Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, July 11, 2010

Peponi

Mijamaa miwili ilikutana baada ya kufa... wakisubiri kuingia peponi. Mmoja akamuuliza mwenzake.

We umefikaje huku?
Mwenzake akajibu ''nilifia kwenye friza''

Na wewe umefikaje huku?
Alieuliza mwanzo akajibu, ''nimekufa kwa furaha ilozidi''

''mh! Umekufa kwa furaha?'' jamaa alimuuliza.
Akajibu, ''ndio, nilirudi siku nyumbani nkakuta nyumba safi sana, na chakula kizuri mezani nkajua lazima mke wangu ana kidume cha wizi ndani, nikasech nyumba nzima sikuona mtu, basi furaha ikazidi mpaka nikafa'

Mwenzake akanena, ''si ajabu ungeangalia kwenye friza sote tungekuwa hai bado.''

*cheka unenepe*

No comments:

Post a Comment