Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, July 18, 2010

Trafiki polisi tena...

Askari mmoja wa barabarani alikuwa kazini kama kawaida yake, jioni yake alikuwa na safari ya kwenda kwa wakwe zake. Basi kila alipoiona gari alisimamisha na kutafuta kosa ili kidogo dogo kipatikane (pesa).

Akamsimamisha mzee mmoja wa makamo, baada ya maongezi na faini alolipa yule mzee muda wa kuondoka kwenda nyumbani kujiandaa ukafika.

Jioni wakati yupo sebuleni akawa anamsimulia mchumba wake jinsi alivyosumbuana na madereva siku nzima ya leo mara akaingia baba mkwe sebuleni, yule trafiki kumuangalia anamuona yule mzee aliemtoza faini...
Aliishiwa maneno...

No comments:

Post a Comment