Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Friday, July 16, 2010

Trafiki, Mume na Mke

Trafiki mmoja alimsimamisha mzee mmoja kwa sababu ya spiidi kali.
Trafiki: Mzee unajua kuwa ulikuwa na spidi kali sana.
Mzee: Hapana askari nilipitiwa tu.
Mke: Mi nimemuambia sana apunguze spidi hakunisikia.
Mzee: Hebu nyamaza bwana.... (akaanza kubwata)

Trafiki: Mzee leseni ya gari imeisha mda wake walijua hilo.
Mzee: Nilisahau kuangalia askari.
Mke: Umezidi nimeimba mwezi mzima hanisikii...
Mzee: Nimezidi nini... (akabwata kama kawaida)

Trafiki akaenda upande wa mwanamke dirishani:
Trafiki: Mama samahani Mumeo huw anakujibu hivi kila siku?
Mke: Hapana mpaka akiwa amelewa.

No comments:

Post a Comment