa hao nipe chanji yangu niondoke...''

Happy New Year...

Mlevi:Happy new year everybody.
Mhudumu: Kelele we mlevi, tupo mwezi june bado.
Mlevi: Mungu wangu wife ataniua sijawahi chelewa rudi home maishani.

Monday, July 19, 2010

Kuona mbali

Mzee kaenda hospital kupima macho. Dokta, ''mzee una tatizo la kuona mbali inabidi tukupe mawani.''
Mzee, ''uongo mi naona hadi mwezi, pale karibu?''

Ndoa ilodumu

Wapendanao wawili waliishi kwenye ndoa miaka 50. Watoto 10, wajukuu 20. Mtu mmoja akauliza 'mmewezaje miaka yote hiyo?'
Mke akajibu, 'tulipeana ahadi atae kua wa kwanza kupaki nguo ili tutengane atatakiwa awachukue watoto wote.'

Siku mbili kabla...

Msichana akimuambia mama yake kwenye simu, 'mama... mama mkwe amenunua gauni kama lako utalovaa kwenye harusi yangu.'

Mama: Usijali ntanunua lingine.
Msichana: Lakini mama sa si umetumia gharama halafu usilivae?
Mama: Ntalivaa siku ya rehearsal dinner.

Harusini

Mtoto mmoja alihudhuria kwa mara ya kwanza harusi. Kaka yake akamuuliza 'mwanaume anaoa wake wangapi?'

Mtoto: 16.
Kaka alishangaa jibu la haraka hivyo akauliza: 16? Kwa nini?
Mtoto: 4better, 4worse, 4rich and 4poor.

Kutoelewana

Siku moja mke na mume walikuwa hawaonge na kati yao.
Mume akamuandikia kiujumbe mkewe 'niamshe saa 11 alfajiri'

Mume akaamka saa 3 asubuhi. Na hasira juu. Na kujikuta keshachelewa ndege.
Juu ya meza akakuta kikaratasi kimeandikwa 'ni saa 11 alfajiri amka.'

Kipofu

Kipofu mmoja aliingia supermarket. Akawa anapita huku na kule.
Mhudumu akamfuata, 'Ndugu nikusaidie nini?'

Kipofu akajibu, 'usijali, nipo okey. Am just lookin around'

Mambo ya ulaya

Mswahili mmoja alienda nje ya nchi. Sasa siku moja alishuhudiwa akitoka toka sana nje kwenda kwenye mail box (sanduku la barua) nje ya nyumba aliyofikia.

Jirani aliekimuangalia akamuuliza, 'inaelekea una barua muhimu kweli unaisubiria?'
Akajibu: Hapana nafanya kazi kwenye kompyuta sasa inaniambia ''you've got mail'' mara kwa mara.

Vivulana viwili

Vivulana viwili vilienda kando kando mwa mto. Mara wakamuona wanamke uchi akioga. Mmoja akakimbia kwenda kujificha. Mwenzake akamuuliza 'unakimbia nini?'

Akamjibu, 'mama aliniambia nikimuona mwanamke uchi ntageuka jiwe na nilishaanza sikia kitu kigumu mwilini mwangu.'

Sokoni

Mwanamke mmoja wakati anatoa pesa kwenye pochi bahati mbaya/nzuri muuza nyanya akaona rimoti.

Muuza: Naona unatembea na rimoti dada ya tv kulikoni?
M'ke: Mume wangu amekataa kunisindikiza hii ndio dawa yake.

Talaka

Mwanamke mmoja alienda kwa mwanasheria kwa lengo la kutaka talaka.

M'sheri: Nikusaidie nini?
M'ke: Nahitaji talaka.
M'sheria: Kwa kigezo gani?
M'ke: Sidhani mume kama wangu ndio baba wa mtoto wangu.

Mama wa kishua

Mama mmoja wa kishua (mambo safi) alienda jifungua hospitali kubwa ya hali ya juu. Baada ya kujifungua daktari akanena baada ya kujifungua:

Daktari: Nna jambo nataka kukuambia kuhusu mwanao.
M'ke: What's wrong doctor?
Dokta: Mwanao has both male and female parts.
M'ke: Oh my God, unamaanishe he has a p***s and a brain?

New place

Kijana mmoja akimsimulia rafiki yake kazini. 'nimegundua chimbo moja (guest house) wanakupa ofa nzuri kweli ukiwa mteja wao mzuri'

Rafiki: Dah, nani kakuonyesha hilo chimbo?
Jamaa akajibu: Mke wangu.

Baba muoga

Watoto wawili:
Wa1: Baba yangu ni muoga usiku kulala peke ake. Anamchukua boby wetu (mbwa) amlinde chumbani.
Wa2: Baba yangu muoga mpaka mama akienda shift usiku anamchukua m'ke wa jirani awe nae usiku.

Ubungo

Mzee mmoja aliendesha gari yake toka mkoani mpaka Dar es Salaam. Alipofika jijini akaenda na gari yake mpaka ubungo - standi ya mabasi ya mkoani. Akaipaki gari yake, kisha akapanda taxi.
''kichwani akijua kua magari toka mikoani hayaruhusiwi kutembea Dar''

Mtoto na puto

Mtoto mmoja akikimbilia ndani baada ya kuona baba yake keshaondoka kwenda kazini. Mlangoni akakutana na mama yake:

Mama: Unakimbilia wapi?
Mtoto: Si kuangalia suruali ya baba.
Mama: Ina nini?
Mtoto: Kama na leo ntakuta puto lingine refu refu ivi linamafuta mafuta (condom).

Mume akiaga

Mwanaume mmoja akimuambia mkewe pembezoni mwake kitandani hospitali alimolazwa.

''Mke wangu nina machache ya kukuambia kabla sijafa, nimetembea na dada yako, best yako na rafiki yako'' mume alinena.

Mkewe akamjibu, ''najua yote, we pumzika sumu ipafanye kazi yake.''

Soseji... (wakubwa tu)

Waskhaji wawili walikuwa na elfu mbili tu na pombe wanaitaka. Mmoja akaichukua na kuingia duka la soseji akaitumia yote wakaanza safari ya bar.

M: Ona sasa umetumia buku mbili yote hata soda hatupati
N: Tulia kijana nna plan kichwani we pata bia tu. Wakaendelea tu pata bia zao.

Muda ukafika jamaa akaitoa soseji na kuiweka ilipo zipu ya suruali na kumuambia ,wenzake ajifanye anai... Mhudumu alipowaona akawatimua.
Wakafanya hivyo kwa bar takribani saba huku wakianza kulewa.

M: Aisee mimi nimechoka sasa, mdomo na magoti pia.
N: Unafikiri mimi je... Nimechoka pia ile soseji tumeipoteza tangu bar ya tatu.

Nasikitika

Jamaa mmoja alikuwa akiongea na mwenzake kuhusu jambo ambalo limemkuta jirani yake.
'Ndugu yangu namsikitikia na kumhurumia rafiki yangu si wametengana na mkewe' alinena jamaa.

Mwenzake akamuuliza: Enhe imekuwaje tena?
Jamaa: si wameagawana nyumba, yeye amepata nje mkewe kapata ndani.

Bibi n a Mjukuu

Mjukuu akimuuliza Bibi yake kipenzi:
Mjukuu: Kwa nini hunywi tena chai siku hizi?
Bibi: Mjukuu wangu tangu tea bag inikabe kooni sina hamu tena...
Mjukuu: Hee bibi ulikula...

Ubongo

Ubongo Uliingia Bar na kuagiza bia, Mhudhumu akamuambia "siwezi kukuhudumia."
Ubongo ukamuuliza mhudumu "kwanini usinihudumie?"
Ndipo Mhudumu akajibu "tayari umeshatoroka kwenye kichwa cha mtu"

Sunday, July 18, 2010

Ugomvi

Mke akimuambia mumewe ''mume wangu wameanza kugombana majirani zetu, wameanza kutupa vitu nje''
Mume akamjibu: Wakianza kutupa TV na friji nistue.

Trafiki polisi tena...

Askari mmoja wa barabarani alikuwa kazini kama kawaida yake, jioni yake alikuwa na safari ya kwenda kwa wakwe zake. Basi kila alipoiona gari alisimamisha na kutafuta kosa ili kidogo dogo kipatikane (pesa).

Akamsimamisha mzee mmoja wa makamo, baada ya maongezi na faini alolipa yule mzee muda wa kuondoka kwenda nyumbani kujiandaa ukafika.

Jioni wakati yupo sebuleni akawa anamsimulia mchumba wake jinsi alivyosumbuana na madereva siku nzima ya leo mara akaingia baba mkwe sebuleni, yule trafiki kumuangalia anamuona yule mzee aliemtoza faini...
Aliishiwa maneno...

Omba*omba na Mlevi

Mlevi mmoja alikuwa pombe nyingi kichwani wakati anarudi nyumbani akamuona ombaomba kipofu.
Akampatia elfu kumi. Hatua chache akkamua ageuke aangalie kama kweli yule ombaomba ni kipofu. Akamuona jinsi anavyoihifadhi pesa si kipofu akarudi.

''Wewe kumbe sio kipofu eenhe?'' Mlevi aliuliza.
Jamaa akajibu: Mimi sio kipofu namshikia rafiki yangu yeye ndio kipofu kaenda msalani kidogo.
Mlevi: Sasa mbona una...
Jamaa: Hata mimi nina ulemavu ni kiziwi, hata sikusikii kabisa.
Mlevi: Ooh pole sana chukua na hii elfu kumi utampa rafiki yako.

Maisha na watoto

Wanaume watatu walikuwa wakizungumzia kuhusu watoto wao wa kiume.

Wa kwanza: Mwanangu wa kiume ana mafanikio sana ni wakili, ana nyumba ya kifahari sana.

