Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, November 9, 2011

Kipofu barabarani

Ombaomba: Anti unaonekana kama malaika, niguse mkono wangu mie kipofu.
Mwanamke: Huyu atakua si kipofu.
Mume: Ni kipofu wala hadanganyi.
Mwanamke: We umejuaje?
Mume: Si amekuona upo kama malaika leo.

Tuesday, November 8, 2011

Kwa jirani...

Mwanamke: Mume wa huyo jirani yetu anambusu mkewe mara 3 kwa siku wewe kwa nini usifanye hivyo pia?
Mume akajibu: Ntafanya kama akiniruhusu kumbusu huyo mkewe.

Swali harusini

Mtoto: Mama kwa nini bibi harusi anavaa nyeupe?
Mama: Kwasababu ni siku yao ya furaha sana.
Mtoto: Mbona bwana harusi anavaa nyeusi?
Hakimu: Kwa nini umempiga mumeo na kiti?
Mshtakiwa: Mh. Hakimu meza ilikua nzito sana ndio nkachukua kiti.

Kutega shule

Simu ilipigwa:
Simu: Haloo naongea na mkuu wa shule?
Mkuu: Ndio, una shida gani?
Simu: Napenda kukutaharifu kuwa mwanangu leo hatoweza kuja shuleni.
Mkuu: Wewe una mahusiano gani huyo mtoto?
Simu: Hiyo ni sauti ya mama yangu inaongea.

Katoto shuleni

Mwalimu: Fredy jana ulitega darasani enhe?
Fredy: Sio sana mwalimu nlikua kantini tu.
Mwalimu: Kantini ukifanya nini?
Fredy: Nkitega kipindi chako.

Babu kwa dokta

Baba alipokua kwa dokta:
Dokta: Babu kwa afya yako utafikisha miaka 90.
Babu: Dokta mbona tayari nna miaka 90.
Dokta: Si unaona nlikuambia utafika 90.

Katika chumba cha upasuaji

Upo katika chumba cha upasuaji halafu kwa mbaali ganzi imepungua unasikia maneno ayaongeayo dokta:
I. Hili ni ini, na hii ni figo hiki kingine ni nini tena?
II. Hebu leta icho kitabu fungua ukurasa wa 4.
III. Hapana uko umepachana sipo rudi huku juu...

Uelewa muhimu

Mama mwenye nyumba alimpeleka mkwewe hospitali. Baada ya shughuli za hospitali alimuuliza mkwewe "mama ivi daktari alichukua na temperature?" Mkwe akajibu "kwa kweli sijui nilipaswa kuja nayo?"

Beki 3 na bosi wake

Beki tatu akimuambia bosi wake "mama mtoto ametumbukia kwenye kisima"
Mama mtoto: Enh! Ulimvisha pampers?
Dada: Ndio mama.
Mama mtoto: Bora maana angechafua maji.

Monday, November 7, 2011

Matamanio

Jamaa alienda saluni kunyoa, wakati ananyoa alomuona mwanamke pembeni akimuosha mteja akamuambia "dada leo unaonaje tukalale hotel?"
Dada akajibu "nimeolewa" jamaa akasisitiza "si unamuambia leo una over time, ntakulipa vizuri"
Mwanamke akamjibu "mwambie mwenyewe huyo hapo anaekunyoa nywele"

Mtoto na baba ake

Mtoto aliona korodani za baba ake akauliza "baba hizo nini?" Baba akajibu "mwanangu haya ni ma-apple" yakaishia hapo. Baada ya wiki akamuuliza mama ake "mama yale ma-apple mawili ndani ya suruali ya baba ni ya kienyeji au kizungu, maana ya mlinzi wetu ya kizungu.”

Taa ya gari

Dereva mmoja wa basi alimuambia kondakta "hebu toa kichwa nje uone indicator kama inawaka?" Konda alifanya hivyo na kumjibu "ndio, hapana, ndio, hapana..."

Swali la msingi

Kama kobe hana lile limfunikalo pale ni yupo uchi au hana nyumba?

Maongezi yao...

Vijana walikua wakiongea kama ifuatavyo:
Kijana 1: Tatizo lako we mbishi sana.
Kijana 2: Sio kubisha tu.
Kijana 1: Sa uliona wapi mbwa hana mguu mmoja.
Kinaja 2: Mie nimeona pahali alipouacha sasa.

Kunywa

Police wa barabarani alimsimamisha dereva mmoja na kumuhoji "mzee vipi umekunywa?"
Mzee akajibu "hapana" papo hapo mwanae akadakia "baba sema ukweli si ulikua unakunywa maji punde tu?"

Saturday, November 5, 2011

Ugenini

Jamaa ugenini alibanwa na haja kubwa. Alienda msalani aliporudi akamuuliza kwa kunong'ona mwenzake "msalani nimekuta toilet paper tatu, ya pinki, blue na nyeupe nkashindwa fahamu ipi nitumie na maji hamna."

