Karibu Sana.
Cheka Unenepe
Friday, April 27, 2012
Diet
"Kaka nasikia siku hizi unafanya diet" kijana mmoja akimuambia rafiki yake aliekua mnene mnene kidogo"
Papo hapo jamaa mmoja mingine kati yao akadakia "mhh! Labda afanye diet ya kunywa bia"
Wednesday, April 25, 2012
Mkopo huo
Jamaa akimshushua mwenzake "mshkaji wangu we tatizo unakopa sana, chuupi unakopa, maji unakoopa, mwanamke ukienda nae gesti unakopa pia"
Jamaa akajibu: Sasa hali tete mie nifanyeje?
Tuesday, April 24, 2012
Kibweka cha leo
Soma hii ucheke kidogo:
KESHO KUNA MAANDAMANO YA WEZI WANATAKA WAONGEZEWE SIKU, BADALA YA SIKU ZA MWIZI NI 4O, SASA ZA MWIZI ZIWE 60. UKIPATA UJUMBE HUU WATUMIE NA WEZI WENZIO WOTE.
Friday, April 20, 2012
Mgonjwa na Dokta
Mgonjwa: Dokta nimekuja nahisi nna umwa malaria na kifua.
Dokta: Sasa ushajua unaumwa nini hapa umefuata nini kwangu?
Mgonjwa: Sasa si nimekuja kwa dokta.
Dokta: Wanaojua kuwa wanaumwa kama wewe wanapitiliza maabara.
Wednesday, April 18, 2012
Pilau la bachela
Bachela mmoja aliekua akiishi kwa muda mrefu peke yake kwenye nyumba aliyopanga siku moja alitaka kupika pilau kwa mara ya kwanza.
Sasa asijue nini kinachobadilisha rangi ya wali kuwa rangi ya brown, yeye akapika kama kawaida (wali) kisha wakati wa kula akavaa miwani yenye rangi ambayo ukiuangalia wali unauona kama pilau wakati anakula.
Nani alaumiwe?
Mwanamke: Nilikubali kuolewa na wewe haraka haraka kwasababu nlikua nna hasira siku ile.
Mwanaume: Ooh! Mie sikuliona hilo nlikua kwenye dimbwi la mapenzi juu yako.
Full tank
Kijana mmoja alinunua gari, akaenda mpaka petrol station akajaza mafuta full tank. Alipotoka pale akaenda kwa fundi na kumuambia "fundi nna shida kidogo" fundi nae bila hiyana akajibu "niambie shida yako tu mkuu"
Mwenye gari akanena "nahitaji unibandikie huu mshale wa mafuta kwa gundi ubaki huku huku juu kwenye full, ili mafuta yasiishe"
Nani kaliwa?
Nani imekula kwake hapa????
Phone call
Girl:hellow
Boy:sweet mambo vp?
Girl: poa
Boy:utakuwa free weekend?nilikuwa nataka uje nyumbani....kwangu.
Girl: oh sorry,sintoweza kuja coz kuna harusi ya aunt yangu na siku ya pili kutakuwa na wageni nyumbani.
Boy:kama ni hivyo sawa just nilikuwa nataka nikufanyie suprise nimekununulia i phone.
Girl: oh usijali mpenzi wangu nitakuja,hata ukitaka nilale huko huko nitalala.
Boy:vp kuhusu harusi?
Girl:harusi ipi?nilikuwa nakutania sweety!
Boy: poa na mimi nilikuwa nakutania hny!!
Hodi hodi
Usiku mkubwa mara ngo ngo ngo mlangoni:
Wenye nyumba: Nani?
Aliepo nje: Mimi.
Wenye nyumba: Ndio wewe naani?
Aliepo nje: Mimi mwizi nimeshindwa fungua mlango nimukuja kuiba tv.
Tuesday, April 17, 2012
Cheka kispoti
Wakulima wawili walikua wanatoka shamban na zana zao za kilimo
wakapita katika uchochoro mmoja gafla waka sikia sauti, "
simameni wote wawili wakasimama bana, weka jembe
chini jamaa akaweka, weka kisu chini mmoja akasema
sina kisu-ok kama huna kisu weka mavi-jamaa akatusua
bana mdimba, ok we lamba mavi hapo fasta-jamaa wapili
akalamba bana gafla wakasikia game sindo imeisha sasa
tuchangen tena karata.
Monday, April 16, 2012
Mtoto alipotea
Mtoto wa miaka miwili na nusu alipotea alipotea na alipokua anaulizwa ili apewe msaada. Msamaria akamuuliza "enhe mama yako anaitwa nani?" Mtoto akajibu "anaitwa mama"
Akaulizwa na "baba yako je anaitwa nani?" Mtoto akajibu "baba yeye anaitwa baba pia"
Sunday, April 15, 2012
Kilo zilipozidi...
Jamaa alienda kupima uzito akajikuta ana kilo nyingi kuliko akivyotegemea akashangazwa na kunena kama ifuatavyo "haiwezekani mi ndio nna kilo nyingi hivi? Embu tupime kimoja kimoja anza na mkono... Tufuate kichwa..."
Mwizi na chizi
Mwizi kaiba tv na kuanza kukimbia nayo, kumbe ile nyumba mlikuwa na chizi akaanza kumkimbiza yule mwizi. Kila mwizi akiongeza mbio chizi nae huyo, mwishowe mwizi akasalimu amri na kusimama, yule chizi akamsogelea na kumwambia.. Daah umesahau remote hii hapa mwizi kafleti.