Wa pili: Mwanangu ni Mkandarasi, ana mafanikio sana ana gari la kifahari sana.

Wa tatu: Mwanangu mimi ni shoga, imebidi nikubali matokeo, na anaishi na wenzake mmoja ni mwanasheria mwingine ni mkandarasi.

Gesti hausi

Jamaa mmoja alienda wilaya fulani, nyumba ya kulala wageni aliyofikia aliikuta bado haijafungwa umeme (ikimaanisha wilaya husika haina umeme bado).

Alipoingia chumbani akaikuta kandiri (taa ya chemli) ndipo alipomuuliza mhudumu baada ya kuona kioo chake kimejaa rangi nyeusi ya moshi uliogandia.

''Dada hii kandiri ndio dizaini yake kuwa na tinted au?'' (toka lini taa ya chemli ikawa na tinted?).

*cheka unenepe*

Godoro la kisasa...

Jamaa mmoja alimuagiza ndugu yake amletee godoro lenye maji ndani maana alichoka kulala kwenye magodoro tuiliyoyazoea wengi ya sponch.

Baada ya wiki kadhaa yule ndugu yake akamtaharifu ndugu yake aliepo Tz alieagiza godoro ''ndugu yangu godoro nimekosa labda mpaka mwezi ujao, kwa wakati huu we kalale kwenye swimming pool na shuka lako.''

Kwenye ndege

Mtoto mmoja kwenye ndege akamuuliza mama yake ''kwa nini ndege zote zinapita juu?''
Mama akajibu: Zimetengenezwa mfano wa ndege viumbe hai ili zipite juu mwanangu.

Mtoto: Na meli nazo ivo ivo?
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto: Mbona baba hajaumbwa kama wewe hana manyonyo kama hayo ya kwako?

Chini kidooogo.

Jamaa mmoja alikua uongo jadi yake, siku moja wakati yupo ulaya akawa anawasimulia kuhusu Afrika wazungu fulani aliokua nao.
Akawa anawaambia kuwa mawingu ya huku Afrika yapo juu sana kuliko Ulaya.

Mzungu mmoja akawa anabisha hapana haiwezekani basi jamaa akasema ''basi chini kidoogo''

Pembezoni kulikuwa na m-kenya ili kumuonyesha kuwa amemstukia kuwa muongo nae akatoa kibomu chake ''kwetu sisi wanawake wanazaa kupitia kitovu''
Jamaa: Aaaa! Haiwezekani.
M-ghana akamjibu: Basi chini kidoogo.

Redio kizungu

Kaka mmoja wakati anasikiliza BBC idhaa ya kiingereza akiwa na mwenzake, aslisikiliza radio uzalendo ukamshinda kwa vile kizungu/kimombo hakipandi.

Akamuuliza mwenzake ''eti hawa jamaa kwenye radio hawana zile zinaitwa 'subtitles?' enhe?''
Subtitle - maandishi tafsiri mfano kwenye sinema.

Saturday, July 17, 2010

Namba ya simu

Kaka mmoja kwenye dala dala alikutana na mrembo mzuuri. Baada ya maongezi kadha wa kadha yule dada wakati anashuka akakumbuka kuomba namba ya simu.

Yule dada akampatia namba tatu za simu na kumfafanilia hivi: ''just incase ukinikosa kwenye namba ya kwanza ambayo ni ya baba nipigie kwenye ya pili ya mama na ya tatu ni kaka yangu.

Maktaba

Jamaa mmoja alipiga simu na kuuliza ''muda gani mnafungua maktaba?''
Akajibiwa: Saa tatu kamili asubuhi, kwa nini unanipigia usiku wote huu kuuliza hilo? Kuna nini mpaka unataka kuingia saa tatu kamili asubuhi.

Aliepiga simu akajibu: Nani amekuambia nataka kuingia? Naulizia muda ili nijue nataka saa ngapi humu maktaba.

Anatafutwa

Polisi wawili walifika sehemu moja wakiwa na picha ya mtuhumiwa wanae mtafuta.
Wakamuuliza yule mtoto wa miaka minne, ''umemuona huyu mtu? (wakimuonyesha picha) sisi polisi tunamtafuta?''

Mtoto akawajibu: Sijamuona.
Halafu akawauliza swali papo hapo.
''kwa nini hamkuzuia wakati mnampiga hiyo picha?''

Friday, July 16, 2010

Kinyozi part ii

Kinyozi mmoja alikuwa na kijibanda chake cha kufanyia kazi yake. Siku moja alihamisha ofisi yake na kuipeleka upande wa nyuma ya jengo. Ili asipoteze wateja wake akaacha kibao kinachoonyesha mahala alipo kimeandikwa "Kinyozi alie kuwa ana nyoa mbele sasa anayoa nyuma."

Trafiki, Mume na Mke

Trafiki mmoja alimsimamisha mzee mmoja kwa sababu ya spiidi kali.
Trafiki: Mzee unajua kuwa ulikuwa na spidi kali sana.
Mzee: Hapana askari nilipitiwa tu.
Mke: Mi nimemuambia sana apunguze spidi hakunisikia.
Mzee: Hebu nyamaza bwana.... (akaanza kubwata)

Trafiki: Mzee leseni ya gari imeisha mda wake walijua hilo.
Mzee: Nilisahau kuangalia askari.
Mke: Umezidi nimeimba mwezi mzima hanisikii...
Mzee: Nimezidi nini... (akabwata kama kawaida)

Trafiki akaenda upande wa mwanamke dirishani:
Trafiki: Mama samahani Mumeo huw anakujibu hivi kila siku?
Mke: Hapana mpaka akiwa amelewa.

Mwalimu wa jografia

Mwalimu mmoja wakati anafundisha darasa mambo ya Longitudo na Latitudo aliamua kutoa mafano darasani, "kwa mfano nikiwaambie tukutane wakati wa lunch kwenye degree 23, Dakika nne kaskazini latitudo na degree 45, dakika 15 Mashariki longitudo..."

Mwanafunzi mmoja akajitokeza na kujibu "Nafikiri utakuwa peke yako mwalimu."

Milionea

Milionea mmoja alikuwa na swimming pool nyuma ya nyumba yake, siku moja akaandaa party. N alikuwa na mtoto wa kike aliye singo. Akatangaza "kwa wanaume wote mlipo humu atakeo ogelea kwenye bwawa hili la kuogelea lenye maji baridi sana ntampatia Dola milioni moja au atamchukua mtoto wangu wa kike.

Punde akaona jamaa mmoja keshajitosa kwenye hayo maji, akafurukuta na kutoka baada. Milionea akaongea nae hivi: Vizuri sana , sasa chagua unataka dola milioni moja au mwanangu wa kike?

Jamaa akajibu: Sitaki pesa zako wala mtoto wako, namtaka mshenzi alie nisukumia kwenye maji...

Kinyozi

Jamaa alienda saloon akauli ''baada ya mda gani utachukua?''
Kinyozi akajibu, ''baada ya masaa mawili''
Wiki na mwezi mmoja baadae jibu lile lile.
Kinyozi akatuma mwenzake amfuate jamaa nyuma.
Aliporudi akicheka akajibu baada ya kuulizwa ''ameenda home kwako.''

Enzi zile

Mwanamke mmoja akimuambia mumewe "mume wangu unakumbuka kipindi kile una-propose kunichumbia nilishikwa na furaha nikakaa kimya kwa saa moja nzima bila kuongea?''

Mume akajibu, ''yes nakumbuka, ile saa nzima ilikuwa siku ya furaha sana maishani mwangu.'

(labda mke wake mhh... analopoka mh....)

*cheka unenepe*

Mchumba

Mtoto mmoja wa kike alimpeleka kijana na kumuambia baba ake ''huyu ndio atanioa.''

Baada ya muda baba akamjibu mwanae kwenye faragha. 'huyu ni kaka yako pia.'
Mtoto wa kike akaenda kwa mama yake na kulalamika.

'Mama baba ananiboa, kila mchumba nkimleta ananiambia ni mwanae wa nje.'
Mama akajibu, 'usimsikilize huyo kwanza si baba yako.'

Burger

Kijana mmoja alienda nunua burger. Bahati mbaya akakuta nywele kwenye burger.
Akamuita mhudumu na kumuuliza, mhudumu akamjibu 'unaishangaa hiyo, je ungeagiza donati...'

Ng'ombe kuzaa

Mtoto mmoja aliachiwa namba za simu za dharura awapo peke yake nyumbani.

Siku moja alipoenda mabandani mwa mifugo yao nyuma ya nyumba ghafla akarudi mbio...
Kwenye simu:
Mtoto: Halo... Haloo... Hapo Hospitali?
Hosp: Ndio tukusaidie nini?
Mtoto: Njoeni haraka haraka na ambulance ng'ombe anazaa uku...

Fundi kaja

Siku moja simu iliita mtoto akaipokea, ilikuwa sebuleni mama yake akiwa chumbani.

Kwenye simu alikuwa baba wa huyo mtoto.
Mtoto: ...Shkaamo baba.
Baba: Marhaba, mama yako yupo wapi?
Mtoto: Yupo chumbani mda mrefu anamsimamia fundi wa sinki. Amesema nisimsumbue mpaka fundi amalize. Usiwe na wasi wasi baba leo hatoki.

Umeona nini?

Mtoto mmoja wa miaka miwili aliulizwa na baba yake, ''umeona nini wakati unasafiri mwanangu?'

Mtoto: Meona miti na nyumba ikirudi nyuma na anko nani vile yule eti mama? Alikuwa akimshika mama mashavu mama akawa anainama chini.

Chalinze

Mtoto mmoja alipandishwa basi kwenda Dodoma. Akamuambia kondakta kuwa akifika chalinze amuambie.

