Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Monday, November 14, 2011

Vioja msibani

Mh. Mmoja alipopewa nafasi ya kuongea neno,alipokuwa msibani ambae ni mwana siasa wa siku nyingi alianza kwa kusema "msiba oyee"

Ugomvi mke na mume

Mke akifoka kwa sauti "ushukuru baba yangu ndio katoa pesa ukanunua flat screen, gari na furniture vinginevyo usingekuwa na jeuri #$€$$%*+=."

Mume nae akajibu "ushukuru baba ako katoa hizo pesa vinginevyo nsingekuwa hapa... #€*+"

Kero za mke

Mwanamke: Kama mumeo anakukera kila siku si uachane nae unde zako tu.
Mke: Sitaki kufanya kitu chochote kitachompa furaha kikiwemo icho.

Machinga complex

G: Hiivi kwa nini Mbeya na Tabora wasiwajengee machinga complex yao?
P: Aah wale wawatolee fotokopi halafu wawapelekee tu.

Sunday, November 13, 2011

Video library

Mteja alienda video library kuazima sinema ya kuangalia ikawa hivi:
Mteja: Nimekuja kuchukua Batman forever si ipo?
Mhudumu: Ipo ndio ila yapaswa kurudishwa sio kuichukua forever.

Kwa dentist

Dokta: Embu acha hizo kelele sijaanza hata kung'oa jino lenyewe.
Mgonjwa: Ndio najua, toa mguu wako umenikanyaga vidole vyangu vyote.

Urithi saluni

Mzee mmoja kutokana na umri aliamua kumpa mwanae saluni yake aiendeshe. Akampa maneno yafuatayo "mwanangu hii kazi inabidi uwe makini sana, wateja wengine wakali na wanatabia ya kugeuka ghafla hivyo angalia usijikate na wembe"

Saturday, November 12, 2011

Kesi ya mke na mume

Mwanamke aliulizwa "nini alisema kwako mumeo mpaka yakawa haya ya kumtwanga na kiti?" Mwanamke akajibu "jina langu naitwa Irene sio Judith, sa muulizeni Judith ni nani?"

Mifupa ya binadamu

Jamaa akipewa majibu na daktari wake baada ya uchunguzi "inaonekana mifupa ya miguuni mwako imekua laini sana saasa..." Akamkatisha na kumuambia "shhh taratibu dokta hapo nje kuna mbwa wanne watasikia"

Kitu cha heshma

Mtoto aliona nyeti za baba ake kuuliza akajibiwa "hii ni heshima mwanangu." Siku ya pilivwakaja wageni mtoto akaambiwa awape heshima si akafungua na kutoa nyeti kisha akanena "mnashangaa hizi baba, ana heshima kubwa zaidi"

Friday, November 11, 2011

Swali la mtego

Mwalimu: Uliona wapi bahari isiyokua na maji au dunia isiyo na watu?
Mwanafunzi: Si kwenye ramani au atlas.

Uzurulaji

Askari wa doria: Wewe kijana unafanya shughuli gani hapa mjini?
Kijana 1: Sina nnachofanya sina ajira kabisa.
Polisi: Na wewe mwingine unafanya shughuli gani?
Kijana 2: Mie ni boss wake.

Jumba la makumbusho

Jamaa bahati mbaya aliangusha bakuli la kuvunjika likavunjika ndani ya jumba la makumbusho. Askari akaja na kusema "mungu wangu hicho ulichovunja ni cha miaka 2000 iliyopita"

Aliyeangusha akajibu "ohh afadhali mi nilidhani kipya"

Baridi kali

Juma: We vipi mbona unatetemeka mikono.
China: We huhisi baridi kama mimi?
Juma: Sa si ingiza mikono mfukoni mwa suruali.
China: Mifuko imejaa nimeweka gloves.

Swali na jibu

Kijana alimuuliza maswali ya chemsha bongo mtoto:
Kijana: Kwa mfano baba kakupa shilingi 500 na mama kakupa shilingi mia 500 utakua na shilingi ngapi?

