Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, July 18, 2010

Omba*omba na Mlevi

Mlevi mmoja alikuwa pombe nyingi kichwani wakati anarudi nyumbani akamuona ombaomba kipofu.
Akampatia elfu kumi. Hatua chache akkamua ageuke aangalie kama kweli yule ombaomba ni kipofu. Akamuona jinsi anavyoihifadhi pesa si kipofu akarudi.

''Wewe kumbe sio kipofu eenhe?'' Mlevi aliuliza.
Jamaa akajibu: Mimi sio kipofu namshikia rafiki yangu yeye ndio kipofu kaenda msalani kidogo.
Mlevi: Sasa mbona una...
Jamaa: Hata mimi nina ulemavu ni kiziwi, hata sikusikii kabisa.
Mlevi: Ooh pole sana chukua na hii elfu kumi utampa rafiki yako.

No comments:

Post a Comment