Konda akajisahau basi likapita chalinze zaidi ya kilomita 70. Konda ndio akakumbuka. Ikabidi wageuze.

Kufika chalinze wakamuambia yule mtoto 'hapa ndio chalinze' mtoto akashika mfuko wake akipekua pekua.
Wakamuuliza 'hushuki?' akajibu ''mama aliniambia nikifika chalinze ndo nianze kula.''

Chakula moto

Mtoto mmoja alipoona amepakuliwa chakula cha moto kwao, si akaenda kwenye friji. Akachukua barafu na kuweka kwenye chakula...

Ng'ombe na Nyasi

Mtoto darasani aliambiwa amchore ng'ombe anakula nyasi tu. Mwalimu alipouliza wapi ng'ombe akajibu 'amednda kunywa maji'

From: Yunus Mwahu.
*cheka unenepe*

Mtoto - ndege

Mtoto mmoja akisafiri na dady yake. Njia wanayopita ni milimani. Jinsi alivyoiona ikilalamika kupanda mlima ghafla kamuonda ndege anaruka akamuuliza baba yake, 'baba yule ndege nae hachoki kupanda mlima?'

Thursday, July 15, 2010

Kweeenye ndege

Dada mmoja na tiketi yake ya economy class (kajamba nani) iendayo Mwanza akahama na kwenda kukaa first class.

Mhudumu wa kwenye ndege alijaribu sana kumsihi arudi economy class jamaa mbishi...
Alikuja piloti msaidizi mambo yale yale.
Akaja piloti mkuu...
Dada akakubali.

Wakamuuliza umewezaje kumshawishi arudi economy class. Piloti akajibu, ''nimemuambia first class haiendi Mwanza.''

Bosi wa kike

Wanawake wawili walikuwa wakimuona bosi wao wa kike akitoka mapema kila siku kazini.

Siku moja bosi alipoondoka mapema mmoja wa wale wanawake nae akaondoka mapema. Kufika nyumbani akamkuta bosi wake chumbani na mumewe, akafunga mlango asionekane.

Siku ya tatu wakati wa chai mwenzake akamuuliza 'utaondoka mapema na leo'
Akamjibu, ''no no jana kidogo wanibambe''

Baba aikumbuka simu

Baba mmoja aliondoka nyumbani kama kawaida yake, ilipofika majira ya saa tatu asubuhi akajiuliza ''leo hamna alienikumbuka tangu asubuhi'' alipotoa simu ahakikishe akajikuta ametoa remote ya tv.

Mabishano

Jamaa wawili wakitoka bar pombe imewajaa kichwani. Wakaanza bishana '' ule pale ni mwezi'' mwingine akasema ''lile ni jua''

Bahati nzuri mpita njia huyo wakamuuliza 'eti ule mwezi au jua?'
mpita njia akajibu 'samahani mi mgeni hapa'
BREAKIN NEWS, pweza Paul azimia baada ya kuambiwa atabiri ni lini TANZANIA itafuzu na kushiriki KOMBE LA DUNIA.

Vituko vya bar

Siku moja jamaa aliingia bar. Mhudumu akaja 'nikupatie kinywaji gani?'

Yule jamaa akaangalia mule bar na kujibu huku akimnyooshea kidole mtu mmoja alielala kwenye sakafu ''niletee alichokunywa yule alie lala...''

Kwa niaba

Cha pombe mmoja kila akienda baa huagiza bia mbili. Mhudumu siku moja uzalendo ukamshinda. Akauliza ''kwa nini waagiza bia 2 kila ukija?''
Mnywaji: Nilikua nakuja na rafiki yangu, amekufa so nakunywa niaba yake.
Siku chache mbele akaja akaagiza 1.
Mhudumu alipouliza 'kulikoni?'
Mnywaji akajibu: Nimeamua kuacha kunywa.

Nguo ya nani?

Jamaa wa kwanza aliingia bar amevaa fulana nzuri, mhudumu akauliza ''umepata wapi hiyo fulana?''
Akajibiwa "kwa Josh''

Wa pili, akaingia kavaa suruali nzuri. Nae akajibu vivyo hivyo.
Wa tatu, akaingia amevaa viatu vizuri nae vivyo hivyo akajibu.

Akaingia mtu akiwa uchi mhudumu akamuuliza, ''wewe nani unatembea uchi?''
Akajibu ''mimi Josh''

Dawa

Jamaa akiongea na simu. Baada ya maneno mawili matatu aliepigiwa akaulizwa 'kwani upo wapi?' na kujibiwa 'nipo makete'

Mwenzake akamwambia ''oh upo makete! Njoo basi na ka-dawa ka biashara''

Kuhama bar

Jamaa alilewa vibaya akaagiza bia ya ziada mhudumu akamuambia 'umekunywa vya kutosha kapumzike leo nyumbani'

Mlevi akahama bar mambo yakawa vile vile, akaenda bar ingine vile vile.

Akaamua aende kwingine alipofika akanena ''bar hii mbona ipo kimya sana?''
kidogo akaona tv na redio kama vyake nyumbani.

Akamrukia alie karibu yake na kumkwida ''wewe hii tv na redio yangu mmepata wapi?''
Akajibiwa ''baba kwani vipi leo?''
Kumbe kuja kuhamaki aliemkwida ni mwanae, na mahala alipo ni sebuleni kwake....

Kupanda ndege

Jamaa mmoja mara ya kwanza kupanda ndege. Akamuita mhudumu wa kwenye ndege na kumuambia kabla ya kupaa ''samahani, kamuambie pailoti asipite njia ya tazara saizi kuna foleni sana.''

Ova spidi

Traffik polisi mmoja alimsimamisha jamaa mmoja kwa sababu ya spidi kali.

Trafiki: Unatambua kuwa ulikuwa spidi sana?
Dereva: Ndio.
Trafiki: Utalipa faidi kwa hilo...
Dereva: Wewe ukishikwa na tumbo la kuhara utaendesha taratibu ili likuharibie siku?
Trafiki: Hapana, tena hata trafiki akisimamisha sisimami.

Pombe ikikole.

Jamaa jinsi pombe ilivyomkolea akarudi kaunta akamuambia mwezake kwa sauti ya kilevi-levi 'aisee siku hizi watatuua walevi, atm mpaka chooni.'

Mlevi mwenzake akajibu 'oh ile atm ya kondom chooni?'
''haa mi nilijua salio.'' Akanena mlevi wa kwanza.

Ajali

Kulikuwa na mke na mume wakiwa wamepaki gari yao aina ya land cruiser wakawa wapo restaurant.

Ghafla gari isiyo na break ikaigonga gari yao pale nje ikaumia vya kutosha.

Mke kwa hamaki akasema ''oh jamani make-up zangu zipo kwenye gari''
Mume nae ''oh iPod yangu ipo kwenye gari.''

Ajali ya moto

Jamaa mmoja alipigiwa simu na mkewe kumpa taharifa za moto ''mume wangu nyumba imeungua, watoto nipo nao hapa hospitalini wana majeraha ya moto.''

Mume akajibu, ''kreti langu la bia limepona?''

!!...

''mpenzi wangu wewe nikiwa na hela ndio unaonekana, nikifulia unanikimbia. Nnachokupendea wewe huna gharama ndogo ndogo, njoo nikubusu''
Mlevi akiongea na bia yake.

Prado

Baba mmoja akiongea na simu ''....Prado? Na Alterza je? Na je Scania sasa?.....''

Alipomaliza kuongea na simu jamaa aliekisikiliza maongezi akamuuliza ''mzee inaelekea mambo yako mazuri kweli....''

Yule mzee akamjibu ''oh hayo ni majina ya wanangu watatu''

House girl

House girl mmoja alipomaliza haja ndogo akasema kwa sauti 'tayari'
Mama mwenye nyumba akaenda hadi mlango wa bafuni akamuuli house girl wake 'tayari nini?'

House giril akajibu, 'si tayari, baba huniambiaga nikimaliza aje kunisafisha ndo memuambia aje.'

Wrong sms

Jamaa alimtumia meseji rafiki yake kimakosa ikaenda kwa mke wa huyo rafiki yake, imeandikwa hivi ''jana si nimeisahau ile kondom kwenye gari yako?''

Mke wa jamaa akaijibu ile meseji, ''usijali nimeitumia, usimuambie mume wangu.''

!

Mtoto akimuambia mama yake ''mama... mama nimemuona baba nje anatema mate upande wa kushoto halafu anafukia upande wa kulia.''

Mama akamjibu, ''oh no ameshakunywa uji wa mtoto.''
Mtoto alibaki haelewi elewi.

Kifurushi

Kulikuwa na matrafiki polisi walikuwa wakiagiza sana kifurushi cha nyama kwa baadhi ya madereva waendapo na kurudia njia hiyo hiyo.

Siku moja jamaa mmoja alimpatia kifurushi kimefungwa vizuuri hata harufu ya kilichomo haikutoka.

Trafiki alipofika nyumbani akambwagia mkewe '' mke wangu nyama hiyo...''
baada ya mda mkewe akiwa jikoni akamuambia mumewe.
''mume wangu umenichoka kiasi hiki...? Yaani unaniletea kifurushi cha kinyesi....''

Kanda

Kaka mmoja alijiazimisha kanda 'video tape' alipofika kwake aliiweka akawa haoni picha ikicheza.

Akampigia simu na kumuuliza mwenye ile kanda. Baada ya kuielezea kanda aliyoichukua mwenye kanda akamjibu, 'oh hiyo ni head cleaner (kaseti ya kusafishia deki ilochafuka).

