Karibu Sana.
Cheka Unenepe
Wednesday, May 30, 2012
Ajali ilivyotokea
Trafiki polisi akihoji palipotokea ajali "ahaa! Sasa naanza elewa embu nielezee jinsi ajali ilivyotokea wewe ukiwa kama dereva mhusika."
Dereva akajibu "hata sikumbuki nlifumba macho"
Dawa yake
Mume alizoea kila mara akirudi usiku ananyimwa unyumba na mkewe kwa kisa anaumwa kichwa.
Siku mume akarudi na moja kwa moja akampelekea panadol mbili na maji, mkewe akanena "nani kakuambia naumwa kichwa?" Mume akajibu "yes nimekukamata leo"
Mshtuko wa moyo
Mume karudi akasikia sauti asiyoielewa toka chumbani kwake, akaenda na kukuta mkewe analalamika amepata mshtuko wa moyo. Mbio anaenda sebuleni kupiga simu kuomba msaada.
Punde mwanae akaja "baba anko Jose kajificha kabatini kwako uchi" mzee mbio mpaka chumbani. Fungua kabati akamkuta ndio na kumuambia "wee mke wangu anapata mshtuko wa moyo we umejificha tu uchi humu unawatisha watoto, njoo tumpe msaada haraka."
4WD
Mwanaume alimnunulia pete ya almasi mkewe, rafiki akauliza "si ulisema anapenda gari yenye four wheel drive, mbona umenunua pete?" Mume akajibu "unadhani wapi ntapata rav4 feki?"
Ya leo mgonjwa
Dokta alipotembelea wodi ya mgonjwa wake aliepata ajali.
Mgonjwa akiwa amening'inizwa mikono juu akauliza "dokta ntaweza kweli kupiga kinanda nkitoka hospitali?"
Dokta: Bila shaka utaweza, wewe ni mpiga kinanda mzuri enh?
Mgonjwa: Hapana sijawahi kabisa bado.
Sunday, May 27, 2012
Pombe basi
Cha pombe alikunywa sana pombe akataka ongeza mhudumu akamjibu "hapana imetosha sasa umekunywa saaana." Mlevi akajibu "nimeanza kunywa miaka 36 ilopita sijawahi jua kama metosheka wewe umejuaje?"
Kwa mama lishe
Jamaa kwa mama lishe baada ya kula wali nyama akaletewa vijiti vya kutolea nyama kwenye meno. Vilipofika tu mezani kwake akahoji "vimechemshwa hivi? Maana kipindupindu nje nje."
Saturday, May 26, 2012
Wasiwasi
Dogo akimuongelesha mama yake aliepo sebuleni yeye akiwa jikoni "mama!" Mama nae akaitikia "ooh mwanangu"
Mtoto: Unaikumbuka ile sahani inayokupa wasiwasi isije niteleza ikavunjika siku moja.
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto: Basi wasi wasi wako umeisha leo.
Swali jibu tofauti
Mwalimu aliuliza wanafunzi wa darasa la 3 wakike kwa kiume "mlikuwaje hapo awali kabla hamjawa hivi mlivyo leo wanafunzi?"
Mwali akisubiria jibu akitaraji watajibu "walikua wadogo" wanafunzi wao wakajibu "tulikua na furaha, wengine wakilia nk"
Home work
Mwalimu: Haya James iko wapi homework yako?
Mtoto: Mwalimu ilmeliwa na mbwa wetu nyumbani.
Mwalimu: Nimefundisha kwa miaka 18 sasa, unadhani nitaamini hilo?
Mtoto: Ni kweli mwalimu nimemlazimisha mpaka kaila.
Friday, May 25, 2012
Mbio za ushindi
Baba: Wewe Japhet hiyo saa umeipata wapi?
Mtoto: Neshinda mbio ndio nkaipata.
Baba: Hizo mbio mlikua na akina nani?
Mtoto: Alikuwepo polisi, mwenye saa na mimi.
Fala wa kwanza
Mume: Unaniambia walikutongoza wanaume wanne ili wakuoe?
Mke: Ndio hivo hivo kama ulivyosikia.
Mume: Bora hata ungeolewa huyo fala wa kwanza kati ya wote waliokutongoza.
Mke: Ndio nlivyofanya hivyo.