Mwenzake akamuuliza "sasa umetumia ipi?"
Akajibu "sijatumia bado mekuja uliza kwanza kwako"

Cha pombe

Cha pombe mmoja alienda kwa daktari akipoulizwa akajibu shida yake "dokta nafikiri nna tatizo moja tu, mfumo wangu wa kilevi umejaa damu ndio sababu nashundwa pata bia nyingi. Nisaidie kupunguza..."

Wednesday, November 2, 2011

Babu kapata ajali

Babu aligongwa na baiskeli akaanguka chini jamaa mmoja akanena "mpeni maziwa fresh huyo atazinduka"

Babu nae akaibuka na kunena "na chapati tatu usisahau"

Saturday, October 29, 2011

Mnyalukolo

Jamaa kwenye daladala pembeni kuma dada alianza kwa kumsalimia halafu akamuuliza "Samahani dada unaitwa google?" Dada akamjibu "hapana, n kwanini umedhani naitwa
hivyo?" Jamaa akamjibu "maana una kila kitu nnachokitafuta"

Toto hili nalo...

Mtoto aligoma kutumwa na beki tatu, Mgeni
aliyekuwepo sebuleni ikabidi aonyeshe
busara zake akamuuliza mtoto "humu ndani
mdogo nani? Mtoto akajibu "mama" Mgeni
akamuuliza "kwanini?" Mtoto akajibu "mama
kila siku anavuliwa chupi na dadii wakati mi yangu kila siku
navua mwenyewe"

Tv kubwa

Babu alienda mjini kwa mwanae. Sebuleni akakuta Tv ya inch 53 na kuishangaa ilivyo kubwa. Siku moja kabla hajaridi kijijini mwanae alikuta Tv imevunjwa kuuliza akajibiwa "ni mimi mwanangu nimejimegea nusu nkaangalie kijijini, rimoti ntatumia yangu"

Babu huyoo

Babu alifanyiwa opereshen ya kusafishwa
korodani na kuanikwa bahati mbaya yaliliwa
na paka dokta akaamua kumbandika viazi ili
asifukuzwe kazi baada ya mwezi dokta
alimuuliza mgonjwa wake vp mzee khali
yako? BABU."ah sijambo najiskia vizuri ila
kuna tatizo jengine" DOKTA" tatizo gani?"
BABU naona badala ya kuota nywele za huku naota
matembele."

Vipofu wawili

Vipofu wawili kwenye basi
wakisafiri ghafla
gari likapata ajali kipofu
mmoja wakati anamtafuta mwenzake katika
kupapasa akashika punje ya mahindi
akashtuka "hee haya meno nini?" katika
kuendelea bahati mbaya akaingiza mkono
kwenye bususu ya mwanamke akalia kwa
uchungu "maskini John meno yote
yameng'oka"

Kuku na sikukuu

Kuku wangejua kusoma na kuielewa kalenda
yaani kipindi cha sikukuu tusingewakuta
kwenye mabanda!

Friday, October 28, 2011

Simama ukaguliwe

jamaa alikuwa kwa mguu alipofika getini
kwenye kampaundi ya mshikaji wake akakuta
kibao "SIMAMA UKAGULIWE" kwakuwa
mlinzi hakuwepo jamaa akajisachi
mwenyewe then akaingia ndani, kabla
hajafika mlangoni mlinzi akamfuata na
kumuuliza kwanini umepita mlangoni bila
ukaguzi? Akajibu "nimefanya auto search"

Redio msalani

Mke mmoja alimpa mme wake radio aende
nayo chooni ili asiboreke kwa vile huwa
anakaa muda mrefu.
Basi alivyotoka akamuuliza: "enhe, mume
wangu, vipi ulienjoy?"
mume: "ah, wajinga hawa! Wameniwekea
wimbo wa taifa nimekunya huku
nimesimama!"

Mume anapobanwa

Mwanamke mmoja alimuona mumewe amevaa nguo ya ndani imevaliwa nje ndani. Kamuuliza "mume wangu mbona pichu umeivaa nje ndani kulikoni?" Mume nae akajibu "ooh nilipitia site nkaamua kuoga huko huko."

Tuesday, October 25, 2011

Mkulima mmoja alifungua akaunti sasa alipopata kadi akaenda ATM alipocheki balance akazimia. Siku ya pili tena akazimia, ya tatu akapata wa kumsomea salio kumbe mkulima akiona namba ya akaunti ndio akidhani fedha.

News

Jamaa walipokuwa bar akimsimulia jambo mwenzake:
Joseph: Umezisikia news mpya?
Ibrah: News gani tena?
Joseph: Fredy kaachwa na mkewe...
Ibrah: Ohh! Mhudumu niongeze konyagi.