Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Sunday, December 25, 2011

Kwenda xmas

Mtoto: Mama! Baba si ameenda xmas?
Mama: Ndio mwanangu.
Mtoto: Mpigie simu muambie mbona xmas yeye amekuja huku?

Xmas

Chekazone inawatakia wadau wote Heri ya Krismas.
Kucheka ni moja ya kuwa na afya njema.
Mungu awatangulie kwa kila jambo.

Saturday, December 24, 2011

Washua nao...

Mshua mmoja akimuuliza mwenzake baada ya kukutana airport, "rafiki yangu unaenda wapi tena?"
Mshua nae akajibu "nna hisi nna ka-malaria naenda india kucheki."

Ombaomba tajiri

Ombaomba: Nimeandika njia 100 za kuwa tajiri.
Mpita njia: Sasa mbona unaomba bado?
Ombaomba: Hii ni njia mojawapo ya kuwa tajiri.

Masumbwi

Kwenye masumbwi:
Kocha: Kwa nini hauzuii ngumi za mpinzani wako?
Mpiganaji: We huoni nnkivyozizuia kwa uso wangu?

Mpenda bia

Jamaa: Ndugu yangu kwa nini unapenda sana bia?
Mlevi: We hujui? Bia ni tamu mno.
Jamaa: Tamu mno kama nini sasa?
Mlevi: Tamu kama bia.

Friday, December 23, 2011

Walevi bwana

Walevi wawili maongezini:
Mlevi 1: Nna mpango wa kuinunua Dunia.
Mlevi 2: Mhh! Huwezi...
Mlevi 1: Kwa nini siwezi?
Mlevi 2: Siiuzi tu.

Si kavunja cha kale

Mhusika wa jumba la mambo ya kale akilalamika "Umevunja seti ya vikombe vilivyotumika miaka 800 iliyopita."
Mgeni/mtalii: Oh asante Mungu mi nlijua ni vipya.

Fundi aje...

Rafiki: Ulisema ungemleta fundi kengele ya, mlangoni siku tatu zilizopita nkaona kimya.
Rafiki 2: Nlimtuma na alikuja akabonyeza kengele wee hamna aliemfungulia.

Tip...

Mhudumu akipewa tip baada ya kumpokea mgeni hadi kwenye chumba cha hotel.
Mhudumu: Mh mh! Mzee tip kidogo.

Mzee akampatia 100Tsh.
Mhudumu: Mzee hapa kama unanitukana angalau ingekua 200Tsh.
Mzee: Siwezi kukutukana mara mbili.

Nani anachapwa?

Kijana: Kwanini ukifanya kosa baba ako anamchapa kaka ako?
Kijana: Tuko mapacha

Mtoto wa nani?

Mwanamke 1: Nna wasi wasi mume wangu anani-cheat.
Mwanamke 2: Unahisi nini haswaa?
Mwanamke 1: Watoto wawili wa mwisho nlowazaa hajafanana nae.

Jumba la makumbusho

Walipoeenda kusoma vikaratasi vya maoni ya wageni watembeleao jumba la makumbusho, walikuta kikaratasi kimeandikwa hivi:

"Kulikua na mvua kubwa nje, ndio maana nkaingia humu. Asanten kwa hifadhi"

Tangazo mume

Mwanamke 1: Nliona tangazo gazetini umetanga kumchoka mumeo ?
Mwanamke 2: Nimepata barua 200 zikisema nichukue waume zao.

Thursday, December 22, 2011

Kupima damu

Jamaa alienda pima malaria, nesi akamtoboa damu ikawa haitoki, akatoboa tena ikawa vile vile. Nesi akaamua kunyonya kidole ili itoke.
Jamaa kuona vile akanena "nesi na mkojo hautoki"

Msosi fasta

Jamaa akimsimulia jambo mwenzake "aisee dah! Ile hotel iko fasta kukuandalia msosi sijawahi ona."
Mwenzake akamjibu "hehe we hujui? Mwenye hotel anafuga simba wawili jikoni"

Wezi wawili

Mwizi 1: Tumesahau kuhesabu pesa kiasi gani tumeiba.
Mwizi 2: Ondoa shaka kesho magazeti yatasema ni Tsh ngapi?

Ndani ya lecture

Mwanafunzi 1: Ukweli sielewi kabisa Prof. Anachotufundisha.
Mwanafunzi 2: Prof. Mwenyewe anasemaga hajui anachotufundisha.

Huyu nae

Mpita njia: umesema umepoteza pochi ndani sasa mbona upo nje unaitafuta?
Mpoteza pochi amajibu: Ndani kuna giza siwezi iona.

Walevi wawili

Walevi wawili walikiongea njiani kurudi makwao:
Mlevi 1: Hiivi nani wanakua wasikilizaji pande zote mke na mume wakipayukiana?
Mlevi 2: Aah iyo simpoo si majirani...

Hakimu na mtuhumiwa

Hakimu: Mara ya mwisho nlikuonya usirudi tena hapa mahakamani hujanisikia.
Mtuhumiwa: Mh. Hakimu niliwaambia hawa polisi ila hawakunisikiliza.

"Diet"

Jamaa akipewa ushauri na dokta "sasa uanze diet, pata yai 1 tu na nusu kikombe cha maziwa"
Mpewa ushauri akauliza "sawa dokta, nifanye ivyo kabla au baada ya lunch?"

Liniumezaliwa?

Mwalimu: Fred umezaliwa tarehe ngapi?
Fred: Tarehe 26 Septemba.
Mwalimu: Mwaka gani?
Fred: Kila mwaka.

Wednesday, December 21, 2011

Mtu na mdeni wake

Jamaa alikua anamdai rafiki yake hela yake siku nyingi na kupeana kalenda tuu juu ya kulipana kila wakutanapo. Siku 1 wakati wapo bar...

Ghafla majambazi hao mara kusanyeni wallet, simu nk... Jamaa akatoa bahasha na kumpa rafiki yake.
Rafiki akauliza "hiki nini wanipatia?"
Akajibu "si ile pesa yakl unayonidai"

Ujumbe wa dokta

Jamaa aliamka asubuhi na kukuta ujumbe toka kwa dokta aliemfanyia upasuaji siku mbili zilizopita ukisema hivi:

"Tafadhali fika hospitalini mara moja, nimeshindwa nunua gazeti leo kuna sarafu yangu ya 100Tsh ilidondokea tumboni wakati nakufanyia upasuaji"

Mume wa 3

Mwanamke: Mungu wangu unaonekana kama mume wangu wa tatu.
Mwanaume: Kwani una wanaume wangapi waliokuoa?
Mwanamke: Wawili tu mpaka sasa.

Kuungama kanisani

Kijana alienda kuungama kwa paroko:
Kijana: Baba paroko nimekuja kuungama...
Paroko akajibu: Haina haja nimesoma blog yako yote.

Swali la leo

Tukikutana Bar twapeana ofa vinywaji... Petrol station mbona twachuniana? (naulisa)

Kikojozi

Mtoto akilalama kwa mama yake "mama unanionea tu, mbona baba usiku namsikia anakuuliza akojoe na unamruhusu?"

Kigugumizi

Mtoto mmoja alimuuliza mama yake swali "mama kwanini baba kila siku anapenda kulala juu yako?"
Mama alikwama kutoa jibu.