Wednesday, July 14, 2010

Maktaba

Kaka mmoja alienda maktaba kurudisha kitabu na malalamiko kwa mtu wa maktaba, ''kitabu nlichoazima jana ovyo kweli nimekirudisha.

Mtu-maktaba: Kwa vipi? Kuna lepi?
Kaka: Kina majina ya waandishi wengi mno.
Mtu-maktaba: Oh, basi wewe ndio utakuwa ndie uliechukua kitabu chetu cha namba za simu (phone book).

Dau

Vijana wawili wakilikuwa wakiangalia habari kwenye tv saa mbili usiku kuhusu mwanaume anaetaka kujirusha toka ghorofa ya saba.

Wa 1: Tuwekeane hela, mi naweka elfu 20 akijirusha yote yako.
Wakakubaliana, matokeo yake jamaa akajirusha na kufa.

Wa 2: Hapana chukua elfu 20 yako.
Wa 1: Kwanini?
Wa 2: Kwasababu habari ya saa moja usiku ilionyesha amejirusha pia.
Wa 1: Hata mi nliangalia huo mda nilidhani asingejirusha tena.

Wajawazito

Wajawazito watatu kwa daktari wakisubiri majibu yao.
Wa 1: Kama ni mjamzito basi atakuwa msichana, kwa sababu mi nilikuwa chini.
Wa 2: Kama ntakua mjamzito basi ni mvulana, kwa sababu nilikuwa juu.
Wa 3: Mh! Kama ntakua mjamzito basi watakuwa puppies (watoto wa mbwa).

Boti

Jamaa mmoja alikuwa anaendesha gari mbele kidogo akakutana na gari ingine inavuta boti kwenye tela lake.

Kwa vile yule wa kwanza alikosa kosa igonga ile boti, akapunguza mwendo na kumujambia yule akieikokota boti na gari yako ''bahati yako sijui kuogelea ningekufuata ulipo nikufundishe adabu...§&**€"

Ndege amekufa

Jamaa mmoja alimwambia mwenzake, ''mwangalie yule ndege amekufa maskini.''
Mwenzake akamuuliza ''wapi?'' huku akiangalia juu/angani.

Kwenye ndege

Siku moja kwenye ndege (boeng) pailot alitangaza kuwa injini moja imekufa lakini zipo zingine tatu itatuchukua saa moja angani.

Nusu saa baadae akatangaza tena injini ingine imekufa na kusema tunazo bado zingine mbili itatuchukua nusu saa angani.

Abiria mmoja akasema kwa mwenzake 'kama zikifa na hizo mbili tuwepo huku angani all day.'

Gari ya polisi

Mama mmoja alikuwa speed akaipita gari ya polisi. Akamwambia mwanae aangalie nyuma kama gari ya polisi inawafuata.

Mtoto akajibu, ''ndio inatufuata!''
Mama: Je wamewasha taa zao za polisi?
Mtoto akajibu tena: Yes...No...Yes...No...Yes...!!
Kama ujuavyo king'ola...

Cha pombe

Cha pombe mmoja alienda bar, pale kaunta akaagiza vipimo viwili vya wiski. Alipomaliza akafungua diary yake na kuangalia kisha aka-oda tena wiski vile vile mpaka mara tatu ikafika.

Mhudumu akauliza, 'unaangalia nini kwenye diary kabla ya kuagiza wiski tena?'

Cha pombe akajibu, ''kuna picha ya mke wangu, namuangalia nkiona ameanza onekana mzuri tu najua ndio mda wa kurudi nyumbani.''

Jeans ya blue

Mwanamke mmoja akimuuliza mumewe, ''mume wangu hii jeans inanitoa bambataa enh kama nyumba yetu?''
Mume: Nyumba yetu si ya bluu lakini.

Mlevi akienda nyumbani

Mlevi mmoja akiwa chakari akielekea nyumbani, njiani alikutana mpita njia akamuuliza ''...hizi ngazi wamejenga saa ngapi mbona nyingi na asubuhi hazikuwepo?''

Mpita njia akamjibu, ''mzee wangu unapita juu ya reli si ngazi.''

Adhabu darasani

Hii ni true story wakati nasoma.

Mwalimu mmoja wa kemia wakati anafundisha darasani aliwasikia wanafunzi wawili wakinong'ona.

Akawaita na kuwapigisha magoti mbele ya darasa. Akawa anaendelea kuandika ubaoni, alipogeuka akamfuma mmoja wa wale wanafunzi kaweka mikono yake mfukoni huku kapiga magoti pale mbele.

Mwalimu kwa sauti ya hasira na ukali akamuambia yule mwanafunzi mmoja mbele ya darasa 'wewe toa mifuko mkononi'
darasa lilicheka loote. Mpaka mwalimu mwenyewe akacheka akaamua awasamehe.

Baiskeli

Mtoto mmoja akimuambia baba ake, ''baba nlivokua mdogo sana nilikuwa nasali nipate baiskeli sijafanikiwa. Sasa ntaiba na kuomba sala ya msamaha.

Mume na Mke

Mume: Mke wangu nikifa utapata mwanaume mwingine kama mimi.
Mke: Nani kakudanganya nataka mwanaume kama wewe?

Mfanyakazi mpya

Jamaa mmoja alipata kazi ofisi fulani. Mwajiri wake akampa barua aipeleke ghorofa ya nne.

Alipoifika kwenye ngazi akajituma aichungulie, alipoisoma akakuta imeandikwa 'you're our kind person. Report to the fifth floor Personnel Office.'

Mbwa anang'ata?

Mtoto mmoja alikuwa na mbwa, mpita njia akamuuliza yule mtoto, 'mbwa wako anang'ata?'
Mtoto: Hapana hang'ati.
Dakika chache mbwa akamng'ata jamaa.
Akauliza 'we si ulisema hang'ati?'
Mtoto: Ndio, lakini huyu si mbwa wangu.

Dinner

Siku moja wakati wanapata dinner mke alimuuliza mumewe... ''uliponioa ulikuwa unanilisha kipande kikubwa cha nyama, wewe unajilisha kidogo. Siku hizi mie kidogo wewe kikubwa, hunipendi tena siku hizi?''

Mume akajibu, ''unapika kitamu mno siku hizi.''

Tuesday, July 13, 2010

Mtoto na shule

Mtoto mmoja akimuambia mama ake ''mama kwani we una miaka mingapi?''

Mama akajibu, 'ni mingi tu mwanangu. Kwani vipi?'
Mtoto: Si nataka nijue imebaki mingapi nikufikie tu....

Polisi

Polisi mmoja aliulizwa kwenye mtihani wa mwisho mwisho kabla hajaapishwa 'utafanya nini pindi ikatokea umemkamata mama yako mzazi?'

Yule polisi akajibu, 'ntamuamkia'

Usingizi

Jamaa mmoja alienda kwa dokta, ''dokta me nashindwa kabisa kupata usingizi. Mbwa wangu nyumbani ana bwaka saana usiku kucha.''

Dokta, ''oh, tatizo lako ntakutatulia. Chukua dawa hizi za usingizi zitakusaidia sana umeze kila siku wakati wa kulala.''

Siku mbili baadae jamaa akaenda kwa dokta, ''dokta nashukuru sana umenisaidia sana.''

Jamaa: Sisikii tena kelele za mbwa wangu.
Dokta: Umemeza kama nlivyokuelekeza?
Jamaa: Hapana, nimekuwa nikimpa mbwa ili alale usiku.

Mwembamba

Kaka mmoja mnene alikutana na kijana mmoja mwembamba kweli kweli akamwambia ''laiti kama watu wangekuona wangehisi dunia yote ina njaa.''

Mwembamba akajibu, ''laiti dunia nzime wangekuona wangesema umenisingizia''

Siti...

Kaka mmoja wakati anaingia 'movie theatre' akamuuliza ''dada mbona una ticket mbili? Yupo wapi mwenzako?''

Dada: Anha nipo peke yangu, nimekata ticket mbili kwasababu viti ya ukumbi huu vidogo sana hivyo nkikaa kwenye viwili ndo ntaenea.''

Yule kaka akamjibu tena yule dada ''mbona tiketi zako zaonyesha kiti namba 31 na 43?''

Watoto na tv...

Siku moja baba na mama walitoka kwenda kuoga wakawaacha watoto wakiangalia tv.

Watoto wakachukua 'video tape' juu ya tv na kuiweka kumbe ni ya x. Wakawa wanapiga mayowe, baba akamwambia mama yao atoke aende akaangalie kulikoni.

Mama akavaa khanga kufika sebuleni akakuta ile x akavua khanga na kuifunika tv, watoto wakazidi kupiga mayowe...

Baba akaona nae aje, akavaa taulo. Kufika sebuleni na yeye akavua taulo ili amfunike mama. Watoto wakapiga kelele zaidi...

Interview

Jamaa mmoja alienda kwenye usahili (interview). Alikuwa msumbufu sana kwenye maisha yake ya ndo.

Alipofika kwenye interview ilipofika zamu yake alipoingia ile meza ya usahahili alikutana na watu wanne, wote wanawake, mbaya zaidi hao wanawake alowakuta wote walishawahi kuwa wake zake....

Monday, July 12, 2010

Uwiii

Huku akionyesha katika ramani ya dunia iliyobandikwa ukutani, mtoto wa miaka mitano alimuuliza baba yake:
Mtoto: Baba eti Brazil iko wapi?
Baba: Muulize mama yako kwa maana yeye ndo mwenye tabia ya kufichaficha vitu humu ndani!!!

Rufaa

Nesi mmoja alipompima mgonjwa mmoja kijiji fulani akagundua kuwa 'option' iliopo ni kumuandikia rufaa mgonjwa yule apelekwe hospitali kubwa.

Ndugu wa mgonjwa wakaja na jogoo ili wampatie nesi aahirishe ile rufaa.