Thursday, May 24, 2012
Mwizi wa atm
Jamaa aliibiwa kadi yake ya benk akaulizwa kama ameripoti polisi akajibu "sijaripoti bado, mwizi mwenyewe hamfikii matumizi kama mke wangu"
Kifamilia zaidi
Mke na mume wakiongelea suala la fedha kifamilia:
Mwanaume: Sikiliza isingekua fedha hii nyumba isingewepo.
Mwanamke: Na wewe sikiliza isingekua fedha zako nisingewepo hapa.
Wednesday, May 23, 2012
Tuesday, May 22, 2012
Monday, May 21, 2012
Msaidie mwenzako
Jamaa mmoja alikua anamrekodi mwenzake kutumia video camera huku mhusika akicheza na moto. Ghafla moto ukashika shati la jamaa...
Mpita njia akamuambia mwenye camera "wewee acha kamera muokoe mwenzako..."
Mwenye Camera akajibu "kaniambia nimrekodi tu sasa mi nifanyaje?"
Saturday, May 19, 2012
Wednesday, May 16, 2012
Mlizi mbio mbio
Tulikuwa bar moja jana mlinzi kaingia spidi, akamwambia jamaa mmoja aliyekaa kaunta,
Mlinzi: Mzee gari lako limeibiwa
Mzee: Umemtambua aliyeiba?
Mlinzi: Hapana lakini nimeandika namba za gari hizi hapa.
Hakimu & hongo
Kesi imeanza hakimu kakaa kwenye kiti chake akatangaza;
Hakimu: Mlalamikaji na mtuhumiwa wote mmeniletea hongo niwapendelee.
Mlalamikaji umenipa laki moja, mtuhumiwa
umenipa umenipa laki moja na hamsini.
Sasa nawarudishia hii hamsini elfu ili nisiwe na sababu ya kumpendelea mtu.
Tunaendelea...
13, 13...
Jamaa alikuwa anapita nje ya wodi ya vichaa akasikia mtu anesema, 13, 13, 13, 13, 13, 13,..... akaamua kuchungulia kwenye kitundu alichokiona ajue kuna nini, ile kuchungulia tu akamwagiwa mchanga wa machoni, sauti ikabadili ikaanza 14,14,14,14,14......
Ushauri wa dokta
Jamaa alikuwa anaumwa sana mkewe akamwita daktari, alipofika akamkuta jamaa kafumba macho;
Dokta: Huyu mbona amekwisha kufa
Jamaa: Sijafa bwana
Mke: Hebu nyamaza bwana acha kubishana na wataalamu.
Mume anaenda kazini
Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa
anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza
mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana"
Mke: Si ndio nimemshangaa huyu
mpumbavu eti kaenda kazini.........
Friday, May 11, 2012
Mama aliporudi
Mtoto "mama afadhali umerudi baba yupo nyumbani na anti, baba kamlalia anti kwa juu wote wanapiga kelel sijui wanaumwa nini mimi meshindwa wasaidia
Simu ya tochi
Jamaa mmoja alikua na simu yenye tochi Po. Kwenye kagiza giza rafiki yake akaiomba awashe kumulikia mwenye simu akamjibu "aahh usiiwashe itamaliza vocha yenyewe kimeo"
Wednesday, May 2, 2012
Kitana mapengo
Dukani: Nikusaidie nini kaka?
Mteja: Kitana changu vile kichanio kimevunjika.
Dukani: Sasa si kimoja tu vilivyobaki vingine si vipo.
Mteja: Hapana kilichovunjika ndio cha mwisho kabisa.
Hasira za mtoto
Baba na mtoto:
Baba: Mwanangu ukiwa na hasira unafanya nini?
Mtoto: Naenda chooni.
Baba: Chooni? Kufanya nini?
Mtoto: Kusafisha.
Baba: Halafu ndio hasira zinaisha?
Mtoto: Ndio nasafisha choo kwa mswaki wako.
Duka la tai
Jamaa alienda nunua tai alipofika ikawa hivi:
Muuza duka: Karibu, nikusaidie nini?
Mteja: Natafuta tai iliyochanganyika na maziwa na kahawa hivi.
Muuza duka: Sijajua na sukari je au hutoitaji?
Tangaza ndoa...
Njemba ilienda kutangaza ndoa:
Njemba: Mzee mimi nataka kumuoa mwanao.
Mzazi: Unafanya nini kusukuma siku?
Njemba: Nakaba, kupora na kubaka.
Mzazi: Mbona vyote na hasi huna hata moja chanya?
Njema: Ohh! Chanya nina HIV +ve.
Subscribe to:
Posts (Atom)