Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, July 14, 2010

Adhabu darasani

Hii ni true story wakati nasoma.

Mwalimu mmoja wa kemia wakati anafundisha darasani aliwasikia wanafunzi wawili wakinong'ona.

Akawaita na kuwapigisha magoti mbele ya darasa. Akawa anaendelea kuandika ubaoni, alipogeuka akamfuma mmoja wa wale wanafunzi kaweka mikono yake mfukoni huku kapiga magoti pale mbele.

Mwalimu kwa sauti ya hasira na ukali akamuambia yule mwanafunzi mmoja mbele ya darasa 'wewe toa mifuko mkononi'
darasa lilicheka loote. Mpaka mwalimu mwenyewe akacheka akaamua awasamehe.

No comments:

Post a Comment