Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, July 6, 2010

Rangi barabarani

Jamaa mmoja alipata dei waka ya kupaka rangi ile mistari pembezoni mwa barabara.

Siku ya kwanza alichora kilometa 5,
Siku ya pili kilometa 2,
Siku ya tatu kilomita 1.

Bosi akawa mkali sana ''kazi yako inavurunda kila kukicha kwa nini?''
jamaa akajibu ''bosi nnavyozidi kwenda mbele dumu la rangi ndo linazidi kuwa mbali na mimi...''

No comments:

Post a Comment