Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Wednesday, October 12, 2011

Simu ilipopigwa

Mwanaume alipiga simu nyumbani akapokea mwanamke si sauti anayoifahamu. Ikawa hivi:
Mwanaume: We ni nani?
Mwanamke: Mimi ni house girl.
Mwanaume: Mbona sijaajiri house girl kwangu.
Mwanamke: Nimeajiliwa asubuhi hii...

Mwanaume: Huyo mwanamke alekuajiri yu wapi?
Mwanamke: Yupo chumbani na mume wake.
Mwanaume: Enhe? Nani? Mi ndio mumewe. Sasa sikiliza unataka kupata milioni 4?
Mwanamke: Ndio baba.

Mwanaume: Nenda kachukue pisto ipo... Kisha uwatungue wote pumbavu zao.
Mwanamke alipofanya akarudi kwenye simu "enhe sasa mzee miili yao naiweka wapi?
Mwanaume akajibu "itupe kwenye swimming pool.
Mwanamke akajibu "lakini hamna swimming hapa nyumbani"
Mwanaume akanena "ngoja kwanza hapo ni nyumba plot. No. 811?"

No comments:

Post a Comment