Chanjo

Mtoto mmoja kwenye shule ya 'no swahili speaking' alichelewa na kuulizwa na mwalimu.

'where have you been?' Mwalimu aliuliza.
Mtoto alitoka kwenye pepopunda chanjo na kimombo hakipandi vizuri. Akajibu hivi, ''teacher i've been at hospital for wind-donkey-vaccination.''

Pombe bwana...

Baba mmoja alirudi kwake akiwa chakari kwa pombe.
Alipofika kwake mkewe akamfungulia mlango punde jamaa akatapika.

Alipoangalia pale alipotapikia akaona mbwa wake mdogo aliemtapikia pia kisha akaongea kilevi levi''huyu mbwa sikumbuki kama nilimla pia....''

Watoto wanne

Vijana wanne walipanga kumnunulia mama yao zawadi mwenye umri mkubwa sana.
1: Mi nitamjengea nyumba.
2: Mi nitamnunulia prado na dereva.
3: Mi ntamnunulia biblia.
4: Mi ntamnunulia kasuku awe anamwimbia na kumpa kampan.

Siku chache baadae bibi akawashukuru wanae wote na kumuambia yule wa 4 ''mwanangu nashuru sana yule kuku alikuwa mtamu sana'

Hii kali

Hii kali....
Jamaa mmoja alimuona mwanaume akisali kwa kuguswa sana juu ya kaburi.
Akaenda na kumkuta akisali yule jamaa 'Kwanini umekufa? Kwanini umeamua kufa?

Jamaa akamuuliza, ''kaka samahani... Nimeguswa sana na unavyo... Je ni nani aliekufa? Mtoto? Mke??

Jamaa makaburini akajibu ''ni mume wa mke wangu.''

Mtihani+kibomu

Mwanafunzi mmoja darasani kwenye mtihani alistukiwa na mwalimu aliekisimamia mtihani.

Wakati mwalimu anamfuata mwanafunzi akafinyanga finyanga ile karatasi yenye majibu 'kibomu' akakitupa nje.

Mwalimu akakifuata nje ili achukue hatua. Alipofika nje akakikuta kile kikaratasi kipo 'plain' kumbe chenye majibu alibaki nacho ndo akakificha vyema...

Mkalimani

Jamaa alikuwa anaangalia mechi kwenye tv. Akaomba apatiwe wa kumtafsiria kizungu kinachotangazwa. Akapatiwa.

Tena hapo hapo akaomba mtafsiri mwingine atakaekua akitafsiri mpira unavyochezwa uwanjani....

Bi. Harusi

Siku kadhaa kabla ya harusi bi. harusi alikuwa hataki aonekane/waonekane kama ni wanafungate (honeymooner) watarajiwa.

Hivyo akamuambia mumewe wajifanye kama wameshaoana mda mrefu sana mbele ya macho ya watu.
Mume mtarajiwa akajibu ''oh, okey. Beba begi langu languo''

Mlo wa jioni

Josh alialikwa mlo wa jioni na rafiki yake. Rafiki yake akawa kila akitaka kitu akawa anamuita mkewe 'mpenzi' 'laaziz' nk nk

Josh, 'wow! Ndani ya miaka yote ya ndoa yenu bado mnaitana hayo majina mazuri mazuri, inapendeza sana.'

Mwenyeji akajibu, ''kiukweli nimesahau jina lake.''

Mbwa

Mwanamke alikua akiendesha gari upande wa juu, mwanaume upande wa chini kwa staili ya kupishana.

Mwanamke akamwambia yule mwanaume ''mbwa''
Mwanaume nae akafungua kioo na kujibu, ''chizi wee''

Hatua chache yule mwanaume akagonga mbwa na gari aliyokiendesha.

Picha

Mama mmoja alimkuta mwanae amepiga magoti chini ya picha kubwa ya ukutani akiichungulia kwa chini/nyuma.

Mama yake akamuuliza ''unafanya nini?''
Mtoto akajibu, 'namchungulia huyu mtoto nione kama na leo umesahau mvisha chupi kama jana.''

Sunday, July 11, 2010

Kifo

Mapacha wawili wakiongea na mchungaji walipofika ofisini kwake.
Pacha: Mama yangu amekufa juzi, na hata huyu pacha mwenzangu nae mama yake amekufa juzi...

Mbio mbio

Kulikuwa na vijana wanne wamekaa mwenzao mmoja alikuwa amefungwa P.O.P mguuni akawa anasinzia pale walipokaa.

Wale wa3 wakamuona akisinzia, wakajipanga kumshtua...
Wakahesabu kwa sauti ya chini sana 1, 2, 3 halafu wakakurupuka mbio na ghafla kama kuna tukio fulani...
Yule mwenye p.o.p alistuka na akikuta yupo juu ya mtu kitaambo, wenzake walicheka sana maana kushuka ilibidi aombe msamaada.

Ndoa ndoa

Kabla ya ndoa (soma juu kwenda chini)
Me: Ndio. Nimesubiri sana.
Ke: Unataka mimi nikuache?
Me: Hapana. Wala usithubutu hilo.
Ke: Unanipenda?
Me: Ofkoz.
Ke: Umewahi tembea nje?
Me: No, kwa nini kwanza unauliza?
Ke: Utanibusu?
Me: Ndio.
Ke: Utakuja nipiga?
Me: No way, sio type hiyo mimi.
Ke: Utaniamini?
Me: Ndio.
(Sasa soma toka chini kwenda juu).

Peponi

Mijamaa miwili ilikutana baada ya kufa... wakisubiri kuingia peponi. Mmoja akamuuliza mwenzake.

We umefikaje huku?
Mwenzake akajibu ''nilifia kwenye friza''

Na wewe umefikaje huku?
Alieuliza mwanzo akajibu, ''nimekufa kwa furaha ilozidi''

''mh! Umekufa kwa furaha?'' jamaa alimuuliza.
Akajibu, ''ndio, nilirudi siku nyumbani nkakuta nyumba safi sana, na chakula kizuri mezani nkajua lazima mke wangu ana kidume cha wizi ndani, nikasech nyumba nzima sikuona mtu, basi furaha ikazidi mpaka nikafa'

Mwenzake akanena, ''si ajabu ungeangalia kwenye friza sote tungekuwa hai bado.''

*cheka unenepe*

Bosi wa kike

Kwenye ofisi moja, bosi mmoja wa kike alimfuata mfanyakazi mpya na kumuambia... ''habari yako, unaitwa nani?''
'naitwa Josh' alijibu jamaa.

Bosi, ''nimezoea kuwaita wafanyakazi majina yao ya pili mfano, allen, ima nk nk, je wewe la pili ni nani?''

Jamaa akajibu 'naitwa Darling. Josh Darling.'

Mwanasheria

Mwanasheria mmoja alifungua ofisi yake. Ikawa bado ina-speed ndogo upande wa wateja.

Siku moja akamuona mteja kwa mbali anakuja. Akanyakua simu ya mezani na ku-act anaongea wakati mteja keshafika, '...ndio ndio.. Nilishasema kesi chini ya milioni moja mimi bado siwezi...''

Alipomaliza maongezi ''oh samahani kwa kukusubirisha sana, kama unavyoona nipo bize... Karibu sana, nkusaidie nini?''

Yule mteja akajibu, ''asante, mimi nimekuja kukata line unadaiwa bill kubwa sana ya simu.''

Wagonjwa wa akili

Daktari mmoja na wagonjwa wa akili watatu. Akawaambia ''atakae weza pita kwenye ule mlango bila kugusa na mikono ataenda nyumbani''

Wa 1: Mi nkifika pale kwenye mlango ntaruka kupitia kitundu cha funguo.
Wa 2: Mi ntaruka pia na kupita kwenye tundu la ufunguo bila kugusa.
Yule wa 3 Akaenda mpaka kwenye mlango akaangali na kujibu, ''mi siwezi ruka kwenye kitundu cha funguo kuna ufunguo.''

Maumivu

Dada mmoja alienda kwa daktari hali ikawa hivi:
Dada: Dokta kila nnapojigusa panauma mwili wote.
Dokta: Ngoja nikufanyie uchunguzi.
Baada ya kumaliza daktari akampa majibu.
Dokta: Inaonyesha kuwa kidole chako ndio imevunjika...
(ndio maana kila agusapo ni maumivu tu)

Bia bia bia

Jamaa aliliona kreti la bia kwake, akachukua chupa moja ipo tupu na kuitupia ukutani ikavunjika akasema 'we ndo sababu sina mke.'
Ya pili, 'we ndo sababu sina watoto.'
Ya 3, 'we ndo sababu sina kazi.'
Ya 4 ilikuwa haijafunguliwa akaiweka pembeni akasema 'kaa pembeni rafiki yangu we huusiki'

Kigeu geu

Jamaa mmoja alipoona mzee wake (baba) anaumwa na kukaribia kufa, akaamua kutafuta mke ili watungue wote mahela ya urithi.

Siku moja akakutana na msichana mzuri, jamaa akajinadi 'nataka nikuoe, baba yangu yupo hoi kitandani na urithi ntaopata hutakuwa shida kabisa maishani.'
Dada akaingia line na kupeana mawasiliano.

Siku tatu mbele yule dada akaja kuwa mama yake wa kambo...

Ujauzito

Mtu mmoja alipiga simu kuomba msaada juu ya mama mjamzito aliepo mbele yake:
Mwanaume: Halo... My wife ni mjamzito na dakika yeyote huku...
Hospitali: Wee! Ni mtoto wake wa kwanza?
Mwanaume: Hapana we kichaa nini mimi ni mumewe.

Kujifungua

Mume alienda kushuhudia mkewe akijifungua. Daktari akasema nina mashine ya kuhamisha maumivu toka kwa mama kwenda kwa baba wakati wa kujifungua.

