Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Thursday, July 15, 2010

Kuhama bar

Jamaa alilewa vibaya akaagiza bia ya ziada mhudumu akamuambia 'umekunywa vya kutosha kapumzike leo nyumbani'

Mlevi akahama bar mambo yakawa vile vile, akaenda bar ingine vile vile.

Akaamua aende kwingine alipofika akanena ''bar hii mbona ipo kimya sana?''
kidogo akaona tv na redio kama vyake nyumbani.

Akamrukia alie karibu yake na kumkwida ''wewe hii tv na redio yangu mmepata wapi?''
Akajibiwa ''baba kwani vipi leo?''
Kumbe kuja kuhamaki aliemkwida ni mwanae, na mahala alipo ni sebuleni kwake....

No comments:

Post a Comment