Uuwii
MAMA:Mwanangu unamjua mkwawa?
MTOTO:Cmjui
MAMA: pumbav kuwa makin na masomo.
MTOTO:Mama unamjua joyce
MAMA:Hapana
MTOTO:Mama kuwa makin na mumeo..
Saturday, April 14, 2012
Jino linauma
Mume akiumwa jino kweli kweli alifika kwa dentist na mkewe. Dokta akamuuliza "jino lipi linauma?" Mgonjwa akamgeukia mkewe na kumuambia "muonyeshe dokta jino linalouma"
Gongo no. 1
Njemba moja ilienda kwenye baa ya uswahilini akaagiza gongo ile namba moja. Wakati anakunywa mwenzake akamuambia "mzee jiangalie utalewa mpaka shati ukatufia hapa buuree, taratiiibu tafadhali"
Njemba akajibu "kama nikifa nistue nilianzishe tifu hatakaa mtu hapa ma*#nin"}...".
Nani ajifiche
Majira ya saa moja usiku mtoto alimuona mama yake anarudi nyumbani akamuwahi na kumuambia "mama... mama usiende nyumbani kwanza baba yupo na mwanamke mwingine, ngoja nkamuulize nani ajifiche kati ya wewe au yeye?"
Live tv
Mtoto mmoja alikua anaangalia kipindi maalumu kilichokua kikirusha kwenye tv moja kwa moja toka eneo la tukio (kipindi cha mahojiano ya hoja). Baba aliporudi nyumbani akamuambia baba ake "baba mekuona kwenye tv, mekugusa hata husikii"
Friday, April 13, 2012
Swali la mwalimu na mwanafunzi
Mwalimu: Ema kulikua na ndege watano ukamtungua mmoja watabaki wangapi?
Mwanafunzi: Wataruka wote hamna atakaebaki.
Mwalimu: Watabaki wanne mmoja atakufa.
Mwanafunzi: Mwalimu na mimi nna swali.
Mwalimu: Uliza tu.
Mwanafunzi: Kulikua na wanawake watatu wanakula koni wa kwanza anailamba, wa pili ana imega, wa tatu anainyonya yupi kati yao kaolewa?
Mwalimu: Mhh! Wa tatu ndio kaolewa.
Mwanafunzi: Umekosa alieolewa mwenye pete ya ndoa kidoleni.
Chemsha bongo
Baba akimuuliza chemsha bongo mwanae anaesoma shule ya chekechea "haya niambie kitu gani hakiwezi kuliwa wakati wa breakfast?"
Mtoto akajibu "iyo mbona rahisi baba, si lunch na dinner"
Mume na mke kaazi...
Mwanamke: Mume wangu naomba hela nkanunua bra.
Mwanaume: Mbona huna cha kuweka humo?
Mwanamke: We mbona umevaa boxer wakati huna cha kukiifadhi humo?
Lipi bora
Mwanamke huki akimchapa mumewe "wee si ulisema umekoma kutembea na wanawake wa nje?"
Mume: Mke wangu basi nisamehe sitarudia ntatembea na wanawake wa ndani tu.
Je umelewa?
Askari wa doria walimdaka mzee mmoja akiwa chakali kwa pombe huku akiendesha gari.
Askari: Mzee unajua kwamba unaendesha ukiwa umelewa.
Mzee: Hapana sijalewa afande kwani vipi (akiongea kilevi levi)
Askari: Naomba leseni na kadi ya gari.
Mzee: Ok, nishikie hii bia yangu nkutafutie hivo vitu.
Simu ya mke...
Mume wa mtu alikua yupo gesti hausi na nyumba ndogo yake. Punde simu ikaita mkewe akiwa anampigia "mume wangu nimekuja ofisini sijakukuta nimeambiwa umetoka upo wapi?" Mume nae bila hiyana "ohh my wife nimetoka nafanya kazi za nje leo"
Pombe hii?
Cha pombe mmoja akifokewa na mkewe "tatizo lako ukilewa huwa unaongea sana" njemba nayo haikukaa tu kimya akaamu kumjibu "mke wangu tatizo pombe nnazokunywa zinakua zisha-chacha ndio maana."
Wednesday, April 11, 2012
Tuesday, April 10, 2012
Mpenzi pombe
Jamaa akiiambia bia yake akiyokiinywa "wewe ndio mpz wngu! Huna wivu hata kdg hata mkiwa watatu meza moja. Tatizo lenu nikiondoka nashindwa kujua nani kati yenu kanilewesha sana"
Monday, April 9, 2012
Wapi ufunguo?
Mwanamke mmoja alipoteza ufunguo wa nyumba maeneo ya nyumbani. Sasa wakati anautafuta mumewe aliporudi akauliza na kuambiwa ufunguo umepotea. Mume akatoa simu na kumuambia mkewe "hebu nipe namba niu-beep"
Sunday, April 8, 2012
Kibweka - Pasaka
Mtoto alienda uganini siku ya pasaka, kabla ya mlo wa mchana akamuuliza mama yake kwa kumnong'oneza "eti mama na hapa watapika na toothpick?"
Mama akajibu "mwanangu hizo huwa hazipikwi"
Mtoto: Mbona nyumba ya jirani house girl huwa anazipika na zenyewe?"
Subscribe to:
Posts (Atom)