Baba akasema ni gud idea. Akakubali.
Dokta akahamisha maumivu kwa 10% bado baba hasikii maumivu. Wakaongeza ongeza mpaka ikafika asilimia zote baba yupo swafi tu.

Mama akajifungua mtoto salama. Kesho yake wakamkuta fundi viatu pale jirani na kwao kafa.

Chuo

Mkufunzi mmoja aliwauliza wanafunzi wawili wa chuo, ''ni wakati gani huwa unadhani ni wa kumpongeza mtu kwa makosa aliyofanya?''

Mwanachuo mmoja kati ya wale wawili akajibu, ''Wakati wa ndoa yao''

Kwenye simu...

Mtoto mmoja akiwa kwao akiongea na simu, alitumia mda wa nusu saa kuongea na simu. Alipokata baba yake akamuuliza ''ajabu kulikoni leo hujaongea mda mrefu kwenye simu?''

Mwanae akamjibu ''ilikuwa wrong namba''

Darasa la kwanza

Mwalimu mmoja akiwaambia wanafunzi wake waandike tisini na tisa.
Mwanafunzi mmoja akauliza ''ndio inaandikwaje?''

Mwalimu: Unaandika tisa halafu tisa ingine.
Wanafunzi wakaandika, mmoja akawa kaandika tisa moja halafu akaulizwa na mwalimu, 'mbona huandiki tisa ingine?'
Mwanafunzi: Sijui tisa ingine naiandika/iweka upande gani?

Mgahawani

Mteje: Nimeona kidole chako gumba kikiwa kwenye supu nliyoagiza.
Mhudumu: Oh usijali. Supu haikuwa ya moto.

Baba na wanae

Baba alimuuliza mwanae kipenzi, ''nini umefanya kumsaidia mama leo nyumbani?''

Mtoto akamjibu baba, 'nimemsaidia kuorha viombo'
Mtoto mwingine akadakia, 'mi nimemsaidia kuokota vipande vya glasi na sahani.'

Saturday, July 10, 2010

Kikombe

Mtoto: Kwanini wale pale wote wanakimbia?
Mama: Wapo kwenye mashindano ili mmoja akishinda kikombe apewe.
Mtoto: Sasa hao wengine wanakimbila nini wakati atapata mmoja tu?

Kwa dokta.

Jamaa mmoja alienda kwa daktari kujiezea...

Mgonja: Dokta nimeng'atwa na nyigu shingoni.
Dokta: Kunywa maji sasa hivi.
Mgonjwa: Yatasaidia?
Dokta: Hapana, ila yataidia kujua kama shingo imetoboka ikavujisha.

Maongezi

Jamaa akimsimulia rafiki yake kuhusu bosi wake, ''...unafikiri nakutania? Bosi wangu amezidi ukali mno mpaka kivuli chake kimekataa kumfuata.''

Mtoto wa kiume

Baba: Nna mtoto wa kiume safi sana.
Rafiki: Anavuta sigara?
Baba: Hapana.
Rafiki: Anakunywa pombe?
Baba: Hapana.
Rafiki: Anarudi nyumbani usiku?
Baba: Hapana.
Rafiki: Kweli una kidume safi sana, ana umri gani sasa?
Baba: Miezi sita sasa.

Chai

Dokta nna tatizo, kila nkinywa chai jicho laniuma! Jamaa akimuambia dokta.

Nae dokta akajibu, ''toa kijiko kwenye kikombe wakati unakunywa chai''

Shuleni siku ya 1

Siku moja baba alimuuliza mwanae 'umeionaje siku yako ya kwanza shuleni?'

Mtoto akajibu, ''una maanisha na kesho naenda tena shule?''

Kidhungu

Mtoto: Baba, shuleni mesikia mwalimu akisema 'idiot' maana ake nini?
Baba: Idiot ni mtu ambae anaelezea jambo fulani kwa urefu kwa mtu mwingine anaemsikiliza na bila huyo tu kuelewa. Unanielewa?
Mtoto: Hapana.

U: Muangalie yule pale mwenye nywele fupi ni msichana au mvulana? T: Ni msichana, na mtoto wangu. U: Oh samahani sijajua kama we ndie baba ake. T: Mimi sio baba ake, ni mama ake.

Homework

Mwalimu: Ni baba yako ndio amekusaidia kufanya homework?
Mtoto: Hapana, amefanya yote yeye mwenyewe. Me mekusanya tu.

Kwenye basi...

Jamaa mmoja alimuona mtu kwenye basi amesimama kwenye basi huku amefumba macho akamuuliza, ''vipi unaumwa? Nini shida?''

Jamaa akajibu, ''siumwi, sijalala ila yule kizee ananikonyeza tangu aingie humu''

Ng'ombe

Ng'ombe akiongea na mwenzake, ''mwenzangu hauogopi ugonjwa wa kimeta?''
Wa pili akajibu, ''wala siogopi mimi ni farasi''

Maskini

Tajiri mmoja akiwa kwenye gari yake ghafla akaona nje kijana anakula manyasi. Akasimamisha gari na kumfuata na kumuambia 'njoo twende kwangu'

Maskini akajibu ''lakini nna mke na watoto wawili''

Tajiri akajibu, 'twende nao pia.'
Walipofika kwa tajiri akawaambia ''hapa ndio kwangu, hakika utansaidia kuzitafuna na hizi nyasi ndefu kuliko zile za kule.''

Kabla ya kufa...

Jambazi mmoja alivamia nyumba na kukuta mke na mume.
Akamkamata mke na kumuwekea kisu shingoni na kumuambia, ''nataka nijue jina lako kabla sijakuua''

Mwanamke akajibu, ''Elizabeth'' jambazi akasema, ''oh mama yangu pia anaitwa Elizabeth'' akamuachia huru.

Alipomkamata Mume, ''na wewe jina lako nani?''
Mume akajibu, ''naitwa Josh ila rafiki zangu huniita Elizabeth''

Hahahaha...

Mke na mume walienda ART GaLLeRY. Wakaona picha kubwa ya M'ke akiwa uchi. Na jani moja tu limefunika sehemu nyeti. Mkewe kama hakuipenda ile hali hivyo, mke akamuuliza mumewe ''tuondoke unasubiri nini?''
Mume akajibu, ''nasubiria upepo mkali upulize''

Injinia...

Kwenye gari kulikuwa na ma-injinia wawili na dereva wakisafiri. Injinia wa umeme na wa madirisha.

Ghafla gari ikaloga na kuzima.

Injinia wa umeme akashauri aangalie wapi tatizo lipo afanye uchunguzi.
Injinia wa madirisha, ''sijui vizuri mambo ya magari lakini nashauri kwa nini tusifunge madirisha yote, tushuke, halafu turudi, tufungue madirisha labda itasaidia.''

Mtihani-hesabu

Mtoto mmoja akimueleza baba ake.
Mtoto: Baba nimepata F hesabu.
Baba: Kwa nini?
Mtoto: Mwl. Aliniuliza 2x3=? Nkamjibu 6.
Baba: Mbona jibu sawa.

Mtoto: Halafu mwl. akaniuliza tena 3x2=?
Baba: What's the f**kng difference?
Mtoto: Hivyo ndivyo nlivo sema.

Beach na mkasa.

Jamaa mmoja alikuwa amejilaza beach akiwa uchi. Ghafla kwa mbali akaona msichana anakuja, akaamua jifunika eneo nyeti na kipande cha gazeti.

Msichana alipofika akamuuliza yule kijana...
'kuna nini hapo chini ya gazeti?' jamaa akamjibu, 'hamna kitu ni ka-ndege tu nimekafunika'
Msichana akaendelea safari yake, jamaa akajilaza na kuuchapa usingizi. Alipokuja kuzinduka akajikuta yupo Hospitali.

Polisi wakamuuliza jamaa akajibu ''nilikuwa nimelala beach kuzinduka najikuta hapa hospital.''
Polisi wakaenda beach na kumkuta yule dada na kumuhoji 'umemfanya nini yule jamaa aliekuwa uchi?'

Dada akamjibu, ''nothin, mi nkicheza na ka-ndege ndio akanitemea mate meupe ndo nikamvunja shingo yake na yale mayai yake...''

Kwenye daladala

Mtoto mmoja alipanda daladala, akawa anajiongelesha akiwa nyuma ya kiti cha dereva ''baba yangu angekuwa ng'ombe mi ningekuwa ndama.'

''Baba yangu angekuwa Nyati mi ningekuwa ndama.''
Dereva akamwambia yule mtoto baada ya kuchoshwa na kelele zake. Akimuambia kwa ukali, ''je baba ako angekuwa shoga, halafu mama yako malaya ungezaliwa nani?''

Mtoto akajibu, ''ningekuwa dereva daladala.''

Elfu tano.

Mtoto mmoja wa kike mmoja aliingia ndani kwa mama yake uku akisema... ''mama... mama... Juma kanipa elfu tano.''

Mama akamuuliza, 'kwa nini amekupa?''

Mtoto akajibu, ''aliniambia nisimame juu ya mti yeye akakaa chini akinambia ninyanyue nyanyue miguu.''

Utani bar

Siku moja jamaa kaenda bar na kuagiza konyagi.
Mhudumu akamuuliza, ''vipi una stress leo?''
Jamaa akajibu, 'ndio nimegundua kuwa mdogo wangu wa kiume ni shoga.'

Siku ya pili ivo ivo alipoulizwa akajibu, ''nimegundua kuwa mdogo wangu mwingine ni shoga pia.'

Alipofika siku ya tatu, jamaa akaagiza vodka na konyagi, mhudumu akauliza tena, ''kuna nini kwani? Nyumbani kwako hamna mtu anaependa wanawake at all?''

