Karibu Sana.

Cheka Unenepe

Tuesday, August 16, 2011

Kazi ipo

Jamaa alimuuliza rafiki yake ampe ushauri kabla hajaingia kwenye dimbwi la kuitwa mwana-ndoa "eti kaka kitu gani cha kufanya mwanamke awe na furaha maisha ya ndoa"
Rafiki akamjibu "mpende sana mkeo na usijaribu kumu-elewa kuhusu wanawawake"

Miguu ya kuku

Mteja alipofika mgahawani akamuita mhudumu na kumuuliza;
Mteja: Una miguu ya kuku?
Mhudumu: Hapana ninayo hii hii yangu tu.

Girlfriend na Boyfriend

Boyfriend: Unataka niku-kiss?
Girlfriend: Hapana.
Boyfriend: Unakumbuka swali nlokuuliza.
Girlfriend: Unataka niku-kiss?
Boyfriend: Ndio, usisitizapo tu.

Monday, August 15, 2011

Mtihani ulivyokawa...

Msichana mmoja akimsimulia boyfriend wake;
Msichana: Ule mtihani ni kama girlfriend?
Mvulana: Unamaanisha nini kufananisha na girlfriend?
Msichana: Ngumu kumuelewa, complication, maswali mengi na majubu yake sasa huwa mhh!

Mlangoni

Mtu: We mtoto mama yako yupo nyumbani?
Mtoto: ndio. Jamaa akagonga sana hamna aliefungua.
Mtu: We mtoto si umesema mama ako yupo nyumbani?
Mtoto: Ndio yupo, hapa sio tunapoishi.

Inzi kwenye supu

Mteja: Mhudumu! Hii supu kuna inzi wawili wameingia...
Mhudumu: Usijali hawajui kuogelea watakufa tu.

Uoga huu....?

Mwanaume mmoja alisikika akisema "Mke wangu muoga kweli, hadi maji eti anaogopa" Mwenzake akamuuliza "kivipi?"
Njemba akajibu: Si kila nikirudi namkuta akioga na mlinzi wetu.

Kasichana & Kavulana

Ka-sichana: Unafikiri kwa nini Mungu alimuumba msichana kabla ya Mwanaume?
Ka-vulana: Alitaka kutengeneza copy ya mwanamke kabla ya final copy.

Sekunde 55

Mgonjwa: Daktari nina sekunde 55 tu kabla sijaaga dunia, nisaidie nisife.
Dokta: Nakuja nisubirie kwa dakika 1 tu.

Mvua.

Boss: Ally nenda kamuagilie maua muda umefika.
Ally: Boss lakini kuna mvua inanyesha nje.
Boss: Chukua mwavuli.

Sunday, August 14, 2011

India

Mvuta bangi anamuliza mlevi, "Eti, India iko mbali?"
Mlevi: "Sidhani, kwa sababu tuko na Muhindi mmoja kazini. Huwa anakuja kwa baiskeli kila siku!"

Meneja na Sekretari

Boss wa kampuni kamkuta meneja anampa mabusu motomoto sekretari wake akauliza kwa ukali "wewee nakulipa kufanya huu ujinga au?"
Meneja akajibu "hapana boss hii ni for free tu."

Mshahara oyee

Mzee aliporudi nyumbani mwisho wa mwezi swali la kwanza aliloulizwa na mkewe "haya mshahara uko wapi?"
Mume: Nimeshautumia wote, nimenunua kwa ajili ya hapa nyumbani!
Mke: Umenunua nini cha kumaliza laki tano yote?
Mume: Nimenunua raundi kumi za bia tuburudike...

Vimbwanga

Mlevi mmoja aliingia choo cha kike, akawa anakojoa huku amekaa chini mtu akamkuta na kumuuliza "vipi?" Mlevi bila hiyana akajibu "wee huoni tangazo limeandikwa kaa chini wakati wa kukojoa" (choo ni kile kukaa).

Saturday, August 13, 2011

Nani zaidi...

Mama alimuuliza mwanae. "Obama ni nani?"
Mtoto akasema "sijui".
Mama akasema "zingatia masomo."

Mtoto nae akamuuliza mama yake unajua "Jenifer ni nani?"
Mama akajibu "Sijui"
Mtoto akamjibu "Mzingatie sana mumeo!"

Friday, August 12, 2011

Pombe bwana

Jamaa mmoja baada ya ku-pombeka vya kutosha ugenini mkoa fulani nchini Tanzania alipangisha kwenye hoteli moja ya ghorofa kadhaa. Sasa baada ya kulewa chakari akapanda Bajaj na kumuambia dereva wa bajaj "nipeleke ghorofa ya tano"

Kizee kwa Daktari

Kizee kimoja kilienda kwa daktari wake na mkewe wote wazee. Dokta baada ya kumfanyia uchunguzi wa mwanzo dokta akamuambia babu "nahitaji mkojo wako, haja kubwa kidogo, na mbegu za kiume tufanyie uchunguzi"

Babu akamgeukia mkewe (bibi) nae bibi akamuuliza "nini?"
Babu akauliza "amesemaje dokta?"
Bibi akajibu: Anataka chupi yako.

