Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, November 9, 2011

Chizi ajibu swali

Kijana: Nasikia mkeo anaongeaga mwenyewe akiwa peke yake.
Mtu mzima: Kwa kweli sijui, siwagi nae akiwa peke yake.

Mgonjwa huyu...

Mume: Daktari amekuja anataka kukuona.
Mke: Najisikia vibaya sitaki onana na mtu yeyote.

Gharama...

Mlala hoi alipoenda kwa daktari kupata huduma ya kiafya:
Dokta: Umeshawahi kuzimia?
Mgonjwa: Ndio, mara ya mwisho ulivyonitajia gharama zako.

Betri ya saa

Kimi: Kwa nini unatoa betri kwanye saa na kuzianika juani?"
Luko: Ili zipate kuwa na nguvu zaidi, nazirudishaga nkitaka angalia muda tu.

Tekinolojia

Dogo aliulizwa "wewe sasa mbona umebeba dvd juu chini na chini juu ndio nini?"
Dogo na akajibu "naogopa data zanaweza anguka njiani nlizozikopi humu."

Bar na maongezi

Jamaa 1: Mtoto wangu hasikii kitu nikimuambia jambo.
Jamaa 2: Anakukosea sana adabu.
Jamaa 1: Hapana ni kiziwi.

Mambo ya facebook

Baba aliingia facebook na kumuandikia mwanae wa kiume kwenye wall yake "Hi Son sio sote wazima, tumekumiss sana.HEBU SHUKA CHINI HARAKA CHAKULA KIPO TAYARI TUNAKUSUBIRI WEWE PUMBAFU.

Ugomvi baba na mama

Mtoto alikua analia nje jamaa mmoja akamkuta na kumuuliza "unalia nini mtoto?"
Katoto kakajibu "wazazi wangu wanapigana ndani?"
Jamaa: Baba yako ni nani?
Mtoto: Ndio icho wanachogombana ndani.

Hotelini india

Mtanzania alienda india, mgahawani:
M-tz: Nipatie Arul Jodi tafadhali?
Mhudumu: Umeona wapi iyo kitu mzee?
M-tz: Kwenye Menu.
Mhudumu: Hilo ni jina la mwenye hotel mzee.

Mke mgahawani

Mume akimuuliza mkewe: Siamini, yaani unakula mguu wa mbuzi wote wewe?
Mke akajibu: Hapana nimeagizia na juice.

Kitu hotelini

Wapendanao walifika mapokezi;
Mwanamke: Tafadhali tupe kitanda kimoja.
Mapokezi: Oh! Vimejaa kipo cha double.
Mwanamke: Nipe icho icho ntavisogeza karibu akikoroma tu nimtwange ngumi ya uso.

Kipofu barabarani

Ombaomba: Anti unaonekana kama malaika, niguse mkono wangu mie kipofu.
Mwanamke: Huyu atakua si kipofu.
Mume: Ni kipofu wala hadanganyi.
Mwanamke: We umejuaje?
Mume: Si amekuona upo kama malaika leo.

Tuesday, November 8, 2011

Kwa jirani...

Mwanamke: Mume wa huyo jirani yetu anambusu mkewe mara 3 kwa siku wewe kwa nini usifanye hivyo pia?
Mume akajibu: Ntafanya kama akiniruhusu kumbusu huyo mkewe.

Swali harusini

Mtoto: Mama kwa nini bibi harusi anavaa nyeupe?
Mama: Kwasababu ni siku yao ya furaha sana.
Mtoto: Mbona bwana harusi anavaa nyeusi?
Hakimu: Kwa nini umempiga mumeo na kiti?
Mshtakiwa: Mh. Hakimu meza ilikua nzito sana ndio nkachukua kiti.

Kutega shule

Simu ilipigwa:
Simu: Haloo naongea na mkuu wa shule?
Mkuu: Ndio, una shida gani?
Simu: Napenda kukutaharifu kuwa mwanangu leo hatoweza kuja shuleni.
Mkuu: Wewe una mahusiano gani huyo mtoto?
Simu: Hiyo ni sauti ya mama yangu inaongea.