Jamaa akajibu, ''ndio, my wife.''

Friday, July 9, 2010

Zebra

Mtoto mmoja akimuambia baba yake alipotoka kuangali wanyama, ''baba, nimeona pundamilia wa aina mbili. Wenye mistari myeusi na wengine myeupe.''
Baba alichoka hoi...

Kwa dokta

Jamaa mmnoja alienda kwa Daktari na kumuelezea daktari matatizo yake kama ifuatavyo, ''dokta mimi nna matatizo jamaa hasimami kabisa kwa mke wangu siku hizi, ntakuwa na matatizo tu.''

Dokta akamuambia, ''mlete mkeo kesho''
Kesho yake ilipofika akiwa na mke wa jamaa chumba cha daktari dokta akamuambia mwanamke ''vua nguo, geuka geuka....''

Baada ya muda akaenda kumjibu mume wa mtu, ''ndugu yangu huna matatizo kabisa hata mimi haijasimama pia.''

Thursday, July 8, 2010

Dereva trekta.

Dereva trekta siku moja alikuwa akiendesha gari ndogo ya kawaida.
Sasa ikawa anapita maeneo yenye majari/matawi ya miti chini chini. Ikawa kila ya kigusa kioo cha mbele na yeye anainama kuyakwepa kama awapo na trekta yake...

Dereva trekta.

Dereva trekta siku moja alikuwa akiendesha gari ndogo ya kawaida.
Sasa ikawa anapita maeneo yenye majari/matawi ya miti chini chini. Ikawa kila ya kigusa kioo cha mbele na yeye anainama kuyakwepa kama awapo na trekta yake...

Kuku part ii

Jamaa njiani vijijini baada ya kuona/kuisi kuwa wamepotea mmoja kwenye gari akamwambia mwenzake, 'hebu tuulize kama tumepotea au tupo sahihi kwa mwanakijiji yeyote?'

Mwenzake akajibu, 'we umemuona nani? Mbona sijaona hata mwanakijiji?'

Alieuliza mwanzo akasema tena, 'basi tuwaulize hata hao kuku hapo mbele.'

Kuku

Jamaa mmoja alikuwa anaendesha gari njia vijijini sasa wakati akiendesha ghafla kuku mbele njiani. Jamaa uku akiendesha akaanza kumfukuza kuku wa ishara huku akisema shhh shhh shh (huku akiendesha gari, akiamini kuku wanamsikia huku kafunga vioo)...

Wednesday, July 7, 2010

Mume, mke, dawa

Mwanaume mmoja alimletea mkewe maji kwenye glass na na panadol.

Mkewe akamuuliza mumewe, ''ya nini, mi mbona siumwi?''

Mumewe akamjibu, ''kutokana na ugali uliopika ulivyo mgumu lazima utakuwa unaumwa viungo.''

Mlevi mwingine

Mlevi mmoja alikuwa akitembea huku akirusha rusha funguo. Akakutana na jamaa akamuuliza 'vipi mwenzetu?'

Mlevi akajibu, 'hii ni funguo yangu ya gari imepotea naitafuta'

Jamaa akamwambia tena yule mlevi 'mbona na zipu ipo wazi ya suruali?'
Mlevi akajibu, ''oh, nimempoteza na mke wangu'

Dereva mlevi

Dereva mmoja alikuwa amelewa akawa anaendesha gari upande sio wake. Polisi akamsimamisha na kumuambia, ''huoni kuwa upo upande sio? Hujaona mshale pale?'

Dereva mlevi akajibu, ''mshale? Wa mmasai? Sijauona, nkusaidie kuutafuta!''

Kwenye ndege

Pilot mzungu alitangaza kuhusu hali ya hewa wakati ndege ipo angani. Ghafla katikati ya maongezi ghafla akasema kwa mshtuko mkubwa...

''...oh my G.O.D.'' halafu kimya kikatawala.

Baada ya sekunde chache akaendelea kutangaza.

''ladies & gentlemen, am sorry if i scared you earlier... Accedentally the flight attendant spilled the hot tee in my lap... You should see the front of my pants''

Abiria mmoja akadakia na kusema, ''that's nothing. He should see the back of mine.''

Fumanizi

Mume mmoja alifurumushwa mbio toka gesti hausi.

Alipofika nyumbani akiwa uchi akawa anamuambia mke ''mke wangu vibaka wamenipora kila kitu''

Mkewe akajibu ''hao vibaka wanakujali kweli na condom wamekuvalisha''

Hausi-dada

Dada mmoja wa kazi za ndani alipogizwa apike chakula cha jioni na mboga iwe samaki.

Basi dada ilipofika jioni wakati anatenga chakula mezani akawa anamuambia mama mwenye nyumba 'mama samaki nlikosa hivyo nimewachukua wale wa kwenye bwawa dogo la kioo sebuleni nimewakaanga'

Panya

Kulikuwa na panya wawili mkubwa na mdogo.

Mkubwa: Leo inabidi utumie ile mbinu ya kung'ata halafu unapuliza umesikia?
Mdogo: Eh!
Mkubwa: Eh nini?
Mdogo: Si miguu ya yule mtu mi naogopa mafua inanuka sana.
Mkubwa: Panya haogopi mafua wewe alah...!

Katoto

Katoto: Mama kwani we na baba mnatumiaga condom?

Mama kwa mshangao alimjibu mwanae, ''hapana mwanangu, kwani vipi?''

Katoto: Si memuona baba ananunua jana kamuliza akasema za mama.

English

Kaka mmoja alikuwa na rafiki yake na mzungu mmoja. Sasa yule mzungu alipokuwa anaongea kimombo na jamaa ilionekana jamaa aliachwa kwenye mataa kidogo.

Hivyo basi akamgeukia rafiki yake mtanzania mwenzake na kumuuliza kwa staili ya kumnong'oneza ''hii aibu sasa, kaka una dictionary (kamusi) hapo?''

Gari latumia nini?

Dogo mmoja alikuwa amekaa na baba ake kibarazani, punde likapita gari dogo linatoa moshi kweli kweli...

Mtoto akamuuliza dad ake ''baba, ile gari inatoa sana moshi. Inatumia kuni?''

Tuesday, July 6, 2010

Taxi

Jamaa alilewa pombe alipokuwa akitoka bar akaingia kwenye gari yake, kwa vile pombe zilikuwa nyingi kichwani akajikuta akiuliza akiwa kwenye gari yake ''taxi driver wa gari hii yupo wapi?'' akimuuliza mlinzi.

Kengele

Mchungaji mmoja alikuwa akitembea ghafla akamuona mtoto akihangaika kubonyeza kengele ya mlango.

Kwa sababu ya ufupi mchungaji akaenda ili amsaidie kubonyeza.
Baada ya kubonyeza mchungaji akamuuliza mtoto 'enhe kinachofuata?'
Mtoto akajibu 'tukimbie'

Bar na kutukanana

Mijamaa miwili bar baada ya pombe walianza tukanana kiasi kwamba bar ikawa kimya kuwasikiza wao.

Wa1: ...*@&§ nimelala na mama ako...
Wa2: Go home dad you're drunk.

Singa singa

Mtoto mmoja alikuwa yupo kwenye mgahawa na mama yake. Pembeni kidogo kulikuwa na singa-singa ana ndevu paka mdomo hauonekani akiwa anakula karanga.

Yule mtoto akamuambia mama yake 'mama... mama... huyo pembeni hana mdomo...'

Singa-singa alimsikia yule mtoto akimwambia mama ake nae akaamua kuufunua mdomo na kumuonyeshea na kuonge huku akionyeshea mdomoni ''na hii k** yako?'

Nyoka na story

Nyoka wawili walikuwa wakiongea na lugha yao. Mmoja akamuuliza mwenzake 'sisi tuna sumu?'
Mwenzake akajibu 'ndio, vipi kwani?'
Wa kwanza akajibu, 'nimejing'ata ulimi'

Minyoo...

Baba mmoja a akijaribu kumfundisha mwanae madhara ya pombe. Akamchukua minyoo (worm) wawili. Mmoja akamuweka kwenye glasi ya maji wa pili kwenye glasi ya whisky.

Minyoo(worm) wa kwenye glasi ya whisky akafa, wa kwenye maji akaishi. Kisha akamuuliza mwanae.

'Enhe, Josh unajifunza nini hapa?'
Mtoto akajibu, "hapa ina maanisha nikinywa pombe sitakuwa na minyoo''

Duh! Duh! Duh!

Mwanaume mmoja alikuwa na watoto 6 siku moja alienda bar na mkewe. Bar ilikuwa imeeurika kiasi.

Jamaa alikuwa anapenda kumwita mkewe 'matha of six' sasa walipokuwa bar baada ya masaa kadhaa mumewe akamuita mkewe kwa sauti ili warudi nyumbani 'matha of 6 twende nyumbani mke wangu'

Mke nae akamjibu 'sawa fatha of 4 tunaondoka asa hivi'

Mtoto kamfuma...

Siku mmoja alimkuta baba ake akimalizia kuvaa kondom, mtoto akamuuza baba ake 'baba hiyo nini?'

Baba akastuka na kuzuga anamtafuta panya...
Mtoto akauliza 'halafu ukimpata utafanya nae?'

Shindano

Mzee mmoja alisikia kumwa tangazo kuwa mwanaume mwenye watoto 10 atazawadiwa milioni 15.

Hivyo yeye alikua na watano akamuaga mke na kumuambia 'nisubiri nkawachukue watoto wengine wa nje wa tano'

Aliporudi na wanae wa nje wale aliowaacha hawakuwepo akamuuliza mkewe 'watoto wapo wapi?'