Vimbwanga vya simu

Jamaa mmoja alimpa rafiki yake simu ili atume ujumbe mfupi maana alikua ana shida na hiyo huduma, jamaa alipompatia akampa na sharti "usiandike meseji ndefu sana wino umebaki kidogo sana"

Dawa ya kichwa

Kaka mmoja alienda kwa daktari, "dokta hiki kichwa chaniuma saaana karibu kila siku ipitayo" Dokta akamjibu ngona nikupe mfano, mimi kilinitokea miaka kadhaa nikamuomba mke wangu awe ananikanda kila siku halafu mwishoni nampa penzi murua kikaacha kabisa kuuma"

Wiki kadhaa mbele jamaa akarudi kwa dokta "aisee dokta umenisaidia sana, ile mbinu imenisaidia sana sana. Sasa nimepona" Dokta akajibu "safi sana"
Kabla mgonjwa wake hajaondoka akamuambia "...na dokta sebule kwako pazuri sana"

Monday, August 8, 2011

Nyani wa mzungu

Mzungu alipita na nyani wake mbele ya kigenge cha muuza ndizi, yule nyani akapora ndizi akala. Muuzaji akamkasirikia, mzungu akasema unakasirika nini wakati kala ndugu yako!

Mzungu akaondoka, aliporudi akuta nyani wake kafa. Akauliza kwa nini mmemuua nyani wangu? Muuzaji akajibu hayakuhusu haya mambo ya kifamilia!!

Sunday, August 7, 2011

Gari inaoshwa

Mzee mmoja alimuagiza mwanae mdogo wa kiume amuoshee gari yake akamuambia "itakate umesikia?" Baada ya muda baba mtu akatoka akamuona baba mwanae anaosha gari na maji ya moto kumuuliza dogo akajibu "si ili itakate baba"

Saturday, August 6, 2011

Mbwa mkali

Nyumba moja yenye geti na kibao kiliandikwa kama tangazo kuwa. "Mbwa mkali" usiku mmoja wezi waliingia kwenye hiyo nyumba wakamuiba na mbwa mwenyewe.
Jamaa alimuuliza mwenzake "ingekua vipi gari ukiipaki ndio unakula mafuta?"

Friday, August 5, 2011

USA waligundua mashine ya kukamata wezi:

USA ilikamata wezi 20 kwa siku.
UK ilikamata wezi 50 kwa masaa 10.
Germany ilikamata wezi 80 kwa masaa 6.
Sudan ilikamata wezi 200 kwa saa 1.
Nigeria ilikamata wezi 500 kwa dk 30.
Tanzania ndani ya dk 15 wakaiba na mashine yenyewe.

Mtishia mtoto

NILIKUWA kwenye basi natoka kazini narudi nyumbani, kwenye viti vya pembeni yangu kulikuwa na mama mwenye mtoto.

Wakati tunaendelea na safari yule mama alitaka kumnyonyesha mwanawe, mtoto akagoma, mama akamwambia nyonya, kama utaki nampa anko anyonye!"
 
Anko ni abiria kijana mwanaume aliyekaa na huyo mama.

Mtoto akanyonya kidogo akaacha, mama yake akamtishia tena kumpa anko.
Yule kaka kwa hamaki akasema,"mama uwe na msimamo, nimepitiliza vituo vinne kwa ajili hiyo!

Chabo

Jamaa wakipiga chabo! Ghafla polisi akatokea na kuwauliza "nyiee mnafanya nini hapo" wale masela wakageuka na kumuambia polisi "shhhhh...." Huku wakimuonyesha ishara ya aje na yeye kushuhudia, polisi nae akanogewa.

Wednesday, August 3, 2011

Bajaj - Kioo

Dereva mmoja wa bajaj niliona kioo cha bajaj yake cha mbele kimepasuka kwa pembeni mithili ya jiwe limevunja, kumuuliza kulikoni akajibu "wamenivunjia kioo wakaingia na kuiba laptop"

Wali nyama

Jamaa mmoja kila akienda kuagiza wali nyama anapewa nyama kidogo, siku ya pili akaenda na kuagiza nyama wali....

Monday, August 1, 2011

Umeme

Jamaa mmoja alimtumia msg rafiki "umeme wamekata"
Rafiki akajibu "sie tuna wiki sasa hawajakati"
Jamaa: Hata sie tangu wiki iliyopita.

Baada ya kama saa moja kupita yule aliemtumua msg rafiki ake akamuandikia msg nyingine tena "hee! Kumbe umeme luku umeisha!"

TV Set

Jamaa mmoja alienda nunua Tv baada ya kutajiwa bei akahoji "samahani hii si mnaiita Tv Set?" Muuza duka akajibu "ndio"
Mnunuzi akamalizia "sasa kama ni Tv Set mbona mwanuza moja?"