Katoto shuleni

Mwalimu: Fredy jana ulitega darasani enhe?
Fredy: Sio sana mwalimu nlikua kantini tu.
Mwalimu: Kantini ukifanya nini?
Fredy: Nkitega kipindi chako.

Babu kwa dokta

Baba alipokua kwa dokta:
Dokta: Babu kwa afya yako utafikisha miaka 90.
Babu: Dokta mbona tayari nna miaka 90.
Dokta: Si unaona nlikuambia utafika 90.

Katika chumba cha upasuaji

Upo katika chumba cha upasuaji halafu kwa mbaali ganzi imepungua unasikia maneno ayaongeayo dokta:
I. Hili ni ini, na hii ni figo hiki kingine ni nini tena?
II. Hebu leta icho kitabu fungua ukurasa wa 4.
III. Hapana uko umepachana sipo rudi huku juu...

Uelewa muhimu

Mama mwenye nyumba alimpeleka mkwewe hospitali. Baada ya shughuli za hospitali alimuuliza mkwewe "mama ivi daktari alichukua na temperature?" Mkwe akajibu "kwa kweli sijui nilipaswa kuja nayo?"

Beki 3 na bosi wake

Beki tatu akimuambia bosi wake "mama mtoto ametumbukia kwenye kisima"
Mama mtoto: Enh! Ulimvisha pampers?
Dada: Ndio mama.
Mama mtoto: Bora maana angechafua maji.

Monday, November 7, 2011

Matamanio

Jamaa alienda saluni kunyoa, wakati ananyoa alomuona mwanamke pembeni akimuosha mteja akamuambia "dada leo unaonaje tukalale hotel?"
Dada akajibu "nimeolewa" jamaa akasisitiza "si unamuambia leo una over time, ntakulipa vizuri"
Mwanamke akamjibu "mwambie mwenyewe huyo hapo anaekunyoa nywele"

Mtoto na baba ake

Mtoto aliona korodani za baba ake akauliza "baba hizo nini?" Baba akajibu "mwanangu haya ni ma-apple" yakaishia hapo. Baada ya wiki akamuuliza mama ake "mama yale ma-apple mawili ndani ya suruali ya baba ni ya kienyeji au kizungu, maana ya mlinzi wetu ya kizungu.”

Taa ya gari

Dereva mmoja wa basi alimuambia kondakta "hebu toa kichwa nje uone indicator kama inawaka?" Konda alifanya hivyo na kumjibu "ndio, hapana, ndio, hapana..."

Swali la msingi

Kama kobe hana lile limfunikalo pale ni yupo uchi au hana nyumba?

Maongezi yao...

Vijana walikua wakiongea kama ifuatavyo:
Kijana 1: Tatizo lako we mbishi sana.
Kijana 2: Sio kubisha tu.
Kijana 1: Sa uliona wapi mbwa hana mguu mmoja.
Kinaja 2: Mie nimeona pahali alipouacha sasa.

Kunywa

Police wa barabarani alimsimamisha dereva mmoja na kumuhoji "mzee vipi umekunywa?"
Mzee akajibu "hapana" papo hapo mwanae akadakia "baba sema ukweli si ulikua unakunywa maji punde tu?"

Saturday, November 5, 2011

Ugenini

Jamaa ugenini alibanwa na haja kubwa. Alienda msalani aliporudi akamuuliza kwa kunong'ona mwenzake "msalani nimekuta toilet paper tatu, ya pinki, blue na nyeupe nkashindwa fahamu ipi nitumie na maji hamna."

Mwenzake akamuuliza "sasa umetumia ipi?"
Akajibu "sijatumia bado mekuja uliza kwanza kwako"

Cha pombe

Cha pombe mmoja alienda kwa daktari akipoulizwa akajibu shida yake "dokta nafikiri nna tatizo moja tu, mfumo wangu wa kilevi umejaa damu ndio sababu nashundwa pata bia nyingi. Nisaidie kupunguza..."

Wednesday, November 2, 2011

Babu kapata ajali

Babu aligongwa na baiskeli akaanguka chini jamaa mmoja akanena "mpeni maziwa fresh huyo atazinduka"

Babu nae akaibuka na kunena "na chapati tatu usisahau"