Mtoto akajibu: Ntakua na shilingi 500.
Kijana: Kw nini unasema hivyo?
Mtoto: Kw sababu mama hawezi kuipata hiyo 500.

Swali la mwalimu

Mwalimu aliuliza swali "enhe Juma, baba yako akikupa shilingi 150 na mama yako akikupa shilingi 150 utakua na shilingi ngapi?"

Mwanafunzi akajibu "ntapata kijoti"

Mabusu motomoto

Sam: Huwa nini m-kiss mke wangu kila siku kabla sijaenda kazini.
Ibra: Hata mimi namfanyia hivyo ukisha ondoka tu.

Macho mabovu

Mgonjwa: Dokta nasumbuliwa na macho sana siku hizi.
Mtu: Ni kweli unahitaji hapa ni mgahawani nenda,hospitali.

Wednesday, November 9, 2011

Ya usiku

Ilikuwa hivii:-
MTOTO: Eti baba unataka kuanza tena shule?
BABA: Kwa nini unauliza ivyo?
MTOTO: Jana ucku nlisikia mama anakwambia anataka muende la pili! Uthikubali baba utachekwa!

Chizi ajibu swali

Kijana: Nasikia mkeo anaongeaga mwenyewe akiwa peke yake.
Mtu mzima: Kwa kweli sijui, siwagi nae akiwa peke yake.

Mgonjwa huyu...

Mume: Daktari amekuja anataka kukuona.
Mke: Najisikia vibaya sitaki onana na mtu yeyote.

Gharama...

Mlala hoi alipoenda kwa daktari kupata huduma ya kiafya:
Dokta: Umeshawahi kuzimia?
Mgonjwa: Ndio, mara ya mwisho ulivyonitajia gharama zako.

Betri ya saa

Kimi: Kwa nini unatoa betri kwanye saa na kuzianika juani?"
Luko: Ili zipate kuwa na nguvu zaidi, nazirudishaga nkitaka angalia muda tu.

Tekinolojia

Dogo aliulizwa "wewe sasa mbona umebeba dvd juu chini na chini juu ndio nini?"
Dogo na akajibu "naogopa data zanaweza anguka njiani nlizozikopi humu."

Bar na maongezi

Jamaa 1: Mtoto wangu hasikii kitu nikimuambia jambo.
Jamaa 2: Anakukosea sana adabu.
Jamaa 1: Hapana ni kiziwi.

Mambo ya facebook

Baba aliingia facebook na kumuandikia mwanae wa kiume kwenye wall yake "Hi Son sio sote wazima, tumekumiss sana.HEBU SHUKA CHINI HARAKA CHAKULA KIPO TAYARI TUNAKUSUBIRI WEWE PUMBAFU.

Ugomvi baba na mama

Mtoto alikua analia nje jamaa mmoja akamkuta na kumuuliza "unalia nini mtoto?"
Katoto kakajibu "wazazi wangu wanapigana ndani?"
Jamaa: Baba yako ni nani?
Mtoto: Ndio icho wanachogombana ndani.

Hotelini india

Mtanzania alienda india, mgahawani:
M-tz: Nipatie Arul Jodi tafadhali?
Mhudumu: Umeona wapi iyo kitu mzee?
M-tz: Kwenye Menu.
Mhudumu: Hilo ni jina la mwenye hotel mzee.

Mke mgahawani

Mume akimuuliza mkewe: Siamini, yaani unakula mguu wa mbuzi wote wewe?
Mke akajibu: Hapana nimeagizia na juice.

Kitu hotelini

Wapendanao walifika mapokezi;
Mwanamke: Tafadhali tupe kitanda kimoja.
Mapokezi: Oh! Vimejaa kipo cha double.
Mwanamke: Nipe icho icho ntavisogeza karibu akikoroma tu nimtwange ngumi ya uso.