Mke akajibu 'wamechukuliwa na baba zao pia'

Bar toilet

Mwanaume mmoja alienda bar na mkewe, punde baada ya bia mbili tatu mwanaume akanyanyuka kwenda msalani. Aliporudi akamwambia mkewe 'choo cha wanawake mbona hakina tishu?'

Mkewe akauliza, 'wewe umejuaje?'
Mume: Nimejuaje? Si nlipotea baada ya kumfuata nyuma nyuma alivaa shanga kiunoni kama zako nkajua ni wewe mke wangu.

Umeme

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake wakati wakitwanga 'storie' huku wakiangalia sinema sebuleni, ''baba... baba... hivi tanesco wanakataga umeme kwenye gari?''

Baba ''hapana mwanangu''
Mtoto: na ulaya je tanesco wanawakatia?
Baba: !!

Kwa dokta

Mwanamke mmoja alienda kwa daktari na mtoto.
Dokta: Mbona mtoto afya yake inazorota.
Mwanamke: Ndio maana nimekuja kwako dokta.

Dokta akaanza mfanyia uchunguzi, akamminyaminya chuchu, akammyonya maziwa kisha akasema ''mbona huna maziwa kabisaya kumnyonyesha?''

Mwanamke: Nalijua hilo mimi ni anti yake, ila nime-enjoy huduma yako.

Buchani...

Jamaa alienda nunua steak buchani. Alipofika muuza nyama wakati anajaribu kukata nyama hakuweza kufikia steak iliopo juu juu kidogo. Akamwambia mnunuaji ''samahani, njoo kesho ya leo ipo juu sana''

Mama kichaa

Mama mmoja mgonjwa wa akili alifanyiwa uchunguzi ajue kama ni amepona ugonjwa wa akili.

Yule mwanamke akamleta buibui mezani mbele ya daktari na kuanza kumuamrisha 'tembea tembea...'
yule buibui akawa hatembei.

Daktari akauliza: Mbona hatembei sasa?
Mama: Akajibu, unaona nilikuambia nimegundua kitu.
Daktari kitu gani?
Mama: Nimemtoa miguu yote so hawezi kunisikia.

Rangi barabarani

Jamaa mmoja alipata dei waka ya kupaka rangi ile mistari pembezoni mwa barabara.

Siku ya kwanza alichora kilometa 5,
Siku ya pili kilometa 2,
Siku ya tatu kilomita 1.

Bosi akawa mkali sana ''kazi yako inavurunda kila kukicha kwa nini?''
jamaa akajibu ''bosi nnavyozidi kwenda mbele dumu la rangi ndo linazidi kuwa mbali na mimi...''

Uzito

Mama mmoja alienda kwa daktari kuhusu suala la kupunguza uzito.

Mama: Dokta bado uzito unazidi nifanye nini kupunguza?
Daktari: Oh! Pole sana. Chukua sindano jichome tumboni upepo wote utaisha na uzito utapungua.

Sunday, July 4, 2010

Wanaume wa3

Walisimama kwenye ghorofa,
M'ume wa kwanza akaiachia saa yake ilipofika chini ikavunjika.
Wa pili na ivo ivo.
Wa tatu akaiachia, kisha akaenda chini kuifuata.

Wale wawili wakajiuliza mwenzetu....?
Yule wa tatu akawajibu ''saa yangu inachelewa dk5''

Treni

Siku moja mwanamke na mwanaume walijikuta wamelala chumba kimoja kwenye, kila mmoja wao ana wake wa ndoa nyumbani.

Usiku ulipofika, jamaa akamwambia yule dada, ''dada samahani naomba nichukulie shuka la pili hapo kwenye kabati'' jamaa akiongea toka kitanda cha juu.

Dada: Kaka, hebu tu-pretend kama tumeoana.
Kaka: Oh, hiyo safi sana.
Dada: Nenda kachukue shuka lako mwenyewe.

Bar pombe changudoa

Jamaa mmoja alikuwa pombe vibaya. Alipokuwa club counter akamuona mwanamke mmoja na kumuambia ''nna laki mbili hapa, nitafanya chochote utachosema''

Mwanamke: Ooh, nipe sasa hivi kabisa.
Jamaa akampatia, kisha mwanamke akamwambia ''kanifulie nguo zangu''

Gari mpya

Mzee mmoja alinunua gari mpya, akawa kila siku akilala anaifunga kijiuzi mnene mnene kidogo halafu anajifunga kwenye kidole ili isiibiwe, au hata ikitaka ibiwa astukie mchezo.

Mume na Padre

Jamaa kaenda kumwambia Padre ''mke wangu anavaa shanga mimi sipendi.''

Padre kajibu ''hata mi nilimwambia bora apunguze ziwe mbili kama za mke wa Swai.''

Saturday, July 3, 2010

Bia

Jamaa mmoja aliomba mkoa wenye baridi. Alienda bar akaagiza bia ya moto ikaletwa, ilipoletwa akasema 'niletee ya moto sio baridi' mhudumu akajibu 'kaka hiyo ni ndio ya moto, labda nikaichemshe kidogo.'

Ajali na kipofu.

Katika ile ajali ya bus kipofu aligundua kuwa kuna mama aliyeumia zaidi baada ya mkono wake kugusa NYETI za majeruhi huyo huku akidhani ameshika mdomo na kusema jamani mkimbilieni kwanza huyo maana ameumia sana na meno yote yameng'oka.

Kanda ya video

Jamaa mmoja alienda kuangalia kanda ya video kwa best ake, kwa kuwa sinema ilikuwa tamu na ilipoisha akamuambia rafiki yake 'aisee igeuze side b sinema kali kweli.'

Kuchora

Darasani siku moja mwalimu akikagua wanafunzi wake, akafika kwa mwanafunzi mmoja akakuta anachora, akamuuliza:

'enh unachora nini?' Mwalimu aliuliza.
Mwanafunzi akajibu 'namchora Mungu'
Mwalimu: lakini hamna aliyewahi kumuona Mungu.

Mwanafunzi: Watamuona sasa hivi.

Friday, July 2, 2010

Hii hata mimi nlicheka sana...

Bibi wa kichaga kapanda treni na mwanae kutoka dar kwenda mwanza. Alipofika tabora kamwambia mwanae lazma dereva kapotea njia siku mbili zote hatufiki!

Day care

Mtoto mmoja akimsimulia mama yake jioni, 'mama mi nadhani yule mlezi wetu ni shoga.'

Mama: Wee! Kwanini wasema hivyo?
Mtoto: Kwasababu naniliu yake ina ladha mbaaya...

Simu ya mkononi.

Jamaa mmoja alidondosha simu ikatumbukia kwenye choo. Akatoka mbio mbio mpaka sebuleni. Mkewe akamuuliza 'vipi?'

Jamaa akajibu 'simu'
mke akauliza, 'simu? Imefanya nini?

Jamaa: imetumbukia chooni, hebu niazime yako...'
Mke: ili uibeep au?

The mchaga

Jamaa mmoja alienda bank kuomba mkopo. Afisa mikopo akajaribu kuangalia jinsi ya kulinda mkopo wa bank wa sh 150,000. Afisa mikopo akashauri jamaa aiweke bondi benz yake.

Bila hiyana jamaa akaweka na kuipaki eneo la benki. Wiki 4 baadae akarudisha mkopo na riba juu elfu 15.

Afisa mikopo akamuambia, 'mzee nimetambua kuwa wewe ni milionea je imekuwaje haya yote?''

Jamaa akajibu, 'ningepata wapi pa kupaki gari yangu kwa elfu 15 siku zote hizi kwa bei nzuri hivi?'

Wodi ya vichaa

Jamaa katika wodi ya vichaa walichorewa gari wakaambiwa wakapande. Vichaa wote wakakimbilia, wawili wakabaki.

Daktari akajua hawa ndio wamepona, akaenda na kuwauliza ''enh nyie mbona mmebaki?''

Wa kwanza akajibu: Me nna washangaa gari yenyewe ina pancha.
Wa pili: Me nasubiri wapande kwanza funguo nnazo mimi.

Chabo...

Kuna jamaa watatu walienda kupiga chabo (chungulia wakiofanya mapenzi) wa kwanza kachungulia fresh, wa pili na ivo ivo.

Wa tatu alipoenda kupiga chabo jamaa c akastukia mchezo, akachukua stick ya kuchomea mishkaki.

Si akamchoma jamaa alipokichungulia, jamaa aliechombwa akasema baada ''aah jamaa kastukia bwana kazima taa bwana''

Konyagi...

Marafiki wawili walikuwa bar, mmoja akamshauri mwenzake anye konyagi siku hiyo.
Alieshauriwa akajibu:

'aah hiyo, unaweza ukasikia kama umedondosha kitu ukadhani labda walet hivi, kumbe maini...'

Thursday, July 1, 2010

Kizee bank

Bibi kizee mmoja alienda bank kufanya shughuli za kibenk.

Nje alikutana na askari mlinda bank kama kawaida ya kila bank.
Alipotoka nje tena baada ya kumaliza shughuli za kibenk yule bibi kizee akamkuta yule askari tena pale pale nje, na akamwambia...

'tayari nimekamilisha kuweka hela zilizonileta benk, unaweza kwenda nyumbani sasa'

Mke hoi hosp

Mwanamke mmoja alikuwa amekaribia kukata roho akamuambia mumewe aliepembeni yake hospitali.

''mume wangu nna kauli ya mwisho kabla sijafa, ni mimi nlieiba zile milioni 40 kwenye SAFE yako''

Mumewe akamjibu, ''usijali mke wangu, na mimi nna machache kabla hujafa ya kukuambia''

Mke akanena, ''ndio mume wangu''
Mume: 'ni mimi nliokuwekea sumu...'